Sawa, hospitali ya wahaya ni lazima wahaya wengi wawepo kama wanazo sifa. Hata hospitali ya kihindi wahindi ni wengi pale, hospitali ya mchaga wachaga ni wengi pale lakini wanazo sifa? Hilo ndilo swali muhimu. Ulichokifanya was not very right - comfrontation. Uliamua kugombana naye, daktari wa meno anashauriwa sana awe anaongea na mgonjwa wake wakati wote anapofanya kazi ili kupunguza mazingira yenye hofu kwa mgonjwa na kuongeza thamani ya mashirikiano. Kuna wagonjwa hawataki hayo, wanataka akifika kwenye kiti daktari afanye kazi yake no discussion. Tena bahati mbaya wengine ni watumishi wa afya, wanawadharau madentist ati "Wang'oa meno" Ukiingia kwa dharau lazima naye atagangamala kulinda hadhi yake. Yaani usitaniwe hata kidogo? Mbona wengine wnamsifu huyo unayemkandia wewe? Kama binadamu alivyo dhaifu kwa namna fulani, huyo daktari anaweza kuwa na mapungufu yake, lakini mfano wako umedhihirisha alichosema Zaleo kwamba wapo wagonjwa wa aina yako. Acheni kudharau watu na kazi zao. Kumkimbia hujasuluhisha, ungepeleka malalamiko rasmi kama unadhani ulikuwa sahihi ili kuondoa uozo pale kulikoni kueneza matatizo binafsi kwa kuyajengea hoja ya ujumla ili watu wote wamchukie. Mie simjui na wala sijawahienda pale, lakini niliwahifika Muhimbili napo nikaona daktari mmoja mgonjwa wa meno anamkomalia daktari wa meno, kosa: ati dentist anamfundisha namna meno yanyooza na namna ya kuzuia. Live nilimsikia dada yule daktari akimaka "Nimetibiwa na dentists wengi lakini sijakutana na dentist kama wewe, mimi nimekuja kutibiwa wewe unanilecture?" Je, katika hali kama hiyo ni dentist gani atakuwa radhi kuvumilia?
Kulaumu ni kuzuri ikiwa kualumu huko kunaleta tija. Bahati mbaya madentist wetu wanashughulika na wagonwa wa meno wenye afya na nguvu ya kugombana. Kama angekuwa gynecologist mbona hatusikii? Dentist hafanyi kazi peke yake chumbani ninawaona, mnaleta kadamnasi mauozo yenu sababu mnajua hamko sahihi na mlichokifanya kwani wasaidizi wa madentist wanakuwapo kushuhudia, tena mara nying jinsia tofauti ndio wakorofi nyie.