Hospitali ya Muhimbili waunda mtandao wa kutibu saratani kwa watoto

Hospitali ya Muhimbili waunda mtandao wa kutibu saratani kwa watoto

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
"Hospital ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Shirika la Tumaini la Maisha inaratibu upatikanaji wa dawa na kuzifikisha kwenye hospitali zinazounda mtandao wa kutibu saratani kwa watoto," hayo yamesemwa na Dkt. Rehema Laiti, Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kwa Watoto
Muhimbili.

Anaendelea: "Idadi ya vifo vya watoto vitokanavyo na saratani vimepungua kwa kiasi kikubwa, ambapo kwa miaka kumi mfululizo wastani wa kuishi kwa Watoto wenye saratani kumeongezeka kutoka 35% mpaka 65%.

"Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Shirika la Tumaini la Maisha imefanikiwa kuunda Mtandao wa kutibu saratani kwa Watoto (Paediatric Oncology Network) katika Hospitali za KCMC, Bugando, Benjamin Mkapa, Hospital ya Kanda Mbeya, Sengerema pamoja na Mnazi Mmoja Zanzibar.

Capture.JPG
 
Back
Top Bottom