Hotel ya bei mbaya duniani

Hotel ya bei mbaya duniani

Bwana pilau leo naona umekuja na topic tofauti,naomba nichangie kidogo maana nilifanya kazi kwenye hiyo hotel kwa miaka mitatu jina lake ni Burj al arab,yaani ni kama story ya kutunga hapo nilikutana na kila aina ya watu,huo kama ungo unaouona hapo juu pichani sio ungo ni helipad(kiwanja cha helicopter ambazo baadhi ya wageni wanazitumia,kuna baa inauza wine mpaka uae dh 40000 ambayo ni kama tsh 16.5ml na watu wanakunywa!!!Naomi campell alifanya birthday yake mwaka juzi alifunga hotel yote alialika rafiki zake tu!!nakumbuka siku moja kuna m russia alikuwa anaishi hapo kwa siku kama sita siku aliyoondoka alisahau pesa kwenye safe box,baada ya kuwaita security na kufungua tulikuta dola 50,000/ hii ni zaidi ya milioni 75 za tz lakini ajabu tulipompigia simu alisema amesahau kwamba alikuwa na kiasi hicho cha pesa.Nakumbuka wakati nafanya pale kuna mtanzania alikuja kupumzika na familia yake!!!pia hiyo hotel inaingiza pesa nyingi sana kwa watu wanaokuja kuingia na kupiga picha kipindi kile ilikuwa Tsh 50,000/cha ajabu kuna bwana mmoja anakaa mle ndani tangia mwaka 2004.
Asante kwa ufafanuzi ndugu lucky sabasaba. Niliona documentary Mtv kuhusu hoteli hiyo, nilidhani wanatania. Usiseme 'Twafa', sema 'Nafa'. Usiku mmoja mtu anaunguza sh m1.62 ilhali kuna mtu anakufa kwa kukosa sh 1000 ya dawa mseto ya malaria.
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu wanaishi naona wengine ni kama abiria tuu room Dola 65000!
One day yes
 
Back
Top Bottom