Hosea aligeuzia Bunge kibao

Hosea aligeuzia Bunge kibao

Mwanakijiji,

Kama sikosei ntakuwa nimekuelewa hivi kwamba:

Vyombo kama CAG kwa Tanzania, viwe na uwezo wa kutafuta makosa na wakiona makosa wanamtaarifu muendesha mashtaka wa serikali. Hawa wote wawili inabidi wawe na wanasheria waliobobea ili wasiwe wanapeleka kesi zisizoshindika mahakamani.

Nimekuwa naona katika film nyingi sana za USA, Afisa wa mashitaka akikataa kupeleka kesi mahakamani kwa kufahamu kuwa hana ushahidi wa kutosha. Tanzania inafanyika mara mbili. Hawa wanakagua, wanampasia DPP na yeey akipata habari anaanza kukagua kilekile ambacho kimeshakaguliwa. Hapo sasa kama hongo haikutokea kwa CAG basi wataitoa kwa DPP na kesi inafutiliwa mbali.

Hawa jamaa wangelibaki kama wanasheria wa kushtaki basi. Wakipata ushahidi, kwa kutumia wanasheria wao, wachunguze kama wanaweza kushinda. Kama hawawezi basi wanakubaliana na CAG kuwa ushahidi ni dhaifu na watafute ushahidi zaidi.
 
Tuwaache TAKUKURU wafanye kazi yao kwa mujibu wa sheria. Bunge pia tufanye kazi yetu ya kuwasimamia hao TAKUKURU ili watende mema. Hiyo ndio checks and balances.

Mh. Zitto naomba kutofautiana na wewe kidogo kwenye hili swala - hebu kwanza turudi nyuma kidogo...mnamo mwezi wa nne mwaka huu Edward Hosea, MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), baada ya kushutumiwa na wabunge na kutaka awajibike kwa uzembe alikuwa ha haya ya kusema kwenye semina iliyowajumuisha wabunge na maofisa wa TAKUKURU:-
Hapa hatukuja kulumbana, tumekuja kwenye semina, si mahala pake, lakini nyie wabunge ndio mlioamua kupitia Kamati Teule ya Bunge na mapendekezo yenu yapo, kwa hiyo iulizeni serikali, lakini hatuko hapa kushambuliana. Acheni kuhoji mambo hayo, kwani tukianza kuchambuana, hakuna atakayebaki salama !. Wapo wabunge wanaohudhuria semina zaidi ya tatu kwa siku moja na kusaini posho, lakini hata baada ya kuwezeshwa kwa posho hizo, hakuna uwajibikaji. Kwa kweli kuna mambo mengi yanayotokea, lakini tunayafumbia macho !

  • Huyu ndiye Hosea aliyeisafisha Richmond akidai taasisi yake haikuona tatizo lolote na hiyo kampuni feki.
  • Huyu ndiye Hosea aliyeonya kuwa watuhumiwa wa EPA ni wazito na wakikamatwa nchi itayumba.
  • Huyu ndiye Hosea ambaye aliwajibu wazalendo waliomtuhumu kwa kushindwa kazi kuwa hajiuzulu ng'o na wakitaka washitaki kwa Raisi aliyemteua.
  • Huyu ndiye Hosea anayetuhumiwa kwa mambo chungu nzima ya kujilimbikizia mali ndani na nje ya nchi.
  • Huyu ndiye Hosea aliyeapa kulivalia njuga swala la Rada toka ripoti ya SFO itolewe halafu hivi leo kama kawaida anataka kula sahani moja na kamati za bunge zilizoanika janja yake na kumuumbua !
Hapana Zitto, hapa sikubaliani na ushauri wako, kama TAKUKURU lazima wafanye huo uchunguzi basi Hosea akae pembeni la sivyo huku ni kutafutana uchawi !!
 
Najua unapenda historia na literature, utakuwa umemsoma Kaisari.

unachojua sicho. sijawahi kumsoma kaisari.

Isitoshe Kaisari ni favorite subject wa idol wako, Mwalimu Nyerere. Naamini umesikia mambo yake.

Sina idol katika binadamu yeyote yule. Na sijui kama Nyerere favourite subject yake ilikuwa ni Kaisari. Kutafsiri kitabu haina maana ndio somo lake kuu. Vinginevyo kwanini lisiwe "Mfanyabiara toka Venice"?

Kwa nini Kaisari alisema mke wake hatakiwi kushukiwa? Nini logic ya hiyo concept iliyo maarufu duniani?

Kwa sababu kaisari alikuwa ni kaisari.. I guess.
 
Kwa hiyo hata wewe kamati yako inachunguzwa. Hiyo ni aibu!

Kwa nchi zilizoendelea ki utandawazi na uwajibikaji wa viongozi, hii ingekuwa ni kashfa kubwa kwa mtu kama Zitto, ambaye ndio kama mwokozi au mtume fulani wa kisiasa akatokea na yeye tume yake inachunguzwa.

Zitto shukuru Mungu uko kwenye uongozi nchi kama Tanzania ambapo kitu kama hicho watu hawajali.

Ndio Kamati za Bunge zinachunguzwa na mimi nadhani ni jambo la heri. Hakuna aliye juu ya sheria. Kamati zote ikiwemo kamati yangu, kamati ya Cheyo na Kamati ya Slaa (hizi ni kamati za mahesabu).

Nchi nyingine uchunguzi ukifanyika inakuwaje?
 
  • Huyu ndiye Hosea aliyeisafisha Richmond akidai taasisi yake haikuona tatizo lolote na hiyo kampuni feki.
  • Huyu ndiye Hosea aliyeonya kuwa watuhumiwa wa EPA ni wazito na wakikamatwa nchi itayumba.
  • Huyu ndiye Hosea ambaye aliwajibu wazalendo waliomtuhumu kwa kushindwa kazi kuwa hajiuzulu ng'o na wakitaka washitaki kwa Raisi aliyemteua.
  • Huyu ndiye Hosea anayetuhumiwa kwa mambo chungu nzima ya kujilimbikizia mali ndani na nje ya nchi.
  • Huyu ndiye Hosea aliyeapa kulivalia njuga swala la Rada toka ripoti ya SFO itolewe halafu hivi leo kama kawaida anataka kula sahani moja na kamati za bunge zilizoanika janja yake na kumuumbua !
Hapana Zitto, hapa sikubaliani na ushauri wako, kama TAKUKURU lazima wafanye huo uchunguzi basi Hosea akae pembeni la sivyo huku ni kutafutana uchawi !!

TAKUKURU ni zaidi ya Hosea.

Hii ni Taasisi. Haiwezi kuacha kufanya majukumu yake kwa mujibu wa sheria kwa sababu eti Bosi wao hatuna imani naye. Lakini ni huyu huyu Hosea tuliyemfurahia kwa kuwafikisha kina Mramba mahakamani.

Tuchunguzwe tu na tukikutwa tumechezea fedha za Umma hatutakuwa na 'credibility' ya kuendelea kushika nyadhifa za Umma. (kesi ya Uingireza na Wabunge wao kutumia vibaya fedha ndio yaweza kutokea hapa nyumbani kufuatia uchunguzi wa TAKUKURU)
 
Zitto; kuna mgawanyo mzuri wa kazi na mgawanyo mbaya wa kazi. Kwa vile umetolea mifano taasisi za Marekani niseme hivi.

Taasisi mbalimbali za hapa zina uwezo wa kukusanya ushahidi ambao unaweeza kutumika mahakamani na zaidi ya yote zina uwezo pia wa kukamata (arresting power). Hivyo utaona kuwa idara hizi zina nguvu tofauti tofauti.

Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Marekani (iliyoko chini ya Wizara ya Biashara) ina wakaguzi wa aina mbalimbali lakini pia ina wale wanaoitwa "Special Agents" ambao ni maafisa wa kusimamia sheria wakiwa na nguvu za kuzuia, kukamata na kupekua kupata ushahidi. Wanapofanya uchunguzi na wanapoamini kuwa uhalifu umefanyika wana uwezo wa kumkamata mhusika na kukusanya ushahidi wa tukio la kihalifu na wakapelaka ushahidi huo kwa Waendesha mashtaka wa Marekani (Federal Prosecutors).

Wale FPs wao wanapitia ushahidi huo na mara nyingi wanafungua kesi kwa kutegemea ushahidi uliokusanywa na maafisa wa Mkaguzi Mkuu ambao huitwa kama mashahidi wa upande wa mashtaka.

Hilo pia linahusu FBI ambao kama unavyojua ni law enforcement agency. FBI wana uwezo wa kupekua kukamata na kukusanya ushahidi wa suala la kihalifu na ushahidi wao huuleta kwa FPs ambao hufungua mashtaka kwa kutegemea ushahidi uliokusanywa na FBI.

Kinachoepukwa ni kurudia uchunguzi mwingine tena. Yaani FPs hawaanzishi uchunguzi mwingine ila wasiporidhika wanawaambia watu wa hiyo idara kuwa ushahidi wao siyo mzuri n.k

Ni kweli tumeondoa uendeshaji mashtaka toka mikononi mwa Polisi lakini bado hatujajenga mfumo mzuri wa kushughulikia uhalifu. Kwenye suala hili tunalolizungumzia naamini CAG anapaswa kuwa na maafisa wa usimamizi wa sheria ambao wakati CAG anafanya uchunguzi na kukuta kuwa jambo fulani lina ushahidi wa kutosha wa uhalifu basi anaweza kumkamata mhusika na idara mojawapo ya CAG ikaandaa kesi na kuipeleka kwa Prosecutor ili waiendeshe.

Kwa kufanya hivyo, tutaondoa duplicity of roles isiyo ya lazima. Kama CAG kaingia Wizara ya Maji na katika uchunguzi wake kaona shilingi bilioni 2 hazina maelezo, kauliza nyaraka hakuna, kauliza vilivyonunuliwa hakuna; anaambiwa nileteeni ushahidi jamaa wanasua sua halafu yeye anaandika kwenye ripoti "nyaraka tuliagiza lakini hatukupewa" na ripoti inapokelewa ikionesha "ufisadi" wa bilioni 2. Hii ni kejeli.

Ingepaswa kuwa baada ya kuulizia taarifa muhimu toka Wizarani na hazipati maafisa wa CAG wawe na "trigger clause" katika sheria yao ambapo mhusika asipoleta taarifa za suala linalozidi shilingi milioni 1 basi wana nguvu ya kuitisha akaunti zake na za ndugu zake wa karibu, mali zake, na zaidi ya yote kumuweka kizuizini wakifanya uchunguzi. Na wakiona kuwa upo ushahidi wa suala la kihalifu basi ushahidi wote haupelekwi tena TAKUKURU bali kwa mwendesha mashtaka (wa wilaya, mkoa n.k, hata Tarafa kama tunaweza kuwa nao)

Jukumu la huyo mwendesha mashtaka utaona siyo tena kuanzisha uchunguzi wa jambo lile bali kuandaa kesi dhidi ya wahusika na maafisa wa CAG wanakuwa ni mashahidi wa upande wa mashtaka.

Mifano mizuri hii ya kujifunza!

Kitu kimoja napenda kuweka sawa, DPP hana mamlaka ya kuchunguza. Hafanyi uchunguzi, yeye anatakiwa kuangalia uchunguzi na ushahidi na kuamua kama kuna kesi na kuendesha mashitaka. DPP Hachunguzi kabisa na Katiba haimtaki kuchunguza..........
 
Nchi nyingine uchunguzi ukifanyika inakuwaje?

Nchi nyingine wewe Zitto ungeweza kutakiwa ujiuzulu kuruhusu uchunguzi huru.

Na usingejiuzulu ungeweza kushindwa uchaguzi maana tayari una doa la kushukiwa ubadhilifu.

Zitto, wewe sio mbunge kama Chenge, wewe ni Zitto Kabwe, kamati yako inatakiwa iwe above suspicion kama mke wa Kaisari. Huwezi kuchunguzwa kwa rushwa bwana Zitto bwana. Ungekuwa nchi za watu waliopevuka ki uelewa, unaenda katikati ya nchi kutangaza chama na kukosoa ufisadi wa CCM watu wangekuuliza, wewe mwenyewe ulifanya nini hicho kilichofanya TAKUKURU wakushuku?

Nakwambia shukuru uko Bongo. Ila watu wa new school of leadership kama nyinyi ndio tulitegemea muanzishe hizo standard za hali ya juu kama nchi nyingine, kwamba kile kitendo cha kudhaniwa Zitto yuko katikati ya ubadhilifu ni kashfa, ni aibu. Utamkosoa vipi Mkapa na Yona na Chenge na Mramba wakati na wewe uko under a cloud of entanglement in corrupt activities?
 
Posho zimewatajirisha saana Waheshimiwa wetu hawa. Wanalipwa kila wanakoenda hasa ile Kamati ya mashirika ya UMMA kiasi kwamba hawaoni kabisa jinsi mashirika haya yanavyotafunwa. Ile taarifa ya Mh Ndasa kuhusu TANESCO imeishia wapi?

Kama kweli hawa wabunge wetu wanalipwa posho mara mbili mbili kwa ujanja ujanja hiyo sio RUSHWA bali ni WIZI kwahiyo sio kazi ya TAKUKURU kupeleleza bali hayo ni makosa ya jinai na wenye kazi hiyo ni wakina Manumba huko polisi!! If it is true that PCCB is investigating the parliamentary committees then they cannot be doing so independent of directives from IKULU; this being another strategy of getting even with speaker Sitta and his colleagues!!
 
Nchi nyingine wewe Zitto ungeweza kutakiwa ujiuzulu kuruhusu uchunguzi huru.

Na usingejiuzulu ungeweza kushindwa uchaguzi maana tayari una doa la kushukiwa ubadhilifu.

Zitto, wewe sio mbunge kama Chenge, wewe ni Zitto Kabwe, kamati yako inatakiwa iwe above suspicion kama mke wa Kaisari. Huwezi kuchunguzwa kwa rushwa bwana Zitto bwana. Ungekuwa nchi za watu waliopevuka ki uelewa, unaenda katikati ya nchi kutangaza chama na kukosoa ufisadi wa CCM watu wangekuuliza, wewe mwenyewe ulifanya nini hicho kilichofanya TAKUKURU wakushuku?

Nakwambia shukuru uko Bongo. Ila watu wa new school of leadership kama nyinyi ndio tulitegemea muanzishe hizo standard za hali ya juu kama nchi nyingine, kwamba kile kitendo cha kudhaniwa Zitto yuko katikati ya ubadhilifu ni kashfa, ni aibu. Utamkosoa vipi Mkapa na Yona na Chenge na Mramba wakati na wewe uko under a cloud of entanglement in corrupt activities?

Nimekwambia ni Kamati zote zinachunguzwa ikiwemo ya Cheyo, Zitto, Slaa, Shellukindo, Anna Kilango, Missanga etc.

Wote tujiuzulu vinginevyo tutashindwa uchaguzi.............! Kamati yangu haifanyi kazi na TAKUKURU sasa mimi nitazuia vipi wao kufanya kazi na uchunguzi kwa uhuru?
 
Kama kweli hawa wabunge wetu wanalipwa posho mara mbili mbili kwa ujanja ujanja hiyo sio RUSHWA bali ni WIZI kwahiyo sio kazi ya TAKUKURU kupeleleza bali hayo ni makosa ya jinai na wenye kazi hiyo ni wakina Manumba huko polisi!! If it is true that PCCB is investigating the parliamentary committees then they cannot be doing so independent of directives from IKULU; this being another strategy of getting even with speaker Sitta and his colleagues!!

100% IKULU................ Spika ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi. Inachunguzwa pia
 
- Sometimes wa-Tanzania tunakuwa kama tumepagawa, Hosea badala ya kujiuzulu kwa kuhsindwa kazi ndio kwanza anaanza kuchunguza wengine, Ooh my! my! kamati ya bunge ya Mwakyembe imemchunguza Hosea na kutaka awajibishwe, nothing happened leo amerudi kuchunguza wengine,

- Uchunguzi wake wa kwanza ulikuwa aibu tupu mpaka akatakiwa kuwajibishwa, sasa kama kawaida kuna wanaotaka tuamini kwamba this time anachunguza for real na it is okay, na Zitto unaiita hii Ze comedy of the Century kuwa ni cheks and balance!

Wewe Mungu wa mbinguni wa-Tanzania tumekukosea nini hasa mweee tukupela kisa jamani mweee! Aaggghhhrrrrrr!

Respect.

FMEs!
 
Nimekwambia ni Kamati zote zinachunguzwa ikiwemo ya Cheyo, Zitto, Slaa, Shellukindo, Anna Kilango, Missanga etc.

Wewe ni Zitto Kabwe, sio Shellukindo, sio Anna Kilango, sio Missanga. Hao ni maadui zako kisiasa.

Tungetegemea wewe uwe tofauti. Usinambie eti hata Anna Kilango anachunguzwa. Hao wote ni ruling elite!

Mtoto akikamatwa kwenye ubadhilifu wa kuiba maandazi ya mama ndio anasema hata Pili nae kala andazi. Huo sio utetezi wa mtu mzima! Ni aibu kwa Zitto Kabwe kuchunguzwa na TAKUKURU kwa ubadhilifu!
 
TAKUKURU ni zaidi ya Hosea. Hii ni Taasisi.

Sawa, kwa hiyo uozo ndani ya taasisi hauhusiani na mapungufu ya kiongozi wake na ufanisi ndani ya taasisi hauhusiani na utendaji mzuri wa boss wake ! Mbona hiki ni kichekesho - kwa nini basi tunawalaumu viongozi wetu na kwa nini taasisi inapoboronga tunataka kiongozi wake awajibike. Mh. Zitto wengine hatutaki kabisa kusikia matamko kama yale ya Ikulu ya kudai Raisi asihusishwe na tuhuma za ufisadi ndani ya seriakli anayoiongoza.

Haiwezi kuacha kufanya majukumu yake kwa mujibu wa sheria kwa sababu eti Bosi wao hatuna imani naye.

Mbona hili linapingana na tabia ya ustaarabu kama ilivyo popote pale ulimwenguni. Kama hatuna imani na bosi wa taasisi yoyote dawa yake ni moja tu, hafai na tutadai kwa nguvu zote ajiuzulu au awajibishwe.

Lakini ni huyu huyu Hosea tuliyemfurahia kwa kuwafikisha kina Mramba mahakamani.

Ule usanii wa kuwafikisha mahakamani Mramba na wenzake wengine tuliukataa tokea mwanzo na siku zinavyosonga mbele, ukweli wenyewe unazidi kudhihirika.

Tuchunguzwe tu na tukikutwa tumechezea fedha za Umma hatutakuwa na 'credibility' ya kuendelea kushika nyadhifa za Umma. (kesi ya Uingireza na Wabunge wao kutumia vibaya fedha ndio yaweza kutokea hapa nyumbani kufuatia uchunguzi wa TAKUKURU)

Huyo kamanda anayeongoza jeshi hilo ndio tuna wasi wasi naye kutokana na rekodi yake ya nyuma baada ya kuisafisha Richmond na mambo mengine kemkem. Sisemi kamati hizi za bunge zisichunguzwe lakini Hosea kwanza awekwe kando. Madaraka aliyo nayo Hosea ndani ya TAKUKURU ni makubwa na mpaka sasa utendaji wake umekuwa hauridhishi.
 
Uchunguzi siku zote lengo lake ni kutafuta kama kuna mabaya. Hakuna uchunguzi wa kutoa zawadi za mazuri.

TAKUKURU wameshuku kwamba tume hizi, ikiwemo ya Zitto, kuna ubadhilifu, ndio maana wanachunguza. Hawaendi pale kutoa zawadi za birthday kwa kina Zitto, bali kuchunguza suspicion za ubadhilifu wa kina Zitto.

Hizo kamati nyingine sio jambo la ajabu, CCM ni wabadhilifu. Zitto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu, Mbunge wa upinzani, anaejiweka kama adui wa ufujaji na rushwa na ufisadi. Kamati yake inachunguzwa kwa kulipana kibadhilifu. Kashfa! Na unajua ni kashfa, Mwanakijiji; Unatetea kwa vile wewe huwa ni shabiki, unaendeleza "a mission." Ukishaniambia uko "on a mission" huwezi kuja kujaribu kunipotosha kwamba una chembe ya objectivity.

Listen man grow a pair and admit your hatred towards Zitto without beating around the bush! Hauwezi kusema lengo la uchunguzi siku zote ni kutafuta KAMA kuna mabaya and then proceed to indict the man on suspicion za ubadhirifu
 
Nafikiri Hosea is mentally sick!!maana yeye anatakiwa ajiuzuru tu,there is nothing he can do or say inayoweza kumwonyesha kuwa ni mtu makini na safi, kwa hivi kuendelea kupoteza resources za walipa kodi ati anachunguza kamati za bunge kwa nia ya kulipiza visasi inamuweka pabaya ajue pana siku na mwaka hata kama atakuwa wapi tutamtafuta alipie huu ubadhirifu wa kupoteza hela za umma kwa his only personnal gains,Lakini kinachotia kinyaa zaidi ni huyo Bosi wake sijui anafikiri bunge linafanya onesho la mipasho!!! I fell to understand and I refuse to comprehend this !! Huyu ni rais wa nchi ama nini au ana urafki gani na Hosea!! God save Tanzania this shame, this man was not supposed to be the head of state!! Never
 
TAKUKURU wana wajibu wa kisheria kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za kwamba Wabunge tumekuwa tukilipwa zaidi ya tunachotakiwa kulipwa kisheria. Wabunge hatuna kinga ya kufanya vitendo vya matumizi mabaya ya fedha za umma na hatua hii ya TAKUKURU itaondoa 'impunity'. Kwamba wanafanya hivi kwa visasi sio kweli. Ni wajibu wao. Uchunguzi huu unafanyika kwa Kamati zote za Bunge na sio hizi tatu peke yake. Hivi kama Mbunge analpwa pesa ili asafiri kwa siku 5, na yeye anasafiri kwa siku moja. CAG anagundua hilo katika ripoti yake, kwa nini TAKUKURU wasichunguze na kufungua mashitaka?

Tuwaache TAKUKURU wafanye kazi yao kwa mujibu wa sheria. Bunge pia tufanye kazi yetu ya kuwasimamia hao TAKUKURU ili watende mema. Hiyo ndio checks and balances.

MH Zitto ni kweli,
Hata hivyo Takukuru ni mabingwa wa kuchagua kwenye monofu na ulaini.
Wanajua wazi si rahisi kumwajibisha Mbunge hata kama watapata ushahidi wa kutosha. Wafanye hiyo kazi kimya kimya si kwa mbwembwe utadhani huko ndo tunapoteza mabilioni.
Yale mafupa heavy ya Dinosaurus ( Wizi mkubwa wa Kimafia serikalini)wanayapita kaa vile si kazi yao.
Ni kazi yao lakini imewashinda kwa kila hali.
 
Sawa, kwa hiyo uozo ndani ya taasisi hauhusiani na mapungufu ya kiongozi wake na ufanisi ndani ya taasisi hauhusiani na utendaji mzuri wa boss wake ! Mbona hiki ni kichekesho - kwa nini basi tunawalaumu viongozi wetu na kwa nini taasisi inapoboronga tunataka kiongozi wake awajibike. Mh. Zitto wengine hatutaki kabisa kusikia matamko kama yale ya Ikulu ya kudai Raisi asihusishwe na tuhuma za ufisadi ndani ya seriakli anayoiongoza.

Mbona hili linapingana na tabia ya ustaarabu kama ilivyo popote pale ulimwenguni. Kama hatuna imani na bosi wa taasisi yoyote dawa yake ni moja tu, hafai na tutadai kwa nguvu zote ajiuzulu au awajibishwe.

Ule usanii wa kuwafikisha mahakamani Mramba na wenzake wengine tuliukataa tokea mwanzo na siku zinavyosonga mbele, ukweli wenyewe unazidi kudhihirika.

Huyo kamanda anayeongoza jeshi hilo ndio tuna wasi wasi naye kutokana na rekodi yake ya nyuma baada ya kuisafisha Richmond na mambo mengine kemkem. Sisemi kamati hizi za bunge zisichunguzwe lakini Hosea kwanza awekwe kando. Madaraka aliyo nayo Hosea ndani ya TAKUKURU ni makubwa na mpaka sasa utendaji wake umekuwa hauridhishi.

Mag3,
asante sana mkuu umeniwekea maneno yaliyokuwa kwenye ubongo wangu. Niazime maneno ya zito mwenyewe "majibu yake ni ya ovyo ovyo." Najua kama atarud kukujibu basi majibu yake yatakuwa ya ovyo ovyo ovyo ovyo (ovyo ovyo)2 . Eti kama yeye alifurahii usanii wa kina Mramba anataka kutusemea wote kuwa tulishangilia. Besides Zito na Hosea ni ndege wa rangi moja na wanaungnishw na Richmond/Dowans.
 
Humu nako kuna watu kazi ni kuwashambulia watu wengine, mtu mmoja (Dilunga) kamshupalia Zitto. Kwani kuchunguzwa ajabu ni nini au ulitaka Zitto asichunguzwe ,we mtu gani husiyeweza kufikilia uchunguzi anaofanya Hosea ni wa kufa na mtu hata kama yeye hataachia kiti lakini huwenda akamtetea mtu mmoja

Tunachotaka sisi ni evidence za rushwa na sio kushambuliana kama wewe Dilunga. Usishangae na wewe siku ukaambiwa unachunguzwa sasa maana yake ndo tayari mchafu!!

Hosea sasa ukipona fanya kazi acha kuwabeba watu si unaona mzigo wote kwako
 
Zitto,

Nashindwa kuelewa ni sababu gani zinazokufanya uiamini hii TAKUKURU iliyo chini ya Hosea kwamba itakuwa impartial ! Mimi siku zote naamini ya kuwa Politics is all about timing ;jambo hili ni la kisiasa especially ukizingatia kuwa mwakani tuna uchaguzi. Ni lazima pia mtambue ya kuwa kama kuna kitu Kikwete's adminstration worries the most is mafisadi's issue. Wanachotaka kufanya ni kuchunguza hizo kamati na kuwalabel wote kuwa ni ......

Na bahati mbaya sana wanacontrol media, kwa hiyo wananchi watawaaamini ! Mimi nadhani mnachotakiwa ni kulizungumzia hili otherwise CCM watawafanya mchezo mbaya .Usijidanganye kamati zinazochunguzwa hapo ni mbili , nyingine hapo wamarekani wanaoupenda mchezo wa football wanaziita Decoys
 
Back
Top Bottom