Katika afya kuna huduma kama 3 hivi
1. Ni medical consultation (Ushauri wa kitabubu)...huyu anakusikiliza, anaweza kukuandikia vipimo vya kufanya na unaenda kufanya kwenye maabara yoyote iliyoidhinishwa na unarudisha vipimo. Anakupa ushauri na kukuandikia dawa ambazo unaenda kununua duka lolote la dawa ambalo limeidhinishwa. Utamlipa consultation fees mnamalizana.
2. Huduma ya maabara/vipimo. Huyu anapokea wagonjwa kutoka kwa consultants na kufanya vipimo then ana mrudishia majibu consultant. Unamlipa gharama za vipimo mnamalizana.
3. Huduma ya kuuza dawa a.k.a pharmacy. Huyu hupokea prescriptions (List ya dawa), iliyoandaliwa na consultant. Unamlipa gharama za dawa mnamalizana.
4. Kuna hospitali ambazo hutoa huduma zote hapo juu. Mara nyingi kwa sababu huduma zote hutolewa pamoja anaweza kuwa ameweka punguzo kwenye huduma fulani fulani na mwisho wa siku inakuwa rahisi kuliko kama ungeenda sehemu tatu tofauti, kama nilivyoeleza hapo juu. Pia kwa sababu huduma zote ziko sehemu moja ni inarahisisha huduma kwa mgonjwa na kupunguza usumbufu wa kwenda na kurudi.
Kuhusu bei ya dawa, inategemea na source (chanzo) cha dawa zake. Dawa aina moja zinaweza kuwa na bei tofauti kulingana na brand. Panadol ya Kenya na panadol ya Tanzania bei yake si sawa. Hivyo inategemea na brand anazotumia. Je ni kutoka Ulaya, marekani, India, china, Tanzania au Kenya.
Pia kwa nini hakuandikii dawa ukanunue sehemu nyingine. Ni kwasababu huduma yote anaitoa kama package moja. Ni sawa sawa na hotel ambayo wana uza chakula kwa style ya Bufee...huwezi kwenda kuchukua sehemu ya chakula halafu ukataka ulipe kidogo.
Lakini pia kama utawaeleza kuwa wewe unataka consultation peke yake watakupa gharama.za consultation peke yake ambazo mara nyingi zitakuwa juu kuliko gharama ya package nzima.
Lakini pia hawatoi orodha ya dawa kwa sababu mbali mbali kama kutunza siri za wagonjwa na kulinda afya ya mgonjwa. Hospital zina jukumu la kutunza siri za wagonjwa. Pia akikuandikia dawa ukaondoka nayo unaweza kutumia vibaya. Labda ukanunua dawa nusu dose usipone au ukanunua dawa zisizo na kiwango usipone, au ukapata tatizo lolote la kiafya wakaingia matatizoni.