Hospitali za REGENCY na TUMAINI zimulikwe!

Hospitali za REGENCY na TUMAINI zimulikwe!

friendsofjeykey

Senior Member
Joined
Aug 12, 2010
Posts
129
Reaction score
13
Ukitaka kufa mapema au kuondokewa na jamaa yako wewe wapeleke jamaa zako hospitali hizi.

Regency is even worse maana madaktari huwa wanakimbia mpaka ndugu wa mgonjwa hali ikiwa mbaya. Hivi Blandina Nyoni na wenzie huko wizara ya Afya kwa nini hawataki kusikiliza kilicho wananchi ambao wanazidi kupoteza maisha ya jamaa zao kwenye death chambers hizi?
 
Ni kweli haswa Tumaini Hospital, lakini nadhani hii thread hapa sio mahali pake.
 
Regency ni hospitali ya wahuni, Hawa wahindi hawana uzoefu wa kutibu
 
Tunakosa REGULATORY BOARDS kwenye huduma muhimu sana za AFYA na ELIMU. Badala yake tumeunda haraka boards hizi kwenye simu( TCRA), daladala(SUMATRA) na dizeli( EWURA). Nilimsikia JK akiahidi kuunda ile ya elimu wakati tayari kuna TEA ambayo ingepewa nguvu za kisheria tu.
 
AgaKhan siku hizi panaitwa hotel...Tumaini na Regency ndio hivyo. Wakuu hivi kwa sasa ni hospital gani ambayo ni afadhali kuikimbilia? Maana muhimbili, Mwananyamala na wale ndugu zao wengine wote tunajua hali ilivyo. Na mgombea mmoja amesema atahakikisha anapandisha daraja hospitali kadhaa! Sijui hiyo inatufikisha wapi
 
Habari za kazi Kaka Michuzi,
Tunashukuru kwa kazi yako nzuri ya kutufikishia taarifa mbalimbali

Ninaomba kushare na watanzania wenzangu juu ya jambo lifuatalo kuhusu kifo cha kijana mmoja (miaka 17) kilichotokea tarehe 19/08/2010 Regency Hospital.

Kijana huyu alifika hospitalini hapo tarehe 14/08/2010 siku ua jumamosi akitembea mwenyewe akitaka kumwona daktari juu ya afya yake. Alianza kuumwa tumbo akiwa shuleni Moshi hali iliyomlazimu kurudi nyumbani Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.

Baada ya kufika hospitali ya Regency alimwona dakatari wa kawaida (general doctor) ambaye alimuandikia vipimo mbalimbali.

Majibu hayakuonyesha kuwa na tatizo lolote hivyo dakatari kumshauri amuone daktari wa magonjwa ya tumbo. Alimuona daktari aitwaye Mponji. Baada ya kuangalia vipimo vya awali alisema hiyo itakuwa ni appendix kutokana na namna kijana anavyoumwa hivyo kushauri afanyiwe upasuaji.

aliingizwa chumba cha upasuaji milango ya saa kumi jioni siku hiyo hiyo ya jumamosi. Mnamo saa moja jioni ndugu zake ikiwamo mama yake na kijana waliitwa na kuelezwa kuwa kijana anashindwa kuaamka kutoka kwenye usingizi mzito baada ya upasuaji na kwamba wanahaingaika kumuamsha.

hali iliendelea hivyo mpka siku ya pili na kuendelea. Cha kusikitisha hakukuwa na jitihada madhubuti za kumsaidia mtoto aamke. baada ya ndugu kuja juu ndipo walipoelezwa kuwa moyo wa mtoto ulisimama wakati wa upasuaji hivyo kuathiri ubongo wake na hatimaye figo zake kushindwa kufanya kazi bila kutoa sababu za moyo kusimama.

Maelezo hayo yalitolewa siku ya nne baada ya upasuaji na ni baada ya ndugu kuja juu kutaka kujua ukweli wa tatizo. Baada ya ugomvi huo na uongozi wa hospitali ndipo jitihada zilipoanza kuchukuliwa kwa kuwaita wataalamu mbalimbali wa ubongo, figo n.k siku ya jumatano. Mtoto alifariki siku ya alhamisi tarehe 19/08/2010 bila ya kuamka tangu jumamosi aliyofanyiwa upasuaji.

Kinachosikitisha ni namna hawa watu walivyolichukulia hili jambo kirahisi bila ya wao kuzingatia uhai na maisha ya mtu. Ninachoweza kusema ni uzembe tu uliofanyika vinginevyo wangetaka wangeweza kuokoa maisha ya mtoto huyu. ninaomba wahusika wizara ya afya waiangalie hospitali hii kwa kuwa malalamiko ya watu kupoteza maisha hospitalini hapo kwa uzembe yamekuwa mengi.

Mwenyezi mungu aiweke roho ya marehemu peponi.

kazi njema

mdau

source :MICHUZI
 
Kwakweli hiki ndicho kinachitwa uzembe wa madaktari, sijui tunatoka wapi na tunaelekea wapi, ni masikitiko kila kukicha.
Mungu ailaze roho ya kijana hutu mahali pema peponi.
 
ukiona mtu anatibiwa kwa hisia na si vipimo vya kitaalamu...KIMBIA

Tunahitaji kuwa na sheria ya kupiga vita uzembe kama vile medical malpractice na kuhakikisha daktari anakata bima ya kumnusuru na hizi kesi za kusababisha maumivu au ata kifo.
 
Mimi
mwezi April,nilipoteza Dada yangu ambaye tulimpeleka hapo hospitali anatembea mwenyewe ilikua Alhamisi na usiku wa kuamkia Jumapili nilipigiwa simu kuwa moyo ulisimama ghafla akifanyiwa operation ya dialysis. Hii hospitali inamatatizo makubwa hatujajua kuna nini hapa.
 
Pole sana, nafikiri kuna haja ya hawa watu kufungia na kufanyiwa uchunguzi wa kina.
 
Inapaswa KUSIMAMISHWA haraka, kabla hatujaendelea kupoteza watu wengi zaidi. Mwandikieni Waziri wa Afya barua! HARAKA!
 
Nakubali Regency kuna uzembe fulani hapo. Namfahamu mgonjwa fulani wa figo (RIP), alifanyiwa dialisis hapo kwa muda wa mwezi tuu, akajikuta ameambukizwa magonjwa ya ajabu, akapelekwa India kufanyiwa transplant, kufika kule, akaambiwa it was too late, dialisis waliokuwa wakimfanyia ilikuwa na contermination, there was no way back, alirudishwa kwenye sanduku!.

Nikatamani ningekuwa na uwezo, kufanya utafiti, ni wagonjwa wangapi wa dialisis ya Regency huwa wanasurvive.

Dialysis ni kubadilisha damu yote kwenye mwili wa binadamu kwa kutumia mashine maalum ili kuisafisha na kuirudisha mwilini.

Hata baada ya kutokea vifo vinavyosababishwa na uzembe, madaktari, wanalindana. Hii issue ya kijana, inaenekana walizidisha dose ya anaesthesia. Postmortem wataandika, mortar brain failure, iliyopunguza heart pulse iliyopunguza blood supply kwenye brain iliyosababisha brain demage na hivyo kusimamisha figo na kusababisha kifo. Ukichunguza zaidi, unaweza ukakuta hata hiyo appendix haikuwa chanzo!.
 
Mkuu Pasco, kuna aja ya kuja na sheria zinazomfanya muhanga [Victim] wa mambo ya medical au any other professional malpractice kuwashtaki hawa madaktari et al.
 
usithubutu kwenda kufanya dialysis hapo Regency..Aga Khan wao wanaishi kwa Oxygen...kila 1 hr wanakuchaji laki moja. Si mnakumbuka mtoto wa Mengi alikufa kwa kukosa Oxygen hospitalini?
 
AgaKhan siku hizi panaitwa hotel...Tumaini na Regency ndio hivyo. Wakuu hivi kwa sasa ni hospital gani ambayo ni afadhali kuikimbilia? Maana muhimbili, Mwananyamala na wale ndugu zao wengine wote tunajua hali ilivyo. Na mgombea mmoja amesema atahakikisha anapandisha daraja hospitali kadhaa! Sijui hiyo inatufikisha wapi

depends na pesa zako

Kama unazo zakutosha bora uende Muhimbili uhonge upate huduma bora...lakini wale mbu ndio watakufaidi
 
haya mambo ya kukimbilia hospital za kulipia yatawaponza watanzania wengi. Mie bora nijibanze pale Muhimbili kuliko kwenda huko. Ukiona vipi bora hata uende hospitali za misheni mikoani kuliko kwenda hizo hospitali. (Ndanda Mission, St. Francis Ifakara, Ilelmbula Mission, nk.)
 
agakhan siku hizi panaitwa hotel...tumaini na regency ndio hivyo. Wakuu hivi kwa sasa ni hospital gani ambayo ni afadhali kuikimbilia? Maana muhimbili, mwananyamala na wale ndugu zao wengine wote tunajua hali ilivyo. Na mgombea mmoja amesema atahakikisha anapandisha daraja hospitali kadhaa! Sijui hiyo inatufikisha wapi

si kosalangu herbal clinic
 
Hali ni mbaya jamani kwenye Hospitali zetu, nakumbuka nikiwa chuoni like 2 yrs ago tulimpoteza mwenzetu ambaye alikuwa na maleria kali wakampiga kwinini bila kushusha homa na kumcheki presha. alikuwa kichwa sana drsni.
 
Back
Top Bottom