Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala yafafanua kuhusu uchache wa madaktari

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala yafafanua kuhusu uchache wa madaktari

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala imeona taarifa zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu muda wa kusubiri huduma kwa baadhi ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kupata matibabu.

Uongozi wa hospitali unapenda kufafanua kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa

Mwananyamala inahudumia wananchi kutoka Wilaya za Kinondoni na Ubungo pamoja na kupokea wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali nje ya Mkoa wa Dar es Salaam, hali inayoweza kusababisha ongezeko la mahitaji ya huduma katika baadhi ya nyakati na hivyo kuchangia baadhi ya wagonjwa kusubiri huduma kwa muda kabla ya kupata matibabu.

Hata hivyo, hospitali imeendelea kuimarisha mifumo ya utoaji huduma kwa kuboresha uratibu wa huduma kwa ufanisi ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma kwa kuzingatia weledi, maadili ya taaluma na ubora wa huduma zinazotolewa.

Soma Hoja ya Mdau:DOKEZO - Mwananyamala Hospital iongezewe Madaktari, foleni ni kubwa kumuona daktari

Hospitali inapenda kuwahakikishia wananchi kuwa itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kuboresha huduma na kuthamini maoni pamoja na ushauri unaotolewa na wananchi na wadau mbalimbali wa sekta ya afya kwa lengo la kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma hospitalini hapo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.

IMG_20260526_194820_109.jpg
Pia soma ~ Mchengerwa: Nikiona hoja za Wananchi najibu, nilijibu moja kwa moja kwenye JamiiForums
 
Back
Top Bottom