Hospitali binafsi zinapotanguliza maslahi badala ya Afya za Watanzania

Naona hawaelewi maana ya private sector. Walikimbilia nini kutoa maagizo kabla hawaja kubaliana na wahusika? Kwa nini wasisitishe tu utekelezaji wa maagizo yao badala ya kulazimisha watumie vitita vya bei ya chini ambavyo wanajua watakataliwa kupandisha kwa arguments mbona mliweza kujiendesha poa tu?
Wakubali tu kujishusha ili kunusuru maisha ya wananchi.

Amandla...
 
halafu watoboaji ni akina nani?

Ukute watoboaji ni serikali yenyewe halafu inataka hospital binafsi iendane na matakwa yao?

Tuache kutesana kila mmoja apate faida

Pamoja na hayo ungali unadhani suluhu Iko humu kwenye kukusanya fedha nyingi?

"Serikali iache kujipendelea bali iwahamasishe wananchi kujiunga na Mifuko ya Bima, wanachama wakiwa wengi na fedha itapatikana nyingi."
 
Pamoja na hayo ungali unadhani suluhu Iko humu kwenye kukusanya fedha nyingi?

"Serikali iache kujipendelea bali iwahamasishe wananchi kujiunga na Mifuko ya Bima, wanachama wakiwa wengi na fedha itapatikana nyingi."
Nahisi ni suluhu moja wapo 'bima kwa wote'
 
Mkuu umejenga hoja nje ya uhalisia.

Serikali iangalie gharama halisi za tiba. Mf kusafisha kidonda Tzs 2,000 je kuna uzingativu wa details za kidonda?

Ninekupa mfano tu
 
Zitajiendeshaje sasa zikijali afya Kodi,maji,mishahara atalipa nani
 
Bora ya hizo za binafsi, za serikali hivi sasa gharama zake ni kubwa kuliko hizo za binafsi japo gharama zake za uendeshaji uko chini. Gharama za uendeshaji hosipitali binafsi ziko juu sana hasa mishahara, umeme, maji na kodi majengo hivyo wanalazimika kutoza viwango vya juu kiasi japo si sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…