#COVID19 Hospitali ya Bugando yakumbwa na upungufu wa mitungi ya Oksijeni kwa Wagonjwa wa Kupumua

#COVID19 Hospitali ya Bugando yakumbwa na upungufu wa mitungi ya Oksijeni kwa Wagonjwa wa Kupumua

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau.

Hali naona imeanza kuwa mbaya kwa upande wetu Tanzania ,nasikia huko Bugando washaanza kukumbwa na upungufu wa mitungi ya oxygen.

Kipindi hiki lockdown haikwepweki bila shaka. Mpaka sasa Bugando Hospital wanaupungufu wa mitungi 500 ya oxygen.

Huku mtaani kwetu Buza sioni kabisa taadhali zikifuatwa ,Mungu atunusuru kwa kweli.

Chanzo: ITV Habari 06/07/2021.

Zaidi, soma: News Alert: - Mitungi ya Oxygen yawasili Bugando; tusichoke kupaza sauti kuishauri, kuipongeza na kuikosoa Serikali
 
Mitungi ndio ventilators?
 
... hata kama wanao mmoja issue ni kwamba mitungi imeisha. Akili kichwani; chukua tahadhari!
Huu ugonjwa ni vita ya kiuchumi Magu alikuwa amewashtukia. Lazima tujiulize kwa nini watu wamedunda tangu May 2020 hadi leo bila barakoa wala chanjo lakini sasa hivi tumeanza kutishana na kutiana hofu kuwa korona ipo tuvae barakoa tena kwa lazima?
 
Nilimsikia Rais akisema kuna pesa zaidi ya US dollar 400ml. kwaajili ya Corona, hizo pesa zielekezwe huko kununua mitungi ya oxygen kwa hospitali za serikali.

Lakini pia, tahadhari dhidi ya Corona ni vyema ziendelee kuchukuliwa kwa kila mmoja wetu kukumbushwa ana jukumu la kumlinda mwingine kwa kuanzia na kujilinda yeye binafsi.
 
Tanzania Oxygen Limited ndo wanatakiwa wapige kazi sasa
 
Mungu ni mwema atatusimamia
Baba yake rafiki yangu kafariki Musoma na Mama yake yupo kwenye oxygen. Rafiki yangu naye kafariki mwaka jana mwezi wa nne na kaka yake katoka hospitali lakini alikaa zaidi ya siku 40 Houston, TX kwenye ICU . Kaka yake bado anatumia oxygen baada ya kupata matatizo kwenye mapafu. Yote hii ni Corona. Mama wanasema atapona anaweza kutoka wiki hii lakini atakuta mzee wamesha zika wiki iliyopita
 
Huu ugonjwa ni vita ya kiuhumi Magu alikuwa amewashtukia. Lazima tujiulize kwa nini watu wamedunda tangu May 2020 hadi leo bila barakoa wala chanjo lakini sasa hivi tumeanza kutishana na kutiana hofu kuwa korona ipo tuvae barakoa tena kwa lazima?
... dunia nzima ni Tanzania tu ndio inapigana vita vya kiuchumi kupitia Corona? Watu wazito kwa wazito; maprofesa kwa maprofesa wameteketea duniani kwa Corona ili kuipiganisha Tanzania vita vya kiuchumi? Kwa lipi hasa? Kuwa serious ndugu!
 
Back
Top Bottom