Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Hospitali ya Taifa Muhimbili imeongoza kitaifa kwa 57% katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kwenye utoaji taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa kati ya taarifa zote zilizopokelewa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kwa miaka ya fedha ya 2020/21, 2021/22 na 2022/23.
Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo amesema hayo wakati wa utiaji saini hati ya makubaliano kati ya MNH na TMDA ya kuimarisha ufuatiliaji wa maudhi, madhara au matukio yatokanayo na matumizi ya bidhaa zinazodhibitiwa na mamlaka hiyo.
Amesema, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imeweza kutumia fursa hiyo na kuwa taasisi inayoongoza kitaifa katika kuwasilisha taarifa za maudhi, madhara au matukio hayo.
Hali hii imeimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizi mbili zenye nia moja ya kuboresha utoaji wa huduma za afya na kulinda afya ya jamii nchini.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amesema pamoja na mambo mengine, makubaliano haya yanalenga kuimarisha mifumo ya utambuzi, ukusanyaji, utoaji taarifa za madhara ya dawa, chanjo, vitendanishi na vifaa tiba.
“Tunalenga kuboresha mifumo ya kubaini na ufuatiliaji wa ubora na usalama wa bidhaa kwenye soko zinazodhibitiwa na TMDA, kuimarisha mfumo wa usimamizi wa ubora, kuimarisha utoaji huduma bora za afya kwa kuzingatia viwango na ithibati za kimataifa,” ameongeza Prof. Janabi.