Hospitali ya Taifa Muhimbili kujenga jengo la kisasa, wagonjwa kuanza kutua kwa helkopta

Hospitali ya Taifa Muhimbili kujenga jengo la kisasa, wagonjwa kuanza kutua kwa helkopta

neema shamuhenya

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
312
Reaction score
216
6dc2020a732a09ad318b98678ea25eca.jpg


HOSP ITALI ya Taifa ya Muhimbili imeweka mikakati kutoa huduma bora nchini na Afrika Mashariki kwa kujenga jengo la kisasa lenye ghorofa saba litakaloanza kujengwa mwezi huu. Jengo hilo litakalojengwa kwa Sh Bilioni 20 za Serikali litakuwa na sehemu ya kutua helkopta (Helipad) kwa wagonjwa wa dharura, chumba maalumu cha kulaza viongozi wa kitaifa, wodi mbili maalumu za upandikizaji go na chembechembe za damu kwenye mifupa.

Pia litakuwa na vyumba vinne vya kulaza watu mashuhuri na vyumba 65 vya kulaza watu wawili (kila kimoja) na 20 kwa mtu mmoja mmoja. Litajengwa ndani ya eneo la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijiniDar es Salaam. Mkurugenzi wa Ufundi, G audence Aksante alisema jengo hilo litajengwa kwa miezi 18 na kutakuwa na mwaka mmoja wa uangazili ili kama kuna kasoro zozote ziweze kurekebishwa.

Alisema mkandarasi wa ujenzi huo atakuwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na pia ujenzi huo utasimamiwa na Mshauri Mwelekezi (BICCO ) kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na ujenzi wake utaanza O ktoba, 2018. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha MNH, Aminiel Eligaesha alibainisha kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo, hali ya utoaji huduma MNH itaongezeka maradufu.

Alisema miundombinu hiyo itawezesha hospitali hiyo kutoa huduma za kitabibu kwa ubingwa wa juu ambazo baadhi ya hospitali za EAC hupata changamoto ikiwamo upasuaji wa upandikizaji wa vifaa vya kusaidia watoto. Muhimbili imekuwa ya kwanza kama hospitali ya umma kutoa huduma hiyo katika ukanda huo.

Alisema pia upasuaji wa upandikizaji go, tiba radiolojia na uchunguzi wa kuondoa mawe kwenye ini na kongosho wamekuwa wa kwanza Ukanda wa Afrika Mashariki kufanya hivyo. “Nakiri sasa Hospitali ya Taifa Muhimbili imeshika nafasi yake kama Hospitali ya Taifa kwa kufanya inachostahili katika utoaji wa huduma za ubingwa wa juu,”alisema Eligaesha. Aksante alisema jengo hilo ni maalumu kwa ajili ya wagonjwa wa kulipia IPPM. Alisema Serikali imeanza kutoa fedha kuanza ujenzi huo na kiasi kikubwa itagharamia uwekaji vifaa tiba.

Huduma nyingine zitakazopatikana katika jengo hilo ni huduma za maabara, famasi, watunza kumbukumbu, uhasibu, huduma za mionzi kama Utra sound, X -ray , vyumba vya na kliniki za wagonjwa wa nje zisizopungua 10 pamoja na sehemu itakayowezesha helikopta kutua. Eligaesha alisema wagonjwa hao ni wanaotumia bima za aina mbalimbali pamoja na kampuni au taasisi zenye mkataba na hospitali kutoa huduma kwa wafanyakazi wake na wagonjwa wanaolipia fedha taslimu. Kuhusu utoaji huduma wa helikopta, Eligaesha alisema wataruhusu kutua helikopta za kampuni mbalimbali inapotokea dharura au ajali ili kuwahisha wagonjwa Muhimbili kupata matibabu.

Alisema jengo hilo litakuwa na vyumba 65 vya kulala watu wawili vinavyojitosheleza,vyenye kila kitu ndani kikiwemo choo, vyumba 20 vya mtu mmoja mmoja na vina kila kitu pia kikiwemo choo na vyumba vinne kwa ajili ya watu mashuhuri (VIP) na chumba kimoja cha hadhi ya juu ya kiongozi kama Rais. Pia kutakuwa na vyumba vya upasuaji wa kawaida viwili, vyumba vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) vyenye vitanda vitano na sehemu ya ICU ya kupumzika yenye vitanda vipatavyo 10.

Mhandisi Aksante alisema jengo hilo litakuwa na sakafu maalum kwa ajili ya huduma za upandikizaji go ambapo kutakuwa na vyumba vya upasuaji viwili vinavyoingiliana kwa ajili ya upasuaji wa go. Pia kutakuwa na chumba cha uangalizi maalum (ICU) ya vitanda vitano na ICU ya vitanda 10 na sakafu maalumu kwa ajili ya upandikizaji wa chembe chembe za damu zilizopo katikati ya mifupa, vitanda 10 vya ICU, vitanda 10 kwa ajili ya sehemu ya kupumzika baada ya mgonjwa kutoka chumba cha ICU. Pia kutakuwepo vitanda 10 kwa uangalizi wa siku kwa wagonjwa wa uboho, eneo la mazoezi ya viungo na vitanda 10 vya watoto wachanga, vyumba vinane vya wajawazito, osi za madaktari na wauguzi.
 
HELKOPTA ZIPO SIJUI NGAPI, KUNA YA JESHI LA POLISI, MSUKUMU, GWAJIMA, NA ZA MAJESHI YA ULINZI SIJAONA ZA SERIKALI (HOSPITALI)
 
wanatua na Helkopte wakitokea wapi?
Wanaweza kutokea popote pale mkuu, mfano mtu kapata ajali anabebwa na chombo anatua pale juu ya helipad anapelekwa wodini...
Mfano wa helipad upo pale holiday inn, ukienda pale Morocco square project mpya ile pia kuna helipad ...
Inasaidia sana kwa wagonjwa wa dharura ambao wanataka huduma ya haraka
 
Jamani nani atolee ufafanuzi wa makinikia, tumechoka kusubiri noah zetu.
Naona wamejua kuwa presha zimepanda sana wanatujengea ma ICU.
 
Jamani nani atolee ufafanuzi wa makinikia, tumechoka kusubiri noah zetu.
Naona wamejua kuwa presha zimepanda sana wanatujengea ma ICU.
Nitawafunga na hawata elewa lolote la maendeleo na nitawafungulia wale nitakao wachagua, huu ndio urithi wa wenye haki walahi!
 
Nitawafunga na hawata elewa lolote la maendeleo na nitawafungulia wale nitakao wachagua, huu ndio urithi wa wenye haki walahi!
Nitafurahije nikiwa ICU? Watupatie noah zetu tumeahidiwa na Thornton kupitia kwa rais, zinatokana na makinikia.

Kwenye hilo jengo kitengo cha machizi kipo?
Kama hakipo wakiongeze!
Makinikia yatazalisha machizi wengi sana kuanzia madokita na maprofesa!
 
Vizuri lakin linajengwa kwenye eneo dogo sana ,pamebanana balaa
 
Write your reply.. Wajenge kigamboni au kibamba kupunguza msongamano
 
vyoo tu ndani ya wodi vimewashinda wanakimbilia huko...hospital ni chafuu
 
Hi kitu inawezekana zikajengwa Kikanda na wagonjwa wakaacha kujazana Dar.
 
Back
Top Bottom