Hot story

Hot story

Maskini mtoto wa mwanajeshi, umekutana na mjeshi ngoja tuone
 
*****SORY MADAM*****(12)

AGE…………………………………18+

ILIPOISHIA
Nikajihisi mwili mzimwa kupoteza nguvu kutokana na maelezo ya mama na moja kwa moja hisia za baba niliye naye sasa hivi si baba yangu zikaanza kuutawala moyo wangu na kujikuta nikiwa mapigo ya moyo yakianza kunienda kwa kasi hadi na kwa maumivu ya kifua yanayotokana na jeraha la risasi yakanisababishai kizungu zungu kikali kilichonipelekea kujilaza kwenye kochi na nikaanza kuliona giza kubwa likitawala macho yangu kama ilivyokuwa siku niliyo pigwa rasasi na Manka

ENDELEA
Nikafumbua macho yangu na kujikuta nikiwa nimelala kwenye sofa jengine lililopo sebleni huku mama akiwa pembeni yangu pamoja na mzee mmoja ambaye nilikuwa nikimuonaga akija kumtibu mama kipindi akipandwa na presha.Mama akabaki akinitazama huku sura yake ikiwa haina tabasamu wala huzuni
"Kijana unajisikiaje?"
"Afadhali kidogo"
"Kwa sindano niliyo kuchoma itakusaidia na utakuwa sawa kwani ni mstuko mdogo uliupata"
"Eddy nikuletee chakula mwanangu?"
"Ehhee ila usinitilie chakula kingi"
"Inakubidi ule ili nguvu zikurudie mwanangu wewe ujioni mwili ulivyo isha tofauti na ulivyokuwa ukienda shule"
"Sawa mama ila chakula kidogo kitanitosha"

Mama akaondoka sebleni na kuelekea kwenye meza ya chakula na kunipakulia chakula na kurudi nacho nilipo kaa
"Haya nyanyuka sasa nikulishe"
"Mmmm mama nitakula mwenyewe"
"Sawa"
"Muheshimiwa naona hali ya mwanao sasa imekuwa nzuri ngoja niwaache"
"Dokta mbona unakimbia wakati chakula kipo mezani?"
"Muheshimiwa yaani pale uliponipigia simu nilikuwa mezani ninakula kwahiyo hapa nipo sawa"
'"Jamani dokta kaa basi ule hata vijiko viwili vitatu"
"Muheshimiwa hapa ni sawa na nyumbani kwahiyo siku yoyote nitakuja kula tena na sasa hivi upo wizara yetu ya afya basi ninajisikia faraja kwa hilo yaani ni zaidi ya kula"
"Sawa ila na wewe siku utanialika kwako alafu sinto kula"
"Muheshimiwa sasa huyo yatakuwa ni malipizo kwani si mara nyingi huwa ninakula chakula hapa…….ila nimekumbuka kitu muheshimiwa"
"Kitu gani?"
"Unajua muheshimiwa Raisi alipo kuhamishia kutoka uwaziri wa maliasili na utalii na kuwa waziri wa afya nikaona kidogo kile kilio chetu kitakuwa kimesikika kutokana nitakuwa na fursa ya kuzungumza na wewe pamoja"
"Kilio gani Dokta Amdanil?"
"Mama kwani umehamishwa wizara?"
"Mwanangu siku zote ulikuwahujui?"
"Sijui kwani shule kwenyewe hata TV yenyewe hatutizami?"
"Ehee makubwa hayo sasa ni kwanini hamtizami TV?"
"Waalimu wanatubania"
"Mwanangu siku hizi unakiswahili cha kiuni kubaiwa ndio nini?"
"Hawataki"
"Eheee dokta endelea mwaya kwani huyu mtu akianza kuzungumza hapa hamalizi na sasa unaweza kusema amemeza CD ya mziki"
"Mamaaa!"
"Mama nini wakati huo ndio ukweli"
"Kweli hali yake imekuwa nzuri uchangamfu kidogo umemrejea………Muheshimiwa mimi ombi langu naweza kusema nimaombi yangu pamoja na madaktari wengi…..Muheshimiwa hembu naomba kidogo mishahara yetu muifikirie kwa mara nyingine kwa maana kodi kila kukicha inaongezeka na ukitazama mishahara haipandi"
"Hilo ndio nitalipa kipaumbele tukirudi bungeni mwezi ujao na wala usiwe na mashaka na hilo"
Nikanyanyuka na kujiweka pensi yangu ya michezo vizuri na kuwafanya mama na Dokta wakinitazama
"Unakwenda wapi?"
"Toilet"(Chooni)
"Hizo ngazi za gorofani upande taratibu usije ukaanguka na urudi umalizie chakula chako"
"Mama nimeshashiba"
"Nimekuambia urudi uje kumalizia chakula chako"
"Sawa mama Eddy"
Nikaondoka na kuwaacha mama na daktari wakiendelea kuzungumza mambo yao ya kikazi,nikaingia katika chumba changu kilichopo gorofani na moja kwa moja nikaingia katika choo kilichopo ndani ya chumba changu na kujisaidia haja ndogo.Nikakumbuka kwenye kabati la chumbani kwangu kuna simu yangu ambayo niliiacha kipindi ninakwenda shule nikatoka chooni na kufungua kabati langu na kuaanza kuchangua vitu na kuanza kuitafuta kwani katika sehemu niliyo iweka haikuwepo.Nikatafuta zaidi ya dakika tano sikuuiona ikanibidi nitoke chumbani kwenda kumuuliza mama ila kabla sijashuka kwenye ngazi nikasikia swali la daktari na kunifanya nisimame na kuyasikiliza mazungumzo yao pasipo wao kuniona
"Yule dada wa kazi amekwenda wapi?"
"Yule niliamua kumrudisha kwao kwani amenivurugia familia yangu"
"Kivipi?"
"Dokta yaani ni makubwa sana yaani watu wa nje wanapo ona mtu uanishi katika jumba kubwa magari mazuri wanahisi haya ndio maisha mazuri ila kusema kweli dokta yaani ingekuwa sio haya majukumu ya kiserikali ningeondoka nchini na mwanangu kwenda kuishi mbali na Tanzania"
"Muheshimiwa kwa nini umezungumza hivyo wakati Mungu amekujalia kila kitu katika maisha"
"Ndio amenijalia kila kitu katika maisha ila sio amani katika ndoa yangu…..Daktari ninakuambia hivi kutokana wewe ni sawa na kaka yangu na mamo mengi umekuwa ukinishauri ila hata hili nahitaji unishaur kutoka kwako"
"Kwani kuna kitu kibaya kilicho tokea kati yako na mzee?"
"Ndio tena ni kikubwa sana ambacho kinaninyima usingizi kila nikikifikiria……Si nilikuwa masomoni kwa kipindi kirefu kidogo"
"Ndio"
"Basi huku nyuma nilimuacha huyu kijana wangu yule binti wa kazi na mzee"
"Ndio"
"Wakati nikirudi nchini sikutaka mume wangu atambue kitu chochote…..Nilifika hapa Tanzania mida ya saa saba usiku na pia sikutumia gari yangu kohofia dereva wangu anaweza kumuambia mume wangu kuwa ninarudi"
"Sasa ni kwanini hukutaka mzee ajue?"
"Nisikudanganye dokta kwa jinsi nilivyokuwa nikimpenda baba Eddy basi kama kuna kitu chochote kibaya kitakuwa kanamtokea basi mimi moyo wangu hujikuta na wasi wasi sana kiasi kwamba hata kama anakuwa na safari ya muhimu huwa nina mzuia asiende na akibaki ujue kuna tukio baya litatoke sehemu aliyokuwa anahitaji kwenda…….Basi miezi mine nyuma hali hiyo ikawa inanisumbua sana kiasi kwamba nikaanza kuwa na mashaka kuwa kuna kitu mume wangu atakuwa anakifanya ambacho ni kinyume na makubaliano ya ndoa yetu……..Basi niliingia hapa usiku kama saa nane kasoro hivi kwa kutumia taxi ya kukodi hadi askari wa getini akanishangaa.Sikustuka kutokana ni kawaida ya nyumba yangu kuwa na ukimya,nilipitiliza moja kwa moja hadi ndani kwangu…..Dokta huwezi amini yaani nilimkuta Baba Eddy akiwa amelala na yule binti"
"Weeeee…..!!?"
"Ndio dokta na mbaya zaidi juu ya kitanda changu nilicho kinunua kwa pesa yangu"
"Yule binti kumbe anatabia chafu kiasi hicho?"
"Dokta weee acha tuu hapo ndipo nikaamini ule usemi wa mfadhili mbuzi kuliko binadamu kwani anamaudhi.Na ninamshukuru Mungu ile siku presha yangu haikupanda"
"Sasa hapo ndio naanza kupata pichaa"
"Picha gani dokta?"
"Mwezi uliopita yule binti alikuja pale hospitalini kwangu"
"Alifwata nini?"
"Ndio nakuja huko ulipo niuliza……Alikuja kwa lengo nimtoe mimba?"
"Mimba…..!!?"
Mama aliuliza kwa sauti ya juu hadi na mimi nikstuka nilipo simama na kunifanya niwachungulie na kumuona mama akiwa amekaa katika kochi lake nililo muacha huku akimtazama dokta kwa umakini
"Ndio alikuwa na ujauzito wa mwezi mmoja na nusu"
"Sasa hiyo mimba atakuwa ameipataje pataje wakati mume wangu hana uwezo wa kumzalisha mwanamke?"
"Ehhee mbona uwezo huo anao tuu wakumzalisha mwanamke?"
"Dokta mbona unanichanganya na wewe…..Mimi ninazungumza hivyo kutokana mimi nilihusika katika oparesheni ya mume wangu kipindi amepeata ajali na tulimchoma sindano ambayo asinge weza kumzalisha mwaanamke wa aina yoyote,K?umbuka hata mimi nilikuwa ni daktari?"
"Ndio nalitambua hilo kuwa wewe ni dokta ila hichi ninacho kuambia mimi nina uhakika kutokana miezi mitano hivi ya nyuma kuna madaktari wa wachina walikuja pale hospitalini kwetu wakijishuhulisha na maswala ya wanaume walio na tatizo kama hilo unalo lisema.Mzee alikuja kunitembelea ila hakujua kama kuna huduma hiyo ya kupima wanaume inatolewa pale hospitalini.Katika mazungumzo yatu nikamtania kiutani utani akapime na yeye ili ajue kama ana uwezo au hana…….Alipo pima kama ulivyo sema wewe kuwa hana uwezo wa kumzalisha mwanamke ndivyo majibu yake yalivyo kuwa.Kutokana wezetu wachina wapo mbele kwa taaluma hiyo basi wakamfanyia upasuaji mdogo akarekebishwa katika mirija yake akapewa dawa na akapona kabisa"
"Ndio akaamua majaribio yake ya kama amepona ua hajapona ndio akaamua ayachukulie kwa mtoto wa watu?"
"Kwa hilo hata mimi sijui….Basi yule binti alinibembeleza sana niweze kuitoa mimba aliyo kuwa nayo kwa akili za haraka haraka nikajua mimba amepewa na vijana wako wa kazi…..Ila nikaja kupata mashaka zaidi pale binti siku ya pili alipo nijia na milioni tano ili nimfanikishe kumtoa mimba"
:Na wewe ukamtoa?"
"Sikudhubutu ukiachilia mbali maadili yangu ya kazi hayaruhusu daktari kumtoa mwanamke mimba pia hata imani ya dini yangu hairuhusu jambo hilo"
"Ehee ikawaje?"
"Nilimfukuza akaondoka akiwa analia.Nikachukua jukumu la kuwasiliana na mzee nikakutana naye ila mimi kama dokta kwa jinsi mzee alivyokuwa akinijibu nikaanza kupata mashaka ila nikaja kuachana nalo kutokana nilijua mzee atalifanyia kazi"
"Kwa nini na wewe usinipigie simu ukanieleza hilo swala?"
"Muheshimiwa niliogopa kutokana wewe upo masomoni na isitoshe ulikuwa unakaribia kipindi cha mitihani"
Mwili wangu ukashikwa na ganzi iliyonifanya nitulie sehemu nilipo huku machozi yakinilenga lenga sikuamini kama baba anaweza kutembea na msichana wa kazi na mbaya zaidi msichana wa kazi maisha ya kwao sio mzuri kabisa na ndugu zake wanasomeshwa na kwa pesa ya mama
"Muheshimiwa futa machozi silie"
"Dokta inauma mwanaume niliye mwamini na kumuinua kimaisha leo hii ananifanyia kitu kama hichi"
"Muheshimiwa hizo ni changamoto za maisha"
"Hapana dokta huo ni upumbavu tena upumbavu ulio pindukia yaani pia nashukuru sijazaa na huyu mwanaume"
Nikastuka kusikia mama akizungumza kitu kama hicho huku akiwa analia kwa uchungu na kunifanya na mimi kujawa na hisia za huzuni na taratibu machozi yakaanza kunitoka,Kutokana na hali yangu ya kuumwa sio nzuri sana ikanilazimu kukaa katika ngazi ya juu huku nikiwa nimeuegemea ukuta na kuendelea kuwasikiliza mama na daktari
"Muheshimiwa unataka kuniambia huyu kijana si mtoto wa mzee?"
Kabla daktari hajajibiwa swali lake na mama simu yake ikaita,akaitoa na kupokea na kumfanya mama akae kimya
"Ajali ya basi gani?'
"Majeruhi 34?'
"Ninakuja ninakuja sasa hivi"
"Dokta ni ajali ya basi gani?"
"Basi la Msulwa Express limegongana na roli la mbao maeneo ya maili moja"
"Eheee wamekufa watu wangapi?"
"Watano ila majeruhi nao wana hali mbaya kiasi kwamba hali ya vifo itaongezeka wakati wowote na majeruhi wapo hospitalini kwetu"
"Duu poleni.Haya mwaya Dokta nikuache ukatumikie majukumu yako"
"Sawa muheshimiwa hali ya mgojwa wangu itakavyo endelea utanijulisha"
"Sawa nahisi atakuwa amelala"
"Haya kama atakuwa bado yupo macho utamuambia mimi nimesha ondoka"
"Hakuna shaka juu ya hilo"
Nikasikia mlango wa kuingila sebleni ukifunguliwa na kufungwa nikajua moja kwa moja dokta atakuwa ameondoka.Mama akanza kupandisha ngazi akaanza kupata wasi wasi baada ya kuniona nimekaa katika ngazi huku machozi yakinimwagika
"Eheee mgonjwa bado hujalala na unalia nini mwanangu?"
"Mom who is my father?"(Mama baba yabgu ni nani?)"
Mama akabaki kimya huku akinitazama akionekana kuto kulitarajia swali kama hilo nililo muuliza.Akapanda ngazi na kukaa ngazi niliyo kaa mimi
"Eddy my son i will tell you tomorrow now your supporse to relax"(Eddy mwanangu nitakuambia kesho sasa hivi unatakiwa upumzike)
"Momy i can't relax because i don't know who is my real blood father"(Mama siwezi kupumzika kwasababu simjui baba yangu wa damu)
Nilizungumza kwa hasira huku machozi yakinimwagika na kumfanya mama aniegemeze kichwa changu kwenye bega huku akinibembeleza
"Eddy my son do you love me?"(Eddy mwanangu unanipenda mimi?)
"I love you mother but i need know the truth"(Nakupenda mama ila nahitaji kujua ukweli)
"Ok my son am happy to hear that you love me.I need you to listen me very carefull"(Sawa mwanangu ninafuraha kusikia kuwa una nipenda.Nahitaji unisikilize vizuri kwa umakini)
"Ok mom am listen up"(Sawa mama nina kusikiliza)
"Now is night give me a chance to go and prepair my some of the office work and tomorrow after i came back i will give you good explaination and i will tell you who is your real father"(Mwanagu sasa hivi ni usiku,nipe nafasi ya kwenda kuandaa baadhi ya kazi za ofisini kwangu na kesho nitakapo rudi nitakupa maelezo mazuri na nitakuambia nani ni baba yako)
Mama alizungumza huku akinifuta machozi kwa kutumia kiganja chake na kunifanya nizidi kulia kwa uchungu
"Mama sitaki tena nimesema sitaki nahitaji kumjua baba yangu ni nani kwa jinsi ninavyo ona hauto shindwa kusema mimi sio mwanao wa kumzaa"
Nilizidi kuzungumza kwa hasira iliyo changanyikana na uchumgu na nikaanza kujihisi upweke ambao nikaanza kuufananisha na mtoto aliye kosa wazazi wote awili
"Eddy what are you say?"(Eddy unasemaje?)
"Yeah you can tell me that your not my mother"(Ndio unaweza ukanimbia kuwa wewe sio mama yangu)
Nlizungumza kwa hasira nikastukia kofi likitua shavuni mwangu kutoka kwa mama na kumfanya anyanyuke kwa hasira na kuelekea chumbani kwake na akaubamiza kwa mguvu mlango wa chumbani kwake.Nikamfwata na kumkuta akiwa amelala gubi gubi kitandani kwake huku akiwa analia taratibu nikakaa kitandani na kumgusa mgongoni
"Momy am sory i d…"(Mama samahani si…&#8230😉
"Eddy leave me alone now"(Eddy ondoka na uniache peke yangu sasa hivi)
"Mom am sory i din't mean to say that words"(Mama samahani sikuwa na maana ya kusema maneno yale)
"Eddy do you whant me to die?"(Eddy unahitaji mimi nife?)
"No mamy"(Hapana mama)
"Your father comfused me and you too so if you need me to die kill me now"(Baba yako ananichanganya na wewe pia.Sasa kama unataka mimi nife niue sasa hivi)
Mama alizungumza kwa hasira huku akiuchukua mkono wangu mmoja na kuuweka kwenye koo lake ili nimkabe afe nikajikuta nikiogopa na mwili mzima ukianza kutetemeka kwani sikuwahi kumuona mama katika hali ya hasira kiasi kwamba anataka mimi nimuue

ITAENDELA


*****SORY MADAM*****(13)

AGE……………………………..18+

ILIPOISHIA
Mama alizungumza kwa hasira huku akiuchukua mkono wangu mmoja na kuuweka kwenye koo lake ili nimkabe afe nikajikuta nikiogopa na mwili mzima ukianza kutetemeka kwani sikuwahi kumuona mama katika hali ya hasira kiasi kwamba anataka mimi nimuue
ENDELEA
Machozi yakaanza kunitiririka kwa wingi huku moyo wangu ukijawa na maumivu ni kwanini nilizungumza kitu kama kile,nikautoa mkono wangu koo ni mwa mama na kumkumbati na kukiweka kachwa chake begabi mwangu na kuanza kumbembeleza taratibu.
"Eddy mwangu kwa nini unataka kuwa kama huyu baba yako?"
"Mama ninakuomba unisamehe sio kusudio langu kuzungumza hivyo"
Nikaendelea kumbembeleza mama taratibu hadi akanyamaza na taratibu usingizi ukaanza kumpitia baada ya muda kidogo akalala,Nikachukua shuka lake na kumfunika vizuri kisha nikatoka ndani ya chumba chake huku nikizima ta ya chumbani kwake na kushuka gorofani na kukaa kwenye sofa huku maneno ya mama akiwa anazungumza na dokta yakaaza kunirudia taratibu katika akili yangu huku yakiwa yanapita kama kanda wa video aina ya VHS.Kitu kinacho niumiza kichwa sana ni nani baba yangu na kitu kingine watu wengi wanasema ninafanana sana na baba yangu
"Au mama atakuwa amechoka ndio maana akazungumza hivi?.........ila hata kama ni kuchoka itakuwaje akamwambia daktari mtu asiye husika katika familia yetu?"
Nikaendelea kujiuliza maswali yasiyo na majibu kiasi ya kujikuta taratibu nikiaanza kupitiwa na usingizi na kujikuta nikilala kwenye kochi.Nikaanza kuisikia sauti ya mama kwa mbali ikiniita taratibu huku akionekana akiomba msaada,Nikayafumbua macho yangu na kuuta mlango wa kuingilia hapa sebleni nikatazama nje na kukuta bado kuna giza jingi.Nikanyanyuka kwa haraka na kwenda chumbani kwa mama nikakuta mlango wake ukiwa wazi nikaingia na kukuta kuna mwanaume yupo juu yake akimkaba huku kichwani kwake akiwa amevaa maski(Kinyago).Nikachukua chombo cha dogo kilichowekewa uwa la pambo na kwenda kumpiga nalo la kichwani na akaangukia kwa pembeni baada ya kuniona mimi akachomoka na kukimbia sikumjali zaidi ya kumuangalia mama kama yupo sawa au laa.Mama akanyanyuka huku akiwa anakooa huku akiwa amejishika koo.
"Mama unajisikiaje?"
"Vizuri mwangu fungua hiyo droo yangu ya kabati na unitolee bastola yangu"
Nikafanya hivyo na kuitoa bastola yake kisha mama akanyanyuka kitandani na kuvaa raba zake za kufanyia mazoezi na taratibu tukaanza kutoka ndani kwa umakini wa hali ya juu huku na mimi nikifwata kwa nyuma.Tushuka chini na kutoka nje kabisa ambapo kwa safari hii mlango umefungwa.Tukazunguka nyumba nzima kutazama kama kuna usalama kwa bahati nzuri kuna usalama.Tukaelekea getini ambap hukaa askari ila hatukumkuta na wala hapakuwa na kitu chochote kinacho ashiria kuna tatizo lililo tokea katika eneo hilo
"Eddy kimbia kaniletee simu yangu ndani"
Nikaaza kujikongoja kongoja huku nikipiga hatua za haraka nikaamini kuwa mama amesahau kuwa mimi ni mgonjwa.Nikapanda ngazi kwa mwendo wa haraka kidogokitendo cha kushika kitasa cha mlango wa kuingilia chumbani kwa mama nikasikia milio mitatu ya risasi ikitokea nje.Nikabaki nikiwa nimesimama huku miguu yote ikiwa inaaza kuishiwa na nguvu kuingia ndan kuchukua simu ya mamai nikawa ninataka kutoka nje nikawa ninataka.Nikaaona hakuna haja ya kuingia ndani kuchukua simu moja kwa moja nikakimbilia jikoni na kuanza kukitafuta kisu ila sikkukiona zaidi ya kuona Umma wa kulia chipsi,nikiona unanitosha kwends kupambana na kito chochote bitakacho kutana nacho nje
Nikafungua mlango na kujikuta mapigo ya moyo yakianza kumienda mbio huku wasiwasi ukiinza kuukamata mwili wangu kwani katika sehemu nilipo muacha mama sikumuona,Nikajikuta ninaaza kupata kiwewe cha miguu kila nikijaribu kusogea mbele ninajikuta ninasheindwa sasa sikujua ni woga ndio unachania kwani sikujua ni wapi mama yupo.Nikiwa bado nimesimama nikasikia mlio mwengine wa risasi ukitokea nje ya geti kwa mstuko nusu nijikojolee kwani sikujua huo mlio ni nani aliye pigwa nao kwani kipindi nipo mdogo mara kwa mara baba alikuwa akinifundisha jinsi ya kutambua milio ya risasi pale inapokuwa imempiga mtu au kumkosa na moja kwa moja mlio nilio usikia nikajua moja kwa moja risasi iliyo lia imetua kwenye mwili wa mwanadamu
Nikajikaza kiume na kuunza kupiga hatua za kwenda nje ila kwa umakini huku uma wangu nikiwa nimeushika kwa umakini wa hali ya juu huku nikiwa makini kwa chochote kutacho jitokeza huku mwili mzima jasho lilinimwagika.Nikafungua geti dogo taratibu huku nikiwa nimetanguliza kichwa,Nikamkuta mama akiwa amesimama na askari kama watano wakiwa na bunduki zao mikonini huku kukiwa na mtu mmoja akiwa amelala chini huku mwili wake ukiwa unavuja damu nyingi.Nilicho kikumbuka kwa haraka haraka ni nguo alizo zivaa mtuu huyo na kukumbuka ni yule mtu niliye mpiga na bakuli la dongo lililo kuwa na uwa la pambo.
"Alafu bado kijana mdogo sana"
"Ndio huyu nahisi ametuwa na mtu wa humo ndani kwako kwa maana haiwezekani ajiamini kiasi kwamba ya kujua moja kwa moja chumani kwako"
"Hilo usemalo litakuwa na ukweli ndani yake"
Mama akaendelea kujadiliana na askari wanaolinda eneo tunalo ishi akiwemmo na askari wetu huku mama akimshushia lawama askari wetu ni kwa namna gani mtu anaingia ndani pasipo yeye kufahamu,askari wengine wakaja na gari lazo na kuchukua maiti huku wakimchukua askari wa getini kweyu kwenda kumuhoji maswali

***
Mama akamfungulia kesi ya mauaji Manka huku lengo lake kubwa ni Manka kwenda kufungwa kifungo cha maisha,Siku ya kesi kusikilizwa ikawadai huku mahakamani kukiudhuriwa na watu wachache baadhi yao wakiwemo ndugu wa upande wa Manka akiwemo dada yake na pamoja na mwalimu Mayange.Tangu tukiwa nyumbani mama niweze kuzungumza kitu kitakacho muhukumu Manka.Ila moyoni mwangu nikaanza kuhofia endapo atasema tulifanya mapenzi itakuwa aibu kwangu na mama yangu.Watu wakiwa wanaaza kuingi ndani ya chumba cha mahakama mimi nilikaa nje huku nikimdanganya mama kuwa kuna mtu nina mpigia simu na muda si mwingi nitaingia ndani.Alipo ingia nikaelekea katika sehemu yenye mtuhumiwa na kawaonga kila askari elfu hamsini na walikuwa wanne ili wanipe nafasi ya kuzungumza Manka ambaye kwa wakati wote sura yake ilijaa machozi na huzuni hadi na mimi nikajikuta nikiwa na huzuni moyoni mwangu
"Eddy nakuomba unisaidie katika kesi hii wewe ndio kiongozi wangu wewe ndio unaweza kuzizima ndoto zangu katika maisha yangu……..Eddy sikukusudia kukuua na wala sikuwa na lengo baya la kukudhuru yote yalitokea kwa sababu ninakupenda Eddy na sikujua ni jinsi gani ya kukushawishi ili unipende nilidhani utanichezea na kuniacha"
Manka alizungumza kwa huzuni huku akilia kwa uchungu akionekana kujutia kwa kitu alicho kifanya
"Sasa Manka kwa nini hukuwa mstaarabu mpaka tushikiane bastola kwa kitu kidogo"
"Eddy nakuomba unisamehe ila nakuomba unisaidie katika hili swala"
"Manka siwezi kukusaidia katika lolote inakubidi na wewe ulipe kwa kitu ulicho nifanyia"
"Kaka muda umekwisha anatakiwa kuingizwa kizimbani"
Askari alizungumaza na kunifanya nianze kupiga hatua za kutoka nje ila Manka akaniwahi na kunishika mkono huku akilia
"Eddy hata nikinyongwa au kuhukumiwa kifungo cha maisha ila tambua kuwa ninazawadi yako nitakayo kupa kama ukumbusho katika maisha yangu"
Nikautoa mkono wake kisha nikaondoka na kwenda katika chumba cha mahakama,Manka akaingizwa na askari huku akiwa analia huku sura yake akiielekeza chini ila mara kwa mara nikiwa ananitazama.Kesi ikaanza kusikilizwa huku mawakili wa pande zote mbili wakianza kumuhoji maswali Manka na kila kitu ambacho Manka alicho kuwa akiulizwa hakujibu zaidi ya kulia.Ikafika zamu yangu ya kuhojiwa maswali na nikaanza kuhojiwa swali moja baada ya jengine
"Mr Eddy ulifwata nini kwa nyumbanni kwa Mwalimu Myange?"
"Nilikwenda kuchukua pesa ya matumizi"
"Ulikuwa una ruhusa ya kwenda kwake?"
"Hapana?"
"Kwahiyo ulitoroka shuleni kwenu?"
"Ndio"
"Basi ninaweza kusema kuwa wewe ni jambazi umwekwenda kuvamia nyumbanni kwa mwalimu mayange ndio maana Manka akakupiga risasi?"
Wakili wa upande wa Manka akaendelea kunibana na maswali yake ambayo ni magumu kupita maelezo nikamtazama Manka kwa jicho la kuiba na kumkuta sura yake akiwa bado ameielekeza chini
"Mimi sio jambazi na Manaka si mtu aliye nipiga risasi"
Miguno ikaanza kusikika ndani ya mahakama nikamtazama mama nikaona jinsi sura yake ilivyo badilika gafla na kuwa na hasira,kutokana na minong'ono hakimu ikamalzimu kugonga nyundo mezani na kuwaomba watu wakae kimya
"Kwa nini unasema kuwa Manka siye aliye kupiga risasi na kwa madai yenu ya washtaki munasema Manka anahusika na wewe kupiga risasi?"
"Narudia kusema Manka hausiki na kitu chochote katika kunipaga risasi wala kunijeruhi mimi.Nilikwenda nyumbani kwa Mwalimu Mayange na kukuta hayupo ila nikamuomba Manka nimsubiri mwalimu hadi atakapo rejea ila kutokana alipata safari ya gafla yeye na mke wake ikanilazimu kuondoka na kupita njia za vichochoroni ndipo nikakutana na majambazi walio waliokuwa wakinilazimisha nitoe pesa ila kutoka na ubishi wangu mmoja wao akanipiga risasi ya kifua na baada ya hapo sikujua ni kitu gani kinacho endelea"
Mahakama nzima watu walikaa kimya huku wakinisikiliza ninavyo zungumza kidogo nikamuona Manka akiwa na tabasumu usoni mwake.
"Kwa hiyo Manka sio mtu aliye kupiga risasi?"
"Wewe vipi kwani hukunisikia nilivyokuwa nikizungumza au?"
Nilizungumza kwa jazba kidogo na umfanya wakili anaye nihoji kuanza kujichekesha chekesha
"Sijasikia labda wewe ndio unaweza ukawa unaidanganya Mahakama tukufu Mr Eddy"
"Sijamdanganya mtu na Manka hajanipiga risasi na muheshimiwa hakimu moja ya sura za majambazi nilio waona mmoja kama ni huyo wakili anaye nihoji maswali yake ya ajabu ajabu"
"Wewe kijana kama umekosa kitu cha kuzungumza sema kuliko kuanza kunipakazia vitu vya kishenzi"
"Kwa hiyo mimi mshenzi si ndio….Hakimu ndivyo jinsi munavyo afundisha hawa mawakili wenu kutukana watu?"
Nilizungumza huku nikiwa makini na kuzidi kumchanganya wakili ambaye nimeamua kumeuzia mastaka
"Muheshimiwa hakimu huyu kijana atakuwa amechanganyikiwa ninaomba mahakama yako akapimwe akili"
"Nani akanipime akili kama si wewe uliye nipiga risasi nna wezako na mbaya zaidi wewe si ulikuja kunichimba mkwara hapo nje kuwa nikikutaja utaniua au sio wewe?"
Hakimu akalazimika kuihairisha kesi na kuomba turudi ukumbini muda wa mchana kwa ajili ya keundelea kwa kesi,Mama hakunisemesha kitu hadi tukatoka nje ya mahakama na kuingia ndani ya gari
"Hivi wewe mtoto ni kitu gani kilicho kupata?"
"Mama hakuna kilicho nipata zaidi ya kwamba Manka hakunipiga risasi ila ni yule wakili na alikuwa na wezake wamelewa"
"Sasa mwangu mbona hayo yoyote hukuyazngumza wakati uatambua fika kwamba Manka ninamchukia kama baba yake?"
"Baba ya ke yupi?"
"Ok tuachane na hiyo mada"
"Mama tena nakumba unaimbie ni kitu gani kinacho endelea kati yako wewe na baba kwani niliwasikia maneno yenu yote kuanzi mwanzo hadi mwisho"
"Unataka kujua ukweli si ndio ni hivi Manka ni mtoto wa baba yako alizaa na mwanamke mwengine kabla hajakutana na mimi"
Nikaanza kuhisi kijasho kikianza kunimwagika huku mwili ukinza kunitetemeka huku nikaanz kufikiria ni jinsi nilivyokuwa nilifanya mapenzi na Manka
"Kwa hiyo nilifanya mapenzi na dada yangu?'
"Unasemaje wewe?"
Nlistuka baada ya mama kuniulizwa swali ambalo nilijikuta nikiopoka bila kutarajia kuwa nitazungumza kitu kama hicho,nikabaki nikimtazama mama huku naye akinitazama kwa macho ya uchungu na hasira

INAENDELEA HAPA
 
daaaaahh...ndo madhara ya ya wazaz kuficha siri kwa watoto.....tupia nyengine basi jamani.....
 
Kitanda hakizai haramu hata hivyo haina mbaya mbona Edd na Manka si ndugu tena ndo wataunganisha familia mana zawadi yake kwa bibie tuingoje. Shusha mavitu
 
Imeisha au
****SORY MADAM*****(14)

AGE………………………18+

ILIPOISHIA
Nikaanza kuhisi kijasho kikianza kunimwagika huku mwili ukinza kunitetemeka huku nikaanz kufikiria ni jinsi nilivyokuwa nilifanya mapenzi na Manka
"Kwa hiyo nilifanya mapenzi na dada yangu?'
"Unasemaje wewe?"
Nlistuka baada ya mama kuniulizwa swali ambalo nilijikuta nikiropoka bila kutarajia kuwa nitazungumza kitu kama hicho,nikabaki nikimtazama mama huku naye akinitazama kwa macho ya uchungu na hasira

ENDELEA
"Hapana mama sijasema kitu chochote"
"Ujasema kitu chochote wakati umezungumza hicho ulicho kizungumza?"
"Mama tupotezee hiyo mada"
"Eddy Eddy wewe lete huo ujinga wako tuu na ole wako nichunguze hilo swala alafu nijue ni kweli oune jinsi itakavyo kama sinto kufunga"
Mama alizungumza kwa hasira huku akishuka ndani ya gari na kuelekea sehemu aliyoingizwa Manka.Sikujua atakwenda kuzungumza nani ikanilazimu nishuke ndani ya gari na kumfwata kwa haraka,nikamkuta mama amesimama na Manka huku akimuonya
"Nisikie siku una uhusiano na mwangangu utanitambua mimi ni nani hapa si anajifanya anakutetea ila ukiingia ndani ya mikono yangu utajuta kuzaliwa"
"Mama mbo……"
"Tena na wewe funga bakuli lako nenda nikukute kwenye gari"
"Lakini mam……"
"Hakuna cha lakini nimekuambia funga bakuli lako na sihitaji uzungumze upumbavu wowote sawa.Angekuua huyo ndio ungefurahi si ndio?"
"Ila mama si nimesha sema Manka hausiki na kitu chochote"
Mama akanitazama kwa jicho la hasira kisha akanisunya na kutoka huku akitembea kwa hatua ndefu kurudi kwenye gari huku mlinzi wake akimfwata kwa nyuma akimtuliza jazba.Wakati wote mama alipokuwa akizungumza Manka alikuwa ameinama chini huku analia kwa uchungu,nikamsogelea taratibu na kumkumbatia japo mikono yake imefungwa pingu kwa mbele.
"Eddy niache tu nikafungwe mama yako amesha tengeneza chuki juu yangu"
"Manka ni maneno gani unayo yazungumza ehee sipo tayari iwe kama hivyo nahitaji utilize akili katika hili nakuomba tena sana mmmm"
"Eddy hata nikiwa huru sinto weza kuwa na uhuru kama mwazonni….Laiti baba yangu angekuwapo nisinge nyanyasika kiasi hichi"
"Kwani baba yako nyupo wapi?"
"Ni historia ndefu Eddy ila kwa ufupi baba yangu ana uwezo mkubwa wa kiuchumi ila alimtelekeza mama baada ya kunizaa mimi……….ila sijui ni wapi alipo japo ninasikia sikia amependishwa cheo kazini kwake"
"Ulisha wahi kukutana naye hizi siku za karibuni?"
"Hapana mara ya mwisho kukutana naye nilikuwa na umri wa miaka mitano kuanzia hapo nina msikia sikia"
Nikajikuta ninapata maumivu mengi moyoni mwangu huku mawazo ya kwa nini baba anafanya hivi yakitawala kichwani mwangu.
"Eddy mama yako anacho kizungumza ni kweli nakuomba uniache nikafie jele"
"Manka acha kuzungumza kitu kama hicho ila tambua kuwa nipo upande wako hadi dakika ya mwisho"
Nilizungumza na kuondoka na kumuacha Manka akibaki ananishangaa.Muda wa kuingia mahakamani ukawa tayari umesha wadia sikuhona haja ya kumsubiria mama kuingia naye kwenye ukumbi wa mahakama nikatangulia mwenyewe na kumkuta mwalimu Mayange na familia yake wakiwa wamekaa kwa masikitiko
"Eddy"
Mwalimu Mayange liniita na nikamfwata katika sehemu waliyo kaa
"Eddy mwanangu nakushukuru kwa masaada wako japo tunasubiria majibu ya mahakama"
"Usijali mwalimu Mungu atasaidia yatakwisha"
"Kumbe mama yako ni waziri?"
"Ndio"
"Hongera"
"Asante"
Nikaondoka na kwenda kukaa katika eneo nililo kuwa nimekaa mwazoni na baada ya muda kesi ikaanza,kutokana muhusika mkuu nilikataa Manka kuwa sio muhusika ikalazimika kesi kufutwa na Manka kuachiwa huru.Upande wa familia ya Manka ikatawaliwa na furaha ila kwa upande wangu mama amekasirika
"Kwenye gari langu hupandi na utakuja kwa miguu"
"Mama….
"Hakuna cha mama Zuhura hembu mpe alfu ya daladala"
"Sawa bosi"
Mlizi wa mama akafungua kipochi chake na kunipa alfu moja ya daladala kisha wao wakaingia ndani ya gari na wakaondoka nikabaki nimesimama ninawashangaa kwani sikuamini kama mama anaweza kunifanyia kitu kama hicho.Nikiwa bado sijui cha kufanya nikasikia sauti ya Manka ikiniita kwa nyuma nikageuka na kumkuta amesimama huku akiwa na tafbasabu usoni mwake
"Eddy nashukurukwa msaada wako yaani sijui hata nikushukuruje"
"Usijali best yangu"
"Ila Eddy nina zawadi yako kama nilivyo kuambia pale mwazoni"
‘Una zawadi gani?"
"Nina ujauzito wako"
Kusema kweli mapigo ya moyo nikahisi yamepoteza muelekeo na kunifanya mwili mzima kuanza kuzizima kiasi kwamba jasho likaanza kunimwagika huku mdomo ukiwa mzito kuzungumza kitu ninacho taka kukizungumza hadi Manka akahisi kitu
"Eddy una tatizo?'
"Hapan…..munarudi Arusha leo?"
"Ndio ninamsubiria shemeji aje kutuchukua amelipeleka gari gereji"
"Ahaa basi Mungu akibariki hilo swala la mtoto tutakuja kulizungumza huko Arusha"
"Lakini mbona unaonekana kama huna furaha nilivyo kuabia kuwa mimi ni mjamzito?"
"Haaa nimefurahi ila tutatafuta muda tulizungumze"
Tukaagana na Manka kisha mimi nikaondoka na kumuacha akazungumza na ndugu zake kisha,Nikakodi boda boda ya pikipiki hadi nyumbani nikamuacha jamaa getininikingia chumbani kwangu kumchukulia pesa ambayo ilipungua kwenye malipo yake kisha nikarudi ndani na kumkuta mama sebleni akionekana akinisubiri.Nikaanza kupandisha ngazi za kwenda ndani kwangu
"Wewe Eddy"
"Naam"
"Hembu shuka hapa"
Nikashuka na kukaa kwenye moja ya sofa kisha na yeye akakaa kwenye sofa jengine
"Hembu wewe mtoto niambie ni nani aliye kupiga risasi?'
"Mama kile nilicho kizungumza mahakamani ndio hicho hicho"
"Ila Eddy manangu kwanini siku ya kwanza nilivyo kuuliza ukasema Manka ndio muhusika?"
"Hapana labda nilikosea"
"Kukosea tena mwanangu…..Ila na kwanini ulisema umetembea na Manka?"
"Ahaaa mama ulinisikia vibaya"
"Eddy Eddy mwanangu jua kuwa mimi ni mtu mzima na kila unacho pitia,mimi pia nilisha pitia kipindi ninakua sasa usitake kunidanganya hembu niambie ukweli mwanangu ni kweli Manka ulitembea naye?"
"Sijatembea naye wewe si umesema ni dada yangu?"
"Ndio ni ndugu yako……Kachukue begi lako la nguo dereva akupeleke shule"
Mama jioni yote hii derive anipeleke shule?"
"Maamuzi ndio hayo kavae ngui zako za sule derive akupeleke Arusha"
"Lakini mama sijapona vizuri"
"Hujapona vizuri au unataka kujidekeza dekaza kumbuka kuwa wewe ni A level tena mwenyewe unajiita PCB sasa sijui huko shule kama unasoma au ndio kuruka ruka vaa upelekwe shule"
Kitendo cha mama kuniambia nijiandae nirudi shule kikanikosesha amani katika moyo wangu na sikuwa na jinsi zaidi ya kujiandaa na taratibu ili dereva anirudishe.Hadi namaliza kujiandaa ikawa imeshatimu saa kumi na moja jioni.Nikabeba begi langu la nguo na kulipakiza ndani ya gari
"Eddy nataka huko shule ukasome sihitaji michezo ya kijinga jinga tambua kuwa wewe umesha kuwa mtu mzima unapaswa kuaanza kufikiria maisha yako na yawanao ila sio kufanya ujinga kama ulio ufanya"
"Sawa mama"
"Kama mutakuwa munachelewa mutalala kwenye Hotel yoyote njiani"
"Sawa"
Mama akanipa kiasi cha kutosha cha matumizi ya pesa ya kutumia shukeni pamoja na pesa ya matumizi njiani na safari ikaanza,kutokana na foleni iliyopo jijini Dar es salaam ikatifanya tusimame simame san njiani
"Kaka naomba niendeshe niendeshe gari"
"Ningekupa mdogo wangu ila huna leseni"
"Kwani usiku huu ni trafki gai atakaye tusimamisha njiani?"
"Mbona wapo wengi hii ni bara bara ya mkoani ni lazima tutawakuta wengi"
"Sawa"
Safari ikaendelea huku nikiwa nimelala kwenye siti ya gari na kumuacha dereva kufanya kazi yake.Dereva akaniamsha na nikakuta tumesha fika katika sehemu moja inaitwa Mombo kwenye hoteli moja inaitwa Liverpool,tukaingia na kuapata chakula cha usiku na tukarudi dani ya gari na safari ikaanza.Kutokana sikuwa na mazoea na huyu dereva mpya wa mama nikaona ni bora kulala kwani sikuwa na chakuzungunza naye.Nikastushwa na breki kali za gari letu na kunifanya nistuke na nikamkuta dereva akijitahidi kuikwepa gari ndogo aina ya PREMORE inayo pinduka pinduka katikati ya barabara.Gari inayo bingiria ikatulia na kuingia ndani yam taro ikamlazimu dereva kulisimamisha gari letu mbele kidogo kutoka sehemu gari ndogo ilipo angukia.Mimi na dereva tukajikuta tumetulia kama kwa dakika tano huku kwa upande wangu mapigo ya moyo yakinienda mbio kiasi kwamba nikashindwa nifanyaje
"Kaka imekuwaje?"
"Mmmmmm?"
"Imekuwaje?"
"Nilikuwa ninamuomba dereva wa lile gari anipishe njiani ila akawa anashindana na mimi katika kukimbiza gari…..ila kutokana na taa za gari zangu kuwa uwezo mkubwa basi nikajikuta ninamuwashia zote ndio jamaa akaanza kijuchanganya changanya hadi akadondoka"
"Mmmmm huu msala tusepe zetu basi"
"Mmmm siwezi hata kuendesha gari"
"Ngoja mimi nije kuendesha"
Nikashuka ndani ya gari nikiwa ninazunguka nyuma kwenye gari ili niiingie kwenye siti ya dereva nikapata mstuko baada ya kumuona msichana akianza kujivuta taratibu kutoka ndani ya gari huku akilia kwa maumivu makali ikanibidi nianze kupiga hatua za kwenda kumsaidia ila kadri jinsi nilivyo zidi kwenda moyo ukazidi kunipasuka kwani mtu anaye jitahidi kujitoa ndani ya gari ni Manka

ITAENDELEA


*****SORY MADAM*****(15)

AGE……………………………….18+

ILIPOISHIA
Nikashuka ndani ya gari nikiwa ninazunguka nyuma kwenye gari ili niiingie kwenye siti ya dereva nikapata mstuko baada ya kumuona msichana akianza kujivuta taratibu kutoka ndani ya gari huku akilia kwa maumivu makali ikanibidi nianze kupiga hatua za kwenda kumsaidia ila kadri jinsi nilivyo zidi kwenda moyo ukazidi kunipasuka kwani mtu anaye jitahidi kujitoa ndani ya gari ni Manka

ENDELEA
Nikaongeza hatua za haraka kwenda kumsaidia Manka,nikamkuta anatokwa na damu nyingi katika paji la uso wake huku mguu wake mmoja ukiwa umebanwa katika siti,Nikajitahidi kuitoa siti iliyombana Manka hadi nikafanikiwa kisha nikamuweka kando kwenye barabara na kwenda kutazama majeruhi wengine akiwemo Mwalimu Mayange.Nikachungulia chungulia ndani ya gari na ila sikuona mtu yoyote anaye omba msaada kwani ukimya mkubwa ulitawala ndani ya gari na kutokana na giza jingi nikajua moja kwa moja watu waliomo ndani ya gari watakuwa wamefarika dunia ua kupoteza fahamu.
Nikarudi barabarani kumtazama Manka na kukuta hali yake inazidi kuwa mbaya nikamnyanyua na kwenda naye ndani ya gari na kumkuta dereva akiwa amekaa kwenye siti niliyokuwa nimekaa mimi huki akiwa kama amepigwa na bumbuazi kiasi kwamba hawezi kufanya kitu chochote huku jasho jingi likimtoka japo ndani ya gari letu aina ya VX G8 lina Air condition(A.C) ya kutosha.Nikamuingiza Manka ndani ya gari na kumuweka siti ya nyuma kisha na mimi nikaingia kwenye upande wa dereva na kuwasha gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi,nikafika kwenye moja ya zahanati na kumkuta daktari mmoja na nesi ambao wapo zamu ya usiku
Nikamtoa Manka ndani ya gari na kumuweka kwenye kitanda cha matairi kilicho tolewa na nesi kisha wakamuingiza ndani ya chumba na kuniomba nisubiri nje na kunihitaji nikatafute PF3 ya polisi ili hata kama kuna hali yoyote itajitokeza juu ya Manka wao wasihusike kwa chochote.Nikarudi kwenye gari na kumkuta dereva nje ya gari akiwa amejiegemeza kwa unyonge huku akionekana kuwa na wasi wasi mwingi
"Oya kuna kituo cha polisi hapa karibu"
Nilimuuliza dereva na kumuacha akiwa ananitazama kama hajalisikia swali langu nililo muuliza
"Oya broo mbona kama umesizi ni wapi kwenye kituo cha polisi ambacho ninaweza kupata huduma yao?"
"Hapo mbele"
"Wapi?"
"Labda Mombo kule nyuma tulipo toka kwani bado tupo Mombo"
"Powa ingia kwenye gari"
Nikawasha gari na kuanza safari ya kurudi kule tulipotoka na safari hii gari nillizidi kuliendesha kwa kasi ili kuwahi kupata alicho niagiza daktari.Nikajikuta nikifunga breki za gari gafla na kusimama hii ni baada ya trafki mmoja kunisimamisha katika sehemu waliyo pata ajali Manka na ndugu zake na kukuta kuna askari wengine wakiendelea na vipimo vya ajali imetokea tokea vipi huku kukiwa na watu watatu wakiwa wamelazwa kando ya barabara na huku wakiwa wamefunikwa na mashuka maalumu ya polisi na baadhi ya wananchi wakiwa wanashangaa shangaa ajali
"Dreva washa taa ya ndani au ushuke ndani ya gari"
Nikawasha taa ya gari na nikamuona trafki akistuka nikajichunguza na kugundua kuwa chati langu la shule kidogo lina damu.Trafki aliye nisimamisha akaniomba tena nishuke ndani ya gari huku bunduki yake akiishika vizuri na sikuwa mbishi nikashuka huku funguo nikiingiza mfukoni
"Ninaomba leseni yako na kadi ya gari"
Nikaanza kujipapasa kama ninatifafuta leseni yangu kwenye mifuko yangu japo najua kuwa sina leseni ya aina yoyote kwenye mfuko wangu zaidi ya wallet yangu yenye kitambulisho cha shule na pesa za matumizi
"Afande nahisi nimeishahau leseni yangu kwenye gari"
"Mbona shati lako limejaa mijidamu.Lete funguo za gari"
Nikamkabidhi trafki funguo za gari na kwaishara akaniomba niende kumchukulia leseni yangu na kumuacha akimnong'oneza mwenzake.Nikafungua mlango wa gari na kumkuta dereva akiwa na wasiwasi mwingi
"Oya kaka hivi una leseni yoyote hapo ulipo?"
"Ninayo ya kwangu"
"Siwezi kutumia ya kwako?"
"Huwezi kwani ina picha yangu"
Nikaufunga mlango na kumfwata trafki aliye nisimamisha na kila nilipozidi kumfwata huku nikimuita akajifanya kama hanisikii na kuzidi kwenda mbele kuwafwata wezake walipo huku mwenzake aliyekuwa akizungumza naye akielekea kwenye gari letu huku akimulika mulika ndani ya gari kwa kutumia tochi aliyo nayo.Nikamkimbilia trafki kidogo na kumshika shati
"Afande si nina kuita"
"Nahitaji leseni yako na kadi ya gari"
"Kiukweli mimi sina leseni ya aina yoyote hapa nilipo nilikuwa ninakuja kituoni kwenu kuchukua PF3 ya majerugi wa hiyo ajali hapo"
"Ahaaa kumbe nyinyi ndio muli wasababishia ajali hawa watu?"
"Hembu kuwa na akili wewe mimi nimsababishie ajali alafu nije kwenu.Mimi nimewasaidia kama masamaria mwema tu"
Nikajikuta nikizungumza kwa hasira huku nikimtazama trafki kwa jicho la hasira.Kabla hajazungumza kuna mwenzake mmoja akamuita akitokea lilipo gari letu huku akimuamrisha dereva wa gari letu kushuka ndani ya gari
"Oya afande John haya ni mijambazi huku kwenye gari lao kumetapakaa mijidamu siti za nyuma na hakuna mtu"
Askari aliyekuwa kwenye gari letu alizungumza na kuwafanya wezake wapatao sita kuzikoki bunduki zao na kuzielekeza upande nilio kuwepo mimi na dereva
"Wee jamaa yangu vipi hivi ukituona hapa kuna sura ya jambazi.Mimi nimemsaidia huyu mmoja wa majeruhi katika hii ajali na wewe unaniletea habari za kise***"
Nilizidi kuzungumza kwa hasira na kuwafanya askari kunijia juu huku kila mmoja akizungumza lake kwa hasira huku mmoja wao akitishia kunipiga mateke
"Jaribu kunipiga hayo mateke yako uone kama hii nchi utaiona tamu kama unavyo iona sasa hivi"
"Afande hembu niachie nimuonyeshe shuguli huyu kijana tandu nitoke depo nijamuwasha mtu mateke siku nyingi"
"Aroo hembu lipige pingu hilo jambazi linajifanya jeuri.Na haya ndio yale yanayoiba magaria Moshi na kwenda kuyauza Dar"
Dereva wetu akakubali kufungwa pingu na akaanza kupelekwa kwenye gari ya polisi aina ya Toyota.
"Aisee wewe nimekuambia lifunge pingu hilo likijana lisiumize vichwa vyetu"
"Sikilizeni hamuwezi kunifunga pasipo kujua kosa langu ni lipi kwani hamuwezi kukuta damu ndani ya gari na moja kwa moja mukaniambia kuwa mimi ni muhalifua"
"Aisee wewe lipige risasi kama linaleta ujinga"
Nikaitoa simu yangu mfukoni na kumpigia mama ila simu yake ikaita hadi ikakatika,nikarudia tena kuipiga na akapokea simu huku akionekana alikuwa amelala
"Vipi wewe mbona muda huu mumesha fika?"
"Hapana mama kuna askari wametukamata eti wanasema kuwa sisi ni majambazi"
"Majambazi tangu lini na mumekamatwa wapi?"
"Maeneo ya Mombo njia ya kuelekea Arusha….."
Gafla askari mmoja akanipokonya simu na kuanza kuzungumza na mama huku akionekana kuw na hasira nyingi
"Kumbe wewe ndio unaye watuma hawa washenzi wako waje wateke teke magari ya kifaharii na munakazi ya kujikalia na kuitana mama mama pumbavu weee mwanamke mzima umekalia kazi ya kuwatumikisha vijana wadogo ili wakuletee mijigari ya kifahari na hili limoja umelivalisha minguo ya shule ili idanganyie raia barabarani wakati wa usiku Malaya mkubwa wee"
Askari akakata simu na kuidumbukiza mfukoni mwake na kuzidi kunipandisha hasira kwani katika maisha yangu kitu nisicho kipenda ni kuzalilishwa kwa mama yangu
"Aisee hatukubembelezi wewe"
"Sasa niacheni nitakwenda mimi mwenyewe sitaki munishike"
"Pumbavu hakuna kuliachia ndio maana jishati lako limejaa damu kwa ujambazi ujambazi wako"
"Mabroo nawaheshimu sana sitaki tuvunjiane heshima"
"Nenda kule"
Askari mmoja alizungumza huku akinipiga makofi mazito ya mgongo akinisukumia kwenye gari lao na kuninyanyua juju na kunisukumia ndani ya gari na kujikuta nikiangukia kifua na maumivu makali yakaanza kutawala katika kifua changu

ITAENDELEA


***SORY MADAM*****(16)

AGE……………………………..18+

ILIPOISHIA
Askari akakata simu na kuidumbukiza mfukoni mwake na kuzidi kunipandisha hasira kwani katika maisha yangu kitu nisicho kipenda ni kuzalilishwa kwa mama yangu
"Aisee hatukubembelezi wewe"
"Sasa niacheni nitakwenda mimi mwenyewe sitaki munishike"
"Pumbavu hakuna kuliachia ndio maana jishati lako limejaa damu kwa ujambazi ujambazi wako"
"Mabroo nawaheshimu sana sitaki tuvunjiane heshima"
"Nenda kule"
Askari mmoja alizungumza huku akinipiga makofi mazito ya mgongo akinisukumia kwenye gari lao na kuninyanyua juju na kunisukumia ndani ya gari na kujikuta nikiangukia kifua na maumivu makali yakaanza kutawala katika kifua changu

ENDELEA
Dereva akanisaidia kuninyanyua na kunikalisha katika sehemu aliyo kaa yeye kisha baada ya muda wakaziingiza maiti moja huku ikiwa imefunikwa na askari wawili wakapanda na kukaa nyuma tulipo sisi huku wakiwa na bunduki zao kusha mwengine wawili wakapanda mbele upande wa dereva na safari ikaanza
"Yaani nyinyi ngojeni tu mutaona ngoja mama aje"
"Funga bakuli lako shenzi kabisa wewe na mama yako wote tutawasweka ndani munakazi ya kukaa na kuiba iba"
"Sawa sisi si majambazi basi nyinyi ndio mutakuwa majambawazii"
"Unasemaje dogo"
"Nasema kwa pua mdomo unatia saini"
Nilizungumza maneno ya kejeli yaliyo andamana na hasira kumfanya askari kukasirika nusu anizabe kofi la kichwa
"Mimi nawaambia masaa yenu ya kujidai ni sasa hivi ila ngoja hiyo asubuhi"
"Alafu wewe dogo mbona unaongea ongea kama mtoto wa kike unajua tutakupeleka Soweto ukafanyiziwe"
"Mpeleke baba yako wewe k*** nini?"
Nilizungumza kwa hasira na kumfanya askari kumkabidhi mwenzake bunduki kisha akanishika shati langu na kunivuta kisha akanipiga kichwa kimoja kaniangusha na kujikuta nimeilalia maiti ambayo sikujua ni ya nani kisha akaninyanyua na kunitandika ngumi mbili za tumbo na kujikuta nikitoa vilio vya maumivu makali
"Oya bro Sele muache utamuua mtu mwenyewe anaonekana mwili maji huyo"
"Muache nimfundishe adamu analeta maswala ya kiboya,watu tupo kazini hatupo kwenye sherehe"
"Kaka tuliza jazba mpotezee ngoja tufike kituoni"
"Oya Suka hawa moja kwa moja tuwapandishe Lushoto"
"Powa kamanda OVER"
"Eddy mdogo wangu hembu kuwa mstamilivu"
Dereva alizungumza kwa sauti ya upole huku akinitazama kwa masikitiko kwani nilianza kuchuruzika damu kwenye sehemu aliyo nipiga kichwa askari.
"Powa wewe nionee sasa hivi ila zamu yako itafika"
"John unajua nitamchakaza huyu mwehu kwa risasi alafu nipotelee zangu huko milimani"
"Broo wewe mpotezee"
"Oya suka simamisha gari"
Askari aliye nipiga alimuamrisha askari mwenzake anaye enedesha gari kulisimamisha naye akafanya kama alivyo ambiwa.Kisha akashuka na kwenda kukaa siti ya mbele na mwenzake mmoja akaja kukaa tulipo sisi.Kutokana ni usiku hakuna magari mengi tukawahi kufika wilaya ya Lushoto mjini na moja kwa moja wakatupeleka kwenye ofisi zao
"Msachi huyo chalii na atoe kila kitu"
Yule askari aliye nipiga alimuamrisha askari mmoja tuliye mkuta katika kituo chao.Jamaa akaanza kunipapasa na kutoa waleti yangu kisha akaiweka pembeni kisha yule askari niliye mkremisha kwa jina la Sele akaichukua wallet yangu na kuanza kuhesabu pesa nilizo kuwa nazo na kukuta kuna laki mbili na sabini
"Kweli hi mijamaa ni mijambazi tazama pesa zote hizi"
Alizungumza huku akiwaonyesha wezake waliopo ndani ya kituo hicho ambacho ndio kikubwa katika wilaya nzima ya Lushoto
"Wewe jishaue na hizo pesa zangu najua humo kuna laki mbili na sabini ole wako nikute kumepungua hata kumi"
"Alafu huyu dogo ananitafuta tangu tukiwa kwenye gari hivi unataka nikufanyaje?"
"Usijichekeshe chekeshe kama umepata bwana wa bure acha hizo pesa na ole wako ipungue hata kumi"
Nilizungumza kwa hasira na kuwafanya baadhi ya askari kumcheka mweznao kichini chini kwa maneno niliyo muambia ila alivyo wageukia wezake wote wakakaa kimya.Jamaa akampokonya mwenzake kifimbo alicho kishika na kutishia kunipiga nikasimama nikimtazama huku mwili wangu ukiwa umejaa kwa hasira
"Hembu waingize chemba nisije nikavunja sheria za Jamuhuri bure"
Nikageuka na kumtazama dereva nikamuona mwenzangu akitetemeka mwili mzima huku machozi yakimwagika kisi kwamba hadi nikaanza kumuonea huruma.
"Oya broo simu yako iko wapi?"
"Nimeiacha kwenye gari niliichomeka kwenye chaji"
"Ahhaaa sasa kwa nini na wewe usishuke nayo"
"Niliisahau ndugu"
"Ahaa na wewe umezidi uzembe"
Askari aliye kuwa akitukagua akatusukuma akiashiria tutembee kuingia ndani ya chumba chenye mwanga hafifu wa taa ya duara kwa haraka haraka ni kama Walti 40 huku kikiwa na nondo ndefu na pana kwenye mlango wake kiasi kwamba sio rahisi kwa mtu kuuvunja mlango huo
"Ingieni ndani hizo story zenu mutazizungumzia humo ndani"
"Na wewe acha sifa za kutusukuma sukuma unajua hili shati limenunuliwa shilingi ngapi?"
"Sina haja ya kujua limenunuliwa shilingi ngapi cha msingi wewe ingia huko chemba ukakutane na vigego wezako"
"Sawa ila sio kutusukuma sukuma uachage ufala wewe"
"Powaa mimi ---- ila ingia ndani"
Sikujua hata maneno machafu nina yatolea wapi kwani nilizungumza maneno yasiyo na maana na kwa mtazamo wa haraka haraka ukinitazama huto tegemea kuwa ninaweza kuzungumza vitu vya ajabu kiasi hicho.Tukaingia ndani ya chumba na kukuta kuna njemba(Jamaa wenye misuli mikubwa) nne zimakaa huku wakiwa hawajavalia mashati na kuvifanya vifua vyao vikubwa kuonekana kirahisi huku sura zao zikiwa mbaya na za kuogopesha kiasi kwamba mtu hata uwe mbabe kiasi gani ni lazima uyasome mazingira ya humo ndani na ndio uendelee na ubabe wako
"Niaje raia?"
Niliwasalimia kwa ucheshi huku nikijitahidi kuiweka sura yangu katika tabasamu ila salamu yangu haikuitikiwa na mtu hata moja zaidi ya wao kuniangalia kwa macho makali.Dereva akazidi kutetemeka hadi ikafikia hatua suruali yake ikaanza kulowa akiashiria ameshindwa kuizuia hali ya kujikojolea.Mkojo wa dereva ukaanza kusambaa kwenye baraza uku ukienda kwenye mfumo wa kajimstari na kufika katika sehemu aliyo kaa jijamaa moja jeusi lenye mwili mkubwa na ndevu nyingi kama za masanii maarufu duniani Rick Rose
"Oya jibaba huyo mse***kakukojolea"
Jamaa jengine lilizungumza kwa sauti nzito na ya kuogopesha na kumfanya mwenzake atazame mstari wa mkojo ulio igusa suruali yake iliyo chafuka kisha kamtazama dereva na taratibu jamaa likaanza kunyanyuka na kunifanya nikae kimya huku mapigo ya moyo yakinienda mbio kiasi kwamba ujeri wote ukakata kama umeme wa Tanesco
"Oya unyonye huo mkojo wako"
Jamaa lilizungumza huku likimuinamisha dereva wetu kwa nguvu zake zote na kumfanya aanguke kifudi dudi na mimi nikajibanza kwenye kona ya ukuta nikiaangalia nini kitakacho fwata kwa dereva.
"Usinitazame kwa macho ya kike kike nimekuambia linywe hilo kojo lako"
Jijamaa lilizungumza huku mguu wake mmoja akiuweka mgongoni mwa deeva na kumfanya dereva kuanza kuunyonya mkojo wake uliopo juu ya sakafu inayo onekana ni mpya na haina sikiu nyingi tangu iwekwe
"Nimekuambia fastaa"
Jijamaa likazidi kumuamrisha dereva wetu na kumfanya aongeze kasi ya kuunyonya mkojo wake hadi akaumaliza ndipo jamaa akamruhusu dereva kukaa kando.Jijamaa likanitazama mimi kwa macho makali na mimi nikanyanyuka na kujifanya na mimi ninamtazama kwa macho ya kibabe ila ndani ya moyo wangu unao enda mbio kama saa mpya laiti jamaa akijaribu kunitisha kwa kitendo chochote ninaweza kudondoka na kuzimia kwa woga hapo hapo
"Dogo unaonekana mjanja sana wewe"
Kwa sentensi ya jamaa kidogo mapigo ya moyo yakakaa sawa na kijiubaridi kikapenya kwenye mwili wangu kwani tangu niingizwe ndani ya hichi chumba sikuweza kuihisi hali ya ubaridi
"Yap"
Jamaa likanitazama kwa muda kisha likatafuta sehemu na kukaa hapo ndipo nikapata wazo la haraka haraka la kuzungumza huku nikikaa katika sehemu yangu
"Broo yaani ingekuwa sio polisi hawa kutuwahi ningemalizia kumkata yule mwenye gari kichwa chake kama nilivyo wafanya watoto wake wawili na mkewe"
Maneno yangu kidogo yakawafanya jamaa kunitazama kwa wasiwasi huku wakinitazama kwenye shati langu na kuziona damu zilizo jaa kidogo laiti wangejua ni damu za Manka nahisi wangenibamiza mamgumi mengi
"Alafu ninausongo wa kujito muhanga na bomu bora nife kuliko kwenda jela.Hivi ule mfuko wa mabomu uliuficha pale pale ulipo uficha?"
Nilimuuliza dereva swali amabalo naye akabaki anashangaa kwani nahisi ananiona kama nimechanganyikiwa ila lengo langu ni kujitengenezea hofu ya kuogopwa na mijamaa kwa maana bila ya kufanya hivyo usiku kwetu utakuwa mbaya na mrefu japo kwa dereva ulishaanza kuharibika.Nikamkonyeza kwa haraka dereva akatingisha kichwa kwa ishara ya kukubali
"Tatizo lako wewe muoga ndio maana ukashindwa kuyachukua yale mabomo sasa kwa mfano polisi wakiyashika itakuwaje?Na huo uoga uoga wako ndio umekufanya umekunywa mikojo yako laiti ingekuwa ni mimi ningehakikisha asubuhi haifiki chumba kizima kimetapakaa damu"
Mijamaa ikanitazama huku ikionekana kuwa na wasiwasi huku nahisi kila mmoja ananifikiria kivyake.Nikaanza kujipapasa kwenye mifuko yangu huku nikijifanya ninatafuta kitu ambacho sikujua ni nini
"Kile kisu hao jamaa wamekichukua?"
"Ita..akuwa"
"Ingekuwa sio hivyo ningeondoka na roho ya mtu"
Jijamaa moja likavunja ukimya wao huku likijikoholesha koholesha na kunifanya nikae kimya kumsikiliza anataka kusema kitu gani
"Oya daogo umeshatoa roho za watu wangapi hadi sasa hivi?"
"Daaa wengi sana kama kwenye tisini na nane au tisini na tisa"
"Ahaa utaonaje wewe ukamalizia list hiyo na ukawa wa mia moja"
"Mmmm……?"
"Usigune kwa maana tangu uiingie humu ndani una kazi ya kuropoka ropoka tuu oohhoo sijui nijitoe muhanga ohhooo nitamwaga damu.Jinsi unavyo tuona sisi humu ndani ni waauji na nimajambazi sugu tena sana kama unajipenda funga domo lako tuna mawazo yetu sawa?"
Jamaa alizungumza na kunifanya nikaae kimya bila kuzungumza kitu cha aina yoyote huku nikimuomba Mungu asaidie asubuhi ifike mapema ili jamaa wasije wakanifanyia kitu cha aina yoyote.Asubuhi na mapema akaja askari huku akiwa ameongozana na mwanamke mmoja aliye valia suti na nikajua moja kwa moja nikajua atakuwa ameagizwa na mama kujua kutuoa
"Ni wapi hao unao watafuta kati ya hao watu humo ndani?"
Askari alimuuliza mwanamke yule na akaanza kutuangalia mmoja baada ya mwengine na mwisho wa siku akatingisha kichwa kuashiria hayupo mtu anaye mtafuta kati yetu nikajikuta machozi yakianza kunilenga lenga huku nikimtazama mwanamke aliye simama nje ya ya mlango wa nondo.Mwanamke akaondoka na kumuacha askaria akisimama na kututizama kisha akaanza kucheka
"Dogo bado upo eheeee"
Askari akazidi kucheka huku akininyooshea kirugu chake na kuanza kukipiga piga kwenye nondo za mlango wa chumba hicho
"Oyaaa wewe ---- unatupigia kelele"
Jijamaa limoja lilizungumza kwa sauti ya kukwaruza kwaruza huku likimnyooshe askari kidole
"Nyamaza wewe subirini hukumu yenu ya kunyongwa"
"Afande hadi sisi!?"
Nilimuuliza askari kwa mshangao na kuyafanya machozi yaanze kunimwagika
"Tena nyinyi ndio mutakuwa wa kwanza na hiyo minjemba mine itafwatia"
"Acha kumrusha roho dogo wewe hembu tutolee hiyo sura yako kama kisigino chenye magaga"
Jijamaa linguine likamjia juu askari japo amembeza askari kuwa ana sura mbaya ila sura ya jamaa imezidi kwa ubaya kwani imechanwa chanwa kiasi kwamba imekuwa kama mistari ya mipaka kwenye ramani ya Dunia.Askari akaondoka huku akicheka,akili yangu ikaanza kumkumbuka Manka na sikujua kama yupo hai au amekufa na kujikuta nikizidi kutokwa na machozi ya uchungu na nikaanza kumuomba Mungu atende muujiza ili aweze kuyaokoa maisha ya Manka.Mida ya saa tatu asubuhi akaja askari mmoja na kutuita mimi na dereva na kabla sijatoka nikawaaga mijamaa kisha tukamfwata askari na kuingia kwenye ofisi ya mkuu wa polisi wa wilaya na kumkuta mama akiwa amekaa kwenye kiti huku amekasirika kiasi kwamba hata sikuweza kumsalimia
" Na wewe hapo kichwani umechanika na nini?"
"Shikamoo mama"
"Marahaba ehee ninakuuliza apo umechanwa na nini hapo kwenye paji la uso?"
"Kuna askari jana alinipiga kichwa na ngumi za kifuani"
"Kijana unaweza kuniambia huyu askari yupo vipi?"
"Mrefu hizi mweusi anaitwa Sele"
"Ahaa ok ngoja"
Mkuu wa polisi akanyanyua mkonga wa simu ya mezani kisha akaiweka sikioni na kuanza kuzungumza na mtu wa upande wa pili wa simu
"Nakuhitaji ofisini kwangu haraka"
"Ehee na nyinyi hembu nielezeni imekuaje kuaje hadi mukawa hapa?"
Mama alituuliza na dereva akaanza kuzungumza huku akijing'ata ng'ata na anavyo onekana anamuogopa sana mama.Ikanilazimu nianze kumuelezea mama kila kitu kilicho tukuta ila sikutaka kumumbia majeruhi niliye muokoa ni Manka.Yule askari aliye nipiga jana usiku akaingia ofisini kwa bosi wake na kumpigia saluti na akaonekana kustuka kumuona mama akiwa ofisini humo
"Wewe ndio uliye mjeruhi mwanangu kiasi hichi?"
"Muheshimiwa mwanao ni mkorofi tena sana na anamaneno machafu sana"
"Kwahito ndio ummpige kiasi kwamba amechanika hapo usoni,wewe unajua ni jinsi gani nilivyo pata naye tabu huyu mtoto hadi kufikia hatua hiyo aliyo kuwa nayo?"
"Hapana mama yangu ila ukitaka kuhakikisha mwanao ni jeuri jana nilirekodi kila kitu alichokuwa akinijibisha na mimi"
Afande Sele akatoa simu yake kisha akaweka sehemu sauti zetu tulizo kuwa tuna jibishana jana usiku kuanzia tulipokuwa barabarani hadi tulipofika kituoni.Mama akaachia msunyo mkali huku akinitazama kwa macho makali kiasi kwamba nikajikuta ninaanza kuogopa
"Haya afande asante na samahani kwa kukusumbua……Afande Methew huyu kijana wangu niachie mimi nitamnyoosha tuu tembo hawezi kushindwa na mkonga wake"
"Sawa muheshimiwa waziri nimestuka san akukuona huku kwetu asubuhi asubuhi"
"Aaaa wee acha tuu ni kwaajili ya huyu mjinga mmoja hapa.Haya kachukueni kila kitu chenu na niwakute kwenye gari"
Tukatoka na dereva na kup
fitia mapokezi na kukabithiwa kila kitu kilicho chetu kisha tukaenda kwenye gari la mama ambalo ni gari la kazini kwake.Baada ya muda mama akatoka huku akiwa ameongozana na yule asjari aliye nipiga huku wakiwa wanazungumza kama marafiki kisha wakapeana mikono na kutufwata sisi tulipo na safari ikaanza huku akiendesha dereva wa kazini kwake
"Eddy hicho kinywa chako kichafu umekianza lini na nani aliye kufundisha matusi?"
"Hakuna mama"
"Kwa hiyo siku hizi wewe umekuwa hadi unawatukana askari wa watu si ndio?"
"Mama wao walipo anza kukutukana wewe ndi….."
"Ndio na wewe ukaamua kuwatukana….Unajua Eddy sishindwi kukuweka ndani hadi hicho kichwa chako kikae sawa…Unaljua hilo?"
"Likini mama wao ndio chanzo mimi nilikuwa ninarudi kuchukua sijui PF nini huku ili nikamtibu majeruhi tuliye muokoa sasa wao ndio wakaaanza chockochoko hadi wakanilaza ndani"
"Na wewe Hamisi kwa nini ulimuachia huyu mwehu aendeshe gari kazi imekushinda?"
"Hapana mama nakuomba unisamehe"
"Sasa ni hivi itabidi ukanionyeshe huyo majeruhi wanu aliye wachanganya hadi mukajikuta munafanya vitu vya ajabu"
"Mama si wewe uendee tuu"
"Niende wapi?"
"Dar"
"Tena tukitoka kwenda kumtazama huyo mgonjwa wenu sote tunarudi Dar ukanieleze huo utumbo wako ulio ufanya"
"Sawa je na gari tulilo kamatwa nalo lipo wapi?"
"Limesha pelekwa nyumbaini"
"Na nani?"
"Eheee usinihoji hoji maswali yako ya kijinga sawa?"
"Sasa mama hilo ni swali la kijinga?"
"Eddy mwanangu hembu niache kichwa changu kitulie"
Kila tulivyo zidi kuifika Zahanati tuliyo mpeleka Manka jana usiku moyo wangu ukaawa unapoteza amaini kisi kwamba nikaanza kuhisi hali yahatari kichwani mwangu.Tukafika kwenye Zahanati na madaktari walipo muona mama wakaanza kuhaha kwani wanadhani amekuja kwa ajili ya kuwakagua.Mtu wa kwanza kukutana naye ni mganga(daktari) mkuu wa Zahanati hiyo
"Huo ndio utaratibu wenu wa kazi?"
Mama alizungumza huku akimshika shati huku likiwa limejikunja kunja kama limetafunwa na ngombe kisha likatwemwa
"Ha….haapa muheshimiwa"
"Na koti la kazi lipo wapi?"
"MMmmm lilipo ofisini?"
"Sasa hivi saa ngapi na muda wa kuripoti kazini ni saa ngapi?"
Daktari akaanza kubabaika babaika huku akijikuna kuna nywele zake zilizokosa kupitiwa na kitana kwani zimejinyongorota kiasi kwamba ni shida tupu
"Daktari mzima huna hata saa ya mkononi,pili haupo smart kimavazi unazani huyo mgojwa ukikuona wewe si ugonjwa wake unaweza kuongezeka kutokanan na uchafu wako,tatu unaonekana ndio unatoka kuamka mida hii na bado unanuka pombe kiasi kwamba unatia kinyaa.Sijui hata huo udaktari umeupataje"
"Hapana muheshimiwa"
"SNikimaliza unione"
Mama akamuacha daktari na kuafwata wananchi walio kaa kwa wingi kwenye foleni isiyo sogee kiasi kwamba wagojwa wamechoka sana. na foleni hiyoAkawasalimia wananchi na wakamuitikia kwa furaha kisha akaanza kuwahoji mwaswali,nikapata upenyo wa kwenda katika chumba alicho ingizwa Manka jana usiku na nikajikuta wasi wasi wangu ukizidi kuongezeka hii ni baada ya kumkuta Manka hayupo ndani ya chumba hicho

INAENDELEA HAPA
 
weka nyengine basiii...maana kila dakika nakuja kuangalia kama umepost....
 
muda ulipofika umeme si ukakatika nadhani tanesko walijua kama mimi leo naua
 
Weka nyingine basi kabla usiku haujaendelea sana mana hadi nachelewa kazini
 
Back
Top Bottom