friendsofjeykey
Senior Member
- Aug 12, 2010
- 129
- 13
Pole sana, nafikiri kuna haja ya hawa watu kufungia na kufanyiwa uchunguzi wa kina.Mimi
mwezi April,nilipoteza Dada yangu ambaye tulimpeleka hapo hospitali anatembea mwenyewe ilikua Alhamisi na usiku wa kuamkia Jumapili nilipigiwa simu kuwa moyo ulisimama ghafla akifanyiwa operation ya dialysis. Hii hospitali inamatatizo makubwa hatujajua kuna nini hapa.
Nakubali Regency kuna uzembe fulani hapo. Namfahamu mgonjwa fulani wa figo (RIP), alifanyiwa dialisis hapo kwa muda wa mwezi tuu, akajikuta ameambukizwa magonjwa ya ajabu, akapelekwa India kufanyiwa transplant, kufika kule, akaambiwa it was too late, dialisis waliokuwa wakimfanyia ilikuwa na contermination, there was no way back, alirudishwa kwenye sanduku!.
Nikatamani ningekuwa na uwezo, kufanya utafiti, ni wagonjwa wangapi wa dialisis ya Regency huwa wanasurvive.
Dialysis ni kubadilisha damu yote kwenye mwili wa binadamu kwa kutumia mashine maalum ili kuisafisha na kuirudisha mwilini.
Hata baada ya kutokea vifo vinavyosababishwa na uzembe, madaktari, wanalindana. Hii issue ya kijana, inaenekana walizidisha dose ya anaesthesia. Postmortem wataandika, mortar brain failure, iliyopunguza heart pulse iliyopunguza blood supply kwenye brain iliyosababisha brain demage na hivyo kusimamisha figo na kusababisha kifo. Ukichunguza zaidi, unaweza ukakuta hata hiyo appendix haikuwa chanzo!.
AgaKhan siku hizi panaitwa hotel...Tumaini na Regency ndio hivyo. Wakuu hivi kwa sasa ni hospital gani ambayo ni afadhali kuikimbilia? Maana muhimbili, Mwananyamala na wale ndugu zao wengine wote tunajua hali ilivyo. Na mgombea mmoja amesema atahakikisha anapandisha daraja hospitali kadhaa! Sijui hiyo inatufikisha wapi
agakhan siku hizi panaitwa hotel...tumaini na regency ndio hivyo. Wakuu hivi kwa sasa ni hospital gani ambayo ni afadhali kuikimbilia? Maana muhimbili, mwananyamala na wale ndugu zao wengine wote tunajua hali ilivyo. Na mgombea mmoja amesema atahakikisha anapandisha daraja hospitali kadhaa! Sijui hiyo inatufikisha wapi