jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Ni mtu wa hovyo kweli kweli maana hili swala la medical report hata mimi limenikuta.Maana kuna kipindi nlikuwa mgonjwa nyumbani nikawa natibiwa na Bima wakuu wangu walitaka Medical report so ili nilazimu nilipie laki kama ilivyo.Unaenda kuandikiwa report na Dokta ukiingia ndani anakujibu subiri amalize kuwa tibu wagonjwa wote Report ataandika mwisho.Ukisubiria mpaka mwisho baada ya kukuandikia report ukienda kwa wale makarani wakuchapie una wakuta wamefunga wanakwambia njoo kesho.
Kesho ukienda ana kuchapia tena vizuri ukienda kwa Dokta wako kwa ajili ya kusaini ana kujibu subiri amalizie wagonjwa wake kuwatibu.Ukienda mwisho baada ya kuwatibu wagonjwa wake anasoma hiyo riport anagundua tena karani kakosea Grammaly na utaratibu ya uwandishi.Unarudi tena karani unaambiwa kaenda kula una kaa unamsubiri akitoka kula ana kujibu muda umeenda sana hiyo kazi ataifanya kesho....
Any way acha niishie hapo tuu maana sitotaka kukumbuka zile taabu.
Inasikitisha sana