******SORY MADAM******(34)
Age…………………………………………18+
Writer…………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Nikiwa nimesimama Sheila akamuachia jamaa na kunirukia mimi na sote tukaanaguka chini huku nikijitahidi kumshika kichwa chake anacho taka kuning'ata kwa meno yake yaliyo machafu huku akidondosha udenda mwingi na akinguruma kama mbwa mkali mwenye njaa kali
ENDELEA
Mlinzi akamuwahi Sheila na kumnyanyua juaa na lipindi tukio linatokea askari waliweza kuliona na wakamkamata Sheila na kabla hawajaondoka naye nikawazuia
"Jamani samahani kaka zangu ninamuhitaji huyo binti"
"Huyu ni mwenda wazimu na ametoroka katika hospitali ya vichaa na karibia wiki sasa tunamtafuta"
"Sawa nimewaelewa sijui tunaweza tukaongozana hadi sehemu ilipo hiyo hospitali?"
"Kwani wewe unamfahamu huyu binti?"
"Hapana ila ninahitaji kuweza kuyafahamu maendeleo yake"
Askari wakanitazama kisha wakaniruhusu kama kuongozana nao,tukaingia kwenye gari letu na kuongozana na askari hadi kwenye hospitali ambayo ni yawatu walio pungukiwa na akili.Sheila akakabidhiwa kwa madaktari na polisi wakanionyesha sehemu ambayo ninaweza kupata kawimu za maendeleo ya Sheila,
"Samahani dada yangu"
Nilimuuliza nesi mmoja niliye mkuta kwenye dirisha la kuudumia wateka wanao hitaji huduma kwenye hospitali hii
"Bila samahani"
"Kuna mgonjwa ameletwa dakika tano zilizo pita na ninaomba kuweza kujua takwimu zake za nyuma"
"Ahaaa juyo dada aliyeletwa hapa akiwa hajitambui na kadris siku zilivyo zidi kwenda alikuwa msumbufu anapiga wezake hadi kunasiku alimuua mwenzake mmoja kwa kumpiga kwa chupa kichwani"
Nikajikuta nikiwa nimeuacha mdomo wangu wazi kwa mshangao kwa maana sikutegemea kusikia taarifa kama hiyo
"Labda tatizo leke kubwa haswa ni nin?"
"Mmmm kwa mimi siwezi kujibu labda ngoja nikukutanishe na daktari ambaye alikuwa akimuhudumia tangu siku ya kwanza alipo kuja"
Akanyanyua mkonga wake wa simu na kuzungumza na mtu aliyo upande wa pili wa simu kisha akaniomba niweze kuingia ndani kwenye ofisi ambayo ipo upande wangu wa kushoto na ikanilazimu kumuacha nje dereva,Nikamkuta daktari wa kiume mwenye umri mkubwa kiasi na akaniruhusu nikae pembeni kwenye kiti
"Nikusaidie nini kijana?"
"Kuna mgonjwa ambaye ameletwa muda mchache ulio pita na sijui ninaweza kupata taarifa yake ya nyuma?"
"Wagonjwa walio letwa muda mcha ulio pita ni wengi labda wewe unamzungumzia yupi kati ya hawa?"
Daktari akawasha Tv yake kwa kutumi rimoti na nikaziona picha za Sheila akiwa ameshikwa na askari
"Huyo picha namba tano"
Nilimuonyesha daktari kwa kutumi kidole na akaizima Tv yake na kunigeukia huku akisaidiwa na kiti chake chenye uwezo wa kuzunguka
"Huyo hapa sisi tunamuita Vaiper Lady"
"Kwa nini?"
"Kwanza nimkali na ninamfananisha na hao nyoka ambao wanasifa ya kung'ata sana,Pili hatulitambui jina lake halisi ni nani"
"Sawa ila tatizo lake ni nini?"
"Huyu binti amedhirika sana kiakili hii ni kutokana na mambo magumu ambayo ameweza kupitia huku nyuma.Pia ubongo wake umetingishika kiasi kwamba imemfanya akili zake kufyatuka"
"Akili yake imetingishika?"
"Ndio ina maana aliweza kupigwa kwa kitu kizito kichwani ambacho kiliipelekea akili yake kucheza kidogo na jambo kubwa la kumshukuru Mungu ni kwamba mishipa ya damu haikuweza kupasuka kichwani mwake"
"Anaweza akapona?"
"Mmmm sidhani kwa maana sisi tumejaribu kutumia ujuzi wetu mwingi ila tumeshindwa ila kitu kibaya zaidi huwa hapendi kuona jinsia ya kiume na alashawahi kufanya tukio la mauaji kwa…."
"Hili nilisha ambiwa……Sasa dokta imi ninahitaji kukaa naye kwa ukaribu sana ili niweze kumtuliza"
"Wewe kijana unahitaji kufa au…..kwa maana hataki kuona jinsia yoyote ya kiume"
"Mimi nitaweza dokta na Mungu akibariki kesho nitakuja kwa kazi hiyo"
"Mmmm kwa kweli si……"
Nikachomo noti mbili za dola mimi kwenye mfuko wa suruali na kumuwekea daktari mezani na akanyamaza
"Kaka utahitaji kiwango kingine zaidi ya hicho nitakupatia"
Daktaria akanyamaza kimya na kushindwa kuzungumza kwa aibu na nikanyanyuka na kumuacha akiwa ananishangaa.Hali ya furaha ikanitoweka kabisa na hata ndani ya gari nikawa kimya huku nikimuwazia Sheila na sikusema kuwa ninamfahamu Sheila hii ni kuepuka maswali mengi yasiyo na msingi kwangu.Tukaingia kwenye moja ya duka la simu na kununua simu aina ya Blackbery.Tukarudi kwenye jengo ambalo baba aliingia na kumkuta akiwa anatusubiri
"Mbona mumechelewa?"
"Ahaa kuna sehemu sehemu nilipitia"
"Hiyo simu umesha nunua?"
"Ndio baba"
"Sasa turudi nyumbai kwa maana lile swala nimesha likabidhi kwa wahusikana wameniahidi ndani ya siku mbili watanipa jibu"
"Kweli baba?"
"Ndio wewe kuwa na amani na kama utataka kuendelea kutazama tazama mji nipige simu nyumbani nije kuchukuliwa na gari nyingine?"
"Hapana kwanza nimechoka ninahitaji kupumzika kidogo alafu ninaomba namba yako baba"
"Sawa"
Baba akanipatia namba yake ya simu na kutokana sikuwa na line ikamlazimu kunipa laini yake moja ya simu ambayo haitumii sana.Tukarudi nyumbai huku msongamano wa mawazo ukiwa umenitawala na moja kwa moja nikagundua baba wa zamani mzee Godwin ndio chanzo cha Sheila kuwa katika hali kama hii.Sikuweza kupata suingiza kabina na kila nilipo jaribu kuivuta amani kutawala usoni mwangu nikajikutani kishindwa kabisa na sura yangu ikawa imetawaliwa na mikunjo ya hasira.Nikiwa nemekaa kwenye moja ya masofa ya kupumzikia yaliyopo kwenye bustani yenye maua mengo mazuri na kuna kijibwawa kidogo chenye maji masafi na upepo mwingi nikamuoana mke wa baba akiwa na yule jamaa wa jana usiku wakiwa kwenye moja ya kijijumba kilicho kwa vioo na ndani yake kukiwa na maua mengi yanayo uteshwa kwa masaada wa mwanga wa jua
Wakanza kushikana shikana na mwisho wa siku wakanza kupeana mambo ya chumbani bila kujali kama wanaweza wakaonekana na mtu.Nilicho kifanya ni kurekodi tukio zima mwanzo hadi mwisho hadi wanamaliza na jamaa akawa wa kwanza kutoka na baada ya dakika kama kumi mke wa baba naye akatoka huku akijifanya kunusa nusa kipande cha ua alicho toka nacho na kwabahati mbaya macho yetu yakakutana na akanipandisha na kunishu kiasi kwamba akaanza kunikera
"Mama ninakuomba"
Akatembea kwa mwendo wa madaha huku mdomo wake akiwa ameubenua kiasi kwamba nikaanza kujiuliza sijui kipigo cha jana amekisaha
"Unasemaje?"
"Hivi baba yangu ni nani kwako?"
"Khaa wewe unamuona ni nani?"
"Jibu nililo kuuliza"
"Ni mume wangu"
"Una uhakika na unacho kizungumza?"
"Ndio kwa maana hata pete hii hapa ninayo"
"Unajua siku zote kwenye maisha usipende kumfanyia mwenzako kile usicho penda kufanyiwa"
"Una maana gani?"
"Utaijua wewe nenda zako"
Akaniandisha kuanzi chini hadi kitendo ambacho maishani mwangu sipendi mwanamke anifanyie akaachia msunyo mkali uliao nifanya ninyanyuke kwa haraka na kumfwata kwa hasira na akaanza kukimbia ila kutonaka na uwezo wangu wa kukimbia nikamdaka katika mlango wa kuingilia sebleni na kukutana na baba akiwa anatoka ndani
"Huyu mwanao ni mwenda wazimu nini?'
Sikumjibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kumfwata na nilipo sikia swala la uwenda wazimu na mimi nikajichetua sana na ili nionekane ni mwenda wazimu kweli.Tukaanza kazi ya kukimbizana huku tukimzunguka baba aliye kosa kitu cha kuzungumza,
"Mume wangu mkamate mwanao atanijeruhi"
Na mimi nikaanza kuuigilizia mlio wa Sheila alio kuwa akiningurumia na kumfanua baba kuhamako na kadri muda unavyo kwenda ndivyo nikazidi kujichetua kaisi kwamba baba akaagiza walinzi wake kunikamata na wakashauriana wanipeleke hospitali ya vichaa kwa ajili ya vipimo zaidia.Kwa bahati nzuri tukafika kwenye hospitali tuliyo toka masaa machache yaliyo pita na kwabahati nzuri daktari aliye pewa jukumu la kunipima na yule niliye mpa dola mia mbili na akawa ananishangaa kuniona nikiwa nimeletwa kama mgonjwa
"Dokta wakikuuliza waambie kuwa itanibidi hapa nikae kwa wiki mbili"
Nilimuambia daktari baada ya baba na watu wake kutoka nje ya chumba nilicho ingizwa
"Saaa….saaa"
"Dokta acha kupata kigugumizi wewe waambie hivyo kuwa mimi ni mgojwa na mutaniweka hapa kwa wiki mbili ili kunichunguza zaidi na kama ni pesa mimi nitakulipa ila hili ni dili kati yangu mimi na wewe"
"Sawa nimekuelewa"
Daktari akanipima pima kiuongo ili kupoteza muda kisha akatoka na baada ya muda baba akaingia huku akiwa na sura ya unyongee na kwambali machozi yanamlenga lenga
"Ohhooo Eeeehee baba ukuwaa mkubwaa kamaaaaa John Cennaaaaaa hahaaa…babaaa huuuyoooo katokaaaa kaziiiniiiiiiiii ohooaaooa"
Niliimba nyimbo za kuwehuka na kuzidi kumfanya baba aamini kuwa mimi nimepata kichaa
"Dokta kweli mwangu atapona?"
"Kama nilivyo kuambia hapo awali tunamuweka hapa ndani ya wiki mbili kisha tutaangalia jinsi maendeleo yake yanatavyo endelea"
"Ahahaa doktaaa wiki mbiliiiii hahajhhhaa mimi takaaa kaaaa mwakaa mzimaaaa baaaabaaa lia liaaa kama totojingaaaaaa hahaahaa"
Nikazidi kuzungumza huku nikirusha rusha miguu na mikono na ikawalazimu watu wa baba kunilaza kitandani na kunifunga mikono na miguu kwa kitumia mkanda maalumu uliopo juu ya hichi kitanda nilicho lalia
"Ohoo Mungu wangu sijui ni kitu gani kimempata mwanangu?"
"Usiwe na wasi wasi atapona tuu cha msingi ni kumuomba Mungu aweze kumjalia afya njema"
Baba akanitazama kwa sura ya simanzi na akashindwa kuyazuia machozi yake na akaanza kulia na ikamlazimu mlizi wake mmoja kutoa kitambaa na kumkabidhi baba kisha akatoka naye nje na walinzi wake wengine wawili wakafwatia nyuma
"Dokra wachungulie wamesha ondoka?"
"Ngoja niangalie"
Dokta akafungua mlango na kuchungulia kisha akaufunga na kunifwata kitandani huku akiwa anacheka
"Ndio wamesha ondoka….hivi wewe kijana mbona msanii kiasi hichi?"
"Ahaaa uanajua unapo amua kufanya kitu mtu inabidi uweze kufanya juu chini unakifanikisha hata kwa staily kama hii pia ni vyema si umeona sasa mpaka mzee ame….hahaaaa chipissssisisisisiiii oohoooo"
Nilirudi katika hali yangu ya kuchanganyikiwa baada ya mlango kufungulia na wakaingia majamaa wawili wenye misuli na wamevalia makoti meupe na suruali nyeupe
"Huyo naye dokta ana tatizo gani?"
"Ahaa mchukueni mumpeleke kwenye chumba chake"
Jamaa wakanifungua mikanda na kuninyanyua kwa nguvu na mmoja akanishika mkono wa kulia na mwengine mkono wa kustoto,tukatoka nje ya chumba na kuwaona baba na watu wake wakija kwenye ofisi ya daktari na ikanilazimu nianze kuchetuka kama kawaida huku nikijirusha rusha juu na kuwafanya majama hawa kutumia nguvu zaidi katika kunibana,Baba akawaomba wasimama kisha akasimama mbele yangu na kunitazama kwa muda huku akijikaza kuto kulia.Akanikumbatia na kuwaruhusu jamaa wanipekeleke wanapo nipeleka
Nikaanza kupata woga kwa maana kila nilipo pita vichaa wakiume walianza kushangilia huku wengine wakiwa na sura za ajabu ajabu
"Sasa dokta naye tulimuuliza anatatizo gani huyu hajatujibu sasa tutampeleka kwenye wodi gani?"
"Kwa jinsi ninavyomuona tumuingize wodi namba nano itamfaa"
Jamaa wakashauriana na kweli wakaniingiaza kwenye wodi yenye vitanda vingi na vingi vinawatu ambao kwa muonekano wao ni vichaa walio pitiliza na mbaya zaidi wengi wana miili mikubwa kupita maelezo kiasi kwamba kila nilipo pita walinitazama kwa macho makali.Jamaa wakanionyesha kitanda changu kisha wakatoka kwa haraka huku wakionekana kujishuku.Majamaa matatu yakasimama kwenye vitanda vyoa na kuanza kupiga hatua za kunifwata kitandani huku ikinguruma kama mimbwa inayo gombania mke mmoja,mapigo ya moyo yakazidi kunidunda huku kijsho kikinimwagika kiasi kwamba ubabe wangu wote ukaniishia
Majaa yakanitazama kwa muda huku yakinguruma na yakaanza kunishika shika kichwa changu huku kila mmoja akitaka nimtazama yeye,Nikastukia kofi moja takatifu likitua kwenye sikio langu na kusababisha uwezo wa kuona vizuri ukakata na kuona vitu vyenye alama kama nyota nyota vikielea angani kiasi kwamba nikajikuta nikiona giza lililo endana na ukungu.Nikastukia nikiwa nimelala chini sakafuni wala sikujua nimeshuswaje kwenye kitanda.Makelele ya vichaa wengine yakazidi kunichanganya kiasi kwamba nikawa sielewi nini cha kufanya.Kipigo kutoka kwa haya majamaa ambayo yanaonekana ni mababe kwenye hii wodi kikanifanya nijikunyate huku nikilia kwa uchungu.Nikaingia chini ya uvungu wa kitanda ili kujinusuru kwani inadi ya vichaa wanao nishambulia ikaongezeka,Nikastukia nikivutwa miguu yangu na wakaanza kuniburuza huku wakishangilia kwa nguvu
Maumivu makali yakazidi kuniumiza kiasi kwamba nikajuta kwa uamuzi nilio uchukua.Wakanigongesha gongesha kwenye kwenye vitanda kisha wakanilaza kwenye kordo iliyo tenganishwa na vitanda na wakanizunguka huku wakinitaza na vijamaa viwili vyembaba vikapanda juu ya vitanda nawezao wakaacha nafasi na sikujua wanataka kufanya nini,Nikastukia wa kwanza akijirusha na kunifanya nimkwepe na akapiga kichwa kwenye sakafu na kutulia tuli.Wa pili akafanya kama alivyo fanya mwenzake na akanitulia kwenye tumbo na kunifanya nitoe ukulele mkali wa maumivu huku kicha kizima kikiwa kimejaa manundu ya kipigo nilicho kipata
Nikastukia wakianza kunikojolea huku wakicheka kwa furaha na kupeana mikono na kunifanya nizidi kulia kwa uchungu japo hasira imenipanda sikuwa na uwezo wa kufanya chochote dhidi yao.Wakatawanyika na kuondoka kila mmoja akarudi kawnye kitanda chake na wakaniacha nikiwa nimejilaza chini pamoja na kale kajamaa lalicho nirukia.Nikaanza kujivuta taratibu hadi kwenye kitanda changu huku mwili mzima ukiwa ninanuka mikojo pamoja na kuvimba juu na nikakaa na baada ya muda mlango ukafunguliwa na wakaanza kutoka mmoja baada ya mwengine.Akachugulia daktari mmoja na kutuona ndani ya chumba tumebaki wawili na baada ya muda wakaingia madaktari wanne ambao wawili wakanifwata mimi na wawili wakaenda kwa kale kalicho zimia
"Huyu ni mgeni eheee?"
"Naona"
"Ahaaa wageni huwa wanapata shida sana"
"Kweli kwa maana walivyo mfanya mmmm ni zaidi ya maumivu"
Madtari wakaendelea kuzungumza huku wakinihudumia na kuniweka kwenye machela na kunihamisha kwenye na kuniingia kwenye chumba cha matibabu.
Ndani ya siku nne nikawa nimepona vuzuri japo sio sana kwani kuna baadhi ya sehemu zinamaumivu kidogo.Nikarudishwa kwenye wodi ambayo nilitembezewa kichapo na nikaanza kazi yangu rasmi ya kumtafuta Sheila kwenye kila sehemu ya hospitali hii,Ndani ya siku mbili sikuweza kumuona Sheila na sikujua ni wapi alipo,Nikaanza kuzoeana na vichaa kadhaa ambao ni wanyonge kama mimi kwa maana jinsi watu wanavyo ishi kibabe kwenye hii hopitali inasababisha kuwemo na mgawanyiko wa vichaa wababe na vichaa wanyonge.Wakati wa kuoga ukawadia na kama kawaidi kila wodi ina mabafu yake ambayo muda wa kuoga unapo wadia ni wote tunatakiwa kufanya hivyo.
Nikatafuta sehemu isiyo na mminyano na kusimama na kuwatazama jinsi vichaa wengine wanavyo minyana kwenye kuoga.Wakaoga wote kisha wakatoka na mimi nikanza kuvua nguo zangu na kabla sijamaliza kuzivua akaingia lile jijamaa ambalo lilinizaba makofi pamoja na wezake na baada ya kuniona likaanza kunguruma na kuanza kunifwata na nikajiandaa kwa chochote atakacho hitaji kukifanya kwangu mimi.Likanisimamia mbele yangu huku likinitazama kisha likanitisha kama ninataka kunipiga kofi na kujikuta nikiinama huku mikono yangu nikiwa nimeiweka kichwani kuziba uso wangu na nikastukia likaanza kucheka sana hadi likakaa chini kwa kucheka na ikanibidi na mimi kuanza kucheka
Hata hamu ya kuoga ikaondoka na kujikuta nikivaa nguo zangu na kutoka bafuni.Kama kawaida muda wa michezo ukawadia na kila kichaa anaye penda mchezo wake anakwenda kwenye eneo lenye kiwanja cha mchezo wake.Nikaanza kuzunguka zunguka nikaangalia jinsi vichaa wanavyo fanya mambo ya ajabu kusema kweli inahitaji moyo wa uvumilivu kuishi nao kwa maana kama akili yako ni nzima basi ukishindwa kuvumilia unaweza ukawaambia madaktari kuwa umepona.Nikakuta wasichana watatu vichaa wakiwa wamekaa chini wakichora chora na katika kuwachunguza vizuri nikamuona Sheila akiwa katikati yao
Na mimi nikajisogeza karibu yao na kukaa huku nikimtazama Sgeila jinsi anavyo chora chora cini kwa kkutumia kijiti huku akifuta futa.Wezake wakasimama na kuondoka zao na akabaki peke yake.Sheila hakuinyanyua sura yake kunitazama na akazidi kuchora chini huku akikigandamiza sana kijiti chini na akiwa anaonekana kama anahasira kali.Machozi yakaanza kumwagika kiasi kwamba akafuta alicho kichora kicha akaanza kuandika herufi moja moja kwa uchungu
{I…….L…..O…….V…….E}
Nikabaki nikimuangalia huku kwa mbali na mimi machozi yakinilenga lenga kwani afya yake imedhohifika sana isitoshe mwili wake umetawaliwa na makovu mengi sana ambayo yamemfanya azidi kuonekana mbaya.Akayafuta maandishi yake kisha akachora vikatuni viwili kimoja kikiwa cha kike huku kingine kikiwa cha kiume na akavipatia majina kwa herufi za mwazo ambacho kikatuni cha kike akakiandikia herufi kubwa ya ‘E' huku cha kike akikiandikia kiherufi cha ‘S'.Hapo ndio nikashindwa kuzizuia hisia zangu na kujikuta nikimwagikwa na machozi na kumuona Sheila akiinyanyua sura yake tartibu na kuniangalia kwa muda kisha akairudisha sura yake chini na akanitazama tena kwa umakini huku akiwa kama mtu anaye jitahidi kuvuta kumbukumbu ya kitu fulani ila anashindwa kujua ni nini anacho kiwazia
"Sheila…..Sheila?"
Akaonekana kustustuka na akanikazima macho hadi akaanza kuniogopesha akajaribu kuzungumza ila akawa kama anashindwa.Aafuta vidoli vyake chini na kuandika maandishi yaliyo nistua zaidi
{MIMI SIWEZI KUZUNGUMZA NIPO SAWA SAWA NA BUBU}
Maumivu makali yakapenya kwenye moyo wangu na kujikuta sura nzima ikitawaliwa machozi.Nikachukua kijiti chake na kumuandikia chini
{KWANINI HUWEZI KUONGEA?}
Sheila akanitazama kwa macho ya mshangao kwa jinsi ninavyo lia kisha akaniandikia chini
{SIWEZI TUU KWANI NILILISHWA MAKAA YA MAWE KWENYE MDOMO WANGU}
Sheila akaufungua mdomo wake na kuutoa ulimi wake nje na nikajikuta nikitetemekwa kwa woga kwani ulimi wake una majeraha makubwa yanayo onyesha vika ni kweli alilishwa makaa ya moto.Sheila akasimama gafla na ni mimi nikasimama na akaanza kutembea na kujikuta nikizidi kuumia kwani hata shepu lake la nyuma lilidhohofika sana.Tukaongozana hadi kwenye moja ukumbi ambao kuna kiwanja cha mpira wa kikapu(basketball) na akazidi kunipeleka hadi kwenye moja ya mabafu na akanitazama na kulivua gauni lake
Nikajikuta hata uwezo wa kuhema ukianza kuwa mdogo kutokana na mstuko nilio upata baada ya kuuna mwili wa Sheila ulivyo jaa majeraha makubwa ya kachanwa chwana na kutu chenye ncha kali.Akanigeukia mgongoni na kunionyesha kuvu kubwa la kutobolewa huku ngozi ya sehemu hiyo ikiwa imekunjamana na kujikuta nikizidi kuteswa na uchungu,Macho ya Sheila yakaanza kuvunjwa na machozi na akatazama tazama ndani ya bafu hili na sikujua anatafuta nini.Akafungua koki ya bomba la maji kisha akachovya kidole chake kimoja ndani ya maji na kuandika kwenye kiio kikubwa kilichopo ukutani
{MIMI SIO KICHAA ILA WATU WANANIISI KUWA MIMI NI KICHAA ILA UKWELI NI KWAMBA NINAAKILI ZANGU VIZURI NA HAYA YOTE YAMETOKANA NA MAUMIVU MAKALI NILIYO PEWA NA MZEE MMOJA AMBAYE NI MKUU WA JESHI NA NIBABA WA MPENZI WANGU EDDY}
Sheila akanigeukia na kuniuliza kwa ishara kama nimeelewa alicho kiandika na mimi nikatingisha kichwa nikimuashiria kuwa nimeelewa
"Unanikumbuka?"
Nilimuuliza Sheila na akabaki akinitazama kwa muda kisha akachovya kidole chake kwenye maji na kuandika kwenye kioo
{HAPANA ILA NINAKUFANANISHA NA EDDY WANGU ILA SIO WEWE KWANI YEYE ANAAKILI ZAKE TIMAMU NA SIO CHIZI KAMA ULIVYO WEWE}
Nikatulia kwa muda huku nikiyatafakari maneno ya Sheila aliyo toka kuniandikia muda mchache ulio pita.Nikamsogelea Sheila na kumkumbatia huku nikiwa ninamwagikwa na machozi.Mlango ukafunguliwa na wakaingia madaktari wawili wa kiume na walivyo tuona tumekumatiana wakanitoa mimi kwa nguvu na kuchomoa virungu vyao na kuanza kunipiga huku wakiniburuza na kunitoa nje
"Sheila….nisaidie ninakufa mimi"
Nilizungumza kwa sauti ya juu huku nikiwa ninalia kwa uchungu na kuzidi kuwaongezea hasira madaktari hawa na kuzidi kunipiga,Sheila kwa haraka akatoka huku akiwa na nguo ya ndani na akamsukuma dokta mmoja ana akajibamiza kichwa ukutani na akaanguka chini kisha akamshika kichwa cha gaktari na kunaza kukibamiza kwenye sakafu kwa nguvu hadi kipasukwa kwenye kisogo chake,Daktari aliye kuwa anaendelea kunipiga baada ya kumuona mwenzake akiwa anaaga dunia akaniacha na kwa nguvu zake zote akarusha kirungu chake na kikatua kichwani mwa Sheila na akadondoka chini na damu za puani zikaanza kumwagika
ITAENDELEA