Hospitali ya Ajabu

Kyandaya

Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
53
Reaction score
9
Kwa kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.Safari za mwisho wa mwaka,zimenifanya niigundue hospitali hii:Ambapo mambo yake ni kinyume kabisa na taratibu za Wizara ya Afya.Wahudumu huingia zamu za usiku{night shift}mara mbili kwa wiki bila malipo.Kila wiki lazima awe night.Isipokuwa wateule wachache hawajui maana ya night.Wao hujilipa posho wapendavyo.HIYO NI MAWENZI.HOSP.YA MKOA WA KILIMANJARO.Wana JF nisaidieni vilevile ukifanya extra duty ya 80000 utalipwa 25000 tena utalipwa baada ya miezi 6.Nasikia MHASIBU Atakuambia fungu halijatoka hii ni km utafuatilia.Na ukilipwa basi ni nusu ya kiwango unachodai.
 
pole sana mkuu hope nawe ni muhanga...bila kuingo'a ccm hakuna kitakachobadilika
 
Hapo ndiyo Nchi ilipofika kwa sasa. Tunahitaji kupigania uhuru kwa mara ya pili dhidi ya watawala wa sasa.
 
mimi sioni cha ajabu apa, yote nisha yazoea haya
 
Hi ndo Tz.Usishang'ae kuna madudu mengne zaidi ya hayo,kila sehemu maujanja ujanja tu.The tm is comin.
 
Mawenzi hosp, si leo tangu zamani ukipeleka mgonjwa wako hapo unaambiwa hapo umepeleka mochuary direct yaan inasifika kwa huduma mbovu na mazingira mabovu,kule inasifika kama hosp inayoua badala ya kuponya.malalamiko yanafika kwa wahusika lakini wapi hakuna linalofuatiliwa,.nakumbuka brother wangu alifariki 1999 kutokana na uzembe wa huduma mbovu hapo,alipata ajali kupelekwa hakuna wa kumhudumia eti mhudumu wa night kachelewa. acha tu mkuu usinikumbushe hapo Mawenzi.
 
Hawa watendei haki watumishi wake, na inaonekana mfumo wa uongozi wa hapo hospital sio mzuri
 
Hii ipo sehemu nyingi tu, wahasibu wamekuwa miungu watu. Mfano kama huu upo hospital ya mkoa Morogoro nimefanya intern pale mwaka mmoja. Angalau Madaktari kidogo ingawa nao extra duty zao zinakatwa au kuchelewa kutoka. Ila manesi ndo wanaonekana kama si wafanyakazi kama vijakazi fulan hivi. Wale wanaonekana kuchonga wanapozwa kwa seminars. Hii ndo Tanzania bwana, ila watanzania wengi ni woga hata kudai haki zao. Any way Mungu bariki ukombozi tuupate.
 
wakati mwingine huwa sielewa kazi za Mbunge ni zipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…