Hot pot family tukutane hapa miaka (25-30s)

Hot pot family tukutane hapa miaka (25-30s)

ubuntuX

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
1,977
Reaction score
2,200
Kwa wale vijana wote tulio na umri kuanza miaka 25 na kuendelea lakini bado tunaishi kwa wazazi na ndugu zetu tukutane hapa

Hizi ni hot pot family, yaani kijana unakuepo kwenu licha ya umri kukutupa mkono, huna kazi wala kipato chochote lakini maisha yanasonga tu kwa kufunua hot pot iliyojaa vyakula vizuri na vitamu kwa kupitia jasho la mtu mwingine

Ni changamoto zipi tunazipitia?

1 shikamoo ni jadi ili uweze kuendelea kufunua hot pot

2 msosi ni wa kengele, lazima ufuate ratiba ya muda wa kula yaani hata kama unashughuli zako lazima ufuate time ya kula

3 Utakula chakula hata usichokihitaji (penda) zaidi wewe utakachofunua ndio hiko lazima ule

Share challenge unazokutana nazo huko kwenu ewe mkuu ambayebado unafunua hot pot na wadogo zako ilhali umri umekutupa mkono
 
Changamoto kubwa kwangu ni hizi aiseee..
..Naambiwa ninatonge kubwa
..Nakomba mboga
Nakula harakaharaka
..Marufuku kunywa mchuzi..
Lazima umuachie mdogo wako chakula..

Bado kuna habari kinga haimalizi hamu, Bado kuna hatari mpenzi ukimwacha na hamu.
-Mond-
 
Dah.... Sasa kama 25 - 30s bado mhot pot.... Life utaanza lini? [emoji15] [emoji15]

Sent from my Osborne II using JamiiForums Mobile App
 
Back
Top Bottom