Hospitali ya Taifa Muhimbili yatoa ufafanuzi hoja ya Mdau kuhusu "Huduma zake ni janga kwa Wagonjwa"

MRN ni nini? Au unamaanisha MRI?
 
Ukiona mtu mmoja ana bilioni 100 alizoiba serikalini, au njia haramu, jua amewanyima na kuwakwamisha watu zaidi ya 1000 fursa za elimu, ajira, maji, umeme, makazi nk. kwa mgao angalau wa milioni 100 kwa hao watu 1000. Kinyume chake anasifiwa mtu mmoja aliyejilimbikizia mali bila kujali wengine wameathirika kiwango gani.
 
kama za bure hakuna, ziwepo za bei nafuu. na swali ni je, kwani unagarimia kitu gani kwenye mashine ambayo tumenunua sisi wenyewe kwa kodi zetu, au unacharge umeme? kwa sababu kama ni wafanyakazi wapo umeshaajiri, umewaletea mashine waifanyie kazi na hata isipokuwepo watafanya tu kazi na mshahara wataupata uleule. kwanini basi hata vipimo viwe bure, ili mtu akijua tatizo umwambie sasa akajipange kununua dawa (tukijua dawa umejumua kiwandani ila mashine haujajumua), akili ya kawaida kabisa isiyohitaji kwenda shule. lipisha watu kile ulichojumua kufanyia biashara kama vile dawa, ila mashine ambayo tumenunua kupima kujua ugonjwa ili utuungishe dawa inakuwaje unacharge? na hapohapo serikali iwe inatoa pesa nyingi tu na kuwalipa mishahara toka kwenye mfuko mwengine (kama ndio hivyo).
 
Kumbe ni kweli kujifungua ni 1.4 million....!?

Wamama walitakiwa kujifungua Bure Nchi nzima....!
 
Gharama ni kubwa na hazieleweki achen kujibu kisiasa, mnamuandikia mgonjwa bill akiuliza vitu alivyotumia hamna majibu
Hasa kitengo cha dressing Ni majanga matupu!
 
Kwahiyo ikiwa ngazi ya nne, hata vitanda vinaacha kuwa vya kupumzikia, vinageuka vya guest houses
 
Kuna baadhi ya vifaa vya wagonjwa Huwa wanadai hawana! Utatao hela vinunuliwe kumbe vipo! Hutapata risiti kamwe!
Pale ni rushwa rushwa rushwa!
 
SGR na Air Tanzania si zimrnunuliwa kwa kodi zetu, mbona tunalips nauli ?

unajus X ray au CT scan inahitaji umeme kiasi gani kutoa mionzi au unabwatuka
 
JF inapenyeza sana, naweza sema wanaichukulia serious kuliko twitter x.. kaz nzur mods.
 
da
SGR na Air Tanzania si zimrnunuliwa kwa kodi zetu, mbona tunalips nauli ?

unajus X ray au CT scan inahitaji umeme kiasi gani kutoa mionzi au unabwatuka
hauisaidii jamii kuja hapa kutuuliza sisi tusio madaktari umeme kiasi gani unatumika kwenye xray na CT scan au MRI. na siamini kama serikali inayolipia taifa stars milioni 700, inayotumbua pesa kwa misafari na wizi kibao, itashindwa kulipa umeme. pia, tunatofautiana sana ufahamu mtu kuja kufananisha hospitali na SGR, tafuta mfano mwingine ili ustahili kujadiliana JF chief.
 
Huu mtandao nilikuwa nauchukulia poa Sana kuna siku nilitoa hoja yangu na ikatolewa ufafanuzi na mamlaka ndipo nilipohuheshimu jamii forum safi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…