Acha dharau anachoongea mtoa mada ni kweli,Binafsi niliona mwaka fulani pale Dar Live,wapiga picha wamejaa kila kona na mtu umeenda kufanya starehe zako kwa faragha,bpia Jangwani Sea breeze nilishindwa sababu hiyo hiyo, Nimekanyaga ufukweni tu na warembo wawili nikashtuka tayari nipo kwenye kurasa yao ya Instagram.
Ilibidi niwasiliane na Admin akagoma kutoa zile picha,nikatafuta namba za meneja ni Mhindi ndio akasema watazitoa.
Next weekend nimeenda tena Nikapigwa picha wakaweka tena Instagram,nikawasiliana tena na meneja kumuomba atoe.
Wametoa zile picha kwenye Instagram siku tatu mbele wakapost tangazo la kuvuta wateja weekend na mie tena nikawepo kwenye lile Tangazo,Sijawahi kanyaga tena pale.