SoC02 Hospitali za Rufaa kuwaachia majukumu yote ya kitabibu wanafunzi wa udaktari pasipo usimamizi wa kutosha - chanzo cha vifo vingi

SoC02 Hospitali za Rufaa kuwaachia majukumu yote ya kitabibu wanafunzi wa udaktari pasipo usimamizi wa kutosha - chanzo cha vifo vingi

Stories of Change - 2022 Competition

cupvich

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
408
Reaction score
247
UTANGULIZI
Nikiwa wodini nauguza mgonjwa wangu katika moja ya hospitali kubwa ya Rufaa nchini, Nilimsikia daktari mmoja akitumia lugha ya kiingereza kuwaambia wanafunzi wanao somea udaktari ambao walikuwa wakitoa huduma kwa mgonjwa aliyekuwa kitanda cha pembeni na alicho mgonjwa wangu maneno haya nanukuu "MMEKOSEA, HAMKUTAKIWA KUMCHOMA SINDANO HIYO". Hakika nafsi yangu iliogopa sana, Nilihisi kana kwamba amefanyiwa mgonjwa wangu, hivyo niliwaza iwapo angekuwa ni mgonjwa wangu na nimesikia maneno yale ya daktari ningechukua hatua gani. Ilinifanya kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Mgonjwa yule tokea siku ile kwasababu nilikuwa pale kwa wiki moja nikimuuguza mgonjwa wangu, Baada ya siku moja nilipewa taarifa kuwa Mgonjwa yule alifariki Dunia.

Hospitali zetu za rufaa zimekuwa kimbilio kwa walio wengi katika suala zima la matibabu, hii ni kutokana na kuaminika kwamba zina wataalamu wa kutosha. Lakini pia zinaweza kutoa huduma za kibingwa. Kwa hapa kwetu Tanzania tumebarikiwa kuwa na Hospitali za rufaa za mikoa lakini pia tuna hospitali za rufaa za kanda kama vile HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA KCMC, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO pamoja na hospitali kubwa ya taifa MUHIMBILI. Hospitali hizi za rufaa za kanda zina Vyuo ambavyo hutoa mafunzo kwa wataalamu wa Afya kama vile madaktari, manesi na wafamasia. Vyuo hivyo ni MUHAS,BUGANDO, MCHAS, na KCMCo pamoja na vyuo vingine vinavyopatikana katika hospitali za mikoa na Hospitali zingine za Binafsi na mashirika ya dini.

Wanafunzi hawa wa udaktari walioko wafunzoni wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya mazoezi kwa vitendo katika hospitali zetu jambo ambalo ni Zuri kwani linawajenga na kuwaimarisha vyema katika Sekta hiyo muhimu ya afya. Lakini pia wamekuwa wakirahisisha utoaji wa huduma za afya kwa kuongeza wahudumu wa afya katika hospitali zetu ukizingatia kwamba vituo vingi vya afya pamoja na hospitali zetu Bado zina changamoto kubwa ya upungufu wa wataalamu wa Afya. Kwa ujumla wanataalamu hawa walioko mafunzoni hususani madaktari wanafanya kazi kubwa.

TATIZO LINAANZIA HAPA.
Kwa Bahati mbaya, hospitali zetu zimewaamini Wanafunzi hawa walioko vyuoni kupitiliza kiasi cha Kuwapangia Zamu za kuwaona wagonjwa pasipo usimamizi wa daktari mzoefu na kufanya matibabu kwa mgonjwa hata kwa wagonjwa ambao wako katika hali mbaya. Jambo ambalo ni Hatarishi kwa afya ya mgonjwa. Hii imesababisha kutokea kwa vifo vingi kutokana na kwamba wanafunzi hawa wa afya hawajawa bado na Utaalamu wa kutosha katika kutoa huduma za afya kwa kiwango kinachostahili ukilinganisha na madaktari wazoefu.

CHANZO CHA TATIZO.
Ni kweli kwamba siku hizi Teknolojia imerahisisha ufanyaji wa kazi katika hospitali zetu.Teknolojia imechukua nafasi kubwa sana katika utoaji wa huduma katika vituo vya afya na Hospitali, na ndio maana utakuta Daktari anayeingia katika zamu ya usiku anaweza kumfahamu vizuri mgonjwa aliyelazwa wodini, matibabu aliyoyapata na matibabu anayotakiwa kuyapata hivyo kumrahisishia kuendeleza matibabu kwa mgonjwa. Lakini ukuaji huu wa Teknolojia usiwe Sababu ya kuwaachia majukumu yote wanafunzi wa udaktari walioko Vyuoni kwani waliowengi bado hawajapata maarifa ya kutosha katika kutoa huduma za kitabibu. Lakini pia wingi wa hawa wanafunzi katika hospitali zetu kisiwe kigezo cha madaktari wazoefu na wenye majukumu ya kutoa huduma za afya kusahau wajibu wao wa kuwahudumia wagonjwa. Wengi wa hawa wanafunzi wa udaktari wamekuwa wakitoa huduma kwa hisia ili tu kukamilisha matakwa ya kozi wanazosomea ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi kwa vitendo. na hivyo kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

ATHARI ZITOKANAZO NA TATIZO HILI.
Utakubaliana nami kuwa Siku zote Mwanafunzi atabaki kuwa mwanafunzi, hata kama ni mwanafunzi wa udaktari mwaka wa nne au wa tano. Na sifa mojawapo aliyonayo mwanafunzi ni kutokujiamini kwa asilimia mia moja, hivyo kupelekea kufanya jambo kwa Jazba na Mihemko ilimradi tu kukamilisha takwa fulani. Hivyo nilazima uongozi wa hospitali zetu uwachukulie wataalamu hawa wa afya kama wanafunzi na kuwasimamia katika huduma zote za kitabibu katika hospitali zetu kwa manufaa mapana ya mgonjwa na mtoa huduma.

Kutokana na kuwatumia madaktari mafunzoni katika hospitali zetu hizi za rufaa, Huduma katika hospitali hizi zimekuwa zikishuka kadiri siku zinavyokwenda licha ya serikali Kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika hospitali hizi, ikiwa ni pamoja na Ununuzi wa vifaa vya kutolea huduma za afya, Uongezaji wa majengo ya kutolea huduma za afya na kuongeza watumishi wa afya. Jambo hili si zuri kwasababu linapunguza imani kwa wananchi hivyo kutumia gharama kubwa kupata matibabu katika hospitali za binafsi.

Usalama wa mgonjwa awapo hospitalini ni muhimu sana. Muda mwingi mgonjwa hubaki na wataalamu wa afya kwa ajili ya matibabu. Hivyo ndugu jamaa na marafiki huamini kuwa Daktari au mtaalamu yeyote wa afya ana nafasi kubwa katika kuokoa maisha ya Mgonjwa. Wote tunaamini kwamba mtaalamu yeyote wa afya anatakiwa awe na ujuzi wa kutosha katika kumhudumia mgonjwa ili kuokoa maisha yake. Iwapo mtaalamu huyo wa afya atakosa ujuzi na maarifa ya kutosha maisha ya mgonjwa yatakuwa hatarini, na hata kuwa ametekeleza majukumu yake ipasavyo. Lakini pia kukosekana kwa maarifa ya kutosha kutamfanya mtaalamu huyo kushindwa kujiamini katika kazi yake.

HITIMISHO
Madaktari walioko mafunzo pamoja na wataalamu wengine wa afya wanafanya kazi kubwa na nzuri katika kurahisisha utoaji wa huduma katika hospitali zetu, Lakini Uongozi wa hospitali zetu kwa kushirikiana na vyuo vinavyotoa wataalamu hawa wa afya hauna budi Kuwasimamia ipasavyo wakati wote wanapotoa huduma kwa wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuwapanga pamoja na Madaktari wazoefu ili kuifanya huduma yao ya matibabu iwe salama na yenye kuleta matumaini kwa mgonjwa na Kuepukana na Vifo vinavyotokana na UZEMBE wa watoa huduma za afya.

Wenu
Mwita Ngutunyi Mohono
S.l.p 237 Mbarali- MBEYA
0762185894
mwitangutunyimohono@gmail.com
 
Upvote 49
Hakuna mwananfunzi anaye achiwa mgonjwa hospital.
Ni kweli mwana jukwaa.nimepita katika hospitali zetu nyingi hususan zile zenye vyuo vya afya na katika utafiti wangu mdogo nimegundua wanafunzi wengi wanaachiwa majukumu na madaktari walioko zamu. Hii inasababisha mgonjwa kuandikiwa dawa ambazo wakati mwingine daktari anaye ingia zamu kuzikataa na kuandika zingine. Jambo hili lipo na linahatarisha sana huduma za afya katika hospitali zetu.
 
Endeleza utafiti huwe mkubwa maana aujashibisha andiko lako kututhibitisha kuwa kuna mwananfunzi asiye sajiliwa kaachiwa mgonjwa kwa sababu hospital zote zenye vyuo ni za serikali.

Labda wewe umeongezea chumvi au maneno yako kwamba mwananfunzi alipo kuwa na daktari ambaye ni mwalimu wake kwa bahati mbaya alikosea dawa aliyo ambiwa na dokta ambaye alikuwa anamtibu mgonjwa alafu mwananfunzi wake akakosea dawa na siyo kaachiwa mgonjwa kwa sababu mwanafunzi ajui chochote.

Alafu ukitaka kujua kwa nini wananfunzi wa udaktari wanakuwa karibu sana maeneo ya matibabu nenda ukajiunge na hivyo vyuo usome ili ujue kwanini wananfunzi wanakuwa karibu na madaktari kwenye kutibu wagonjwa lakini hakuna mwananfunzi anaye achiwa mgonjwa kaka.
 
Wanafunzi wenyewe wa udaktari mgogoro tupu. Kila sekta Tanzania imeoza. Sijui tulikosea wapi. Si uinjinia, si biashara siyo IT, lakini vyuo vyetu ni chaka la kuzalisha wazembe. Kuna jamaa nawajua wansoma udaktari lakini hata ukiongea nao maongezi ya kwaida tu wako empty vichwani.
 
Nakuelewa fika mwana jukwaa mwenzangu. Nimefanya utafiti na ndio maana nimeamua kuandika andiko hili. Jambo kubwa ambalo unatakiwa kulifahamu ni kwamba SI PINGI hata kidogo utaratibu wa madaktari mafunzoni kutoa huduma za afya kwasababu ni njia mojawapo ya wao kusoma kwa vitendo ni kama kwa walimu, wahandisi na nk. na ndio maana katika andiko langu nimepongeza kazi kubwa wanayoifanya ya kurahisisha utoaji wa huduma za afya. Lakini pia nimesisitiza kuwa wao ni muhimu sana kwasababu wanaongeza watumishi wa afya katika hospitali zetu.

Lengo kuu la andiko langu nikuonyesha kwamba pamoja na wanafunzi hao wa udaktari kufanya kazi kubwa na ya maana. Mamlaka za hospitali zetu hizi za rufaa zisiwaachie majukumu Asilimia zote katika kuwahudumia wagonjwa pasipo usimamizi wa daktari mzoefu. Kwasababu watu wengi wanalalamikia Huduma duni katika hospitali zetu hizi licha ya serikali yetu kuwekeza kiasi kikubwa cha pesa.

Jaribu nawe kufanya utafiti katika hizo hospitali kubwa zenye vyuo utakubaliana nami kuwa wengi wa wanafunzi hawa ndio wanatoa huduma za afya mawodini.
 
Wanafunzi wenyewe wa udaktari mgogoro tupu. Kila sekta Tanzania imeoza. Sijui tulikosea wapi. Si uinjinia, si biashara siyo IT, lakini vyuo vyetu ni chaka la kuzalisha wazembe. Kuna jamaa nawajua wansoma udaktari lakini hata ukiongea nao maongezi ya kwaida tu wako empty vichwani.
Asante mwana jukwaa mwenzangu. Nadhani ipo haja ya serikali kupitia upya mfumo wa elimu nchini ili tuweze kupata wataalamu wazuri katika fani mbalimbali ikiweno kada hii muhimu ya afya. Haiwezekani daktari amalize miaka mitano pamoja na internship halafu ashindwe kutoa huduma stahiki. Nadhani kuna sehemu tunakosea.
 
Baada ya kuuguza katika hospital moja ya rufaa ilinibidi nichore upya ramani ya maisha na kifaumbele Cha kwanza kikawa pesa,Cha pili pesa,tatu pesa
Sio wewe tu mwanajukwaa. Tunaweza kujiuliza sote kwamba. Nini kinasababisha watu wengi kupeleka wagonjwa kupata matibabu katika hospitali za binafsi zenye gharama kubwa licha ya serikali kuwekeza kiasi kikubwa katika hospitali zetu hizi za rufaa ikiwa ni pamoja na kuongeza vifaa vya utoaji huduma, kuongeza majengo na watumishi.

Utagundua kwamba watu walio wengi wanakosa imani na hospitali hizi kutokana na namna zinavyotoa huduma. Ikiwa na pamoja na kuwatumia hao wanafunzi walioko vyuoni bila usimamizi wa kutosha. Kwahiyo ipo haja ya wizara ya afya kuliangalia jambo hili.
 
Wanafunzi wenyewe wa udaktari mgogoro tupu. Kila sekta Tanzania imeoza. Sijui tulikosea wapi. Si uinjinia, si biashara siyo IT, lakini vyuo vyetu ni chaka la kuzalisha wazembe. Kuna jamaa nawajua wansoma udaktari lakini hata ukiongea nao maongezi ya kwaida tu wako empty vichwani.
Ongea nao mambo ya taaluma yao hayo ya siasa hawayajui...😂😂😂
 
Yaaani hapa unakoseaa!! Sisi wananchi ndio tunaweza toa ushahidi!! Wamejaa tele, na ndio wanafanya kazi!! Mimi ni muathirikaa
Asante mwanajukwaa kwa kuwa shahidi wa hili. Kwakweli kama halijakupata au hujashuhudia ni vigumu kuelewa. Jambo kubwa hapa ni wizara ya afya kupitia management za hospitali zetu kuchukua hatua..kwakweli inakatisha Tamaa na kuwafanya wananchi kuogopa hospitali zetu hizi ambazo ndizo zinatakiwa kuwa kioo.
 
Mwandishi unaandika hii makala lakini bado hujafikiria na kuona umuhimu wa vitendo katika mafunzo kwa upande wa afya.
Ungekuwa Mtu wa afya au mwanao anasomea Afya, usingeandika ulichoandika usichona utafiti nacho!
Mwandishi waombe radhi uliowagusa
 
Hajasema wasifanye mazoezi kwa vitendo,mleta mada anachopinga ni kuwaachia majukumu peke yao bila uangalizi wa daktari mzoefu/aliyeko kazini
 
Mwandishi unaandika hii makala lakini bado hujafikiria na kuona umuhimu wa vitendo katika mafunzo kwa upande wa afya.
Ungekuwa Mtu wa afya au mwanao anasomea Afya, usingeandika ulichoandika usichona utafiti nacho!
Mwandishi waombe radhi uliowagusa
Kama utasoma andiko langu mwana jukwaa utagundua kuwa Nimewaelezea madakrtari mafunzoni kama watu MUHIMU sana katika utoaji huduma za afya katika hospitali zetu.

Na kwakweli Nina unga mkono wao kufanya mazoezi ya vitendo katika hospitali zetu kwasababu.licha ya kufanya mazoezi ya vitendo wana saidia sana katika UTOAJI wa huduma za afya na napendekeza waendelee kwasababu hospitali zetu hazina watumishi wa kutosha.

HOJA yangu mwana jukwaa ni kwamba wanapokuwa katika hospitali zetu hizi BASI WASIACHIWE MAJUKUMU YOTE YA MATIBABU KWA WAGONJWA BILA USIMAMIZI WA KUTOSHA...kwasababu unakuta bado hawajaiva vya kutosha. Mwanafunzi yuko mwaka wa tatu tu anapewa zamu..HII SI SAWA.

Na malalamiko mengi yanatoka kwa wananchi wenyewe, jambo ambalo si sawa kwasababu serikali yetu imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kupitia kwa Raisi wetu mpendwa Mama SAMIA.
 
Hospital tena za rufaa wanafunzi wanaachiwa wagonjwa jambo likiwashinda au mgonjwa akichachamaa ndo unamuona daktari na viongozi wa Hospital wanakuja!!
Sahihi kabisa mwanajukwaa. Sasa hii si sawa. Madaktari pamoja na watumishi wote walioajiriwa katika hospitali wanafanya kazi kubwa sana na tunatambua mchango wao mkubwa. Lakini isifike mahali wakawaachia majukumu yao yote wanafunzi wa udaktari PASIPO USIMAMIZI WA KUTOSHA.
 
Back
Top Bottom