Hospitali ya Mkoa Shinyanga yafafanua madai ya kutoza gharama kubwa kwa wanaohitaji Ambulance

Hospitali ya Mkoa Shinyanga yafafanua madai ya kutoza gharama kubwa kwa wanaohitaji Ambulance

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kulalamikia gharama wanazotozwa wahitaji wa huduma ya Ambulance katika Hospitali ya Mkoa Shinyanga, kumsoma Mdau bonyeza hapa ~ Gharama za “Ambulance” Shinyanga ni mateso kwetu walalahoi Uongozi wa Hospitali umetoa ufafanuzi.

TAARIFA INAYOSAMBAA MTANDAONI DHIDI YA HUDUMA YA GARI LA WAGONJWA (AMBULANCE) HOSPITALI YA RUFAA YA MКОА SHINYANGA

Kumekuwa na taarifa inayosambaa mtandaoni ya Juni 29, 2024 ikisomeka kwa kichwa cha habari "Gharama za Ambulance Hospitali ya Mkoa ni mateso kwa walala hoi".

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga inapenda kuujulisha umma kuwa taarifa hiyo haina ukweli kwa kile kilichochapishwa.

Katika muongozo wa huduma ya rufani kunatoka sehemu A kwenda B, unaelekeza mgonjwa kuchangia gharama za mafuta na siyo kulipia gharama za gari.

Pili, Hospitali huwezesha kutoa gari, dereva na mtaalamu ambaye hujumuika ili kutoa huduma kwa mgonjwa wakati wa safari husika, kwa maana pande zote mbili zinachangia (Cost Sharing).

Hivyo, si kweli kuwa pindi inapotokea kuna wagonjwa (zaidi ya mmoja) kila mmoja anachangishwa shilingi 250,000/= kama ilivyochapishwa na Mtandao wa Jamii Forum, na badala yake pande mbili huchangia kwa ajili ya gharama za mafuta (lita 65) za kwenda na kurudi ambapo hata gharama ya 250,000/= haijawahi kufika, na risiti hukabidhiwa kwa mteja.

Aidha, katika kujali hali ya mteja kulingana na hali yake kiuchumi, Hospitali huwezesha gharama zote kama mgonjwa hajiwezi, lakini pia kuna ambao huchangia kiasi kidogo kulingana na hali zao za kiuchumi.

Uongozi wa Hospitali unawahakikishia wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na watanzania kwa ujumla, utaendelea kusimamia huduma bora ambazo zinatolewa na kufuata miongozo yote iliyowekwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya.

Vilevile, uongozi wa Hospitali umesikitishwa na Habari hiyo kwani inaleta taswira hasi na nia ovu ambayo inachafua taswira ya Hospitali na Serikali kwa ujumla.

Tunatoa rai kwa vyombo vya habari kuhakikisha vinafika fuata miongozo na miiko inayo simamia taaluma husika kwa ajili ya kupata taarifa rasmi (balanced story) ili kufikisha taarifa sahihi kwa umma.

George M. Mganga AFISA HABARI
Snapinsta.app_449428741_988940572551388_3481774182931226252_n_1024 (1).jpg
Screenshot 2024-07-01 085958.jpg
 
Kukanusha ni lazima lkn kilichosema ni ukweli kabisa na hii ni kwa hospital zote za serikali hasa zle za mikoani. Hata ukiitoa hiyo hela bado hawatakosa visingizio. Kwa mfano miezi miwili iliyopita nilikuwa namuuguza ndugu yangu ambaye kwa bahati mbaya tarehe 12 mwezi Mei alitutoka.
Issue ilikuwa hivi ndugu yangu alijisikia mguu wa kushoto kupoteza nguvu. Akapelekwa hosptali ya Manispaa ya Musoma zamani hosptali ya mkoa. Akiwa pale ikatakiwa kupewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa Kwangwa. Kuhusu Ambulence issue ilikuwa ni hivo tulitakiwa kujaza ambulance mafuta kutoka Mjini kwenda Kwangwa ambapo siyo mbali sana na tulitakiwa kutoa shilingi elfu 75. Ambayo baada ya kutoa tukaambiwa tusubiri amepatikana mgonjwa mwingine. Mpaka ambulance inaondoka pale ilikuwa na wagonjwa watatu na wote walilipishwa shilingi elfu 75 hiyo ni sawa na shilingi 234K kutoka mtaa mmoja kwenda mwingine.
Baada ya kufika Kwangwa mgonjwa akalazwa kwa siku mbili na kutakiwa kwenda Bugando ambapo hapa pia tuliambiwa tujaze lita 90 kwenye gari ambayo thamani yake ilikuwa ni shilingi 350,000. Ilipofika wakati wa kulipia tukaambiwa tusubirie kwanza mpaka apatikane mgonjwa mwingine. Baada ya kuhoji sana tukaambiwa tusubirie mpaka mgonjwa ajisaidie. Na kwa kuwa mimi nilikuwa nina facilitate nikiwa mbali nikahoji vipi ikiwa tatizo la kupata choo ndo ugonjwa unaomsumbua? Hakukuwa na majaibu.

Hatua iliyofuata nikaomba tupewe barua ya rufaa ili tutumie usafiri binafsi huwezi amini ilituchukuwa siku mbili kusainiwa rufaa na hii ni baada ya kumuonga nesi mmoja shilingi elfu 20.

Kufika Bugando nako mambo ni yale yale. Kwa kweli hospitali za serikali huko mikoani ni makaburi ya walalahoi. Kama hauna Daktari unayemfaham mgonjwa atakata kamba ikiwa unaangalia kwa macho. Rushwa Rushwa Rushwa.
 
Back
Top Bottom