Kumekuwa na malalamiko ya wagonjwa hasa wanaokwenda kutibiwa KAIRUKI hasa katika kitengo cha meno, kuhusu DR anayehusika na kutibu meno kuwa anakauli chafu, vitisho na kejeli.
hapo kwenye red...hayo malalamiko waliyatolea wapi???kumekuwa na malalamiko ya wagonjwa hasa wanaokwenda kutibiwa kairuki hasa katika kitengo cha meno, kuhusu dr anayehusika na kutibu meno kuwa anakauli chafu, vitisho na kejeli.anapotibu mgonjwa hutoa kauli za vitisho ambapo inampelekea mgonjwa kuogopa habari zilizotufikia hapa zinasema dr huyu kwa siku hutibu wagonjwa 10 tu tena kwa mda maalum, ambapo hii inapelekea kulazimisha mgonjwa atibiwe kwa presha.
Katika dept ya dawa! Hawa watu wamekuwa wakibana dawa hasa kwa wale wanao2mia bima, zikiandikwa dawa 3 tofauti wao wanakupa dawa mbili.
Mjirekebishe!
Kumekuwa na malalamiko ya wagonjwa hasa wanaokwenda kutibiwa KAIRUKI hasa katika kitengo cha meno, kuhusu DR anayehusika na kutibu meno kuwa anakauli chafu, vitisho na kejeli.Anapotibu mgonjwa hutoa kauli za vitisho ambapo inampelekea mgonjwa kuogopa habari zilizotufikia hapa zinasema Dr huyu kwa siku hutibu wagonjwa 10 tu tena kwa mda maalum, ambapo hii inapelekea kulazimisha mgonjwa atibiwe kwa presha.
Katika dept ya dawa! Hawa watu wamekuwa wakibana dawa hasa kwa wale wanao2mia bima, zikiandikwa dawa 3 tofauti wao wanakupa dawa mbili.
MJIREKEBISHE!
Tatizo kuna baadhi ya madaktari pale Kairuki sio rafiki wa wagonjwa, binanfi nilikwenda kutibiwa pale jioni kwenye saa 10.30 nikaingia chumba namba 21 kuna daktari wa kiume muhaya jina limenitoka kidogo alikuwa very rude yaani utafikiri alilazimishwa kufanya kazi, nilishindwa kumvumilia nikamweleza live kuwa kama daktari hutakiwi kuwa rude kwa wagonjwa na kama unaona umelazimishwa kufanya kazi ama unamatatizo yakifamilia basi usinge hudumia wagonjwa, nikatoka nikachukua file langu nkaenda reception nikawaambia siwezi hudumiwa na huyo daktari kama hakuna dokta mwingine wanirudishie pesa yangu niondoke, dada wa pale mapokezi akaomba msamaha kwa niaba ya hospitali ila akasema huyo daktari ndivyo alivyo watu wengi huwa wanamlalamika but uongozi hautaki kumwondoa kisa ni muhaya mwenzao.
nilipatiwa dakrati mwingine na nimeapa kutorudi tena pale
Sawa, hospitali ya wahaya ni lazima wahaya wengi wawepo kama wanazo sifa. Hata hospitali ya kihindi wahindi ni wengi pale, hospitali ya mchaga wachaga ni wengi pale lakini wanazo sifa? Hilo ndilo swali muhimu. Ulichokifanya was not very right - comfrontation. Uliamua kugombana naye, daktari wa meno anashauriwa sana awe anaongea na mgonjwa wake wakati wote anapofanya kazi ili kupunguza mazingira yenye hofu kwa mgonjwa na kuongeza thamani ya mashirikiano. Kuna wagonjwa hawataki hayo, wanataka akifika kwenye kiti daktari afanye kazi yake no discussion. Tena bahati mbaya wengine ni watumishi wa afya, wanawadharau madentist ati "Wang'oa meno" Ukiingia kwa dharau lazima naye atagangamala kulinda hadhi yake. Yaani usitaniwe hata kidogo? Mbona wengine wnamsifu huyo unayemkandia wewe? Kama binadamu alivyo dhaifu kwa namna fulani, huyo daktari anaweza kuwa na mapungufu yake, lakini mfano wako umedhihirisha alichosema Zaleo kwamba wapo wagonjwa wa aina yako. Acheni kudharau watu na kazi zao. Kumkimbia hujasuluhisha, ungepeleka malalamiko rasmi kama unadhani ulikuwa sahihi ili kuondoa uozo pale kulikoni kueneza matatizo binafsi kwa kuyajengea hoja ya ujumla ili watu wote wamchukie. Mie simjui na wala sijawahienda pale, lakini niliwahifika Muhimbili napo nikaona daktari mmoja mgonjwa wa meno anamkomalia daktari wa meno, kosa: ati dentist anamfundisha namna meno yanyooza na namna ya kuzuia. Live nilimsikia dada yule daktari akimaka "Nimetibiwa na dentists wengi lakini sijakutana na dentist kama wewe, mimi nimekuja kutibiwa wewe unanilecture?" Je, katika hali kama hiyo ni dentist gani atakuwa radhi kuvumilia?
Kulaumu ni kuzuri ikiwa kualumu huko kunaleta tija. Bahati mbaya madentist wetu wanashughulika na wagonwa wa meno wenye afya na nguvu ya kugombana. Kama angekuwa gynecologist mbona hatusikii? Dentist hafanyi kazi peke yake chumbani ninawaona, mnaleta kadamnasi mauozo yenu sababu mnajua hamko sahihi na mlichokifanya kwani wasaidizi wa madentist wanakuwapo kushuhudia, tena mara nying jinsia tofauti ndio wakorofi nyie.
Mmh; hapana huyu daktari ninamfaham tena is my familly dentist. Ni dactari mzuri sana kati ya madentist ninaowafahamu.ila ni mtu serious sana na kazi yake .kama ulienda kwake ukitegemea kumuuzia sura kwa yule utachemsha.Anaitwa Dr Lemi! Idara ya Meno! Pande la mtu hivi.