Hot story

***SORRY MADAM 24***
ILIPOISHIA
Gafla nikastukia kibao kikali kikitua shavuni
mwangu kikitokea kwa jaamaa na kunifanya
niyumbe na kumgonga nesi mmoja anaye saidiana
na mwenzake katika kusukukuma kitanda cha
matairi na juu yake kuna mgonjwa ambaye
sikuamini macho yangu kwani ni Manka ndiye
aliyelazwa juu ya kitanda hicho kuku sura yake
ikajaa michubuko na amewekewa kifaa maalumu
cha kuhemea huku macho yake akiwa ameyafumba
na hali yake inaonekana sio nzuri
ENDELEA
"Kaka kuwa makini?"
Nesi alizungumza huku akijiweka vizuri na nikabaki
nimeduwaa huku nikiwaangalia wanavyokisukuma
kitanda wakielekea kwenye moja ya chumba
ambacho kina maandishi mekundu makubwa juu
ya malango ambayo yameandikwa ICU huku chini
kukiwa na maandishi yaliyo andikwa CHUMBA CHA
WAGONJWA MAHUTUTI.
Jamaa akanishika tisheti na kunigeuza huku
akirusha ngumi ambayo kabla haijanifikia nikaidaka
na kumuangalia kwa macho ya kumshangaa na
kuzifanya kumbukumba za tukio lake na langu
linalo endelea katika sehemu hii kurudi
"Oyaa brother vipi wewe?"
"Sio vipi stozi zako nimezipata na utajuta kunijua"
Jamaa alizungumza huku akilivua koki lake la suti
kwa dhumuni la kupigana na mimi,Akiwa
anakamilisha kazi yake ya kulivua koti lake la suti
nikampiga ngumi ya pua na kumfanya atoa ukulele
mkali huku akiwa ameinama na kuishika pua
yake,Watu na waauguzi walipo kwenye eneo hili
wakanza kujisogeza kwa haraka huku wengine
wakiomba ugomvi usiendelee,
"Wewe dogo lazima nikutafute tuu sehemu yoyote
na nilazima nikuue"
Jamaa alizungumza huku akishikwa na baadhi ya
watu,sikutaka kumjibu kitu cha aina yoyote zaidi
ya kuelekea kwenye chumba ambacho nilimuona
Manka akiingizwa kabla sijakifikia madaktari wawili
wakanizuia
"Huwezi kuingia humu ndani?"
"Kwa nini?"
"Hichi ni chumba cha wagonjwa mahututi
haturuhusu mtu wa aina yoyote kuingia humu
hususani wewe ambaye umetuchafulia hewa ya
hospitli"
Daktari mmoja alizungumza huku akinitazama kwa
macho makali kiasi kwamba nikajikuta nikibaki
nimemtazama.Nikatoka nje na kuifungua simu
yangu sehemu ya Internet na kuingia kwenye
mtandao wa google na kuanza kuitafuta habari
ambayo nimeiona kwenye Tv,Nikaingia kwenye
tovuti ya BBC Swahili na taarifa ya kwanza kuikuta
ni ambayo inahusiana na kupotea kwa ndege
ambayo hadi wanakwenda mitamboni hawakujua ni
wapi ilipo.Nikajikuta nikizidi kuchanganyikiwa na
kuanza kuzungumza mwenyewe
"Ila mama mimi nilikuwambia usiende ila wewe
umejifanya mbishi unaona sasa yaliyo kukuta"
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika,N
ikaingia kwenye taksi nilio kuja nayo na kumuomba
dereva anipeleke kwenye hospitali aliyolazwa Sheila
"Kaka mbona unalia?"
"Ahaaa hakuna kitu kaka"
"Hapana una ndugu aliye fariki nini hapo
hospitalini?"
"Hapana ila kuna mambo yangu binafsi tuu"
"Sawa kaka ngoja nikuwashie redio usikilize muziki
upunguze mawazo"
Dereva wa taksi akawasha redio ya gari yake na
tukaanza kusikiliza nyimbo kwenye stesheni moja
ambayo sikujua ni stesheni ya wapi.Mara gafla
miziki ikakatishwa na kukaja taarifa ya habari na
sauti nzito ya muandishi wa habari ikaanza
kusikika vizuri masikioni mwangu
"TAARIFA KUTOKA IKULU ZINASEMA NDEGE
ILIYOBEBA VIONGOZI WA NCHI YA TANZANIA YA
SHIRIKA LA KLM IMEPOTEA KATIKA MAZINGIRA
YA KUTATANISHA NA INASADIKIKA KUWA
IMETEKWA NA MARUBANI HAO AMBAO
WAMEZIMA MITAMBO YA RADA INAYO ONYESHA
SEHEMU AMBAZO NDEGE HIYO HUPITA.
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ANAWAOMBA
WANANCHI WAWE WASIKIVU KWANI UMOJA WA
MATAIFA WAMETUMA NDEGE ZA KIJESHI KWENDA
KUIFWATILIA NDEGE HIYO"
Nikajikuta nikijifunga mdomo huku machozi yakizidi
kunimwagika na sura yangu nikaiinamisa chini na
sikutaka dereva aelewe ni kitu gani kinacho
endelea
"Ahhh acha watekwe bwana kwa maana wamezidi
kula pesa za serikali.Watu wanakaa na kujaziana
matumbo yao na sisi wananchi wa hali ya chini
tanazidi kufa kwa tabu kila siku vitu vinapanda
bei"
Maneno ya dereva Taksi yakazidi kuumiza moyo
wangu huku hasira ikinipanda na kujikuta
nikiyang'ata meno kwa nguvu ili kuizuia hasira
yangu na mbaya zaidi katika maisha yangu mimi ni
miongoni mwa watu wagonjwa wa hasira na siku
zote huwa nikikasirika ninaweza kufanya maamuzi
ambayo yatapelekae baadaye kujutia
"Unajua hawa vionngozi wetu wamezidi
kutunyanyasa hapa utakuta walikuwa wanakwenda
kula bata na hao Marubani wamewapatia kweli
kwa maana ni washenzi sana"
Dereva alizidi kuzungumza huku akiongeza sauti
ya redio ili asikilize majina ya viongozi sita
waliomo ndani ya dege hiyo huku wengine
wakitokea Kenya.Jina la mama yangu likwa ni
lasita katika kutajwa na kumfanya dereva taksi
kuanza kucheka
"Haaa huyu mama naye yuopo.....Kweli Mungu
hapendi dhambi kuna siku bwana alikuwa na
dereva wake sasa kwa bahati mbaya
nikamchomekea kwa mbele ile barabara ya
kuingilia K.C.M.C nilikuwa namuwahisha mgonjwa
hospitalini.Ahaaaa alikwenda kunilaza polisi hadi
siku anaondoka Arusha ndio wakaniachia......Tena
hao watekaji kama wanajua wamfanye wa kwanza
kufa kwa maana yule mama roho mbaya sana"
Maneno ya dereva yakazidi kunipandisha hasira
hadi mwili mzima ukaanza kunitetemeka huku
misuli ya mwili wangu ikikaza na kujikuta nikikunja
ngumi na kuipiga kwenye sehemu niliyokuwa
nimeinamisha kichwa na kusababisha kifuniko
chake kuchangukuka
"Aiiseee inakuwaje chalii wangu mbona unanaribia
gari yangu,"
"Funga bakuli lako"
Nilizungumza huku meno yangu nikijitahidi
kuyang'ata kwa nguvu kwani kiwango cha hasira
kinazidi kuongezeka huku mapigo yangu ya moyo
yakienda kwa kasi huku jasho likinimwagika
"Haa wewe vipi umearibu gari yangu unaniambia
ninyamaze....Kama umechanganywa na mambo
yangu ndio unizingu mimi na utalipa tuu"
"Funga bakuli lako nitakuua"
"Wewe ---- kweli nani umuue?"
Dereva alizngumza huku akipunguza mwendo wa
gari,Nikakishika kwichwa chake kwa nyuma na
kukigongesha kwenye mskani mara tatu mfululizo
na nikasababisha gari kuanza kuyumba na likatoka
barabarani na tukajikuta likiingia kwenye mtaro na
kulalia upande wa dereva huku kichwa changu
kukichanwa na kioo kwenye sehemu ya paji la uso
na damu zikaanza kunijaa usoni,Sikutaka
kumuangalia dereva taksi anaendeleaje na
nikaanza kujitahidi kuufungua mlango wa gari na
watu wakaanza kukusanyika na kunisaidia katika
kuufungua kwa kwa nje na kunitoa ndani ya
gari.Kutokana na wenge nikataka kuondoka eneo la
ajali ila wakanizuia huku wakinikalisha chini
kiulazima
"Jamani musimzunguke mpeni hewa ajisikie vizuri"
Jamaa mmoja alizungumza huku akiwasogeza
watu wanao nishangaa,dada mmoja akaanza
kunifuta damu zilizo samba usoni kwangu na
sikujisikia maumivu ya aina yoyote
"Begi langu lipo wapi?"
Niliwaauliza watu na mtu mmoja akaniletea begi
langu na kuliweka sehemu niliyokaa,Nikawaona
wakijitahidi kumtoa dereva taksi ambaye sikujua
kama amekufa au laa,
"Jamani tumuwahisheni hospitali"
"Nipo salama"
"Kaka umeumia damu zinakutoka bado"
"Zitakata zenyewe"
"Dada huyo mnamsemesha hapo akili sio zake cha
msingi ngoja kuna teksi imekwenda kuchukuliwa
tumpeleke hospitali"
Simu yangu ikaanza kuita na dada aliyekuwa
akinifuta damu akaanza kunisaidia kuitoa mfukoni
na akanionyesha namba ambayo kwa ukungu ulio
nitawala machoni mwangu sikuweza kuigundua
kwa haraka
"Ipokee"
Dada akaipokea na kuisikilizia huku akiwa
ameiweka laud speaker
"Eddy upo wapi mume wangu mbona makelele?"
"Samahani dada yangu"
"Wee ni nani unaye ipokea simu ya mume wangu?"
"Mimi ni masamaria mwema mume wako amepata
ajali ya gari na hapa alipo hawezi kuzungumza
vizuri"
"Mungu wangu ni mzima?"
Nikagundua ni sauti ya Sheila na kukumbuaka hali
yeka aliyo nayo ikanibidi nimpokonye dada simu na
kuiweka sikioni
"Baby sijaumia sana?"
"Eddy ni wewe?"
"Ndio mke wagu sijaumia sana na usiwe na
presha"
"Baby usife....nitabaki na nini jamani mume
wangu"
Sheila alizungumza huku nikimsikia akiwa analia
"Baby siwezi kufa nakuomba uache kulia si unajua
hujapona vizuri utazifanya hizo nyuzi za kidonda
kuachia"
"Baby kama haujaumia basi waambiea wakulete
huku hospili"
"Sawa baby ila nyamaza kulia"
Nikakata simu na kuiweka mfukoni na kunyanyuka
nikisaidiwa na baadhi ya watua na tukaingia
kwenye moja ya taksi na nikawaomba wanipeleke
kwenye hospitali aliyo lazwa Sheila na madaktari
wakanipokea na kuniingiza kwenye chumba
ambacho wakananishona kwenye jerala langu la
usoni na kunifunga bandeji.Nikaelekea kwenye
chumba alicholazwa Sheila na kumkuta akiwa yupo
na nesi wakiomba huku mikono yao wakiwa
wameiweka juu ya Biblia na macho yao wakiwa
wameyafumba.Nikawaacha wamalize kuomba na
wakafumbua macho na kuniona nikiwa nimekaa
pembeni ya kitanda alicho lala Sheila na
akaonekana kunishangaa huku machozi
yakimwagika
"Eddy upo salama?"
"Nipo nipo mke wangu sawa"
"Pole mwanangu"
Nesi ambaye ni miongoni mwa masister wa kanisa
la katoliki wanaofanya kazi katika hospitali hii
alinipa pole na nikamuitikia kwa sauti ya upole na
yenye unyonge ndani yeke
"Mwanangu hujaumia sana?"
"Sijaumia sana ni hapa usoni ndio nimechanwa na
kiio cha gari"
"Eddy afandhali hujumia sana ila gari halina
dhamani kwangu kuliko wewe"
"Sikwenda na gari yetu nilikuwa nimepnda taksi"
"Pole sana mwanangu.....ngoja niwaache
ninakwenda kuendelea na shuhuli nyingine"
Nesi akatoka ndani ya chumba na kutuacha tukiwa
kimya,Nikamsogelea Sheila na kumfuta machozi
taratibu na ukimya ukatawala ndani ya chumba
"Eddy"
"Naaamm"
"Mbona unaonekana una mawazo?"
"Ni mama?"
"Amefanyaje?"
"Ametekwa kwenye ndege?"
"Weee"
"Ndio"
"Wewe umejuaje?"
"Nmesikia kwenye taarifa ya habari"
"Mmmm Eddy turudi Dar tukajue ni nini kinacho
endelea"
"Tutarudi hadi wewe upone"
"Nmeshapona mume wangu?"
"Haujapona vizuri mpaka madaktari wakikupa
ruhusa ndio tutarudi Dar"
Simu yangu ikaita na kukuta ni namba ngeni ndio
inayopiaga tena ni namba ya mezani.Nikaitazama
kwa muda kisha nikaipoke
"Habari yako Eddy"
Sauti nzito ya kiume ilisikika kutoka upande wa pili
wa simu na kunifanya nistuke kidogo
"Salama nani mwanzangu?"
"Mimi ni mkuu wa upelelezi wa Taifa nimepewa
jukumu la kukujuisha kitu kinachoendelea juu ya
mama yako"
"Sawa"
"Nina taarifa ambayo sio nzur sana kwa
mama,kwanza tunakuomba usiwe na wasiwasi kwa
maana hali ya abiria wote waliomo kwenye ndege
ya shirika la KLM tumegundua wanaendelea vizuri
akiwemo mama yako na hapa tunafanaya juhudi
za kuwaokoa na nitazidi kukujulisha kila kitakacho
endelea"
"Sawa nashukuru kwa taarifa yako"
Nilizungumza kwa sauti ya unyonge na simu
ikakatwa na nikairudisha mfukoni huku
nikimtazama Sheila
"Wamewapata?"
"Bado"
"Ohoo Mungu wangu msaidie mama yangu mkwe
anusurike na matatizo hayo"
Maneno ya Sheila yaliyojaa huzuni yakaamsha
hisia zangu za kulia na kujikuta nikimkumbatia
Sheila na akaanza kuniliwaza na maneno matamu
"Ni wapi nimekosea kwenye maisha yangu Mungu
wangu kwa nini kila siku ni mimi..Likiiasha hili
linakuja hili kama ni vipi ni bora nife kuliko kupitia
kipindi hichi kigumu kwenye maisha yangu"
Nilizungumza huku machozi yakizidi kuni
kunitiririka huku moyoni mwangu nikiwa nimekosa
amanani na kukata tama ya kushi kabisa duniani
"Eddy kwanini unazungumza hivyo.....Unataka
mimi niishi peke yangu? Unadhani wewe ukifa
mimi nitaishije ninaamini kwamba wewe unaijua
historia ya maisha yangu.Sina baba,Mama,kaka,
dada wala jamaa wa karibu.Eddy wewe ndio
mwanga wangu...wewe ndio baba yangu..wewe
ndio mama yangu.Ukifa wewe na mimi nilazima
nife"
Sheila akazidi kuniongeza uchumgu wa kulia kwani
kusema kweli kila hatua ya maisha yangu
ninayopitia kwangu inamikosi
"Sheila hata mimi nikifa nakuomba usijiue...Mimi ni
mwaname natambua wewe utapata mwanaume
mwengine wa kukuoa ila usije ukafanya hivyo kwa
ajili yangu"
"Eddy hapana wewe ndio kila kitu kwangu kwa
sasa..Japo tunamuda mfupi ila kwako nimepata
tulizo la moyo wangu"
Nikanyanyuka kitandani na kufungua dirisha na
kuchungulia kwa chini nikiangalia watu wanao
ingia na kutoka ndani ya hospitalini hii.Mawazo ya
ajabu yakaanza kunitawala akilini mwangu na
gafla nikamuona mama kwa chini akiwa amekaa
pembeni ya jeneza huku akiwa amevalia nguo
yeupe huku puani akiwa na pamba na akaanza
kuniita huku akilia kwa uchungu kiasi kwamba
nikaanza kuchanganyikiwa,Kwa nyuma yake
akatokea mtu mwenye nyundo kubwa na
kuinyanyua juu na kuanza kumshindilia nyondo za
kichwani na kusababisha damu kuruka na mtu
huyo akaanza kucheka huku akuninyooshea
kidole.Kwa hasira nikapanda kwenye dirishana
kabala sijajirusha nikastukia nikishikwa kwa nyuma
na kuaza kuvuta na madaktari wawili wa kiume
"Eddy mume wangu nini unataka kufanya....Kwa
nini unataka kujiua,Eddy nakupenda tena
nakupenda sana mume wangu kwa nini jamami?"
Sheila alizungumza huku akilia kiasi kwamba
akataka kushuka kitandani ila madaktari
wakamzuia
"Mama yangu amekufa"
"Eddy mama hajafa"
"Mama yangu amekua mimi nitaishi na nini.....Hadi
sasa hivi simjui nani na baba yangu halisi"
"Eddy mama hajafa nakuomba usimpe shetani
mawazo kama hayo yakatawala kichwani kwako"
"Sheila nimemuona mama pele chini yupo kwenye
jenezaa na kuna mtu amempiga hadi amekufa"
"Baby sio mama.....Dokta namuomba mumlete
hapa"
Madaktari wakanikalisha kwenye kitanda na Sheile
hakujali kama anajeraha kifuni kwake,akanivuta na
kunikumbatia kwa nguvu huku sote tukiendelea
kulia
"Mama amekufa"
"Eddy acha kuzungumza hivyo nakuomba
tafandali"
"Sheila"
"Mmmm"
"Unanipenda?"
"Eddy nakupenda tena sana"
"Nakuomba nife"
"Eddy ni nini unacho kizungumza?"
"Sheila mama yangu ameshakufa sina dhamani
tena duniani...Mama yangu ndio rafiki yangu wa
karibu.....Sheila mimi sina upendo wa baba si..."
Sheila akanivuta na kuanza kuninyonya mdomo
kwa nguvu kunizuia nisiendelee kuzungumza,Mada
ktari wakatoka ndani ya chumba na kutuacha
tukiendelea na kitendo ambacho kilianza
kuusisimua mwili wangu.Sheila akauchukua mkono
wangu na kuushikisha kwenye chuchu yake ya
kushoto na nikaanza kuiminya taratibu ila
nikajikuta nikimuachia Sheila
"Sheila unaumwa sitaki tufanye sasa hivi"
"Eddy...."
"Hapana unaumwa"
"Ok mume wangu asante kwa kunijali.....Alafu
baby ukilia unakuwa kama yale makatuni ya Tom
na Jerryjea yakilia"
Nikajikuta nikitabasamu na kumfanya Sheila na
yeye kutabasamu huku akiishika shika pua yangu
na kuanza kuiminya minya kiasi kwamba furaja
yangu ikaanza kunirejea taratibu
"Na wewe ukilia unakuwa kama wale katuni wa
powefull girl machozi yao yanaruka kama maji
haswa yule Babon akilia machozi yanaruka hayo
kama bomba lililo pasuka"
"Jamani baby kwa hiyo machozi yangu yanaruka
kama maji ya bomba lililo pasuka?"
"Ndio unatisha kama nini?"
"Hata wewe ukilia unatisha unakuwa kama yale
mazombi ya wrong turn...Kuna ile sijui ni part one
kuna kazombi kamoja kaliuliwa wacha baba mtu
aanze kulia sasa yule ndio unafanana nye"
Nikazidi kucheka huku na kujikuta nikisahau tukio
lililo tokea katika dakika chache zilizo pita
"Basi na wewe unakuwa kama yule kale kasichana
kwenye wrong turn kalicho mfumania jamaa yake
akiwachungulia jamaa wakifanya mapenzi....Uliona
jinsi kalivyokuwa kanalia kwa hasira"
"Mmmmmm haya baby wewe ndio umeshindi....Mu
me wangu unapenda nikuzalie mtoto wa kike au
wa kiume"
"Nataka wa kike ili mtu akija kumchumbia
kitangulizi cha mahari nataka mabasi saba"
"Hahaa mume wanagu hayo mabasi saba jamani
mtu wa watu atayatolea wapi au ndio hivyo
unataka ujipatie mtaji kupitia mtoto wako?"
"Ndio na atakuwa mzuri kama wewe mama yao"
"Mmmmm mimi nataka wachukue lipsi zako na
macho yako?"
"Sawa itakuwa ni vizuri pia.....Eddy nikuambie
kitu?"
"Niambie"
"Mungu akipenda nahitaji unioe kwa ndoa ya
kanisani"
"Nikimaliza kusoma tuu nafunga ndoa na wewe"
"Kwelu mume wangu?"
"Kweli kwani nahitaji kuyaanza maisha mapema"
"Kweli mume wagu...Alafu nilikuwa nimesahau,Vipi
shuleni kwenu hali inaendeleaje?"
"Mmmm hata mimi sijui inaendeleaje alafu sina
namba ya simu ya mtu wa shule nikamuuliza"
"Mume wangu ninahitaji usome na mimi baada ya
kukuzalia tu mtoto nitarudi shule kusoma kwa
maana nahitaji familia yetu iwe ya wasomi zaidi
hata ukimuhimiza mtoto asome kweli awe
anasoma kweli.....Sio mama unamumbia mtoto
nenda shule wakati wewe mwenyewe shule
hukuipenda"
"Kweli mke wangu ila vipi umeshakula?"
"Baby nilionja onja kwani muda ule nilipopiga simu
na ikapokelewa na mwanamke ndio muda ambao
nilikuwa ninakula chakula na baada ya simu ile
hamu ya kula yote ikapotea"
"Ngoja nikanunue chispi tuje tule...Tena
nimekubuka nikakununulie na simu kabisa sipendi
hivi unavyo azima azima simu za watu"
"Sawa baby ila nakuomba usichelewe na kama
unakwenda tumia gari usipande kwenye hizo
ndubwasha zinazo endeshwa na wavuta bangi na
ukapata ajali bure"
"Sawa baby...ila kwa mbali ninaanza kuhisi kichwa
kinaniuma"
"Pole baby nenda ukanywe dawa kwanza ndio
uende huko unaotaka kwenda"
"Hapa dawa nitazipatia wapi?"
"Mume wangu hospitali nzima ukose dawa za
kunywa.....Sikia nenda kwenye ofisi iliyopo pale
chini ya ngazi kuna masister utawakuta waombe
na watakusaidia"
"Sawa baby"
Nikambusu Sheila mdomoni na kufungua mlango
na kutoka na moja kwa moja nikashuka hadi
kwenye chumba alicho nielekeza Sheila.Nikagonga
mlango mara tatu na suti ya kike iliyopo ndani ya
chumba hicho ikaniruhusu niingie.Nikafungua
mlango na kuwakuta manesi watatu wakiwa
wameshika mashavu yao huku wakionekana
wanyongea na macho yao wameyaelekezea kwenye
kioo cha Tv iliyopo ndani ya chumba hicho.Na
mimi ikanibidi ninagalie wanacho kitazama na
kukuta mipigo ya moyo yakiende kwa kasi baada
ya kuiona ndege kubwa ikiwa imeanguka huku
inawaka moto na kutoa moshi mwingi na mweusi
huku kikosi cha zima moto ambacho sikujua ni cha
nchi gani wakijitahidi kuzima moto kwa kutumia
magari yao maalumu ya kuzimia moto huku baadhi
ya miili inayoonekana kuwa imefariki ikitolewa
ndani ya ndege hiyo

INAENDELEA HAPA
 
Hii hadithi kiboko, Eddy nu mzee wa mikasi tu aisee
 
Tuma moja nyingine please Leo weekend ndio imeanza kesho Hakuna kazi
 
Usiku mwema wapendwa,loh!! Huyu Eddy chiboko...
 
Jamani google mbona kimya? Wk end hii watu tushamaliza kazi zetu tunafanya kuchungulia uhondo lkn hamna, weka hata 5,
 
*****SORY MADAM*****(25)

ILIPOISHIA
Nikambusu Sheila mdomoni na kufungua mlango
na kutoka na moja kwa moja nikashuka hadi
kwenye chumba alicho nielekeza Sheila.Nikagonga
mlango mara tatu na suti ya kike iliyopo ndani ya
chumba hicho ikaniruhusu niingie.Nikafungua
mlango na kuwakuta manesi watatu wakiwa
wameshika mashavu yao huku wakionekana
wanyongea na macho yao wameyaelekezea kwenye
kioo cha Tv iliyopo ndani ya chumba hicho.Na
mimi ikanibidi ninagalie wanacho kitazama na
kukuta mipigo ya moyo yakiende kwa kasi baada
ya kuiona ndege kubwa ikiwa imeanguka huku
inawaka moto na kutoa moshi mwingi na mweusi
huku kikosi cha zima moto ambacho sikujua ni cha
nchi gani wakijitahidi kuzima moto kwa kutumia
magari yao maalumu ya kuzimia moto huku baadhi
ya miili inayoonekana kuwa imefariki ikitolewa
ndani ya ndege hiyo
ENDELEA
"Karibu kaka yangu tukusaidie nini?"
Nesi mmoja aliniuliza swali ila sikumjibu nikabaki
nikiitazama taarifa inayorushwa kupitia kituo cha
televishion ya SKY NEWS kinachopatikana nchini
uingereza.Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio
kana kwamba nimekimbia umbali mrefu pasipo
kupumzika.Nikayasoma maandishi makubwa
yaliopo ubavuni mwa ndege hiyo na kukuta
yameandikwa Emirates kiasi kwamba nikajikuta
nikishusha pumzi taratibu na manesi wote
wakabaki wakinitazama
"Kaka kaka"
"Naam"
"Mbona unashangaa?"
"Ninatazama hiyo taarifa ya habari"
"Inasikitisha sana kwa maana watu wote waliopo
kwenye hiyo ndege wamefariki"
"Imekuwaje hiyo ndege ikaanguka?"
"Ilianguaka kipindi inapaa imesababishwa na hali
ya hewa kutokuwa nzuri"
"Imeangukia nchi gani?"
"Imeangukia Tailand"
Kidogo nafsi yangu ikapata unafuu na tabasanu
likarudi usoni mwangu taratabu kwani nilidhani
itakuwa ni ndege ambayo amepanda
mama.Nikawaomba dawa za kutuliza maumivu ya
kichwa wakanipatia pamoja na maji nikazinywa na
kuwashukuru na kuondoka na kuwaacha
wakiendelea na shughuli zao.Nikaenda kwenye
maduka ya simu ambayo hayakuwa mbali sana na
hopsitali na kununua simu kwa ajili ya Sheila na
kupitia kwenye sehemu wanapouza chipisi.Nikanun
ua chips za kutosha na kurudi hospitali na
kumkuta Sheila akizungumza na madaktari
"Hali yako inazidi kuridhisha na baada ya siku
kadhaa tunaweza kukupa ruhusa ya kutoka
hospitali"
"Kwani hamuwezi kunipata hata leo?"
"Kwa leo ni vigumu inabidi umalizie dozi yako ya
vidonge na sindano za kukausha kidonda na baada
ya hapo tutakuwa huru katika kukuruhusu."
Tukakaa hospitalini siku mbili huku nikiendelea
kumuuguza Sheila na ndani ya siku mbili sikuweza
kupata taarifa yoyote kuhusiana na Mama juu ya
kupatikana kwa ndege yao ambayo imetekwa na
watu wasio julikana.Sheila akaruhusiwa kutoka
hospitalini na akapewa vidonge ambavyo endapo
atajisikia maumivu ameze.Nikapepeleka gari gereji
kufanyiwa ukarabati wa vitu vidogo vidogo na
kumuacha Sheila akijiandaa kwa ajili ya safari ya
kurudi Dar es Salaam
"Kaka hii gari umeinunua wapi?"
"Kwa nini?"
"Nina mwaka wa 21 tangu nianze kutengeneza
magari ila sijawahi kuiona gari ya dizain hii kwa
maana mmmm imekusanya mambo mengi"
"Ahaaa hizi gari mbona zipo ukihitaji unazipata
tuu"
"Aise ila hii gari si chini ya milioni mia na kitu"
"Imezidi zaidi ya hapo"
Niliendelea kuzungumza na fundi mkuu wa gareji
ambayo nimeileta gari yangu,Nikastukia nikiguswa
bega kwa nyuma nikageuka na kukutana na sura
ya Madam Rukia na kunifanya nistuke kiasi
kwamba mapigo ya moyo yakaaza kunienda mbio
"Mbona unastuka Eddy?"
"Ha.....pana nimeshangaa tu kukuona hapa"
"Wife(mke) unajuananaye huyo kijana?"
Fundi gereji aliuliza swali na kujikuta nikizidi
kupata kigugumizi chakuzumza kiasi kwamba
nikaabaki nimekaa kimya
"Ndio ni mwanafunzi wangu wa kidato cha
tano,huyo ndio chanzo cha shele yetu kufungiwa"
"Kaka sura yako inaonyesha mpole kumbe ni
mkorofi kiasi hicho?"
"Hapana mambo ya kawaida"
Nilizungumza huku nikibabaika kwani kila
nikimtazama Madam Rukia ninakumbuka tukio
lililotokea porini na jinsi nilivyo fanya naye mapenzi
kwenye kichaka isitoshe nikakumbuka niliusikia
mlio wa bunduki na kujua ni lazima atakuwa
ameuawa na mkuu wa shule
"Ehee lete story Edy ile siku ilikuwaje?"
Madam Rukia aliniuliza swali baada ya mume
wake kuondoka na kuingia kwenye moja ya
chumba na kuanza kuzungumza na wafanyakazi
wake.Nikamuadisia Madam Rukia kuanzia tulipo
achana hadi nikafika hopsitalini na yeye akaanza
kuniadisia tangu tulipo achana
"Mimi ile siku bwana nilikutana na vijana ambao ni
wanakijiji cha karibu kwenye ule msitu wenyewe
walikuwa wanakwenda kuwinda.....Sasa pale ulipo
niacha mkuu wa shule na wezake si wakawa
wananifwata basi wale vijana wakatanda ile
sehemu tuliyopo na kuanza kuwashambulia
waalimu na kuwatoa mbio za kufa mtu basi ikawa
ndio pona pona yangu"
"Mbona nilisikia mlio wa bunduki alipigwa nani?"
"Ahh mkuu wa shule si alikuwa anajifanya kidume
anapiga bastola juu hewani ili kuwatisha wale
vijana......Wee alipigwa gongo moja la pua hata
sijui ile bastola aliitupia wapi nilisikia akitoa
ukulele wa uwii na kuanza kukimbia....sasa na ile
miguu yake yenye matege ya kaekejea upande
mmoja ungekuwepo ungecheka"
"Mmmm sasa ulirudije mjini?"
"Wale vijana wakaniazimisha simu na nikampigia
my husband(mume wangu) nikamuelekeza nilipo
akaja kunichukua na tukarudi mjini pamoja"
"Ulimuambia jamaa kuhusiana na jinsi ulivyo fika
porini?"
"Ndio ila nilimuambia kuna majambazi ndio
waliniteke...Ehee Madam Merry anaendelea vizuri
amefanyiwa upasuaji na kizazi chake
kimerekebishwa vizuri ila sasa hivi yupo powa"
Madam Rukia alibadilisha mada baada ya mume
wake kufika katika eneo tulilopo na sikuwa na haja
ya kujiuliza ni kwanini amebadilisha mada nikajua
moja kwa moja ahitaji mumu wake atambue kuwa
mimi nilikuwa naye porini
"Hivi wamesemaje kuhusiana na swala zima la
shule kuendelea?"
"Wamesema watatoa tangazo kwenye vyomba vya
habari pele shule itakapo funguliwa ila kwa sasa
wameunda tume ya madai yaliyopelekea shule
kufungwa ambayo itachunguza kila kitu na
wanafunzi walio kamatwa na polisi wapo wengine
wanahojiwa"
"Sasa hiyo tume watatumia muda gani
kuchunguza hayo madai yato kwa maana siku
zinakwenda mbele na masomo ndio hivyo
yamesimama?"
"Mimi wala sielewi ila kidato cha sita na cha nne
wamesambazwa kwenye shule za jirani ili
kuendelea na masomo hadi pale majengo yatakapo
fanyiwa ukarabati nao ndio watarudi"
"Ahaaa...."
"Wewe sasa hivi unakwenda wapi Dar au kwa
Marry?"
"Huyo Merry mimi wala sihiaji kumsikia kwa
maana mume wake amenizingu sana majuzi"
"Wee amekuonea wapi?"
"Si nilikwenda kumcheki hospitalini sasa
nikawakuta wana mazungumzo yao basi mimi
ikanibidi niwaache niondoke zao basi jamaa
akanifwata na kuanza kunipiga vibao mbele za
watu na mimi nikampiga basi mambo yakaharibika
pale hospitali nikaamua kumpotezea"
"Ndio ukaumia hivyo?"
"Hapa nilipata ajali ya gari ndio maana nikafungwa
huu mbadeji"
"Pole mwaya ila yule mume wa Marry anajisikia
sana"
"Kwani anafanya kazi gani?"
"Ni muwekezaji kwenye madini anasimamia
kampuni ya baba yake kwenye kuchimba madini"
"Tena nimekumbuka kuna kitu nahitaji unisaidie?"
"Kitu gani?"
"Si unamjua yule mdogo wa mke wa mwalimu
Nyange"
"Yupi?"
"Tuye mrefu refu kiasi na nimweupe"
"Ahaaa unamzungumzia Manka"
"Ehee huyo huyo"
"Mmmm yule mtoto wa watu anamatatizo sana
kwani ni juzi juzi aliungua na maji ya moto usoni"
"Kwa nini?"
"Akili yake si imemruka yaani zinaingia na
kutoka.Kuna kipindi akili yake inakuwa sawa na
kuna kipindi akili yake inapote hii nikutokana na
ajali iliyo mpata"
Nikaanza kujisikia vibaya moyoni mwangu kwa
maana Manka ni dada yangu japo nimefanya naye
mapenzi pasipo kujua ila bado ni dada yangu
"Hivi kwenye ajali ndugu zake walisalimika?"
"Yaaa dada yake alipona na shemeji yake siku ya
ajali wao walibaki Dar na kutokana na gari yao
kujaa watu"
"Mmmm.......nasikia alikuwa na ujauzito?"
"Ulitoka chezea ajali wewe ila mbona unaniuliza
maswali mengi ambayo ni vigumu kwa mtu kama
wewe kutambua hayo mambo?"
"Kawaida tuu"
Madam Rukia akaondoka na mume wake
wakaniacha nikilisimamaia gari langu lioshwe na
mafundi wasaidizi wa mume wa madam
Rukia.Wakamaliza kulisafisha gari langu
nikawalipa pesa na kuingia kwenye ofisi waliyo
ingia Madam Rukia na mumewe
"Jamani mimi ndio ninaondoka zangu hivi"
"Bwaba mdogo karibu sana"
"Asante na pesa ya matengenezo nimewalipa
vijana wako"
"Hakuna shida nakukaribisha tena na tena"
"Asante madam mimi ngoja niamshe popo"
"Eddy unakiswahili cha kihuni kuamsha popo ndio
nini?"
"Maana yake ni kuondoka"
"Ahaa sasa hembu nianchie namba yako ya simu
endapo kutatokea lolote nitakujulisha"
"Sawa"
Nikamuandikia Madam Rukia namba yangu ya
simu kwenye simu yake kisha na mimi nikajibipu
na nikaisave namba yake nikaanachana nao na
kurudi zangu hospitakini nikamkuta Sheila
akimaliza kuagana na manesi wake ambao
alishaanza kuwazoena kama dada zake na
kuwafanya baadhi ya manesi kumwagikwa na
machozi haswa nesi aliyekuwa akimuhudumia
Sheila kwa karibu sana na ndio alikuwa akiitoa
simu yake kwa ajili ya mawasiliano.Tukaondoka
hospitalini na kurudi katika hoteli tuliyo fikizia na
kuchukua mizigo yetu ambayo tulikuta
imehifadhiwa kwenye sehemu malumu hii ni baada
ya muda wetu wa vyumba tulivyo lipia
ulikwisha.Safari ikaanza taratibu huku nikiendesha
gari kwa umakini mkubwa kuepuka ajali zisizo na
ulazima
"Eddy nakupenda sana mume wangu"
"Nakupenda pia mke wangu"
"Yaani natamani hata tuishi pamoja kabisa"
"Usijali mke wangu tutaishi pamoja"
Tukaendelea na safari huku ukimya ukiwa
umetawala ndani ya gari,Sheila akaweka vizuri siti
yake aliyo kalia na kuanza kulala na kuniacha mimi
nikiendelea kuendesha gari hadi tunafika Mombo
mida ya saa tisa alasiri nikamuamsha Sheila na
tukaingia kwenye hoteli ambayo ninapenda kuingia
kwa kupata chakula nikiwa kwenye safari kati ya
Dar na Arusha.Simu yangu ikaingia meseji na
namba ngeni ambayo si yatanzania huku ujumbe
wake ukiwa ni mfupi sana na kunistua kidogo
‘NIPIGIE'
Nikabaki nikiwa nimeutazama kwa muda huku
nikiwa na maswali kichwani ni nani aliye nitumia
ujumbe wa namna hiyo.Nikaingia kwenye akaunti
yangu ya simu na kununua muda wa kutosha wa
maongezi kisha nikaipiga namba ya simu
"Eddy mwangu hujambo"
Nikaisikia sauti ya mama na nikajikuta nikisimama
kwa haraka na kuelekea kwenye vyoo kuzungumza
na simu ambayo kwangu ni muhimu sana
"Sijambo mama shikamoo"
"Marahaba mwanangu sina muda wa kupoteza ila
ninakuomba uje nchini Iraq tupo kizuizini na
hap....."
Nikasikia mama akitoa kelele za kupigwa na watu
ambao wanazungumza kiarabu ambacho sikuwa
ninakielewa na baada ya muda kidogo simu
ikakata na kujikuta nikianza kupandwa na hasira
huku jasho likinimwagika.Nikatoka na kwabahi
mbaya kwenye mlango wa kuingilia chooni
nikagongana na jamaa anaye onekana ni
sharobaro na kuifanya simu yake ya gharama
aliyokuwa anaichezea kuanguka chini na kupasuka
kioo,Nikataka kuondoka jamaa akanishika mkono
na kunivuta nirudi sehemu aliyo simama
"Wewe ---- umeangusha simu yangu hata
kuniomba msamaha unaondoka ondoka"
"---- mwenyewe kwanza niachie mkono wangu
kati ya simu hako kakopo kako ndio unakaita ni
simu"
"Kwa hiyo mimi unaniita ---- si ndio"
Jamaa alizungumza kwa hasira kiasi kwamba
akanishika tisheti yangu kifuani na kuanza kuikinja
huku akinivuta kiasi kwamba akazidi kunipandisha
hasira.Nikaitoa mikono yake kwa nguvu kifuani
kwangu na kumsukuma jamaa na akarudi nyuma
kidogo na kuanza kunirushia ngumi ambazo
zilinipata kifuani.Nikajirusha na bega langu
kilampiga tumboni kwake kama wanavyofanya
wacheza miyereka na nikamsukuma na sote
tukajikuta tukiangukia mlango wa choo hadi
ukavunjika.Nikanyanyuka haraka na kamkaba
jamaa shingoni kwa muda na kuwafanya watu
walio liona tukio kuja kutuamua
"Eddy mume wangu ni nini unacho kifanya"
Sheila alizunumza huku akinishika mkono
akisaidiana na watu wanao amua ugomvi
kuniondoa katika sehemu ya tukio
"Wewe boya tuu kamlale mama yako ambaye ni
Malaya"
Jamaa alinitukana tusi lililoamsha hasira zangu
upya na kujikuta nikiwazidi nguvu watu walio
nishika na kwenda kumvaa jamaa na safari hii
nikaanza kumshindilia ngumi za hasira kiasi
kwamba jamaa akapasuka sehemu ya jicho lake na
uso wake kujaa damu idadi ya watu ikazidi
kuongezeka na kunitoa katika sehemu ya ugomvi
na kuniingiza kwenye moja ya chumba
kinachotumika kama ofisi ya eneo hili la hoteli.
"Eddy mume wangu punguza hasira nakuomba
tafadhali nipo chini ya miguu yako.Nakuomba
baby"
Sheila akazidi kuendelea katika kunituliza kiasi
kwamba nikabaki nimekaa kimya huku mwili ukiwa
unanitetemeka kwa hasira huku meno yangu nikiwa
nimeyakaza kwa kuyang'ata kwa uchungu na
hasira kwani katika maisha yangu kitu ambacho
kinanichukiza ni mtu kumsema mama yangu vibaya
"Eddy wangu nakuomba uachene na wapumbavu
mume wangu wasikupotezee muda wako...Ehhee
tulia mume wangu sawa"
Sheila alizungumza huku akinikumbatia na kuanza
kunifuta machozi yanayonitoka kwa
hasira,wakaingia askari wawili na wakasimama
mbele yetu huku wakijishauri kitu cha kuniuliza na
mmoja wao nikamkumbuka haraka ni miongoni
mwa askari walio nikamata siku Manka na familia
yake walipo pata ajali na wakanipeleka kituo cha
polisi mimi na dereva wa mama
"Kaka zangu niwasaidie nini?"
"Ahaa tulikuja kumchukua jamaa akatoe maelezo
kituoni kwa tukio zima lililo tokea"
"SIENDI KOKOTE NA OLE WAKE MTU ANIGUSE
NINAKUFA NAYE"
Askri wakakaa kimya huku wakinitazama na
kumfanya Sheila awakonyeze kwa ishara ya
kuniacha hadi hasira zipungue.Askari wakatoka na
kuniacha na ndani ya lisaa hali yangu ikarudi kama
awali hii ni baada ya Sheila kunibembeleza kwa
kila aina ya maneno mazuri ya kuvutia.Tukatoka
ndani ya chumba tulichopo huku Sheila
akinipigisha stori za kunifurahisha na kunifanya
nicheke,Nikakutana na askari waliokuja kunikamata
wakanifwata kiustaarabu na kuniomba niongozane
nao hadi kwenye kituo chao na sikufanya
ubishi.Tukaingia kwenye gari letu na kuongozana
nao huku na wao wakiwa kwenye gari lao na
haikichukua muda tukafika kwenye kituo cha polisi
Nikakutana na baadhi ya wazee wapatao wanne
wakiwa mamevalia mashati ya kijani sura zao
zikiwa zimejikunja baada ya sisi kuingia na
pembeni yao akiwa amekaa kijana niliye pigana
naye na sura yake ikiwa na maplasta huku ikiwa
imevilia damu.Wakaanza kuzungumza lugha ya
kipare ambacho ninakielewa viruzi kwani walianza
kumuuliza kijana wao ni nani aliye mpiga na
akawajana kwa kuninyooshea kidole kuwa mimi
ndio nilio mpiga hadi akaumia sura nzima
"Mimi ni diwani kwani umepiga mwanangu"
Mzee mmoja mwenye kitambi cha wastani
alizungumza kwa hasira na kabla sijamjiu Sheila
akanifinya mkononi na kunifanya nimtazame bila
ya kumjibu chochote kwani nilipanga kupa tusi
ambalo asinge nisahamu maishani mwake
"Mzee wangu ninakuomba umsamehe mume
wangu kwani ni hasira tuu ndizo zilipelekea ugomvi
kati yake na huyo mwenzake"
"Wewe koma mwanamke Malaya mkubwa usiye na
haya wewe unaweza ukamuita huyu kapupwe wako
mume ehee kwanza sijazungumza na wewe"
Mzee akazidi kuzungumza kwa hasira kiasi
kwamba nikajikuta na mimi hasira zikaanza
kunipanda taratibu na Sheila akanishika kifuni ili
jazba ishuke na sikuelewa ni kwanini askari
wamekaa kimya mzee akiwa anazungumza
"Sawa mzee wangu ila ninakomba mumsamehe na
kama kuna gharama zozote tupo tayari kuwalipa"
"Wewe mwanamke huwezi kunilipa mimi....Uliza
hapa mjini mzima wananijua mim ni nani?'
"Mzee wangu naona ustaarabu umekushinda...S
ijaja hapa kusikiliza kuwa wewe ni nani au unakazi
gani.....Na nyinyi mumekuja kunichukua kule ili nije
nikutane na wazee kama hawa wasio na aki....."
Sheila akaniziba mdomo ili nisimalizie nilichokuwa
nikikizungumza kwani kingeamsha ugomvi upya
"Mzee wangu tukauomba utusamehe kwa yaliyo
jitokeza sema kama kuna kiasi chochote chapaesa
ninaweza kukulipa"
Kuepusha shari nikatoka kwenye kituo cha polisi
na kuingia ndani ya gari na kumsubiria Sheila
ambaye baada ya robo saa akatoka na kuingia
ndani ya gari
"Wamesemaje?"
"Wametaka tuwalipe gharama za matibabu pamoja
na gharama za vitu vilivyo haribika kwenye
hoteli.Kumbe yule mzee ndio mmiliki wa hoteli na
yule mwanaye alikuwa kama msimamizi pale"
"Na wanataka kiasi gani cha pesa"
"Milioni moja na nusu"
"Waache upuuzi wao tuondoke watapewa na babu
zao"
"Eddy"
"Tuondoke zetu wasilete uhuni yeye si amesema
sisi hatuwezi kumlipa basi achana nao"
"Edd achana kuwa mbishi mume wangu
wameniomba nije kujadiliana na wewe ili tujue
tunawalipa nini?"
"Ahaa basi majadiliano yetu mimi na wewe ni
kwamba hakuna swala la kuwalipa cha msingi
tuondoke zetu kwanza ninahitaji tufike Dar leo hii
kabla ya saa nne usiku na sasa hivi ni saa kumi na
mbili jioni"
"Eddy nakuomba tuwalipe mume wangu
tuepushane na shari dhidi yao kwani watu
wenyewe wanaonekana hivi hivi ni washirikina"
"Funga mkanda wewe unaogopa wachawi?"
"Ehhhee"
"Na waturoge basi kama niwacawi kweli"
Nikawasha gari na kuondoka eneo la kituo cha
polisi nakuendela na safari huku gari nikiizidisha
mwendo na kumfanya Sheila kuwa na wasiwasi na
mwendo ninao tembea nao kwani ninatembea na
zaidi ya spidi 220 ambacho ni kiwango cha juu na
gari za kawaida za Tanzania mwisho wa spidi
yake ni 180.
"Eddy punguza mwendo basi"
"Ninaharaka mke wangu"
"Jamani baba angu haraka ya wapi wakati
tunaekelekea nyumbani"
"Nataka niwahi kufika ili nipange safari ninahitaji
kwenda Iraq"
"Eddy nimesikia vibaya au.....Unataka kwenda
wapi?"
"Iraq ndipo mama alipo kamatwa na hapa ninataka
kwenda kutoa taarifa kwenye wizara ya mama
wajue wananisaidiaje"
"Mume wangu nitabaki na nini?"
"Si nitarudi kwani ninakwenda kufa huko na hapa
breki ya kwanza ni nyumbani kwetu"
"Sawa mume wangu"
Tukafanikiwa kufika Dar es Salaam saa tano na
robo usiku na moja kwa moja tukafikizia nyumbani
na kupiga honi na akatoka askari huku akiwa
ameishika bunduki yake kwa umakini na kuniomba
nishuke kwenye gari kwani ninahisi hakujua kama
ni mimi
"Eddy habari yako"
"Salama vipi kaka"
"Safi tuu nifungulie geti niingie"
"Siwezi kufanya hivyo kwani bosi ameniambia
nisimruhusu mtu yoyote kuingia ndani"
"Bosi gani na wewe si unajua kuwa hapa ni kwetu
sasa kwanini usiniruhusu?"
"Baba yako ndio amesema nisiruhusu mtu yoyote
kuingia ndani kwani anawageni humo ndani"
"Amerudi lini?"
"Anasiku nne tangu arudi hapa"
"Na ha wageni ndio wamefungua mziki huo kwa
sauti ya juu hivyo?"
"Ndio"
Nikashuka ndani ya gari kufungua geti dogo na
kuingia ndani huku Sheila akinifwata kwanyuma
kwa hatua za haraka,Nikaufungua mlango na
kukuta wasichana nane wakiwa wamevalia chupi
huku wawili wakiw uchi kabisa wakikatika mauono
mbele ya baba ambaye anaonekana amelewa huku
akipiga kelele za kufurahia
"BABA....BABA"
Baba akastuka na kuchukua rimoti ya redio na
kuizima kisha akanyanyuka huku akiwa anayumba
yumba na mkononi kwake akiwa ameshika chupa
ya whyne na akaanza kupiga hatua za taratibbu
kunifwata kwenye sehemu niliyo simama
"Baba ni nini unacho kifanya ina maana wewe hujui
kitu kilicho mpata mama na unakula raha na hawa
machangudoa zako?"
Nilizungumza kwa uchungu huku machozi yakianza
kunilenga lenga
"Wee koma kwanza ni nani aliye kupa ruhusa ya
kuingia humu ndani kwangu?"
"Kwahiyo kwenye nyumba hii mimi sina ruhusa ya
kuingia?"
Nikastukia kibao kikali kikitua kwenye shavu langu
na kunifanya niyumbe na Sheila akanisaidia
kisimama wima nisianguke chini
"Huna mamlaka ya kuzungumza mbele yangu na
kuanzia leo hii mama zako ni wale pale wanao
cheza mbela yangu na mama yako kwanza hajui
mapenzi kitandani.....Ni mzito hajui kukatika
anakaa kama boga lililo ozeana"
Maneno ya baba yakazidi kunipandisha hasira na
mbaya zaidi wasichana alio kuwa nao wakaanza
kucheka kwa dharau huku wakinizomea na
kuongea maneno ya kejeli.Baba akanitazama kwa
macho yaliyo jaa pombe nyingi na kumfwata Sheila
na akatazama kwa muda na kumfanya Sheila
kuanza kutetemeka na gafla akamshika ziwa na
kunifanya nishindwe kuvumilia.Nikamsukuma baba
na akanguka chini na akanipiga teka la kustukiza
na lililonifanya nianguke kama mzigo kisha
akasimama na kuanza kuruka ruka kama
wapiganaji wa kick boxre na kunifanyia kidole
chake akiniomba ninyanyuke ili tupigane
"Eddy usifanye"
Sheila akanishika mkono na kuninyanyua na
kunivuta kwa nyuma huku akinizuia nisipigane na
baba
"Eddy twende zetu nyumbani"
"Wewe malaya unataka kumpeleka wapi
mwanangu"
"Mimi sio mwanao na ninawapa hawa Malaya zako
dakika mbili watoke humu ndani la sivyo nitawaua"
"Ohhh Eddy hii ni nyumba yangu na kuhusu mama
yako hawezi kurudi ndani ya hii nyumba tena
kwani tayari AMESHAKUFA"
Moyo ukaanza kuniuma baada ya kusikia mama
kuwa amekufa,Sheila akanishika kiuno na
tukafungua mlango na kutoka nje huku machozi
yakinimwagika na chuki zidi ya baba ikazidi
kunipanda kiasi kwamba nilatamani kurudi na
kupiga naye ila Sheila akazidi kunionya nisifanye
kitu cha namna hii
"KUANZIA LEO HII MAMA ZAKO NI WALE PALE
WANAO CHEZA MBELA YANGU NA MAMA YAKO
KWANZA HAJUI MAPENZI KITANDANI.....NI MZITO
HAJUI KUKATIKA ANAKAA KAMA BOGA LILILO
OZENA"
Maneno ya baba ya baba yakezidi kujirudia
kichwani mwangu na kuzidi kunichanganya na
kuanza kupanga mipango ya kumuua baba pale
nitakapo pata nafasi,Sheila akaniingiza kwenya
gari na akaingia upande wa dereva na tukaondoka
katika eneno la nyumbani.Ndani ya dakika ishirini
tukafika nyumbabi kwake na tukashuka kwenye
gari akanifungulia mlango ni nakapitiliza mojakwa
moja hadi ndani kwake na kujitupa kitandani na
kumuacha akifunga miliango,Sikutegemea ata siku
moja baba yangu atakuja kinidhalilisha mbele za
watu mbaya zaidi ananizalilisha kuhusia na mama
yangu kipenzi.Sheila hakunisesha chochote zaidi
ya kuvua nguo zake na kupanda kitandani na
kukaa pembeni na akaanza kunivua nguo moja
baada ya nyingine na kubakiwa na boxr.Kutokana
na hasira na kuchoka usingizi mzito ukanipitia na
kulala fofo
***
"Eddy baby kumepambazuka amka ukanywe chai"
"Saa ngapi sasa hivi?"
"Saa tatu"
Sheila akaninyanyua kitandani na kunivalisha ndala
na kuniingiza bafuni na kila kitu anachonifanyia
Sheila sikuwahi kusanyiwa na mwanameke wa aina
yoyote na taratibu nikajikuta upendo ukijijenga
ndani ya moyo wangu na kujiapia kuto kumuacha
Sheila.Nikamaliza kuoga na kwenda moja kwa
moja mezani na tukaanza kunywa chai kwa
pamoja huku akiendelea kunifariji
"Sheila yale ndio maisha ambayo nilikuwa
nikukuambia kuhusiana na baba yangu.....Na sijui
ni kwanini anamfanyia mama vile na kitu kingine
ambacho kinaniumiza roho ni jinsi baba
alivyotembea na mfanyakazi wa ndani na kumpa
mimba tena juu ya kitanda wanacholala na mama"
"Mmmm pole mume wangu ila hapa ninahisi kuna
kitu tu kinachoendelea kwenye hili swala zima la
kutekwa kwa mama na ninavyo kumbuka baba
yako alisema kuwa mama amefariki.......Ina
maana anajua mama kuwa ametekwa"
Nikakaa kimya na kunyanyuka kwenye kiti na
kuingia ndani na kuvaa nguo kwa haraka na huku
Sheila akinitazama
"Baby unakwenda wapi?"
"Nakwenda kutoa taari juu ya sehemu aliyopo
mama kama jana alibvyo niambia kwenye simu"
"Unaonaje tukaenda sisi wenyewe Iraq kwa maana
hapa ninahisia mbaya kuhusiana na lilicho yokea
kwa mama mkwe"
"Ila ngoja kwanza niende nikazungumze nao"
"Eddy nisikilize mimi ninakuomba twende pasipo
kuzungumza na mtu wa aina yoyote kwa maana
hili swala lina mikono ya watu wazito na si bure"
Wazo la Sheila nikalikubali na akaanza kuvaa nguo
zake na kuchakua hati zake za kusafiria na
ikatulazimu kwenda nyumbani kuchukua hati
yangu ya kusafiria kwa maana nisingeweza
kwenda sehemu yoyote pasipo hati hiyo.Tukakodi
taksi hadi nyumbani kwetu nikamuomba dereva
kusimamisha gari mbali kidogo na ilipo nyumba
yetu na nikashuka na kutembea hatua chache hadi
nyumbani na kugonga geti na akatoka askari
"Eddy umerudi tena mdogo wangu"
"Huyu pimbi yupo humo ndani?"
"Ametoka muda huu ameondoka na wale wadada
wa jana usiku"
"Powa naningia ndani dakika kadhaa tuu nitatoka"
"Fanya fasta asije akakukuta"
Nikaingia ndani na moja kwa moja nikaingia ndani
kwa mama na kufugua kwenye droo yake aliyo
tengenezwa kwa chuma na kujengewa ukutani na
nikaingiza namba za siri na ikafunguka na kukuta
vitu maalumu ambavyo ni vya siri sana pamoja na
pesa ya kutosha,Nikachukua hati yangu ya
kusafiria pamoja na pesa zote zipatazo dola za
kimarekani laki moja na nusu ni sawa na milioni 24
za Kitanzania na kuziweka kwenye begi la
mgongoni na kabla sijakifunga ndipo nikaona
katatasi zilizo ambatanishwa kwa pamoja zipatazo
tano huku zikiwa na maandishi makubwa na
nikaanza kuzisoma haraka haraka na kukuta ni
maelezo ya mama
"MIMI GRACE J.MAPUNDA NINAANDIKA NIKIWA
NA AKILI ZANGU TIMAMU PASIPO KUSHAURIWA
NA MTU WA AINA YOYOTE.MALI ZOTE AMBAZO
NINAZIMILIKI NI ZA MWANAGU EDDY GODWIN
PALE ITAKAPOTOKEA NIMEFARIKI YEYE NDIO
ATAKUWA MSIMAMIZI NA MMILIKI MKUU WA
MALI ZOTE AMBAZO NI
1.NYUMBA NINAYOISHI YENYE DHAMANI YA
SHILINGI BILIONI 1.5 ZA KITANZANIA PAMOJA NA
NYUMBA ZANGU TANO ZA KIFAHARI
ZINAZOPATIKANA ARUSHA ZIPO MBILI,MWANZA
MOJA NA TANGA MOJA"
2.MADUKA NANE.HOTEL MBILI ZILIZOPO AFRIKA
KUSINI NA VITEGA UCHUMI VILIVYOPO
UINGEREZA NA MAREKANI IKIWEMO HISA ASILIMI
35 ZILIZOPO KWENYE KAMPUNI YA
UTENGENEZAJI WA MAGARI NCHINI MAREKANI"
3.GARI 8 ZA KIFAHARI"
Sikutaka kuzisoma aina za magari ambayo mama
ameyaorodhesha kwa maana ninayafahamu yote
na kuachana na mambo mengi ambayo mama
ameyaandika na nikajikuta nikistushwa na maneno
yaliyopo karatasi ya mwisho
"MUME WANGU ASIHUSISHWE KWENYE
CHOCHOTE KILICHO ANDIKWA KWENYE HUU
WOSIA WANGU KWA MAANA HAJAHUSIKA KATIKA
KUPANDA NILIVYO NAVYO NA SI BABA HALISI WA
EDDY"
Nikahisi nguvu zikiniishia na swala zima la nani ni
baba yangu liakaanza kunijia kichwani na nikazitoa
karatasi zote zilizopo ndani ya kisanduku maalumu
cha mama na nikafungua droo zake na kutoa cheni
na pete zake za dhahabu na vitu vyenye dhamani
na kuviingiza ndani ya begi na kabla sijatoka ndani
kwake nikakumbuka kubeba albamu yenye picha
zake na zangu kisha nikaridhika nafsini mwangu na
kuufungua mlango na kutoka kabla sijashuka
kwenye ngazi nikasikia mlango ukifunguliwa na
nikaisikia sauti ya baba ikizungumza na watu wa
wili nikachangulia nikawaona watu wawili wakiwa
wamevalia nguo za jeshi huku wakiwa wameshika
nyundo na sururu mikononi mwao
"Nimeshindwa kufungua kijidro kilichopo ukutani na
huyu mwanamke amebadilisha namba za siri"
"Kipo wapi mkuu tukushuhulikie?"
"Kipo huku juu twendeni mukaking'oe"
Nikaingi jikoni na kujibanza kwenye mlango na
wakapita bila kuniona na kuingia chumbani kwa
mama na nikatoka na kushuka kwenye ngazi kwa
haraka na kutoka nje na kuanza kukumbia na kabla
sijafika getini nikaisikia sauti ya baba
"Wewe mpumbavu hapo getini mkamate huyo
mshenzi"
Sikusimama na askari wa getini akanipisha na sote
kwa pamoja tukatoka getina na tukaingia kwenye
taksi na kumuomba dereva aondoke kwa kasi.
"Mbona hujanikamata?"
"Siwezi kufanya hivyo kwa maana mama yako
amanisaidia kwenye mengi na nikifanya hivyo
nahisi hata mbinguni sinto kanyaga"
"Nashukuru ndugu yangu"
Nikafungua begi langu kutoa noti kumi za dola mia
mia na kumpa askari wa getini akanishukuru
kupita maelezo kwa muonekano wake tangu
azaliwe hakuwahi kushika kiasi cha pesa nilicho
mpatia kwa maana anaonekana kuzishangaa
"Eddy kuna gari inatufwatwa kwa nyuma hembu
iangalie sio ya baba yako?"
Sheila aliniambia na kunifanya nigeuke na mapigo
ya moyo yakanza kunienda mbio baada ya kuiona
gari ya baba ikija kwa kasi nyuma yetu na gafla
dereva akafunga breki za kistukiza hii ni baada ya
basi dogo aina ya DSM kujaribu kilipita lori lenye
tela refu na kugongana uso kwa uso na gari ndogo
aina ya VOXY iliyokuwa ikija kwa kasi kwenye
upande na kusababisha ajali mbaya huku gari hizo
zikiziba barabara nzima
ITAENDELA

*****SORY MADAM*****(26)
AGE........................... ..............................
..................18+

ILIPOISHIA
Sheila aliniambia na kunifanya nigeuke na mapigo
ya moyo yakanza kunienda mbio baada ya kuiona
gari ya baba ikija kwa kasi nyuma yetu na gafla
dereva akafunga breki za kistukiza hii ni baada ya
basi dogo aina ya DSM kujaribu kilipita lori lenye
tela refu na kugongana uso kwa uso na gari ndogo
aina ya VOXY iliyokuwa ikija kwa kasi kwenye
upande na kusababisha ajali mbaya huku gari hizo
zikiziba barabara nzima
ENDELEA
Nikafungua begi langu kwa haraka na kutoa noti
mojaya dola mia na kumkabithi dereva taksi kisha
sisi tukashuka ndani ya gari na kuanza kukimbia
rukijichanganya na watu walio anza kukusanyika
wakitoa misada kwa majeruhi wa gari mbili
hizi.Mimi na Sheila tukapanda bodaboda za pikipiki
pasipo baba na watu wake kutuona na kuwaomba
boda boda kutupreleka kiwanja cha ndege cha
mwalimu Julias Kambarage Nyerere pasipo baba
na watu wake kujua ni wapi tulipo elekea.Tukaingia
kwenye sehemu ya kutazama ratiba za ndege
zilizopo kwa wakati huo na kukuta zimesalia
dakika kuni na tano ndege ya shirika la Qatar
Airways na nafasi za tiketi zilibakia tatu
tu.Tukakata tikakata tiketi mbili na kuwa miongoni
mwa abiria wa ndege hii itakayo ondoka ndani ya
dakika kumi zijazo.Kwa haraka haraka tukapanda
mstari na kuanza kukaguliwa na wakaguzi tulio
wakuta kwenye uwanja wa ndege.
"Wewe kijana kaa pembeni"
Askari aliye valia sare zake za kazi huku mwili
wake ukiwa umepanda juu na kujazia kwa misuli
mizito aliniambia huku akininyooshea mkono wake
na kunifanya nianze kupata wasiwasi.Sheila
akaruhusiwa kuingia upande wa pili ili kujumuika
na abiri wengine wanao iwahi ndege.Nikamkonyeza
Sheila asiondoke na anisubiri kwani sikujua ni kitu
gani kilicho mfanya askari huyo kuniambia nikae
pembeni.Wakaja askari wengine wawili wakiwa na
mbwa wakubwa na kusimama karibu yangu huku
mbwa wao wakianza kunimusa nusa
"Kijana tunakuomba utufwate tunamazungumzo na
wewe"
Askari aliye niambia nisimame pembeni
alizungumza huku akiwa amelishika begi langu
lenye pesa na vitu vyangu muhimu.Sikuwa na jinsi
zaidi ya kuanza kumfwata kwa nyuma askari hadi
kwenye moja ya chumba na kuingia naye na
kukutana na askari wengine wawili wakiwa
wamekaa kwenye moja ya meza moja kubwa na
baada ya kumuonamwenzao wakampisha na
kuanza kuuanali kwa macho ya dharau kuanzia
chini hadi juu na kwaishara wakanionyesha
sehemu ya kukaa na nikatii nikiwasubiria
waniambie kitu ambacho wanataka
kuniambia.Nikashangaa kumuona askar mmoja
akilifungua begi langu na baada ya kuziona pesa
zangu akaanza kushangilia kisha akavimwaga vitu
vyote juu ya meza
"Mbona munamwaga vitu vyangu?"
"Tunakagua tunakuomba uwe mtulivu la sivyo
hutotoka mikononi mwetu"
Ikanibidi nikae kimya huku mara kea mara
nikiitazama saa ya ukutani na kuona dakika
zikikatika taratibu huku zikiwa zimebakia dakika
tano tuu ili ndege ifungwe na kuaondoka.Wakaa
nza kuchagua kitu kimoja baada ya kingine na
kuanza kuzisoma baadhi ya karatasi za mama
nilizo ziweka kwenye begi na askari mmoja
akaanza kuipisha kila karatasi kwa wezake na
wakaanza kuisoma taratibu huku wakinitazama
usoni
"Hii si nyaraka ya serkali?"
"Ndio inabdidi atueleze vizzuri kuwa hizi karatasi
za mikataba amezito wapi"
Askari wakaendelea kubishana wao kwa wao huku
wakiendelea kuzitazama karatasia ambazo
sikuzisoma na sikujua ni nyaraka gani wanazo
zizungumzia.Ikanilazimu kuwaomna ili
wanionyeshe karatasi hizo ila wakakataa
"Wewe mikataba ya wizara ya Afya umeitoa wapi?"
"Ehee...."
"Umelisikia vizuri swali langu sina haja ya
kulirudia"
"Mikataba hiyo ni ya mama yangu ambeye ni
waziri wa hiyo sector"
"Aaaa kumbe nyinyi ndio munaowapelekea wazazi
wenu mikataba ili wakasaini ili kuidhulumu serikali
yetu si ndio?"
"Sikia mkuu mimi sio kwamba nimeichukua hiyo
mikataba kwa ajili a kwenda kumpa mama
yangu.....Nyote ninaamini kuwa mujua ya kwamba
mama yangu pamoja na viongozi wengine
wamekamatwa na sijui kuwa nyinyi muna kazi gani
kwa maana hamuonyeshi juhudi zozote katika
kuwakomboa viongozi hao"
Nilizungumza kwa hasira huku nikinyanyuka
kwenye kiti na kuwafanya askari kuchomoa virungu
vyao na kuanza kunisambulia kwa kunipiga
sehemu mbali mbali za mwili huku nikimshuhudia
mmoja waoa akiingiza pesa zangu kwenye mifuko
yake ya suruali na kujikuta nikikasirika na
kumsukuma na kuanza kuminyana naye
kuzichomoa pesa zangu mifukoni mwake na kuzidi
kuwongezea wezake hasira na kuzidi kunipiga
virungu na mateke yaliyo tua tumboni na kifuani na
kuuufanya mwili wangu kunifanya nianze kutokwa
na damu za mdomoni na puani
Gafla mlango ukafunguliwa na akaingia Sheila
akiwa ameongozana na waziri mkuu Bi.Maimuna
Ramadhani na akaonekana kushanga na
kuwafanya askari kuancha kitendo chao cha
kunipiga.Nikabaki nikiwa nimejikunyata chini huku
damu zikiwa zinaendelea kunimwagika huku mwili
mzima ukiwa umetawaliwa na maumivu na uvimbe
kwenye sehemu za kichwa chanu.Sheila akapiga
magoti hukua akilia kwa uchungu na kutoa
kitambaa chake na kuanza kunifuta damu zinazo
nitoka
"Hii ndio kazi muliyo agizwa na serikali kuwapiga
watu kiasi hichi?"
Swali la wa waziri mkuu likawafanya askari wote
kukaa kimya na sikujua waziri mkuu imekuaje
akaja katika chumba hichi ila uzuri ni kwamba ni
rafiki wa mama na muda mwingi huwa
wanashirikina sana katika maswala yao ya kina
mama hususani katika uanzilishi wa mambo ya
vikoba kwa wanamama wajasiriamali
"Eddy Eddy"
"Mmmmm"
Mdomo wangu haukuweza kufunguka kutokana na
kuvimba kwa mdomo ambao pia umejeruhiwa kwa
kupiwgwa na askari hawa ambao sasa hivi
wamejikausha kama wamemwagiwa maji ya baridi.
"Kwahiyo hamuna majibu ya kutoa"
Nikamnyooshea askari mmoja aliye chukua pesa
zangu na kumf anya waziri mkuu kunimtazama
huku akiwa haelewi ni nini kinachonifanya
nimnyooshee mkono,Nikajitahidi kunyanyuka kwa
msaada wa Sheila na akanikalisha kwenye kiti
"Eddy mwanangu pole sana......"
Waziri mkuu akamnong'oneza Sheila na
kumfanaya Sheila kutoka ndani ya chumba na
baada ya muda akarudi akiwa ameongozaa na
mlizi wa waziri mkuu
"Nipe simu"
Mlinzi wa waziri mkuu akatoa simu na kumkabidhi
waziri mkuu na akaminya batani na kuiweka simu
yake sikioni
"Habari yako kaka"
"Sasa kuna vijana wako wamemjeruhi kijana
wangu pasipo kuwa na sababu ya msingi sasa ni
hivi ninakuomba uwafute kazi mara moja"
"Asante"
Waziri mkuu akampa mlinzi simu kisha
akanisogelea na kunitazama kwa macho ya
huruma
"Mwanangu pole sana"
"Asa...n.te"
"Ulikuwa unakwenda wapi?"
"Tulikuwa tunakwenda Iraq mama jana alimpigia
simu Eddy na kumuomba amfwate"
Sheila akajibu kwa niamba yangu kwani mdomo
wangu ulivimba sana na kunifanya nishindwe
kuzungumza vizuri na kumfanya waziri mkuu
kuhamaki
"Alisema you Iraq sehemu gani?"
"Hakusema kwani alipokonywa simu na watu walio
wateka"
Waziri mkuu akaichukua simu yake na kupiga
namba baadhi na kuisikiliazia simu yake na
kukifanya chumba kizima kikiwa kimya
tukimsikiliza
"Shikamoo muheshimiwa Raisi"
"Mimi nipo salama tu kuna taarifa hapa nimeipata
kuwa viongozi wetu wapi Iraq na ndipo walipo
shikiliwa mateka"
"Ndio taarifa nimeipata kwa mtoto wa Grace na
anadai jana alizungumza na mama yake"
"Sawa mkuu nashukuru kwa ushirikiano wako"
Waziri mkuu akakata simu na kuwatazama askari
walio nipiga na kumuagiza mlinzi wake awaandike
majina yao pamoja na namba zao za kwenye
mashati
"Wa..napes....a zan..gu"
Nilizungumza kwa kujikaza japo ninapata maumivu
makali ila ikanilazimu kufanya hivyo na Sheila
akasima na kumsogelea askari niliye mnyooshea
mkono kwa mara ya kwanza na akanza
kumpapasa mifukoni na kuzitoa pesa zangu na
kumfanya waziri mkuu kuzidi kupandwa na hasira
na kumpiga kibao askari huyo na kumfanya azidi
kutetemeka
"Pumbavu...binti watazame na hao wengine"
Sheila akaanza kumpitia askari mmoja baada ya
mwengine na kuzitoa wallet zao na kuchomo pesa
zote walizo kuwa nazo na nyengine hazikuwa za
kwangu ila Sheila akazichukua.Akaingia mkuu wa
usimamizi wa uwanja ambaye ni askari mkuu
"Vijana wako hawa kuanzia sasa hivi sitaki
kuwaona kazini.SAWA"
"SAWA MKUU"
Tukatoka kwenye chumba huku Sheila akinisaidi
katika kutembea na baadhi ya watu wakaanza
kutushangaa kila tunapopita.Tukaingia kwenye gari
ya waziri mkuu na maja kwa moja wakanipeleka
Hospitali ya Muhimbili na madaktari wakanipokea
na kuanza kunifanyia huduma huku wakinichoma
sindano za kupunguza maumivu.Waziri mkuu
akatoa maagizo kwa madaktari nitibiwe katika
uangalizi mzuri la sivyo watakiona cha moto kisha
yeye akaondoka na kutuacha mimi na Sheila.
Baada ya siku mbili nikapata uwezo wa
kuzungumza vizuri kama awali japo kuna sehemu
za mwili zina maumivu makali bado.
"Sheila ile simu ilikuwaje wazari mkuu alikuja
kwenye chumba tulichopo?"
"Alikuwa kwenye dhiara pale uwanja wa ndee na
ndio alikuwa anamaliza kuzunguka kwenye baadhi
ya ofisi.Nikamfwata na kumuelezea na kwabati
nzur nilivyomuelezea kuhusu wewe akanielewa ndio
tukaja mule ndani"
"Aaha nashukuru kwa hilo mke wangu"
"Ila zile tiketi nimezirudisha na nimewaambia kuwa
tumepata dharula ila hadi utakapo pona ndio
tutakwenda Iraq"
"Sawa ila waziri mkuu hakukupigia siku mbili hizi?"
"Alinipigia na nilimuwambia kuwa unaendelea vizuri
na yeye akaniambia zoezi la kuwatafuta viongozi
linaendelea vizuri hatuna haja ya sisi kwenda kwa
Iraq kwani itaongeza matatizo zaidi"
"Sawa ila ndini ya mwili najisikia maumivu sana"
"Sehemu gani?"
"Hapa kwenye kifua kunaniuma sana nikihema hivi
niihisi harufu ya damu"
"Weee ngoja basi nimuite dakari"
Sheila akasimama na kwenda kumuita daktari aliye
kabidhiwa kwa kuniangalia kwa ukaribu
sana.Sheila akaanza kumuelezea dakatari hali
ninayojisikia na kumfa ya daktari kutoa agazo kwa
wezake wanifanyie uchunguzi zaidi.Wakanipeleka
kwenye chumba cha X-reys na wakaniweka
kwenye mashine kubwa iliyokaa kama mfumo wa
jeneza na kunipitisha kwenye mitambo yao na
kutokea upande wa pili wa sehemu hiyo na
wakanitoa kwenye kifaa chao na kunirudisha
wodini na kumuomba Sheila kubaki na madaktari
kwa mazungumzo zaidi.Baada ya muda Sheila
akaingia huku akiwa na sura ya unyonge iliyo anza
kunipa wasiwasi kiasi kwamba nikajikuta ninaaza
kupata wasiwasi na mimi
"Sheila wamekuambiaje?"
Badala ya Sheila kunijibu akaanza kulia na kuzidi
kunichanganya na sikujua ni nini kinacho mliza.
"Eddy ninakupenda sana mume wangu"
"Sawa hata kama unanipenda ila niambie kitu
kinacho kuliza"
"Eddy sitaki kukupoteza mume wangu bado
hatujafikia malengo yetu"
Sheila akazidi kunichanganya kiasi kwamba
nikataka kunyanyuka ila kutokana na maumivu ya
kifua changu nikajikuta nikurudisha kwichwa
changu kwenye mto nilio uegemezea kichwa.
"Eddy madaktari wanasema maisha yako yapo
hatarini kupotea....siku yoyote"
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kiasi
kwamba nikajikuta ninazidi kuchananyikiwa huku
jasho likinimwagika
"Eddy kumbe ulisha wahi kupigwa risasi kwanini
hukuniambia hadi leo madaktari wameniambia
kuwa kidonda chako cha risasi hakikupona
kikamilifu na jinsi askari waliyo kupiga
imesababisha damu kuvilia kwenye mapafu na
kuanza kujenga uzo kwenye moyo wako"
Nikazidi kuchanganyikiwa na kujikuta nikitokwa na
machozi na kumzidisha Sheila kulia kwa uchungu
"Sheila kwahiyo mimi ndio nitakufa?"
"No Eddy huwezi kufa mume wangu.....usizu
ngumze hivyo kumbuka wewe ndio mwanga wangu
we...."
Kabla Sheila hajamaliza kuzungumza akaiingia
daktari mkuu na akasimama kwa muda
akitutizama huku akwa ameshika kikaratasi
mkononi mwake
"Binti umemuambia?"
Sheila akaitikia kwa kutingisha kichwa
akimuashiria daktari kuwa ndio amenimbia
"Binti nilikuambi usimuambie hii itamsababishia
matatizo zaodi kwani moyo wake kwa sasa
unaweza kushindwa kufanya kazi yake muda
woote kuanzi sana na inaweza ikampelekea kifo"
Sikujua daktari kama akili zake zimekamilika vizuri
au laa kwa maana kitu anacho kizungumza mbele
yangu kikazidi kunichanganya zaidi ya alivyo
niambia Sheila na isitoshe amemkataza Sheila
kuniambia kiitu kama hicho na yeye ndio
anakizungumza.
"Sasa hapa kuna karatasi unatakiwa usaini ili
tukamfanyie upasuaji mume wako"
"Ngoja kwanza dokta ni nani munataka kumfanyia
upasuaji?"
"Ni wewe kwani maisha yako yapo hatarini"
"Nyinyi si ndio wale mulio mpasua mgonjwa wa
mguu kichwa na wakichwa mguu"
"Hilo sio jukumu lako na mimi ni mgani.....Binti
siani kwa ajili ya kuyaokoa maisha ya mume wako
na kama upo tayari kumpoteza basi itakuwa hivyo"
Sheila alachukua katatasi mikononi mwa daktari na
akaifungua na kabla hajaandika chpchote
nikamuomba nanionyeshe ili nipitie na mimi.
"CHOCHOTE KINAWEZA KUTOKEA IKIWEMO KIFO"
Maandishi madogo yaliyomo kwenye karatasi
yakanichanganya sana na kujikuta nikimtazama
Sheila ambaye amaeshika peni mkomoni kwa
kusaini kwa niaba yangu.Sheila akasaini na
kumkabidhi daktari karatasi yake na daktari
akatoka kwenye chumba
"Eddy nakuomba ujikaze mume wangu"
"Kwenye kufa Sheila hakuna kujikaza hawa
madaktari mimi sina imani nao kabisa"
"Usijali kwa hilo mume wangu"
"Kwani hiyo oparesheni ninafanyiwa lini?"
"Leo hii mida na yamebaki masaa kama mawili"
"Sasa imekuwaje na wewe ukasaini pasipo
kuniambia kama ninafanyiwa leo kwa maana hapo
kwenye hiyo karatasi kumeandikwa chochote
kinaweza kutokea ikiwamo kifo sasa unaona ni
haki kweli?"
"Eddy acha kupanic"
"Sio kupanic......Wewe kwanini usaini si
uneniambia kuwa yamebaki masaa mawili nisinge
kubali kufanyiwa ningesubiria hadi mama
apatiakene ili hata nikifa nife vizuri"
"Eddy usitake unilize sasa hivi mume wangu
hembu tulia madaktari wanajua ni nini wanafanya"
Baada ya masaa wawili wakaingia amadaktari
wawili akiwemo yule daktari wa familia
akaonekana kushangaa kuniona ndani ya
chumba,Hakunisemesha akatoka ndani ya chumba
na sikumfwatilia sana kwani manesi walianza
kuniandaa kwa kunpeleke kwenye chumba cha
upasuji huku wakinibadilisha nguo na kunivisha
vazi maalumu kwa ajili ya upasuaji.Wakamaliza na
kuniweka kwenye kitanda cha matairi na kuanza
kukidukuma huku Sheila akiwa pembeni yangu na
machozi yakaanza kumwagika tena
Nikastukia nikamuona daktri anaye sukuma
kitanda akisukumwa na kuanguka chini na macho
yangu yakakutana na macho ya baba yaliyojaa
hasira hadi yakawa mekundu.Akanishika kifuani na
kunivuta na kunitupa chini na kuanukia mgongo na
kusababisha maumivu makali kuzidi kunitawala
kwenye mwili wangu hususani kifuani
mwangu.Madaktari wakataka kumsogelea baba ila
akachomoa bastola yeka na kuwafanya madaktari
kusita.Mguu wa baba ukatua kifuani kwangu huku
ukiwa umevalia buti lake la jesi kisha bastola yake
akaikoki tayari kwa kunifyatulia risasi

INAENDELEA HAPA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…