SoC02 Hospitali za Rufaa kuwaachia majukumu yote ya kitabibu wanafunzi wa udaktari pasipo usimamizi wa kutosha - chanzo cha vifo vingi

Stories of Change - 2022 Competition

cupvich

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
408
Reaction score
247
UTANGULIZI
Nikiwa wodini nauguza mgonjwa wangu katika moja ya hospitali kubwa ya Rufaa nchini, Nilimsikia daktari mmoja akitumia lugha ya kiingereza kuwaambia wanafunzi wanao somea udaktari ambao walikuwa wakitoa huduma kwa mgonjwa aliyekuwa kitanda cha pembeni na alicho mgonjwa wangu maneno haya nanukuu "MMEKOSEA, HAMKUTAKIWA KUMCHOMA SINDANO HIYO". Hakika nafsi yangu iliogopa sana, Nilihisi kana kwamba amefanyiwa mgonjwa wangu, hivyo niliwaza iwapo angekuwa ni mgonjwa wangu na nimesikia maneno yale ya daktari ningechukua hatua gani. Ilinifanya kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Mgonjwa yule tokea siku ile kwasababu nilikuwa pale kwa wiki moja nikimuuguza mgonjwa wangu, Baada ya siku moja nilipewa taarifa kuwa Mgonjwa yule alifariki Dunia.

Hospitali zetu za rufaa zimekuwa kimbilio kwa walio wengi katika suala zima la matibabu, hii ni kutokana na kuaminika kwamba zina wataalamu wa kutosha. Lakini pia zinaweza kutoa huduma za kibingwa. Kwa hapa kwetu Tanzania tumebarikiwa kuwa na Hospitali za rufaa za mikoa lakini pia tuna hospitali za rufaa za kanda kama vile HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA KCMC, HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO pamoja na hospitali kubwa ya taifa MUHIMBILI. Hospitali hizi za rufaa za kanda zina Vyuo ambavyo hutoa mafunzo kwa wataalamu wa Afya kama vile madaktari, manesi na wafamasia. Vyuo hivyo ni MUHAS,BUGANDO, MCHAS, na KCMCo pamoja na vyuo vingine vinavyopatikana katika hospitali za mikoa na Hospitali zingine za Binafsi na mashirika ya dini.

Wanafunzi hawa wa udaktari walioko wafunzoni wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya mazoezi kwa vitendo katika hospitali zetu jambo ambalo ni Zuri kwani linawajenga na kuwaimarisha vyema katika Sekta hiyo muhimu ya afya. Lakini pia wamekuwa wakirahisisha utoaji wa huduma za afya kwa kuongeza wahudumu wa afya katika hospitali zetu ukizingatia kwamba vituo vingi vya afya pamoja na hospitali zetu Bado zina changamoto kubwa ya upungufu wa wataalamu wa Afya. Kwa ujumla wanataalamu hawa walioko mafunzoni hususani madaktari wanafanya kazi kubwa.

TATIZO LINAANZIA HAPA.
Kwa Bahati mbaya, hospitali zetu zimewaamini Wanafunzi hawa walioko vyuoni kupitiliza kiasi cha Kuwapangia Zamu za kuwaona wagonjwa pasipo usimamizi wa daktari mzoefu na kufanya matibabu kwa mgonjwa hata kwa wagonjwa ambao wako katika hali mbaya. Jambo ambalo ni Hatarishi kwa afya ya mgonjwa. Hii imesababisha kutokea kwa vifo vingi kutokana na kwamba wanafunzi hawa wa afya hawajawa bado na Utaalamu wa kutosha katika kutoa huduma za afya kwa kiwango kinachostahili ukilinganisha na madaktari wazoefu.

CHANZO CHA TATIZO.
Ni kweli kwamba siku hizi Teknolojia imerahisisha ufanyaji wa kazi katika hospitali zetu.Teknolojia imechukua nafasi kubwa sana katika utoaji wa huduma katika vituo vya afya na Hospitali, na ndio maana utakuta Daktari anayeingia katika zamu ya usiku anaweza kumfahamu vizuri mgonjwa aliyelazwa wodini, matibabu aliyoyapata na matibabu anayotakiwa kuyapata hivyo kumrahisishia kuendeleza matibabu kwa mgonjwa. Lakini ukuaji huu wa Teknolojia usiwe Sababu ya kuwaachia majukumu yote wanafunzi wa udaktari walioko Vyuoni kwani waliowengi bado hawajapata maarifa ya kutosha katika kutoa huduma za kitabibu. Lakini pia wingi wa hawa wanafunzi katika hospitali zetu kisiwe kigezo cha madaktari wazoefu na wenye majukumu ya kutoa huduma za afya kusahau wajibu wao wa kuwahudumia wagonjwa. Wengi wa hawa wanafunzi wa udaktari wamekuwa wakitoa huduma kwa hisia ili tu kukamilisha matakwa ya kozi wanazosomea ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi kwa vitendo. na hivyo kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

ATHARI ZITOKANAZO NA TATIZO HILI.
Utakubaliana nami kuwa Siku zote Mwanafunzi atabaki kuwa mwanafunzi, hata kama ni mwanafunzi wa udaktari mwaka wa nne au wa tano. Na sifa mojawapo aliyonayo mwanafunzi ni kutokujiamini kwa asilimia mia moja, hivyo kupelekea kufanya jambo kwa Jazba na Mihemko ilimradi tu kukamilisha takwa fulani. Hivyo nilazima uongozi wa hospitali zetu uwachukulie wataalamu hawa wa afya kama wanafunzi na kuwasimamia katika huduma zote za kitabibu katika hospitali zetu kwa manufaa mapana ya mgonjwa na mtoa huduma.

Kutokana na kuwatumia madaktari mafunzoni katika hospitali zetu hizi za rufaa, Huduma katika hospitali hizi zimekuwa zikishuka kadiri siku zinavyokwenda licha ya serikali Kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika hospitali hizi, ikiwa ni pamoja na Ununuzi wa vifaa vya kutolea huduma za afya, Uongezaji wa majengo ya kutolea huduma za afya na kuongeza watumishi wa afya. Jambo hili si zuri kwasababu linapunguza imani kwa wananchi hivyo kutumia gharama kubwa kupata matibabu katika hospitali za binafsi.

Usalama wa mgonjwa awapo hospitalini ni muhimu sana. Muda mwingi mgonjwa hubaki na wataalamu wa afya kwa ajili ya matibabu. Hivyo ndugu jamaa na marafiki huamini kuwa Daktari au mtaalamu yeyote wa afya ana nafasi kubwa katika kuokoa maisha ya Mgonjwa. Wote tunaamini kwamba mtaalamu yeyote wa afya anatakiwa awe na ujuzi wa kutosha katika kumhudumia mgonjwa ili kuokoa maisha yake. Iwapo mtaalamu huyo wa afya atakosa ujuzi na maarifa ya kutosha maisha ya mgonjwa yatakuwa hatarini, na hata kuwa ametekeleza majukumu yake ipasavyo. Lakini pia kukosekana kwa maarifa ya kutosha kutamfanya mtaalamu huyo kushindwa kujiamini katika kazi yake.

HITIMISHO
Madaktari walioko mafunzo pamoja na wataalamu wengine wa afya wanafanya kazi kubwa na nzuri katika kurahisisha utoaji wa huduma katika hospitali zetu, Lakini Uongozi wa hospitali zetu kwa kushirikiana na vyuo vinavyotoa wataalamu hawa wa afya hauna budi Kuwasimamia ipasavyo wakati wote wanapotoa huduma kwa wagonjwa ikiwa ni pamoja na kuwapanga pamoja na Madaktari wazoefu ili kuifanya huduma yao ya matibabu iwe salama na yenye kuleta matumaini kwa mgonjwa na Kuepukana na Vifo vinavyotokana na UZEMBE wa watoa huduma za afya.

Wenu
Mwita Ngutunyi Mohono
S.l.p 237 Mbarali- MBEYA
0762185894
mwitangutunyimohono@gmail.com
 
Upvote 49
Karibu kwa maoni na Ushauri katika makala hii. tafadhari usiache KUPIGA KURA YAKO.
 
we km siyo kichaa umelewa.
 
Tuendelee kusoma Andiko hili nakulipigia KURA.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
USIACHE KUSOMA NA KUPIGIA KURA ANDIKO HILI.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mwandishi umeelimishwa kwa Namna nyingi jinsi staff na utaratibu wa hospital ulivyo ila umegoma kuelewa.

Kwasababu umeegemea upate kura Basi kwa kuwa unataka Basi tukuache na msimamo wako lkn utaratibu Tayari umepewa huko juu.
Ni wazi kuwa wkt unaandika andiko hili hukuwa na taarifa sahihi yupi Ni mwanafunzi wa chuo yupi Ni intern na tofauti za majukumu yao ni zipi?

Umeambiwa mwanafunzi wa chuo kamwe haachiwi majukumu makubwa ya kutoa uamuzi kwa afya ya mgonjwa lkn bado umezidi kuufanya Moyo wako kuwa mgumu usipokee hayo maelekezo ni wazi andiko lako limekosa sifa ya kuwepo hapa.
Hivyo Ni Rasmi kuwa andiko liliandikwa bila uelewa mpana
 
Nadhani hujasoma andiko langu. Tafadhari soma tena ili upate ujumbe niliokusudia mwana JF.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Ndugu yangu mtoa mada hongera sana kwa kuleta uzi wako hapa na wachangiaji wameeleza mambo mengi.

Yangu ni haya

1. Nikuhakikishie kuwa hata siku moja mwanafunzi wa Udaktari hawezi kufanya maamuzi yoyote ya kumtibu Mgonjwa bila uwepo wa Seniors. HUO UTAMADUNI HAUPO,

MAELEKEZO YA KIPI MGONJWA AFANYIWE HUANDIKWA kwenye faili la Mgonjwa.. na anayeruhusiwa kufanya hivyo ni Registered Medical Practitioner. Pamoja na kuwa huduma zetu za afya zina mapungufu mengi lakini hatujafikia hatua hiyo.

Huenda ulisikia kauli hiyo kutoka kwa huyo Senior lakini ilikuwa ni lugha ya mazingira hayo ambayo mtu baki asingeweza kuielewa.

NOTE: Kwenye tertiary hospital ulizozungumzia wapo Maprofesa, Super specialists, Specialists, Residents (Madaktari wanaosoma shahada ya pili), Registrar's (Medical Officers), Intern Doctors na Medical students.

Katika kufundisha hawa wanafunzi zipo Scenario nyingi ambazo zinaendana na mazingira hayo... Kuna kutukanwa mbele za wagonjwa na n.k n.k lakini nikupe mfano huu chini.

SPECIALIST (SP) - Tunaanza round yetu muda huu.. naomba kila Mgonjwa tutakayemuona awe anafahamika na Medical student, Intern Doctor, Registrar na Residents.

-haya huyu ni Mgonjwa wa nani?

Medical student 1 (MS1) - Huyu ni wangu Chief.

SP - Ok... Tupe historia yake na matibabu yake.

Hapo MS1 ameshaongea na Mgonjwa na kuandaa historia yake, kumfanyia uchunguzi na baadae ku_plan matibabu yake. Hivyo atasoma mwanzo hadi mwisho wa yale yote aliyofanya.

Atasikilizwa, ataulizwa maswali na kurekebishwa..

Katika kurekebishana utaweza kusikia kauli Kama... KWANINI UMEMPATIA HIYO DAWA?
KWA MATIBABU HAYO TAYARI UMEMUUA MGONJWA.. na kauli zingine za kufanana na hizo.. lakini haimanishi kuwa hao wanafunzi wanakuwa wametoa matibabu hayo kwa Mgonjwa... Hiyo historia ya Mgonjwa anakuwa ameiandika pembeni kwenye karatasi zake. Sasa ni rahisi sana kwa mtu ambaye hana exposure kufikiria kuwa tayari mwanafunzi keshatoa dawa kwa Mgonjwa.

2. Intern Doctor ana temporary license ya kupractice lakini anakuwa bado yupo mafunzoni.. kwa bahati mbaya sana Senior Doctors wamekuwa wakiwaacha wenyewe wapambane na wagonjwa.. hi siyo sahihi japokuwa pia Kuna challenge kubwa ya human resources kukabiliana na changamoto hiyo.
 
daaah sure
watatuua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…