Kwa kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.Safari za mwisho wa mwaka,zimenifanya niigundue hospitali hii:Ambapo mambo yake ni kinyume kabisa na taratibu za Wizara ya Afya.Wahudumu huingia zamu za usiku{night shift}mara mbili kwa wiki bila malipo.Kila wiki lazima awe night.Isipokuwa wateule wachache hawajui maana ya night.Wao hujilipa posho wapendavyo.HIYO NI MAWENZI.HOSP.YA MKOA WA KILIMANJARO.Wana JF nisaidieni vilevile ukifanya extra duty ya 80000 utalipwa 25000 tena utalipwa baada ya miezi 6.Nasikia MHASIBU Atakuambia fungu halijatoka hii ni km utafuatilia.Na ukilipwa basi ni nusu ya kiwango unachodai.