*****SORY MADAM*****(32)
AGE..........................................18+
WRITER...................................EDDAZARIA
G.MSULWA
WAALIKE RAFIKI ZAKO WALIKE HII
PAGE,ASANTENI SANA
ILIPOISHIA
Kwa haraka nikanyanyuka na kutoka nje ya
mgahawa na kutokana na magari mengi
ikanilazimu kuvunja seheria za barabara na
kujikuta nikivuka kwa haraka barabara na kabla
sijamalizia nikashtukia nikikumbwa na gari lililo
nirusha na kuangukia pembeni ilipo simama
taksi aliyopo Sheila
ENDELEA
Nikatulia chini kwa muda na kumuona Sheila
akifungua mlango kwa haraka na kushuka ndani
ya gari na akaonekana kunishangaa baada ya
kunijua ni mimi,nikajaribu kujinyanyua ila
nikajikuta nikishindwa kutokana na mguu wangu
mmoja kutawaliwa na maumivu makali.Nikastuka
baada ya kugundua mguu wangu wa kushoto
umevunjika japo kichwani na mikononi
nimepatwa na michubuko iliyosababishwa na
kuaanguka na kuserereka kidogo kwenye
barabara ya lami.Sheila akaoanekana kupigwa na
bumbuazi kwani hakuzungumza kitu cha aina
yoyote zaidi ya kubaki akinitazama hadi watu
walipo anza kukusanyika na kuwaomba wauguzi
wa hospitalini kunisaidia,
Nikawawekwa kwenye machela na kuingizwa
ndani pasipo Sheila kuzungumza kitu cha aina
yoyote kwangu,Nikaingizwa kwenye moja ya
chumba ambacho ni chaupasuaji na kwa haraka
nikachomwa sindano za ganzi kwenye mguu wa
kushoto ambao umevunjika na kawanipaka
mafuta kisha wakamipitishia kifaa maakumu
kinachotoa mwanga mwekundu wenye miyonzi
mikali huku dakitazama picha inayopita kwenye
Tv ndogo iliyopo ndani ya hiki chumba wakaona
ni sehemu ya ambayo mguu umevunjika na
wakaanza kazi ya kunihudumia
Ndani ya lisaa moja wakamaliza upasuaji wao na
kunifunga bandeji kubwa kisha majeraha madogo
madogo wakayapaka dawa kisha wakanihamishia
kwenye wodi kitu ambacho ninakiona ni
chatofauti ni huku kufanyiwa upasuaji pasiopo
kuchomwa sindano ya usingizi.Sikuweza kupata
rafiki wa kunijulia afya yangu na kitu kinacho
niumiza sana akili yangu ni jinsi hali ya mama
ilivyo na kingine sikujua kama ameweza
kusalimika mikononi mwa baba ambaye ndio
amekuwa adui yetu namba moja kwenye familia
yetu.Sikua ya kwanza ikakatika huku nikiwa sijui
kitu kinacho endelea ila zaidi nikawa
ninahudumiwa na kupewa chakula na wauguzi wa
hospitalini.
Wiki moja ikakatika na hali yangu ikaendelea
kuwa nzuri zaidi na nikaanza kufanyishwa
mazoezi ya kutembea na siku hii nikamuomba
muuguzi kunipeleka kwenye sehemu kilipo
chumba alichomo mama na hakusita na kwa
mwendo wa taratibu tukafanikiwa kufika ila
sikuweza kumpata mama na ikanibidi kumuuliza
muuguzi huyu kwa lugha ya kingereza
Hivi huyu mama humu ndani amekwenda wapi?
Mama yupi?
Kuna mama waziri ambaye alilazwa humu
chumbani
Sijajua labda tukaulize sehemu zenye rekodi ya
wagonjwa kwa maana mimi sihusiki katika kitngo
hichi na kama unavyo iona hospitali yetu ilivyo
kubwa siwezi kuwajua wagonjwa wote
Sawa dada yangu basi nakuomba unifikishe hiyo
sehemu wanayo angalizia orodha ya wagonjwa
Cha kumshukuru Mungu huyu nesi hana makuu
zaidi ya alicho kifanya ni kunipeleka hadi sehemu
wanayo angalizia idadi ya wagonjwa walipo
kwenye hospitali hii na kadri tunavyo litafuta
jina la mama kwenye kumputer yao hawakuliona
na ikanibidi niweze kuuliza jina la daktari Emmy
na jibu nililo lipata kutoka kwa mfanyakazi wa
ofisi hii ya takwimu za hospitali likazidi
kunichanganya
Hapa hospitalini kwetu hatuna jina la daktari
anaye itwa Emmy na dokta anaye anziwa na
herufi ya E ni mwanaume na anaitwa Emmanuel
Kweli huyo daktari hayupo....Mbona ana hadi
kitambulisho na kitambulisho kinacho
muonyesha kuwa yeye ni daktari wa hii
hospitali?
Wewe ulikutana naye wapi?
Tanzania na nikapanda naye ndege moja hadi
hapa
Mmmm hapa mulikuja lini?
Kama wiki moja iliyo pita
Ngoja kwanza
Msichana anayehusika na maswala ya takwimu
akanyanyua mkonga wa simy ya mezani kisha
akaminya baadhi ya namba na kuiweka simu
yake sikioni
Kiongozi ninashida moja ninakumba unisaidie
Kuna tatizo limejitokeza la hawa madaktari feki
kuendelea kuivamia hospitali yetu na
wanaendelea kufanya matukio ya ajabu
Basi ninakuja sasa hivi
Akakata simu na kuniomba niogonzane naye
huku nesi anaye nifanyisha mazoezi akinishikilia
vizuri na tukaingia kwenye lifti na ikatupeleka
hadi gorofa ya tatu na tukaingia kwenye chumba
ambacho nikakuta tivi nyingi ndogo ndogo
ambazo idadi yake kwa haraka haraka zinaweza
kufika hamsini na kila Tv inaonnyesha sehemu
yake na nikagundua zinaonyesha picha za kamera
za ulinzi zilizo fungwa ndani ya hii hospitali
Una rekodi za wiki nzima?
Ndio ninazo
Ninaomba utuwekee za siku saba za nyuma
Jamaa anaye onekana ndio muongozaji wa
kamera za humu hospitali akaigeukia Tv moja
kubwa kama nchi 32 kisha akachuku CD ndogo
na kuziingiza kwenye deki ndogo na tukaanza
kuangalia video zilizo chukuliwa ndani ya wiki
moja na nikajikuta nikinyoosha kidole changu
kwenye moja sehemu hii ni baada ya kujiona
nikiingia hapa hospitalini siku ya kwanza nikiwa
na Emmy na kumfanya jamaa kuisimamisha
sehemu hii kisha akaisogeza kwa ukubwa kiasi
(ZOOM) na kuiangalia sura ya Emmy ambaye
alizidi kunichanganya baada ya kumuona dada
wa ofisi ya takwimu akitingisha kichwa huku
akiibenua midomo yake
Mmmm hatuna daktari kama huyu
Kaka hembu peleka mbele
Jamaa akairuhusi CD kutembea na kuanza
kuangalia picha za mbele na kujiona nikiingia
ndani ya chumba alichokuwa mama kipindi
ninatoka kuzungumza na Emmy baada ya kuanza
kuhisi hali ya ajabu,Video ikamuonyesha Emmy
akizungumza na askari ambaye alikuwepo pale
mlangoni kisha yeye akaingia ndani huku
akiitazama camera ya ulinzi iliyokuwepo juu.
Hii ni Camera namba 38 ngoja niweke video
zake kwani huu ni mkanda wa jumla
Sawa fanya hivyo
Na huyo askari hapo ni wa hapa?
Askari huyo aliletwa na ubalozi wa Tanzania
kumlinda huyo mama.....Kwani wewe huyo
mama ni nani yako?
Mama yangu mzazi
Jamaa akaito CD aliyokuwa ameiweka kwenye
deki kisha akatafuta CD nyingine ndogo na
kuuweka kwenye deki yake na tukaendelea kuona
matukio yaliyo endelea eneo la nje ya chumba
alicho lazwa mama baada ya mimi kuondoka
kuelekea banki.Tukamuona askari akipewa soada
ya kopo na Emmy na akaianza kuinywa baada ya
Emmy kuingia ndani na baada ya muda
akaonekana kama anaumwa na tumbo na
akandoka katika eneo la nje ya chumba akielekea
sehemu vilipo vyoo na baada ya muda kidogo
mlango ukafunguliwa na kumshuhudia Emmy
akiwa amevalia koti la kidaktari akikisukuma
kitanda cha mama huku mama akiwa amefumba
macho yake na kulala kama mtu aliye poteza
fahamu
Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio huku
nikiema kwa hasira na kujikutani nikiyangata
meno yangu kwa hasira kiasi kwamba nikatamani
nipone kwa haraka ili niweze kumsaka Emmy
sehemu yotote akatakayo kuwepo nchini Afrika
kusini.Nikashusha pumzi huku nikiwa macho
yangu yamebadilika na kuwa mekundu na
kujikuta nikikitazama kioo kilichopo ndani ya
chumba hichi kinacho nionyesha vizuri sura
yangu na kila mtu akabaki akinitazama kwa
umakini pasipo kuzungumza kitu chochote
Hemu rudisha hiyo CD ya kwanza
Jamaa akairudisha CD ya kwanza na kipelea
mbele kidogo na kumuona Emmy akimuingiza
mama ndani ya gari la wagonjwa huku
akisaidiana na watu wawili ambao niliwaona
wakishuku na baba huku nao kwa sasa wakiwa
wamevalia makoti meupe wakionekana kama
madaktari.
Kaka hembu simamasha kidogo hape na zoom
kwenye kioo cha dereva wa hilo gari
Jamaa akafanya kama nilivyo muagiza na
akaikuza picha ya dereva na kugundua ni baba
japa amevalia miwani huku akiwa amebandika
ndevu za bandia na kumfanya aonekane kama
mtu wa makamo
Kwani Flora ina maana hawa jamaa sio wafanya
kazi wa hii hospitali?
Ndio
Mbona wanavitambulisho kwa maana mimi hili
tukio linatokea sikustushwa kwa maana ni jambo
la kawaida kwa wagonjwa kuhamishwa hapa
hospitalini kwetu
Nikamshuhudia Flora ambaye ndio muhusika
kwenye ofisi ya takwimu akikuna kichwa pasipo
kuzungumza kitu cha aian yoyote.
Je daktari wenu mkuu yopoje?
Yupoje kivipi?
Yaani muonekano wake?
Ni mweusi kiasi kiasi na sasa yupo Captown
kwenye kikao cha madaktari wakuu hapa nchini
Mbona alikuja mzee wa kizungu huyo dada
akasema ndio daktari mkuu?
Mmmm atakuwa amekudanganya kwani ni wiki
ya pili daktari mkuu yupo kwenye kikao cha
madaktari kama nilivyo kuambia hapo awali
Sikuwa na lakuzungumza zaidi ya kuumiza
kichwa ni jinsi gani ninaweza kumpata mama
yangu na moja kwa moja nikajua ametekwa na
baba na sikujua ni wapi alipo mpeleka.
Tutawasiliana na polisi kuweza kulifwatilia hili
tukio
Naombeni mufanye hivyo kwani mama yangu
ndio kila kitu katika maisha yangu kwa maana
nimetoka Tanzania kwa ajili yake na mwisho wa
siku mambo yanakuwa kama hivi
Usijali wa hilo
Nikakaa hospitali zaidi ya wiki nne na nikapona
kabisa mguu wangu na kufunguliwa bandeji nililo
fungwa.Habari za wapi alipo mama kila
nilipojaribu kuwaulizia walio sema
watalishuhulikia wakadai bado askari
wanaendelea na uchunguzi ambao sikujua
utaisha lini
Kaka gharama zako za hospitalini zimesha
lipiwa
Zimelipiwa na nani?
Aliye kulipia ni yule aliye kugonga na gari na
yupo nje anakusubiria?
Nikaanza kujiuliza ni nani huyu aliye ni gonga na
kuwa na moyo wa kujitolea kiasi kwamba
amenilipia gharama zote za ajali yangu wakati
mimi ndio nilikuwa ninamakosa.Nikatoka nje
pamoja na daktari aliye niambia habari hii
ambayo kwangu ni nzuri kiasi japo bado akilini
nimetawaliwa na wazo la wapi alipo mama.
Daktari akanionyesha mzee mmoja aliye valia
koti jeusi la suti na alinipa mgongo kwani
anazungumza na simu,ikatulazimu kumsubiria
amalize ndio daktari amjulishe uwepo
wetu.Baada ya muda akakata simu na kugeuka
na kujikuta nikihamaki kwa kiasi kikubwa kwani
mtu aliyepo mbele yangu anafanana kabisa na
baba yangu ambaye kwa sasa ni adui yangu
namba moja.
Habari yako kijana
Sh...ikamaoo
Nilipata kigugumizi cha gafla kiasi kwamba mzee
naye akaanza kunitazama kwa umakini huku
akionekana kunichunguza kuanzi kichwani hadi
miguuni.Daktari akatutizama kwa muda na
kuzungumza kitu kilicho tufanya sote tumtimame
HUYO NI MWANAO?
HAKUNA aliye lijibu swali la daktari zaidi ya
kukaa kimya kimya na tukageukiana na
kuendekea kutazama na kadri tulivyo zidi
kutazamana ndivyo nilivyohisi ukweli wa maisha
yangu juu ya baba yangu kwani kuanzia macho
pua midomo na sura hakuna kilicho pishana na
mwenzake kiasi kwamba machozi yakaanza
kunilenga lenga huku moyoni mwangu nikijihisi
amani na furaha iliyo kuba tofauti na ninavyo
kuwa na baba yangu gaidi.
Jina lako ni nani kijana?
Eddy
Eddy nani?
Godwin
Nikastukia mzee akinikumbatia kwa furaha huku
akicheka kwa kicheko kikubwa cha furaha na
akaninnyanyua juu kidogo na kuanza
kunizungusha kisha akanisimamisha na
kunitazama tena usoni huku machozi ya furaha
yakimwagika na mimi nikajikuta nikiachia basabu
pana
Dokta nahitaji vipimo vya DNA na huyu kijana
Sawa ila inabidi na yeye aridhie
Eddy upo tayari kwa hili?
Ndio mzee
Sikuweza kumuita baba moja kwa moja japo
tunafanana kwa asilimia 99(tisini na tisa) ila
nikahofia endapo majibu yatakuwa siyo sijui sura
yangu ningeiweka wapi.Tukaingia kwenye
maabara nzuri na yakisasa kisha tukachukuliwa
damu na kuombwa kusubiri nje.
Eddy mimi ninaitwa Godfrey nani Mtanzania
japo sasa hivi nina uraia wa hapa Arfrika kusini
hii ni kutokana na kuishi miaka mingi hapa
Afrika kusini
Ahaa sasa ni kwanini uliondoka Tanzania
ilikuwaje?
Ni historia ndefu sana iliyo nipata hadi kufikia
hapa ni vikwazo na mambo mengi nilipitia ila
ninamshukuru Mungu hadi leo hii nipo salama
Ni kitu gani kilicho kupata?
Ni mambo mengi sana yaliyo nipata na hapa sio
wakati muafaka wa kulizungumzia hilo
Kabla sijamuuliza swali jengine mlango wa
chumba cha maabara kikafunguliwa na akatoka
daktari aliye tuchukua vipimo vya damu na
kutuomba twende naye ofisini kwake ambapo
akatupa mikono huku usoni mwake akiwa na
furaha
MAJIBU NI ASILIMIA 100 DAMU ZENU
ZINAFANA
Ikawa ni habari mpya yenye furaha maishani
mwangu kwani siku zote kilio changu ni
kuhusiana na baba yangu.Baba akanyanyuka kwa
fauraha na kunikumbatia huku mkono wake
mmoja akiupiga piga mgongoni mwangu,machozi
ya furaha yakanibubujika na hata wazo la mama
kichwani mwangu kwa wakati huu likafutika
kidogo.Baba akatoa simu yake na kupiga namba
fulani
Andaa tafrija kubwa na waalike watu wangu wa
karibu kwani nina kitu cha kuzungumza nao
Fanya hivyo na ndani ya lisaa nitakuwa hapo
nyumbani
Waambie ni saa mbili usiku
Sikujua baba anatoa maagizo kwa mtu gani kisha
akatoa kitabu kidogo cha kuchukulia pesa na
kuandika kiasi anacho kijua yeye kisha akampatia
daktari na nikaondoka huku nikiwa nimebeba
baasha yenye majibu yetu ya DNA.Tukatoka nje
na kulekea eneo la maegesho ya magari na
dereva aliye valia suti nyeusi akafungua mlango
wa gari aina Astorn Martin na kidogo dereva
akawa ananishangaa.Safari ikaanza huku kila
nilipo tazamana na baba tukajikuta tukitabasamu
ikiashiria ni furaha iliyotawala kati yetu
Geti kubwa likajifungua na mbele yangu kwa
mbali kidogo nikaliona jumba kubwa midhili ya
ikulu na kuna eneo kubwa lenye kila aina ya kitu
cha kuburudika pamoja na bustani kubwa zenye
maua ya kupendeza sana
Karibu nyumbani mwanangu
Kwa wingi wa walinzi walioo kwenye eneo hili
hadi nikaanza kuogopa japo ni baba yangu ila
sikujiamini sana juu ya usalama wangu
Karibu sana nyumbani Eddy
Asante baba
Tukashuka kwenye gari huku macho yangu
yakitazama tazama pande zote za sehemu
tuliyupo.Mlango wa kuingilia ndani ukafungulia
na macho yangu yakakutana na seble
inayoendelea kupambwa na wafanyakazi na
akashuka mama mmoja wa kizungu kwenye ngazi
na kuja kumkumbatia baba kisha akambusu
mdomoni na mama huyo akabaki akinishangaa
Huyu ni nani?
Mwanangu
Mama wa kizungu akanipa mkono kwa dharau
kisha akaondoka huku akionekana kukasirika kwa
uwepo wangu katika nyumba hii hadi nikajihisi
vibaya
Eddy mwanangu karibu na jisikie upo huru na
mwenye amani kwa maana hapa ni kwako
Asante baba yangu
Niliitikia kwa sauti ya kinyonge ila moyoni
mwangu nikaanza kuhisi kuna mapambano
yatakayo endelea kati yangu na huyu mama wa
kizungu.Tukaongozana hadi kwenye chumba
kikubwa chenye mali nyingi za dhamani na baba
akanikaribisha kwenye moja ya kiti kilicho
tengenezwa kihalisi na yeye akakaa kwenye
sehemu nyingine
Una hitaji kinywaji?
Hapana
Sawa Eddy kwanza ninakuomba unisamehe kwa
kile ulicho kiona pale mlangoni
Bila samahani kwani yule ni nani?
Yule ni mke wangu wa ndoa ambaye nimefunga
naye ndoa miaka mitano iliyo pita
Aaaahaa sasa mbona ameonekana kuchukizwa
baada ya kuniona?
Ahaa nahisi hakutegemea kuupata ujio wako leo
kwani hata mimi sikuwahi kumuambia kuwa
mimi nina mtoto
Sawa na yeye ume zaa naye?
Hapana na sina mtoto mwengine zaidi yake japo
yeye naye ana mtoto wa kike hayupo hapa yupo
Johnsburg anasoma chuo
Mama yako hivi hajambo?
Siwezi kujiu kama hajambo au anaendeleaje kwa
maana alikuwa yupo hospitalini na amatekwa?
Ametekwa na nani?
Ametekwa na baba?
Ina maana kaka Godwin anaweza kumteka mke
wake?
Babahiyo ni historia ndefu sana,na chanzo
kikubwa cha mimi kuja huku ni yeye kwa maana
alikuwa amelazwa kwenye ile hospitali uliyo
nikuta
Duu kweli malipo ni hapa hapa duniani?
Kwa nini baba?
MAMA YAKO NI KATILI SANA TENA ZAIDI YA
SANA JAPO USONI MWEKE NI MWAMA
KUPITILIZA
Maneno ya baba yakanicha mdomo wazi huku
nikishangaa nisijue ni kwanini amesema mama
yangu ni katili sana
ITAENDELEA