Hot story

Hot story

Hii ni weekend jamaa aweza kuwa kazidiwa majukumu ya kifamilia au hana Internet access tuwe na subira. google2014 senkyuu berimachi.
 
Last edited by a moderator:
Mmh! Hadi mwili umesisimka, maskini Eddy, pole!
 
*****SORY MADAM*****(27)
AGE.................................................18
ILIPOISHIA
Nikastukia nikamuona daktri anaye sukuma
kitanda akisukumwa na kuanguka chini na macho
yangu yakakutana na macho ya baba yaliyojaa
hasira hadi yakawa mekundu.Akanishika kifuani na
kunivuta na kunitupa chini na kuanukia mgongo na
kusababisha maumivu makali kuzidi kunitawala
kwenye mwili wangu hususani kifuani
mwangu.Madaktari wakataka kumsogelea baba ila
akachomoa bastola yeka na kuwafanya madaktari
kusita.Mguu wa baba ukatua kifuani kwangu huku
ukiwa umevalia buti lake la jesi kisha bastola yake
akaikoki tayari kwa kunifyatulia risasi
ENDELEA
Nikastukia baba akitoa ukulele na kuanguka chini
na kumuona Sheila akiwa ameshika kipande cha
mbao kinachoonekana kimechomolewa kwenye
benchi huku kikiwa kinavuja damu kwenye sehemu
ambayo ilitua kichwani mwa baba.Sheila akaanza
kutetemeka baada ya kumuona baba akiwa
anavujwa na damu za kichwa,Madaktari
wakaninyanyua na kunirudisha kwenye kitanda
huku hali yangu ikizidi kuwa mbaya na mamcho
yangu yakaanza kutawaliwa na ukungu na
kwambali nikamuona Sheila akishikwa na askari
wawili na wakaanza kumtoa enje akiwa ananililia
kwa uchungu.Kitanda nilicho kilalia kikaanza
kusukumwa taratibu na jinsi ninavyo isililizia hali
yangu yenye maumivu makali ya mwili nikajikuta
macho yangu yakitawaliwa na ukungu mwingi na
sikujua ni kitu gani kinacho endelea
***
Baridi kali ikaanza kunisumbua mwili wangu na
kujikuta nikianza kufumbua macho yangu na
kujikuta nikitazama sehemu ya juu ambayo kwa
haraka haraka sikujua nipo wapi.Mwili wangu
ukawa umebanwa kidogo na na kwa haraka haraka
nikagundua kuwa nipo kama nilivyo zaliwa kwani
kiwamgo cha baridi kilitawala mwili wangu
mzima,nikajariu kujigeuza ila nikajikuta nikishindwa
na nikaanza kujisukuma na kumbukumbu za akili
yangu ikagundua kuwa sehemu niliyopo ni katika
majokofu ya kuhifadhia miili ya watu walio fariki
dunia.Nikajaribu kuita ila sikusikia msaada wa mtu
wa aina yoyote wala kitu kikitembea nje ya
majokofu hayo,Nikazidi kujitahidi huku miguu
yangu nikiigonga gonga kwenye sehemu ya chini
ya jokofo ambapo ndipo miguu yangu ilipo elekea
na kujikuta sehemu niliyo ilalia ikienda mbele na
kufunguka.Nikaendelea kujikaza huku nikizisidi
kujitahidi kujitoa ndani ya jokofu hili na
chakumshukuru Mungu nikafanikiwa kulifunua kwa
uwazi mdogo ulio niruhusu kuitoa mikono yangu
kwa nje na kujivuta na likafunguka na kupata
uwezo wa kukaa na kitako na kuanza kushangaa
Woga ukaanza kunitawala na baada ya kujikuta
nikiwa nimeshonwa katikati ya kifua changu na
kitu kingine kilichoizidi kuniogopesha ni miili mingi
ya watu walio lala chini huku wakiwa
wamefunikwa malailoni yanayo waonyesha vizuri
huku miili yao ikiwa imeharibiwa sana huku
wengine vichwa vyao vikiwa vimepasukwa na
kurudishiwa rudishiwa kiasi kwamba wanatisa kwa
muonekano wao.Nikashuka kwenye jokofu nililo
kuwepo na taratibu nikaanza kuutafuta mlango wa
kutokea katika chumba hichi na kabla sijauona
nikastukia taa za chumba zikizima na giza kali
likazidi kutawala
Nikajikaza na sikutaka kuuruhusu woga kutawala
katika mwili wangu kwa wakati huu,Nikapapasa
papasa ukutani kwa dakika zaidi ya mbili na
kufanikiwa kukuta mlango na kabla sijaufungua
nikasikia watu wakizunumza kwa nje
"Muambie huyo Mudi awashe hilo genereta la
upande huu kuna maiti tunataka kuziingiza humu"
"Kwani hao nao wametokea wapi?"
"Kuna basi limeanguka na kuua watu ishirini"
"Sasa huku ndani si kumejaa hadi maiti nyingine
tumeziweka chini tutafuta ustaarabu wa kuwatoa
kesho wakazikwe na manispaa kwa maana hata
ndugu zao hawajitokezi"
"Hawa tutawaweka hivyo hiyo bwana kwani hatuna
seemu nyingine ya kwenda kuwaweka na hospitali
zote za wilaya mochwari zao ni ndogo"
Watu waliopo nje wakaendelea kujibishana
nikataka kupiga kelele za kuomba msaada ila roho
yangu ikasita na kujua ni lazima watu waliopo nje
wataogopa na kukimbia na ningelisitisha zoezi
zima la wao kuingiza maiti wanazo
zizungumzia,Taa zikawaka na mlango nikausikia
ukifunguliwa na baada ya dakika kakika moja
mlango ukafunguliwa
"Hembu shika huko vizuri usije ukamuachia"
Gafla umeme ukakatika na kuwafanya watu walio
ibeba maiti wanayo taka kuuingiza kuanza
kutukana matusi mazito na kwakupitia uwazi
mdogo wa mlango nikastukia kuona wakiondoka
kwa hasira huku maiti wakiwa wameilaza chini na
sikujua ni wapi wanapo elekea,Nikachungulia nje
na kukuta kuna giza ila mwanga wa mbalamwezi
uliweza kunisaidia kuona baadhi ya majengo na
kungundua bado nipo sehemu ya Muhimbili.Nikaa
nza kuoiga hatua za haraka na kutoka ndani ya
chumba cha kuhifadhia maiti na nikafika kwenye
jengo ambalo nikakuta kamba nyingi zikiwa
zimeanikwa makoti meupe ya madaktari.Nikal
ishusha moja kwenye kamba na kulivaa kwa
haraka kisha nikachukua suruali nyepe na kuivaa
na muonekanao wangu ukawa kama wauduzi wa
kiume kwenye hospitali hii.Nikaanza kutembea
kuelekea getini huku miguuni nikiwa nipo peku
peku na nikafanikiwa kutoka pasipo walinzi
kunitilia mashaka ya aina yoyote.Nikatafuta
sehemu na kukaa huku akili yanu ikianza kufikiria
ni kitu gani kilicho wafanya madaktari hadi
wakanipeleka kwenye chumba cha kuhifadhia
maiti.Nikajikuta nimejishika tama na kugundua
mashavu yangu yamejaa ndevu nyingi na
kwaharaka haraka nikagundua ni kipindi kirefu
nimekaa hospitali kwani ndevu zangu huchukua
muda mwingi sana katika kuota na kuwa ndefu
kama nilivyo zikuta sas
Nikapata wazo la kwenda nyumbani kwa Sheila
japo ni mbali sana na sehemu niliyopo nikaona
sina budi kufanya hivyo.Nikapiga moyo konde na
kunyanyuka sehemu niliyo kaa na kuanza
kutembea japo njaa kali inanisumbua tomboni
kwangu ila nikajitahidi kwenda kutembea kwa
haraka ili niweze kufika,Nikatumia kama masaa
mawili na kufika nyumbani kwake na kukuta
ukimya mwingi ukiwa umetawala ila kitu kingine
kilicho anza kunipa wasiwasi ni nyasi nyingi na
ndefu zilizo oto nje ya geti lake na kwaharaka
nikajua Sheila hayupo ndani ya nyumba yake kwa
maana kama angekuwepo kusingekuwa na nyasi
nyingi huku geti lake likiwa lemetawaliwa na vumbi
jingi.Ikanibidi kuchungulia kwenye eti lake ili
kujionea mwenyewe nikipingana na mawazo yagu
ya kusema Sheila hayupo ndani ya nyumba
yake.Giza lilitawala kwenye nyumba yake na
hapakuwa na dalili yoyote ya mtu kushi na jinsi
mlango tulivyo ufunga siku ya mwisho ndivyo jini
ulivyo kwa sasa.Nikashusha pumzi nyingi huku
nikitazama wapi nielekee na mbaya zaidi sikua na
jirani yoyote wa Sheila ninaye mjua ambaye
ninaweza kumuulizia habari za Sheila
Hali ya uchunu ikaanza kunitawala na kwa mbali
machozi yakaanza kunilenga lenga na kujikuta
nikitamani utokee muujiza Sheila kusimama mbele
yangu,Wazo la kuwa na mama likaanza kunijia ila
kutokana na kuchoka nikashidwa kujua kama
nitaweza kwenda nyumbani ambapo tulikuwa
tunaishi ila woga ukaanza kunijia kwani
kumbukumbu ya baba siku alivyokuwa akinipiga
ikanijika kichwani kama mkanda wa video ila
ukakata gafla baada ya kusikia mnguruo wa mbwa
ukitoka nyuma yangu.Nikageuka na kukutana na
mbwa wakubwa wawili wakiwa wananguruma huku
wakinitazama kwa macho yao makali kiasi
kwamba nikajikuta nikiaanza kutetemeka.Nikatulia
kwa muda huku mwili wangu ukishindwa kukimbia
kabisa kutokana na njaa kali iliyopelekea nguvu za
mwili wangu kuniiishia.Nikasikia mlunzi wa mtu
akiwaita mbwa walio karibu yangu na wakaelekea
walipo itwa na kumuona mlinzi wa nyumba ya
jirani akiwa amesimama huku mbwa wake wakiwa
wamenzunguka na mkononi mwake akiwa
ameshika bunduki yake aina ya gobore
"Samahani kaka"
Nilimuita mlinzi kwa sauti ya kukwaruza kwaruza
huku nikianza kupiga hatua za taratibu za
kumfwata sehemu alipo na kabla sijamfikia
akaikoki bunduki yake na kunielekezea
"Usipige atua nyingine ya kunfwata la sivyo
nitakulipua"
Nikasimama huku nikiwa ninamwangalia mlinzi na
sikua na cha kufanya zaidi ya kuwa mnyonge
mbele ya mlinzi huyo
"Samahani kaka yangu kuna kitu ninaomba
nikuulize"
"Uliza fasta fasta"
"Eti huyu dada aliyekuwa akiishi humu ndani yupo
wapi?"
"Kwani wewe ni nani yeke?"
"Mimi nilikuwa ni mchumba wake?"
"Unaudhibitisho gani kwamba wewe ulikuwa ni
mchumba wake?"
"Ninaweza kukutajia jina lake"
"Anaitwa nani?"
"Sheila"
"Sasa wewe itakuwaje usijue habari za mchumba
wako?"
"Ni hstoria ndefu ndugu yangu"
"Sasa kwa ufupi huyo demu yupo jela"
"JELAA.....!!!?"
"Unashangaa nini sasa.........? Wewe si ulitaka
kujua ni wapi alipo huyo demu?"
"Jela gani?"
"Sijui yupo gereza gani ila ukweli ni kwamba
amefungwa"
"Amefungwa kwa kosa gani?"
"Kaka mimi sio hakimu bwana kama unataka
nenda Kisutu kaulizie watakuambia"
Wasiwasi ukaanza kunijaa mwilini mwangu na
kujikuta chozi likinitoka na sikutaka nilie mbele ya
mlinzi
"Kwani leo ni tarehe ngapi?"
"Wewe jamaa umevurugwa na nini hata tarehe
umesahau?"
"Naoma tu nijue ndugu yangu"
"Ni terehe 15 mwezi wa sita haya hadi mwezi
niemkutajia unaweza ukachapa lapa kwani bosi
wanu akitoka hapa akikuta ninazungumza na watu
kibarua changu kinaweza kikaota mbawa bure"
Nikajikuta nikizidi kufadhaika kwani nimiezi mine
imepita tangu nilipo kutana na tatizo la kupigwa na
walinzi wa uwanja wa ndage.Nikaondoka kinyone
huku nikitazama tazama nyuma nikitamani
nimueleze mlinzi njaa ninayo ihisi tumboni kwangu
hata kama anaweza kunipatia chakula kidogo ila
nikashindwa kwani tayari alishapandwa na
hasira.Nikaendelea kutembea huku sijui ninapo
elekea kwani mawazo mengi yanakizungusha
kichwa changu kiasi kwamba ninajikuta nikiongea
ongea mwenyewe.Nikakuta watu wapatao sita
wakiwa wamelala kwenye maboksi nje ya baraza
za maduka mengi na kujikuna mimi nikikaa kwenye
moja ya baraza ambayo ukuta wake umechorwa
picha za wasichana na kugundua ni saloon ya
wanawake.Usingizi haukuweza kunijia na kila nilipo
jaribu kuutafuta nikajikuta nikijipiga piga mwilini
kuwaua mbu wanao ning'ata mwilini mwanu.Hadi
kunaanza kupambazuka nikajikuta nikipitiwa a
kausingizi kazito na kujikuta nikilala kwenye sakafu
pembezoni mwa geti la salooni hii ya kike
Nikastukia mguu ukinigonga gonga begani
nikayafumbua macho yangu na kukuta mwanga wa
jua ukiwa uemshatawala eneo zima,Macho yangu
yakakutana na msichana mrembo akiwa amevalia
suruali nyeupe iliyo mbana vizuri na kuyafanya
makalio yake makubwa kuonekana vizuri huku sura
yake akiwa ameipamba kwa vipodozi vinavyo
onekana ni vyagharama.Mkononi mwake akawa
amezishika funguo nyingi na tukabaki
tumetazamana
"Unanianaliangalia nini hembu nyanyua mindevu
yako nahitaji kufnugua geti langu"
Nikanyanyuka na kusogea na kukaa pembeni
kidogo,akafungua geti lake la saloon na kuingia
ndani na kuanza kupana vitu vyake.Watu wengi
wanapita mbele ya macho yangu huku kila mmoja
akionekana kuwa na mihangaiko yake ya kutafuta
chochote kwa siku hii.Nikapiga miyayo ya uchovu
na kusimama ila nikashindwa kupiga hatau yoyote
kutokana na kuchoka sana,Nikakaa chini na
kuanza kutafakari ni nini nifanye ili kuweza kupata
hata kifungua kinywa nikachungulia ndani ya
saloon na kumuona dada wa saloon akiendelea
kufanya usafi.
"Samahani dada ninaweza kukusaidia japo kufagia
fangia"
"Kwani nilikuomba unisaidie?"
"Hapana ila nimeomba tuu kama ninaweza
kukusaidia"
"Usije ukawa kibaka ukaniibia vitu vyangU humu
ndani"
"Hapana dada mimi sio kibaka"
"Haya njoo unipigie deki"
Nikanyanyuka huku nikiwa na fauraha kidogo ya
kuweza kupata chochote cha kula,akanipa tambara
la deki pamoja na kindoo chenye maji kidogo na
nikaanza kupiga deki taratibu huku nikijitahidi
kusafisha kila sehemu ya salooni hiyo.Nikamaliza
na kupiga deki kwenye eneo zima la Saloon
"Tayari dada yangu"
"Haya asante"
"Dada yangu naomba japo kajipesa nikanunue
kifungua kinywa"
"Haaa kumbe ulikuwa unapiga deki ili nikulipe.......
? Mimi nilidhani umenisaidia bure"
"Hapana mimi ninaomba japo kidogo tu niweze
kupata kifungua kinywa"
Dada akafungua pochi yake na kutoa shilingi mia
mbili na kunipa nikabaki nikiitazama kwa sekuende
kadhaa pasipo kusema chochote na kwajinsi ya
ugumu wa maisha ya Dar es Saalam yalivyo
magumu kwa shilingi mia mbili siwezi kupata
chochote nitakacho weza kula.
"Dada yagnu huwezi kuniongeza japo mia tatu ili
iwe mia tani niweze kupata chochote tuu"
"Kaka yanu hiyo ndio hela niliyo nayo na kama
unataka kifungua kinywa jana niliacha kiporo cha
ubwabwa wa mchana unaweza kufungua hilo
hotpot hapo juu ya meza utakiona chakula"
Sikuwa na jinsi nikalisoelea hotpot alilo nelekeza
na kulifungua na kukutana na harufu kali ya
ubwabwa ulio chacha ambao umepikwa na nazi
huku ukiwa na maharage yake.Nikakitaama kwa
muda kisha nikaanza kukila haraka haraka na
kunya dada wa Saloon akibaki akiwa ananitazama
kwa macho ya mshangao.Ubwabwa ukaanza
kuniongea ila nikajikuta ukiwa unaelekea ukingoni
kwani niliufakamia fakamia kwa haraka,nikajilamba
vidole vyangu kwa utamu nilio upata kisha
nikasima na kunawa mikono yangu kwa maji niliyo
pigia deki
"Asante dada yangu"
Dada wa Saloon akabaki akiwa amenitazama huku
akikiangalia kifua changu na kugundua kuwa
anatakuwa amestushwa na mstari wa oparesheni
niliyo fanyiwa
"Nakuomba utoke ndani ya Saloon yangu kabla
sijakuitia polisi kwani unaonekana wewe ni
jambazi"
"Kwa nini?"
"Usitake kujua kwa nini au unataka nikupigie kelele
za mwizi?"
Sikutaka makuu ya kubisha na dada wa Saloon
nikaondoka huku nikiwa ninajisikia vibaya kwa jinsi
maisha yangu yalivyo badilika.Nikaondokoka na
kuelekea nyumbani kwetu huku nikijifariji liwalo na
liwe.Nikiwa njiani nikajiku nikisimama na baadhi ya
watu wanaosoma magazeti kwenye kibanda kidogo
na gazeti moja lina pichwa kubwa ya Sheila huku
pembeni yake kukiwa na kitanzi na juu yake kukiwa
na maandishi makubwa yaliyo nistua na kujikuna
nikianza kutetemeka yanayo someka
"MUUAJI WA MTOTO WA WAZIRI AHUKUMIWA
KIFUNGO CHA KUNYONGWA HADI KUFA"
ITAENDELEA

***SORY MADAM*****(28)
AGE........................... ..............................
.....................18+

ILIPOISHIA

Sikutaka makuu ya kubisha na dada wa Saloon
nikaondoka huku nikiwa ninajisikia vibaya kwa jinsi
maisha yangu yalivyo badilika.Nikaondokoka na
kuelekea nyumbani kwetu huku nikijifariji liwalo na
liwe.Nikiwa njiani nikajiku nikisimama na baadhi ya
watu wanaosoma magazeti kwenye kibanda kidogo
na gazeti moja lina pichwa kubwa ya Sheila huku
pembeni yake kukiwa na kitanzi na juu yake kukiwa
na maandishi makubwa yaliyo nistua na kujikuna
nikianza kutetemeka yanayo someka
"MUUAJI WA MTOTO WA WAZIRI AHUKUMIWA
KIFUNGO CHA KUNYONGWA HADI KUFA"
ENDELEA
"Haaa...!!"
Nilishanga kwa sauti ya juu na kuwafanya watu
walipo pembeni yangu kunishangaa kiasi kwamba
nikajikuta nikitazamana nao huku wakinishangaa,N
ikataka kuondoka ila dada muuza magazeti
akaniita na kunifanya nirudi sehemu alipo
"Kaka nahisi nimesha wahi kukuona sehemu?"
"Labda utakuwa unanifananisha"
"Hapana wewe ndio Eddy?"
Moyo ukanistuka na kujikuta nikitaka kukimbia ila
miguu ikaishiwa ujasiri wa kufanya hivyo na
kujikuta nikianza kutetemeka.
"Huyu si ndio jamaa aliyesemekana kuwa
ameuliwa?"
"Ndio huyu"
Watu wakaanza kubishana mmoja baada ya
mwengine huku kila mmoja akionekana
kunishangaa hadi wakanizunguka
"Jamani muacheni kaka wa watu aondoke
munamshangaa hadi anajisikia vibaya"
"Sasa si tunataka kujua ni nini kilicho mpata"
"Jamani hembu acheni wanga mimi ndio
nimemuita sasa kila mmoja akiwa anataka kujua ni
nini kilicho mpata kaka wa watu ni umbea"
Watu wakaendelea kubishana wenyewe kwa
wenyewe na dada mwenye kibanda cha kuuza
magazeti akanishika mkono na kunivuta pembeni
na tukaingia kwenye moja ya duka lililopo pembei
ya kibanda hicho na kumuomba muhisika wa duka
hilo kutupa nafasi kidogo ya kuzungumza na
muuza duka hakuwa na lakupinga akatupatia viti
viwili na tukakaa
"Najua utajiuliza ni kwani ni nimekutoa kule
kukuleta huku ila ngoja kwani nijitambulishe.
...Mimi ninaitwa Judith na nimuuza maazeti pale
kwenye kibanda ndio ofisini kwangu na mimi
nimekuwa ni msomaji mkubwa sana wa stori ianyo
endelea sasa kwa huyu dada Sheila kumuua mtoto
wa waziri hadi jana alipo hukumiwa kunyongwa
hadi kufa"
"Ina maana Sheila ndio ameniua mimi?"
"Kaka yangu mimi wala sijajua kama huyo dada
ndio muhusika ila kwa msaada ngoja nimpiie
mchumba wangu ambeye ndio muandishi wa
habari yako aje hapa tujuae ukweli"
Judidh akatoa simu yake na kumpigia mtu aliye dai
ni mpenzi wake na baada ya muda jamaa akafika
sehemu tulipo akitumia usafiri wa pipipiki aina ya
boxer.Judith akampisha mpenzi wake kwenye kiti
alicho kaa na yeye akasimama pembeni na jamaa
akanipa mkono huku akionekana kunishangaa kwa
jinsi nilivyo
"Mimi ninaitwa John ni muandishi wa habari wa
gazeti"
"Nashukuru kukufahamu"
Judidh wakabaki wakiwa wametazamana pasipo
kuzungumza kitu cha aina yoyote kisha John
akakohoa kidogo huku akiaachia tabasamu pana
mdomoni mwake na kuanza kuzungumza
"Kaka mimi ni miongoni mwa watu walio tokea
kuguswa na tukio lako la kusemekana kuwa
umekufa ila nikaamua kulifwatilia kina ubaga hadi
sasa hivi ninaanza kupata picha ambayo itaweza
kumsaidia mpenzi mpenzi wako katika kuachiwa
huru.......Nilizungumza na Sheila akanielezea kisa
kizima na alidai kuwa ameonewa kwa maana
tangu siku ambayo wewe ulipelekwa katika
chumba cha kufanyiwa oparsheni ndio siku ya yeye
alipo kamatwa na polisi kwanza akashikiliwa kwa
kosa la kutaka kumuua mkuu wa jeshi ila kutoka
na ushaidi kutoka kwa manesi na madaktari
ukamsaidia sana Sheila kuishinda kesi ya
kumjerehi baba yako ambaye alitaka kukuua
hadharani"
"Ina maana baba yangu yupo hai?"
"Ndio yupo hai na nimiongoni mwa watu walio nipa
vitishi endapo nitaendelea kulifwatilia hili
swala......."
"Mama yangu je yupo hai?"
"Mama nilipata habari kuwa amelazwa nchini
Afrika kusini kwani alipata ugonjwa wa mstuko wa
moyo na hadi sasa hivi sijajua anaendeleaje"
Nikashusha pumzi nyingi huku nikijaribau kusubiria
ni nini kilitokea katika maisha yangu ila sikupata
pichaya aina yoyote
"Ishu ilikuwa hivi.......Alitengenezwa mtu anaye
fanana na Sheila na kwakupitia picha rada zilizopo
hospitali alionekana akitoka kwenye chumba
ulichokuwa umelazwa huku akiwa ameshika
sindano mkononi na kwamadai ya madaktari
wakasema kuwa msichana huyo ndio amehusika
kwa kukuchoma sindano ya sumu iliyo pelekea
maisha yako kuwa mwisho"
"Ngoja kwanza unataka kuniambia kuwa Sheila
yeye hakuuhusika na chochote?"
"Ndio Sheila hajausika na kiyu cha aina yoyote juu
ya kukuchoma sindaono kwa maana kipindi tukio
la wewe kuchomwa sindano linatokea Sheila
alikuwa mikononi mwa polisi na hadi sasa hivi
ninavyo zungumza Sheila ndio huyo siku zake zina
hesabika"
"Huyo daktari aliye dhibisha kuwa nimechomwa
sindano ya sumu ni yupi huyo?"
"Ngoja nikuonyeshe"
John akatoa simu yake na kuwela upende wa video
na nikamuona daktari wa familia akiwa
anazungumza kwa masikitiko makubwa na mbele
ya waandishi wa habari na kunifanya nibaki
mdomo wazi
"Sasa huyu mzee ndio mbaya wenu katika hii
familia?"
"Kwa nini?"
"Yeye ndio chanzo kikubwa cha baba yako na
mama yako katika kugombana?"
"Wewe umejuaje?"
"Mimi nilimuhoji siku akiwa amelewa sana kwa
maana huyu mzee ni mjomba wangu na akanieleza
vitu vingi sana juu ya familia yako"
"Vitu gani?"
"Kwanza yeye ndie aliye muambia baba yako kuwa
wewe sio mtoto wake wa kumzaa na kitu kikubwa
kilicho msababisha baba yako kuchukua uamuzi
wa kutaka kumuua mama yako pamoja na wewe ili
kuweza kuzirisi mali zote ambazo mama yako
anazo"
"Mmmm sasa mimi mbona ninafanana sana na
baba yangu?"
"Ndio kutokana baba yako ana pacha wake
ambaye ni doto na yeye ndio baba yako wa damu
na wao wanafanana sana kiasi kwamba ni vigumu
sana kwa mtu kuweza kutambua kuwa wewe baba
yako si huyo mkuu wa jeshi"
Ni habari mpya katika maisha yangu kwani mama
yangu hakuweza kuniambia siku hata moja kuwa
baba yangu ni pacha wa baba yangu wa sasa
ambaye amejenga chuki kubwa juu yangu na
mama yangu,Nikajikuta machozi yakianza
kunimwagika
"Kaka jikaze usilie ila huo ni ukweli ambao mimi
ninakuambia na huyu daktari mimi ni mtu wangu
wa karibu ukiachilia kuwa ni mjomba wangu ila ni
zaidi ya hapo kwani vitu vyake vingi huniambia
kiasi kwamba vingine siwezi kuvizungumza
hapa........Ila ninakuomba sasa hivi tukajaribu
kuyaokoa maisha Sheila ambeye niliapa kumsaidi
Sheila hadi mwisho wa maisha yake tana kuna hii
sauti niliirekodi kipindi anazungumza kwa uchungu
na mimi"
‘NI KWELI SIJAMUUA EDDY WANGU MIMI
NINAMPENDA SANA NA YEYE NDIO MWANAUME
WA NDOTO ZANGU.....MIMI NIPO RADHI KUFA
KWA AJILI YA MUME WANGU EDDY NIKAONANE
NAYE PEPONI KWA MUNGU.....JOHN NAKUOMBA
USIJISUMBUE SANA KWA AJILI YANGU KWANI
MIMI HUU NDIO MWISHO WA MAISHA YANGU"
"HAPANA SHEILA USILIE MIMI NIPO TAYARI
KUKUSAIDIA KUUVUMBUA UKWELI JUU YA HILI
KWANI SIAMINI KAMA WEWE NDIO MUUAJI"
"HAPANA JOHN WEWE NIACHE TU NIKAFUNGWE
SINA JINSI YA KUFANYA NA HUU NDIO MWISHO
WA MAISHA YANGU BAI JOHN"
John akazima simu yake baada ya kuniona
ninazidi kutokwa na mahozi mengi na akaniomba
nikaze twende tupate msaada wa mwana sheria
wa serikali.Tukasimama na John na kutoka nje ya
duka huku sura yangu nikiwa nimeiinamisha chini
ili watu wasiyaone machozi yangu,Tuakapanda
kwenye pikipiki yake na moja kwa moja tukaelekea
kwenye mahakama ya Kisutu na John akanipeleka
kwenye ofisi za mwanasheria wa serikali aliye
simamamia kesi ya kuhukumiwa kwa Sheila na
kitendo cha kuingia kwenye ofisi yake kikamfanya
mwana sheria huyu kustuka kiasi kwamba
akanyanyuka na kubaki akinitazama
"Mkuu samahani kwa kukuingilia ofisini kwako
pasipo kuwa na taarifa maalumu ila kama unavyo
one mbele yako nimekuja na Eddy ambaye
inasadikika ni mfu"
Mwanaheria wa serikali akabaki amesimama
pasipo kujibu kitu cha aina yoyote na kubaki
akibabaika pasipo kujibu kitu cha iana yoyote
"Mkuu tunahitaji msaada wako wa hali na mali"
"Ehhee umesema amefufuka?"
"Hilo mimi sijui atasema mwenyewe kwamba
amefufuka ila kidhibitisho ni kwamba Eddy
mwenyewe huyu hapa na hajafa kama mulivyo
mdhania ila ninakuomba uweze kutusaidi
kuhairisha mauaji ya Sheila"
"Dooo watakuwa wanakaribia kumua kwani
zimebaki dakika 45 tu kabla hajanyongwa"
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kiasi
kwamba nikajikuta nikanza kuzunguka zunguka
ndani ya ofisi ya mwanasheria wa serikali na
kuwaacha John na mwanasheria wa serikali
wakizungumza
"Tunakuomba sana uweze kutausaidi kama
tunaweza kwenda kumuona"
"Ahaa sasa hiyo ni ngumu kwa maana amesha
kabidhiwa kwa askari maalamu wana shuhulika na
hilo swala kwa hiyo mimi siwezi kwenda"
"Nipo chini ya miguu yako kiongozi ninakuomba
twende au tuambie tu niwapi alipo"
"Kwa hilo mimi siwezi kuzungumza chochote juu
ya hilo"
John akapia maoti huku sura yeke ikiwa ina
mwagikwa na machozi na ila mwasheria akaanza
kutingisha kichwa cheke akishiria hataki
kukubaliana na kile anacho obwa na John.Kwa
hasira nikapiga hatua hadi sehemu aliyo simama
mwanasheria wa serikali na kumvuta tai yake na
kumsogeza karibu na sura yangu iliyo jaa ndavu
nyingi na nikamuangalia jocho kali kiasi kwamba
akabaki akiwa ananitazama kiwoga
"UNAKWENDA AU HUENDI?"
"Mmmmm"
Nikaishika shingo ya mwanasheria mkuu na
kuinamisha kwenye meza yake kwa hasira na kwa
haraka nikachukua peni iliyopo kwenye meza na
kuishusha kwa kasi hadi kwenye shabu lake na
kuanza kuigandamiza kwa kwa nguvu huku mwili
mzima ukiwa unanitetemeka kwa hasira
"Nakwenda nakwenda......"
Mwanasheria mkuu alizungumza huku akitoa
ukelele wa kulia,nikamnyanyua na kumuamrisha
kutangulia mbele huku nikiwa ninamfwata nyumba
huku nikiwa karibu yake sana endapo atajaribu
kukimbia tu ningemfanya kitu ambacho asinge
kisahau kwenye maisha yeke.Kila tulipo pita watu
walinishangaa na hatua chache kabla mwanasheria
wa serikali hatujafika kwenye maegecho ya magari
akachomoka kwa kasi akikimbia kitendo
kilichonifanya na mimi kukimbia kwa kasi zaidi
yake na uzuri wenyewe yeye ni mnene na
anakitambi likubwa
Kwa nguvu zungu zote nikarusha teke lililo mpiga
kwenye miguu yake kwa nyuma na kumfanya
aanguke kama mzigo wa kuni na akaangukia pua
kitendo kiliho shuhudiwa na watu wengi ikiwemo
askari walio anza kukimbia wakija kwenye eneo
tulilopo huku bunduki zao zikiwa mikononi mwao
huku wakinimrisha nisifanye kitu cha iana yoyote
na John akabaki akiwa haamini kitu alicho kiona

INAENDELEA HAPA
 
Back
Top Bottom