Hood bus Service -hatimaye legend wa biashara ya usafiri wa mabasi ameanguka

Hood bus Service -hatimaye legend wa biashara ya usafiri wa mabasi ameanguka

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Kwa wakongwe kama mimi nakumbuka misemo iliyokuwa inaandikwa kwenye mabasi mfano;

Bata kapata bwana...! hood
hapa hood anamtania Islamu kwa kuongeza basi la pili.

Bata hapewi pumba ! Islamu
hapa Islamu anamtania hood.

Jino moja mswaki wa nini?... Hood
Hapa Hood anamnanga Islamu kwa kuwa na basi moja tu njia ya Dar-Arusha.

Meno mengi yote mabovu....Islamu
hapa Islam anamjibu hood kuwa ana mabasi mengi lakini hayana kiwango.

Hii ni baadhi ya misemo na vionjo vya vilivyokuwa vinaandikwa kunogesha ushabiki wa kampuni za mabasi hususani mabasi ya Arusha na morogoro enzi hizo.

Leo hii nimepata taarifa ya msiba wa legend wa usafirishaji enzi hizo akishika njia ya Dar-moro, Arusha - Moro , Arusha-Mbeya n.k

Mzee Hood kampuzika kwa amani na sasa rasmi amemuachia njia mzee Abood.
 
Back
Top Bottom