Hospitali ya Taifa Muhimbili yatoa ufafanuzi hoja ya Mdau kuhusu "Huduma zake ni janga kwa Wagonjwa"

 Hospitali ya Taifa Muhimbili yatoa ufafanuzi hoja ya Mdau kuhusu "Huduma zake ni janga kwa Wagonjwa"

Baada ya Wanachama wa JamiiForums.com kuandika hoja zinazoitaja Hospitali ya Muhimbili - Mlonganzila kuwa na gharama kubwa na changamoto nyingine za kiutendaji, taasisi hiyo imetoa ufafanuzi. Kusoka hoja za Wadau bofya hapa chini:

~ DOKEZO: Serikali iimulike hospitali ya Mloganzila, Huduma zake ni janga kwa wagonjwa na ndugu wanaouguza pale
~ Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru
UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA ILIYOCHAPISHWA NA MTANDAO WA JAMIIFORUMS KUHUSU HUDUMA ZA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI-MLOGANZILA

DAR ES SALAAM: NOVEMBA 22, 2024
Mtandao wa JamiiForums umechapisha taarifa yenye kichwa cha habari "Serikali limulike Hospitali ya Mloganzila, huduma zake ni janga kwa wagonjwa na ndugu wanaouguza." Kutokana na taarifa hiyo, Uongozi wa Hospitali unapenda kutoa ufafanuzi ufuatao;

1. Wagonjwa 20 hadi 25 kufariki kwa siku
Miaka ya hivi karibuni hadi Novemba 21, 2024, idadi ya wagonjwa wanaoonwa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeongozeka kutoka wagonjwa wa nje 400 hadi 1,000 kwa siku na idadi ya wagonjwa waliolazwa wodini wakati wote imeongezeka kutoka 200 hadi 400 kwa siku. Hii ni kutokana na uboreshaji mkubwa wa mifumo na huduma uliofanywa hospitalini hapo na hatimaye kuvutia wananchi wengi kuitumia hospitali hiyo.

Idadi ya wagonjwa wanaofariki kwa siku hospitalini hapo kutokana na sababu mbalimbali ni kati ya wanne (4) hadi sita (6) kati ya wagonjwa 400 waliolazwa na siyo 20 hadi 25 kwa siku kama ilivyoelezwa katika taarifa iliyochapishwa na JamiiForums.

2. Kutoa taarifa za mgonjwa
Ni kinyume na maadili ya kitabibu kwa mtoa huduma kutoa taarifa za mgonjwa bila ridhaa yake na kwa wale ambao hawajiwezi taarifa hutolewa kwa ndugu aliyeandikishwa au kupewa idhini ya kupokea taarifa hizo (next of kin). Ndugu wengine wanaopenda kufahamu taarifa za mgonjwa wanazipata kutoka kwa mgonjwa mwenyewe au ndugu aliyeandikishwa endapo watapenda kufanya hivyo. Tutaendelea kusimamia jambo hili.

3. Gharama za matibabu kuwa juu
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila inapokea na kuhudumia makundi manne ya wagojwa ambayo ni wagonjwa wa bima, wanaolipa fedha taslimu, wagonjwa wa rufaa wanaochangia huduma na wagonjwa wa msamaha. Mwaka wa fedha 2023/2024, Hospitali imetoa huduma kwa njia ya msamaha zenye thamani ya TZS. 3.9 Bil na kwa robo mwaka wa fedha 2024/2025 huduma zenye thamani ya TZS. 970 Mil zimetolewa kwa wananchi wasiokuwa na uwezo.

Ikumbukwe kuwa, Hospitali hii ni ngazi ya nne (ngazi ya juu) ya utoaji huduma nchini, hivyo teknolojia ya huduma za uchunguzi na matibabu imebalidika kutoka za kawaida kwenda kwenye ngazi za ubingwa bobezi ili kumpa mgonjwa matibabu stahiki. Endapo kuna mgonjwa ana changamoto ya malipo utaratibu wa hospitali uko wazi kupitia Huduma za Ustawi wa Jamii.

4. Kauli za Watoa Huduma
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeendelea kutekeleza azma ya Serikali ya utoaji huduma bora kwa wananchi. Kauli zisizo na staha kutoka kwa watoa huduma zimepungua kwa kiasi kikubwa. Uongozi wa Hospitali hauvimilii kauli za namna hii. Tumelipokea jambo hili, tutaendelea kulifanyia kazi,

Aminiel Buberwa Aligaesha
MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMΜΑ

Gharama za kitanda kwa siku hazijajibiwa,
 
Mkuu sekta ya afya ni Pana sana Ina matibabu,Kinga na tafiti vyote vinahitaji pesa tukitaka huduma za Bure haiwezekani ikawa Bure labda iwe huduma zitolewe kwa bei nafuu sana. Naipongeza. hospital ya kisarawe iliyopo mkoani Pwani huduma pale zinatolewa ni za kibingwa kwa wananchi wengi wa mkoa wa Pwani wengi kutoka manerumango, chole,vikumbulu,Malui ni maskini kweli kweli lakini wanada ikiwa kupata matibabu kwa gharama nafuu sana.

Tunaposema matibabu yanaendana na Kinga na tafiti nani atagharamia hizo kinga na tafiti au tukae tukiwategemea wafadhili .

Hiyo mitambo inaharabika pesa ya service itoke Tena serikalini hapana ,inabidi tukubali matibabu yatolewe kwa kulipia kiasi sio hicho kopimo unaambiwa laki SITA operation unaambiwa milioni na nusu ,kitanda elfu hamsini hapana Kwa hospitali za serikali hizo ni bei za hospital binafsi ambazo hazipati msaada wowote kutoka serikalini.
Rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za Kodi za Wananchi huko Serikalini ndio chanzo kikuu cha haya madhila yote katika nchi ya Tanzania ikiwamo na kudorora kwa huduma mbaya na duni kabisa za afya hapa nchini. Serikali ina uwezo kabisa wa kutoa huduma za Afya bure kabisa bila malipo endapo kama vitendo viovu vya rushwa, ufisadi na ufujaji wa Kodi vitakomeshwa hapa nchini.
Nakumbuka huko miaka ya nyuma wakati huo nilipokuwa naishi kwenye Moja ya nchi fulani hivi, Wahamiaji wote wa kimataifa ambao tulikuwa na Visa halali za kuishi kwenye nchi hiyo tulikuwa tunapata huduma A Afya bure kabisa bila malipo yoyote yale sawasawa na raia wazawa wa nchi hiyo ilahi sisi tulikuwa ni Wahamiaji tu kwenye hiyo nchi.
Huduma zote za matibabu tulikuwa tunapata bure kabisa bila malipo yoyote Yale.
 
kitu ambacho huwa sikielewi kwenye hospitali za serikali ni kwamba, LABDA KAMA HAWAPOKEI FUNGU LA KUENDESHEA HOSPITALI TOLA SERIKALINI. nijibuni maswali haya;

1. hospitali hizi za serikali, zinajiendesha? au zinaendeshwa kwa kodi/bajeti ambayo ni kodi yetu. kama jibu siyo, kwanini?

2. serikali huwa inanunua mitambo mara kwa mara. mfano; mtambo wa MRN, xray na mingine, na vipimo vingine. mitambo hiyo huwa inanunuliwa kwa pesa zinazotokana na kodi za wananchi au na pesa zinazotozwa hospitali?

3. kama jibu namba 2 litakuwa vinanunuliwa kwa pesa za kodi, wanapata hasara gani wakiamua kupima watu bure badala ya kuwalipisha? mashine umepewa na serikali haujanunua wewe au umepewa msaada, unao wafanyakazi wa kila siku uliowaajiri wa kuziendesha, umeme zinatumia wa kawaida hata usipozitumia bili inakuja hat akuongezeka itakuwa kidogo sana, kama mashine hizo ni zetu sisi watanzania, KINACHOWAFANYA MSIPIME WATU BURE NI NINI? mngepata hasara gani? au mna shetani wa kulipisha watu msipolipisha mtu akapata huduma bure mnajisikia vibaya sana? si mali yetu sote, hamjanunua, au mmenunua kwa pesa za kodi zetu, pimeni watu bure, wengi wanakufa kwa kukosa huduma ambazo kodi zao zimenunua vifaa mnavyotumia.

4. serikali, inashindwa nini, kwa pesa hizo samia anabukia kwenye masafari yaliyojaa wasanii wasio na faida yeyote kwa nchi, wanashindwa nini kununua vitendea kazi mahospitalini ili ibaki kwa madaktari kuvitumia kwa watu bure. mnashindwa nini? safari mbili za samia zinanunua MRN moja. hata hizi za mkoani zina garama sana. pesa wanazotumbua na kuiba wangeweza kununua mashine nyingi, na kwa sababu ni za kwetu? tutumie bure, na wafanyakazi tunao tayari hawatalipwa ziada kwa kuendesha mashine za vipimo.

5. mnajisikiaje mtu kwenda hospitali ya umma leo hii, analipia hata ultrasound? au mnataka watu wawe wanakufa tu.
Nakuhutaji kwenye huu uzi
 
Rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za Kodi za Wananchi huko Serikalini ndio chanzo kikuu cha haya madhila yote katika nchi ya Tanzania ikiwamo na kudorora kwa huduma mbaya na duni kabisa za afya hapa nchini. Serikali ina uwezo kabisa wa kutoa huduma za Afya bure kabisa bila malipo endapo kama vitendo viovu vya rushwa, ufisadi na ufujaji wa Kodi vitakomeshwa hapa nchini.
Nakumbuka huko miaka ya nyuma wakati huo nilipokuwa naishi kwenye Moja ya nchi fulani hivi, Wahamiaji wote wa kimataifa ambao tulikuwa na Visa halali za kuishi kwenye nchi hiyo tulikuwa tunapata huduma A Afya bure kabisa bila malipo yoyote yale sawasawa na raia wazawa wa nchi hiyo ilahi sisi tulikuwa ni Wahamiaji tu kwenye hiyo nchi.
Huduma zote za matibabu tulikuwa tunapata bure kabisa bila malipo yoyote Yale.
Umeandika vitu viwili;
1. Rushwa ,ufisadi na wizi wa Kodi za wananchi
i.e. nakubaliana Hilo endapo vitendo hivyo vitakomeshwa pesa nyingi sana itaokolewa na itasaidia katika upatikanaji wa huduma Bora kwa gharama nafuu au Bure kabisa kama ilivyokuwa enzi za utawala wa awamu ya kwanza.

2. Umeandika ulipoishi ughaibuni kama mmataifa mlipata huduma.za afya Bure hapa Mkuu naomba tutofautishe nchi za ughaibuni na zetu huku Dunia ya tatu huko ughaibuni wao wanajitosheleza na bajeti zao kwa 100% wakati huku kwetu bado bajeti zetu na ukusanyaji WA Kodi ni 40% to 60% vyanzo vyetu vya mapato vimegota,sio rahisi Tena tukawa na uwezo wa kutoa huduma Bure mpaka tutakapomesha wizi wa pesa za Kodi ,kuongeza vyanzo vya mapato na wananchi tukawa na.moyo wa kuchangia Kodi na ushuru kama.watu wa ughaibuni Walivyozoea.
 
PEsa za kununua goli kwa million 5 na million 700 za stars. Kuwapeleka wasanii vacation korea wanatoaga wapi.

Anaway nahitaji maoni yako kwenyu huu uzi
 
Waambie ufafanuzi wao ni batili! Kwanini hawaja ainisha gharama kama mlalamikaji alivyosema?
Lugha Chafu Hilo linasemwa na wengi hata huko Facebook wamekuwa wakisema.

Maandiko kadhaa nimesoma Nje na jf yanasema ukipelekwa mlonganzila uwezekano wa kupona ni mdogo sana.
Kinachotakiwa mtaje kwa jina mhusika aliyefanya hivyo ikiwezekana kama kuna voice record inapendeza zaidi.
 
Mmmh!

Gharama za kitanda kwa siku zinaelezwa kuwa ni Tsh. 50,000/- bila ya huduma nyingine yoyote ile ya ziada, Je, kuna Ukweli gani kuhusu suala hili?

Mbona sasa gharama hizi ni kubwa sana kama gharama za Malazi kwenye Hoteli ya Kitalii ya kifahari kwa hapa Tanzania? Kulikoni Jambo hili?
Kitanda,A.C,Maji,umeme........though watu hao hao wanajaa gesti kutombana kwa siku elfu gesti elfu 60,
Akitoka hapo anaenda kuvuta mashisha na mapombe makali
 
Kaulizwa mchele anajibu PUMBA.
Kwanini kulazwa kwa siku ni elfu 50?.
Hilo ndo alitaliwa alijibu sio maelezo mengi alafu hamna kitu
 
Mimi nilitaka kujua gharama za Kitanda cha chuma kwa siku ni Tsh ngapi na si kuja na maelezo ya Ustawi wa Jamii tena.
 
Mbona hajatoa ufafanuzi kuhusu gharama wanazotozwa hao wagonjwa? Tena ingekuwa vyema aeleze kila kundi namna wanavyochajiwa.
Halafu huo msamaha anaosema mbona msamaha wenyewe ni kutolipa hela ya kumuona Daktari tu lakini vipimo na dawa mgonjwa anatakiwa alipie? Wasitumie kigezo cha msamaha kufanya ufisadi wakati hakuna msamaha wowote wa maana kwa wagonjwa.
 
Mim nashangaa sana,nikajua kwamba muhimbili itakuwa kimbilio la wananchi masikini lakn ndo kwanza mambo yamekuwa tofauti,yawezekana ni kituoa cha kupga pesa

Ova
 
Siasa tu,nakumbuka kusoma hoja ikiwemo ya kitanda kwa siku mgonjwa anatozwa 50K nilitegemea niione kwenye hicho walichoita ufafanuzi kwamba ni kweli?

Mwanangu alilazwa MNH Upanga nimemtoa juzi lakini nahisi kwa sababu yupo under five kwenye bill sikuona gharama za malazi so sikutozwa ada ya kitanda kasheshe ni sisi watu wazima.
 
Mkuu sekta ya afya ni Pana sana Ina matibabu,Kinga na tafiti vyote vinahitaji pesa tukitaka huduma za Bure haiwezekani ikawa Bure labda iwe huduma zitolewe kwa bei nafuu sana. Naipongeza. hospital ya kisarawe iliyopo mkoani Pwani huduma pale zinatolewa ni za kibingwa kwa wananchi wengi wa mkoa wa Pwani wengi kutoka manerumango, chole,vikumbulu,Malui ni maskini kweli kweli lakini wanada ikiwa kupata matibabu kwa gharama nafuu sana.

Tunaposema matibabu yanaendana na Kinga na tafiti nani atagharamia hizo kinga na tafiti au tukae tukiwategemea wafadhili .

Hiyo mitambo inaharabika pesa ya service itoke Tena serikalini hapana ,inabidi tukubali matibabu yatolewe kwa kulipia kiasi sio hicho kopimo unaambiwa laki SITA operation unaambiwa milioni na nusu ,kitanda elfu hamsini hapana Kwa hospitali za serikali hizo ni bei za hospital binafsi ambazo hazipati msaada wowote kutoka serikalini.
Zanzibar huduma za afya ni Bure, x-ray, ultrasound, ct scan MRI zote ni bure ili mradi Dr muhusika akuandikie tu.
 
PEsa za kununua goli kwa million 5 na million 700 za stars. Kuwapeleka wasanii vacation korea wanatoaga wapi.

Anaway nahitaji maoni yako kwenyu huu uzi
Mkuu wa nchi anasimamia bajeti ya nchi ya. trilioni 3 kutoa hamasa kwa Timu ya Taifa milioni 700 mbona pesa kidogo sana sio sawa na kununua ma MRI Kwa hospital za rufaa nchi nzima bajeti yake ni mabilioni.

Hao wasanii tusiwabeze ,Dunia ya kwanza usanii unaheshimiwa sana ndio maana Reagan mchekeshaji akawa Rais wa USA hata Zelensiky wa Ukraine ni msanii ndiye. Rais wa Ukraine ,wasanii wetu wanahitaji pongezi na exposure sababu wamedhubutu kujiajiri na kujidharirisha kwenye movie kitu ambacho wengi hasa wasomi hawakiwezi.

Sisi turudi kwa hao jamaa wa Muhimbili Kwa Nini wanatoza gharama kubwa za vitanda,vipimo na dawa?
 
TUpia maoni kwenye huo uzi
 
Back
Top Bottom