Hospitali ya Wilaya ya Chato yakumbwa uhaba mkubwa wa dawa

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
HOSPITALI ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita, inakabiliwa na uhaba wa dawa hali inayotishia baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha.

Wakizungumza na Nipashe baadhi ya wagonjwa na ndugu katika hospitali hiyo, wamesema wanalazimika kutumia fedha nyingi kupata matibabu kutokana na kutakiwa kununua dawa kwenye maduka ya watu binafsi.

Gelard Nyambele, mkazi wa Kijiji cha Kanyama, amesema ndugu yake ambaye ni mgonjwa amefanyiwa upasuaji mkubwa wa kuondoa bandama tumboni, lakini dawa nyingi aliagizwa kununua kwenye duka la Serikali lililopo kwenye maeneo ya hospitali hiyo.

"Tuliambiwa ili kumsaidia mgonjwa wetu tunapaswa kuwa na fedha za kununulia dawa zinazohitajika kwa kuwa hospitali hiyo haina dawa zinazofaa kwa ajili ya mgonjwa wetu," alisema Nyambele.

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kutokuwapo kwa baadhi ya dawa muhimu zaidi ya miezi sita ikiwamo 'panadol' hali inayowakatisha tamaa baadhi ya wagonjwa na kulazimika kutafuta huduma vituo binafsi vya afya na wengine kutibiwa kwa waganga wa jadi.

Aidha, hali hiyo imechangia kushuka kwa mapato yatokanayo na uchangiaji huduma kutokidhi Kiwango cha kuagiza dawa hizo kutoka Bohari ya Dawa Nchini (MSD) na kusubiri kudra za dawa zilizolipiwa kupitia ruzuku ya serikali kuu.

Uchunguzi umebaini pia mapato yameshuka kwenye hospitali hiyo kutokana na baadhi ya makundi kutotakiwa kuchangia huduma hizo ikiwamo wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na wazee zaidi ya miaka 60.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Cha to, Dk. David Mudeba, alikiri kuwapo kwa uhaba wa dawa muhimu kwenye hospitali hiyo na kudai kuwa tatizo hilo ni la kitaifa.

"Ni kweli tuna tatizo la uhaba wa baadhi ya dawa..hii inatokana na matatizo ya kimfumo MSD ndiyo wanapaswa kutusambazia huduma hiyo..fedha zetu nyingi zipo kwao ndiyo maana hata Rais Samia Suluhu, ameamua kupangua pale MSD ili kuboresha huduma," alisema Dk. Mudeba.

Uhaba wa dawa umekuja ikiwa ni siku chache tangu baadhi ya wajawazito kulalamika mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, kwamba wanatozwa fedha na vifaa vingine wanapokwenda kujifungua kwenye hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Christian Manuga, alipotakiwa kuelezea tatizo hilo, alisema hana taarifa hizo huku akiahidi kuambatana na Mganga Mkuu wa wilaya hiyo kwenda kujiridhisha kabla ya kutoa majibu kwa vyombo vya habari.

Source: Nipashe
 
Kwani hospitali ya wapi ina dawa japo kidogo?

Mbona kote iwe kumwona daktari au kuchukuliwa vipimo ni malipo na dawa zote ni za kununua?

Hiki kiini macho cha bajeti ya dawa ni upigaji uliohalalishwa serikalini na mahospilalini.

Mgonjwa gani au ndugu atahoji nini kuhusiana na kutokuwepo kwa dawa hospitalini?
 
HOSPITALI ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita, inakabiliwa na uhaba wa dawa hali inayotishia baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha.

Wakizungumza na Nipashe baadhi ya wagonjwa na ndugu katika hospitali hiyo, wamesema wanalazimika kutumia fedha nyingi kupata matibabu kutokana na kutakiwa kununua dawa kwenye maduka ya watu binafsi.

Gelard Nyambele, mkazi wa Kijiji cha Kanyama, amesema ndugu yake ambaye ni mgonjwa amefanyiwa upasuaji mkubwa wa kuondoa bandama tumboni, lakini dawa nyingi aliagizwa kununua kwenye duka la Serikali lililopo kwenye maeneo ya hospitali hiyo.

"Tuliambiwa ili kumsaidia mgonjwa wetu tunapaswa kuwa na fedha za kununulia dawa zinazohitajika kwa kuwa hospitali hiyo haina dawa zinazofaa kwa ajili ya mgonjwa wetu," alisema Nyambele.

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kutokuwapo kwa baadhi ya dawa muhimu zaidi ya miezi sita ikiwamo 'panadol' hali inayowakatisha tamaa baadhi ya wagonjwa na kulazimika kutafuta huduma vituo binafsi vya afya na wengine kutibiwa kwa waganga wa jadi.

Aidha, hali hiyo imechangia kushuka kwa mapato yatokanayo na uchangiaji huduma kutokidhi Kiwango cha kuagiza dawa hizo kutoka Bohari ya Dawa Nchini (MSD) na kusubiri kudra za dawa zilizolipiwa kupitia ruzuku ya serikali kuu.

Uchunguzi umebaini pia mapato yameshuka kwenye hospitali hiyo kutokana na baadhi ya makundi kutotakiwa kuchangia huduma hizo ikiwamo wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na wazee zaidi ya miaka 60.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Cha to, Dk. David Mudeba, alikiri kuwapo kwa uhaba wa dawa muhimu kwenye hospitali hiyo na kudai kuwa tatizo hilo ni la kitaifa.

"Ni kweli tuna tatizo la uhaba wa baadhi ya dawa..hii inatokana na matatizo ya kimfumo MSD ndiyo wanapaswa kutusambazia huduma hiyo..fedha zetu nyingi zipo kwao ndiyo maana hata Rais Samia Suluhu, ameamua kupangua pale MSD ili kuboresha huduma," alisema Dk. Mudeba.

Uhaba wa dawa umekuja ikiwa ni siku chache tangu baadhi ya wajawazito kulalamika mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, kwamba wanatozwa fedha na vifaa vingine wanapokwenda kujifungua kwenye hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Christian Manuga, alipotakiwa kuelezea tatizo hilo, alisema hana taarifa hizo huku akiahidi kuambatana na Mganga Mkuu wa wilaya hiyo kwenda kujiridhisha kabla ya kutoa majibu kwa vyombo vya habari.

Source: Nipashe
Kwani Waziri wa Afya yuko wapi? Hebu njoo hapa ueleze wananchi kwanini nisikutumbue hapahapa? Au nakosea wananchi???
 
Huyu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato alimchimba mkwara Prof. Tibaijuka wakati Prof alipotoa maoni yake kupinga kuanzishwa kwa Mkoa wa Chato.

Baada ya Team mwendazake kunyooshwa kisawasawa naona amekuwa mpoleee na kukumbuka kumbe na yeye ni Mwenyekiti tu kama wa Wilaya ya Tanganyika huko Katavi
 
Back
Top Bottom