Mwili wa binadamu una hormones nyingi sana zikiwa na kazi mbali mbali...na hivyo sababu zake za kuwa nyingi au kidogo ni tofauti pia, na hii inategemea na hormone husika inatengenezwa sehemu gani ya mwili.
Kila hormone ina range ya kiasi chake cha kawaida kwenye mwili ili kuweza kutimiza effect husika (ni vigumu kiwango cha 800 unachoongelea ni kwa hormone gani). Lakini kutokana na hali au matatizo fulani, hormone hiyo inaweza ikawa nyingi kupita range ya kiasi kinachoptakiwa, au chache chini ya kiasi kinachotakiwa! Ikiwa nyingi husababisha overactivity ya system husika, na ikiwa kidogo basi underactivity, na hayo yote ni matatizo.
Sababu tofauti kutokana na sehemu inayozalishwa hormone hiyo zinaweza kusababisha kuzalishwa kwa wingi...mfano kansa ya kiungo kinachozalisha hiyo hormone (mfano adrenal tumor, pituitary tumor etc), lakini pia kuna magonjwa au uvimbe mwingine ukasababisha kuzalishwa kwa kiasi kidogo cha hormones (mfano ovarian tumor).
Ni rahisi kama ungekuwa specific unaongelea hormone gani ili kuweza kufahamu sababu specific zinazosababisha hormone hiyo ipungue au iongezeke mwilini!