KERO Hospitali ya TIBA (zamani Tumaini) iliyopo Upanga haihudumii wagonjwa wa NHIF

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hospitali ya TIBA (zamanı TUMAINI) iliopo Upanga jirani na Diamond Jubilee haichukui wagonjwa wanaotumia bima ya NHIF wiki moja sasa.

Wagonjwa wanarudishwa nyumbani na wengine wanaambiwa walipe cash. Waliokuwa hawana huduma zimesitishwa.

Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu tunaomba waingilie kati hili jambo kwani ugomvi uliopo baina ya Hospitali ya TIBA na NHIF hauleti taswira njema kwa wananchi na hii inachochea wananchi dhidi ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali anayoiongoza.
 
Ukiona hivyo wameona miyeyusho

Ova
 
Bima ya NHIF tunaitumia Kwa sababu ya umasikin tu lakin kiukweli hamna Bima humo
 
NHIF inatakiwa ifumuliwe ifanyiwe overhaul hata ikibidi tukodi management ya wazungu waje kuiendesha maana wenyewe tumeshindwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…