Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Naandika nikijua wasio na ABC ya sheria wanitupia mishale lakini sijali. Lakini Kwa mara ya Kwanza tunashuhudia Migogoro ya usajili ya mwaka 1994 ikirejea 2024 Kwa timu ya Simba kuwa na mwanasheria anayetafuta Kwanza maslahi binafsi kabla ya maslahi ya timu. Migogoro ya Mohamed Mwameja na Kenneth Mkapa kusaini huku na huku imepata copy 2024 kwenye mkataba wa Kagoma. Lakini pia Mikataba ya Valentino Mashaka na Awesu Awesu ni Sawa na kumtuma Mtoto akaibe kwao Bahati mbaya alikamatwa unajifanya hujui, muulizeni mwenyewe.
Migogoro ya Aina hii ilizoeleka Yanga Hadi likawa tusi kwao na kutakiwa kwenda kujifunza Simba. Lakini safari hii mwalimu ndo kafanya wonders Kwa 4in1.
Kisheria haya ni madhaifu Makubwa ya mwanasheria. Ni wakati wa viongozi wa Simba kuangalia Mtu mwingine makini wa kufanya kazi hiyo adhimu badala ya huyu anayewapaka mafuta Kwa mgongo wa chupa huku akijua timu inaumia. Nachelea kusema kuna percent anapokea si bure.