SoC02 Hospitali za Rufaa kuwaachia majukumu yote ya kitabibu wanafunzi wa udaktari pasipo usimamizi wa kutosha - chanzo cha vifo vingi

Stories of Change - 2022 Competition

cupvich

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
408
Reaction score
247
UTANGULIZI
Nikiwa wodini nauguza mgonjwa wangu katika moja ya hospitali kubwa ya Rufaa nchini, Nilimsikia daktari mmoja akitumia lugha ya kiingereza kuwaambia wanafunzi wanao somea udaktari ambao walikuwa wakitoa huduma kwa mgonjwa aliyekuwa kitanda cha pembeni na alicho mgonjwa wangu maneno haya nanukuu "MMEKOSEA, HAMKUTAKIWA KUMCHOMA SINDANO HIYO". Hakika nafsi yangu iliogopa sana, Nilihisi kana kwamba amefanyiwa mgonjwa wangu, hivyo niliwaza iwapo angekuwa ni mgonjwa wangu na nimesikia maneno yale ya daktari ningechukua hatua gani. Ilinifanya kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Mgonjwa yule tokea siku ile kwasababu nilikuwa pale kwa wiki moja nikimuuguza mgonjwa wangu, Baada ya siku moja nilipewa taarifa kuwa Mgonjwa yule alifariki Dunia.

Hospitali zetu za rufaa zimekuwa kimbilio kwa walio wengi katika suala zima la matibabu, hii ni kutokana na kuaminika kwamba zina wataalamu wa kutosha. Lakini pia zinaweza kutoa huduma za kibingwa. Kwa hapa kwetu Tanzania tumebarikiwa kuwa na Hospitali za rufaa za mikoa lakini pia tuna hospitali za rufaa za kanda kama vile HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA KCMC, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO pamoja na hospitali kubwa ya taifa MUHIMBILI. Hospitali hizi za rufaa za kanda zina Vyuo ambavyo hutoa mafunzo kwa wataalamu wa Afya kama vile madaktari, manesi na wafamasia. Vyuo hivyo ni MUHAS,BUGANDO, MCHAS, na KCMCo pamoja na vyuo vingine vinavyopatikana katika hospitali za mikoa na Hospitali zingine za Binafsi na mashirika ya dini.

Wanafunzi hawa wa udaktari walioko wafunzoni wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya mazoezi kwa vitendo katika hospitali zetu jambo ambalo ni Zuri kwani linawajenga na kuwaimarisha vyema katika Sekta hiyo muhimu ya afya. Lakini pia wamekuwa wakirahisisha utoaji wa huduma za afya kwa kuongeza wahudumu wa afya katika hospitali zetu ukizingatia kwamba vituo vingi vya afya pamoja na hospitali zetu Bado zina changamoto kubwa ya upungufu wa wataalamu wa Afya. Kwa ujumla wanataalamu hawa walioko mafunzoni hususani madaktari wanafanya kazi kubwa.

TATIZO LINAANZIA HAPA.
Kwa Bahati mbaya, hospitali zetu zimewaamini Wanafunzi hawa walioko vyuoni kupitiliza kiasi cha Kuwapangia Zamu za kuwaona wagonjwa pasipo usimamizi wa daktari mzoefu na kufanya matibabu kwa mgonjwa hata kwa wagonjwa ambao wako katika hali mbaya. Jambo ambalo ni Hatarishi kwa afya ya mgonjwa. Hii imesababisha kutokea kwa vifo vingi kutokana na kwamba wanafunzi hawa wa afya hawajawa bado na Utaalamu wa kutosha katika kutoa huduma za afya kwa kiwango kinachostahili ukilinganisha na madaktari wazoefu.

CHANZO CHA TATIZO.
Ni kweli kwamba siku hizi Teknolojia imerahisisha ufanyaji wa kazi katika hospitali zetu.Teknolojia imechukua nafasi kubwa sana katika utoaji wa huduma katika vituo vya afya na Hospitali, na ndio maana utakuta Daktari anayeingia katika zamu ya usiku anaweza kumfahamu vizuri mgonjwa aliyelazwa wodini, matibabu aliyoyapata na matibabu anayotakiwa kuyapata hivyo kumrahisishia kuendeleza matibabu kwa mgonjwa. Lakini ukuaji huu wa Teknolojia usiwe Sababu ya kuwaachia majukumu yote wanafunzi wa udaktari walioko Vyuoni kwani waliowengi bado hawajapata maarifa ya kutosha katika kutoa huduma za kitabibu. Lakini pia wingi wa hawa wanafunzi katika hospitali zetu kisiwe kigezo cha madaktari wazoefu na wenye majukumu ya kutoa huduma za afya kusahau wajibu wao wa kuwahudumia wagonjwa. Wengi wa hawa wanafunzi wa udaktari wamekuwa wakitoa huduma kwa hisia ili tu kukamilisha matakwa ya kozi wanazosomea ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi kwa vitendo. na hivyo kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

ATHARI ZITOKANAZO NA TATIZO HILI.
Utakubaliana nami kuwa Siku zote Mwanafunzi atabaki kuwa mwanafunzi, hata kama ni mwanafunzi wa udaktari mwaka wa nne au wa tano. Na sifa mojawapo aliyonayo mwanafunzi ni kutokujiamini kwa asilimia mia moja, hivyo kupelekea kufanya jambo kwa Jazba na Mihemko ilimradi tu kukamilisha takwa fulani. Hivyo nilazima uongozi wa hospitali zetu uwachukulie wataalamu hawa wa afya kama wanafunzi na kuwasimamia katika huduma zote za kitabibu katika hospitali zetu kwa manufaa mapana ya mgonjwa na mtoa huduma.

Kutokana na kuwatumia madaktari mafunzoni katika hospitali zetu hizi za rufaa, Huduma katika hospitali hizi zimekuwa zikishuka kadiri siku zinavyokwenda licha ya serikali Kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika hospitali hizi, ikiwa ni pamoja na Ununuzi wa vifaa vya kutolea huduma za afya, Uongezaji wa majengo ya kutolea huduma za afya na kuongeza watumishi wa afya. Jambo hili si zuri kwasababu linapunguza imani kwa wananchi hivyo kutumia gharama kubwa kupata matibabu katika hospitali za binafsi.

Usalama wa mgonjwa awapo hospitalini ni muhimu sana. Muda mwingi mgonjwa hubaki na wataalamu wa afya kwa ajili ya matibabu. Hivyo ndugu jamaa na marafiki huamini kuwa Daktari au mtaalamu yeyote wa afya ana nafasi kubwa katika kuokoa maisha ya Mgonjwa. Wote tunaamini kwamba mtaalamu yeyote wa afya anatakiwa awe na ujuzi wa kutosha katika kumhudumia mgonjwa ili kuokoa maisha yake. Iwapo mtaalamu huyo wa afya atakosa ujuzi na maarifa ya kutosha maisha ya mgonjwa yatakuwa hatarini, na hata kuwa ametekeleza majukumu yake ipasavyo. Lakini pia kukosekana kwa maarifa ya kutosha kutamfanya mtaalamu huyo kushindwa kujiamini katika kazi yake.

HITIMISHO
Madaktari walioko mafunzo pamoja na wataalamu wengine wa afya wanafanya kazi kubwa na nzuri katika kurahisisha utoaji wa huduma katika hospitali zetu, Lakini Uongozi wa hospitali zetu kwa kushirikiana na vyuo vinavyotoa wataalamu hawa wa afya hauna budi Kuwasimamia ipasavyo wakati wote wanapotoa huduma kwa wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuwapanga pamoja na Madaktari wazoefu ili kuifanya huduma yao ya matibabu iwe salama na yenye kuleta matumaini kwa mgonjwa na Kuepukana na Vifo vinavyotokana na UZEMBE wa watoa huduma za afya.

Wenu
Mwita Ngutunyi Mohono
S.l.p 237 Mbarali- MBEYA
0762185894
mwitangutunyimohono@gmail.com
 
Upvote 49
Kwahiyo waganga wakuu wa hizi hospitali wote hawajasoma maadili au "Ethics" za kazi ya udaktari kuwaachia madktari wanafunzi kuchoma wagonjwa sindano?

Pili, mgonjwa akiwa wodini huchomwa sindano na daktari au nesi?

Tatu, weye wafahamu vipi kuwa hao ni wanafunzi wa udaktari, pengine waweza kuwa ni wanafunzi wa chuo cha uuguzi?

Nimeuliza tu kutaka kufahamu mimi si daktari.
 
Wataalamu wa afya wanafanya kazi vizuri. Na tunawapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya. Tunatambua mchango wao mkubwa kwa Afya za watanzania.Mungu awabariki. Na nadhani wanatambua ethics za kazi zao vizuri.

Lakini wapo ambao sio waaminifu katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo either kwa kupitiwa au kwa makusudi..na kuacha majukumu yao ya Msingi.

Madaktari mafunzoni wanafanya kazi kubwa na tunatambua mchango wao. Lakini isifike mahali wakaaminiwa kupita kiasi katika hospitali zetu hizi ambazo ndizo zinatakiwa kuwa mfano.

Iwapo mgonjwa atapatiwa huduma kwa ubora unao takiwa hakuta kuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi walio wengi juu ya huduma.

SHIDA KUBWA ya hospitali zetu sasa pamoja na kuwepo kwa mifumo ya taarifa katika hospitali hizi lakini cha ajabu ndugu wasipofuatilia maendeleo ya mgonjwa hawawezi kutoboa. Mtaalamu huyu anaandika dawa mwingine anakuja anazikataa WHY???

nadhani kuna haja ya kukubali madhaifu ili kuwa bora zaidi.
 
Shida ya binadamu ni kutokukubali madhaifu yake hata kama yapo.

Hajui kuwa kuyafahamu madhaifu kuna mfanya kuwa bora zaidi.
 
Nadhani kesi yako ungeifikisha juu zaidi kwenye bodi ya usimamzi wa madaktari nchini ili wafuatilie madai yako.

Weye andika tu uzuri na utume na ueleze kwa kina ulichokiona na ushahidi wote.
 
Naomba msaada tafadhal....wap ni click...ili ni andike story yang
Ingia kweye Account yako.. utaona kwa juu sehemu imeandikwa new threads katika STORY OF CHANGES.
 
Braza umeongea point una onekana wewe ni health care.
 
Kwani ma staff huwa hawakosei?
 
Uvivu wamadaktari husika usisababishe vifo vyawatu.kufanyakaz kwamazoea hadikuleta wanafunzi kufanyamzaa kwa uhai wamtu.sisawa kabisa
 
Uvivu wamadaktari husika usisababishe vifo vyawatu.kufanyakaz kwamazoea hadikuleta wanafunzi kufanyamzaa kwa uhai wamtu.sisawa kabisa
Asante mwanajukwaa kwa mchango wako. Haina budi kwa mamlaka husika kusimamia huduma bora zinazotolewa.

NAKUOMBA UPIGE KURA YAKO KATIKA ANDIKO HILI KWA KUBOFYA SEHEMU ILIYOANDIKWA VOTE chini ya andiko hili
 
Uvivu wamadaktari husika usisababishe vifo vyawatu.kufanyakaz kwamazoea hadikuleta wanafunzi kufanyamzaa kwa uhai wamtu.sisawa kabisa
Asante mwanajukwaa kwa mchango wako. Haina budi kwa mamlaka husika kusimamia huduma bora zinazotolewa.

NAKUOMBA UPIGE KURA YAKO KATIKA ANDIKO HILI KWA KUBOFYA SEHEMU ILIYOANDIKWA VOTE chini ya andiko hili
 
Nyie nyie juzi ndo mlisema wasipewe call allowance.....! Leo mnasema ni wavivu......
 
Endelea kupitia andiko hili na kutoa maoni yako.. TAFADHARI USIACHE KUPIGA KURA YAKO KATIKA ANDIKO HILI MWANAJUKWAA.
 
Nadhani hujasoma andiko langu na kuelewa KIINI cha andiko. Tafadhari tenga muda kusoma tena. Na iwapo utashindwa kuelewa usisite kuuliza mwanajukwaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…