Hospitali yetu kuu ya taifa muhimbili inasikitisha!!

Hospitali yetu kuu ya taifa muhimbili inasikitisha!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Kijana akiwa yuko Chini baada ya kukosa Kitanda katika Moja ya Wodi Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam
clip_image001%25255B8%25255D_thumb%25255B2%25255D.jpg
clip_image001%25255B10%25255D_thumb%25255B2%25255D.jpg


Hali si shwari Hospitalini Hapo kwa Mazingira haya…..


HOSPITALI YETU KUU YA TAIFA MUHIMBILI INASIKITISHA!! - GUMZO LA JIJI

KAMA NDIO MIMI NI WAZIRI WA AFYA BORA NIJIUZULU KULIKO HALI MBAYA YA NAMNA HII HUKO HOSPITALI YA TAIFA

YA RUFAA YA MUHIMBILI. AHHHHH INALETA WOGA SANA TAIFA LINAKWENDA WAPI LINATOKA WAPI JAMANI? HAKUNA

HATA VIONGOZI WENYE ROHO ZA HURUMA KUWAONEA HURUMA WAGONJWA?
 
Huyo hapo mwisho mwenye kulazwa kwenye shuka imelowa damu ni kwa ajili ya kukosa miundombinu ama? Uongozi mbovu ndio donda letu. Hakuna anaewajibika, sio waziri wala raisi wala mfagiaji!
 
inasikitisha sana kwakweli, haya mambo ya kulaza watu chini ilibidi mpaka sasa wawe wamerekebisha. Ubaya wa hapo hospitali ni kuwa akija kiongozi wanaficha hali halisi iliyopo hapo hospitali ya ufinyu wa vitanda. huu si uadilifu
 
OMG, niliwahi kuingia iyo wodi once, it was terrible. Hakuna thamani ya binadamu kwenye iyo wodi.
 
Nilipataga referral from Agakhan to Muhimbili, mwaisela ward, aisee nilianza kulia kama mtoto,,,hali ilikuwa mbaya sijapata ku experience, nilikaa reception masaa mawili wananitafutia kitanda cha kulala,,,sehemu imejaa, nikapelekwa sehemu ya watu wa figo , na mimi siumwi figo, kule watu wamebanana,,,hakuna distance kubwa kitanda na kitanda,,,yaani unaona kuambukizana kwa magonjwa ya hewa rahisi mno! Hali ni tete sana, sema wao wakubwa huwa wanaenda VIP, ila wange experience kule kwa kajamba nani, wangekuwa na uchungu kidogo, very sad
 
Tatizo la nchi yetu ni kuficha ukweli,
akienda mheshimiwa rais atakuta kila mtu kalala kitandani
tena amepewa shuka mpya,

wangekuwa wanaweka mambo hadharani
kama huyu mpiga picha alivyofanya naamini
hali ingerekebika tu. chama huku ni maeneo yako haswa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom