Hoteli ya nyota Tatu inajengwa Chato, Wana-CCM mnafurahishwa na kitendo cha kupeleka kila mradi wa ujenzi Chato?

Hivi Mheshimiwa Rais wangu ingekuwa ndo ametoka Bagamoyo ambako ni very justifiable kwa miradi kama hii, si wangejenga hadi mahotel ya Nyota 5?! Si wangesema Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam umejengwa sehemu iliyobana kwahiyo uhamishiwe Bagamoyo?! Si wangesema msongamano wa magari kutoka Dar to Tegeta ni mkubwa sana kwahiyo ijengwe barabara ya juu kwa juu kutoka Mwenge hadi Bagamoyo?! Si wangesema ijengwe satellite city Bagamoyo ili kui-backup Dar es salaam?! Si wangehamishwa wanyama kutoka kila kona kupelekwa Saadan?! Hivi hata ile Mlonganzila Hospital ingejengwa Bagamoyo?

Ukweli ni kwamba, Bagamoyo ingekuwa na vigezo vingi vya kuhalalisha massive investments, vigezo ambavyo kwa Chato hata mtoto mdogo huwezi kumshawishi. Hivi kuna mtu kawahi kufika Masasi humu?! Kwa mara ya kwanza, nilienda Masasi last week. Ni mji mkubwa, umechangamka kweli kweli. Hivi Mheshimiwa Rais wetu angekuwa ndo Mkapa Masasi hivi sasa si ingekuwa ndo Manispaa huku ikipelekwa miradi kadhaa ili hatimae iwe ndo center ya kusini?! Kinyume chake, ukitembea Masasi unaona wazi yaliyopo hayatokani na upendeleo wowote wa serikali bali uchakalikaji wa wananchi wenyewe.
 
Umewaza kama nilivyowahi kusema,the Guy is there to stay.Like Mu7,PK&co.
 
Mbona kila mkoa kuna vyote hivyo?!
Hakuna cha ajabu, uzandiki tu...
 
Wana-CCM wanasherehekea hata kuchinjwa kwao. Tazama wananyosherehekea kutovaa barakoa kwenye misongamano ya watu. Hawa binadamu hawajali chochote hata miradi kama hiyo itajengwa mbinguni au jehanam.
 
Kusahau tumeumbiwa wanadamu.
Kuna waziri wa fedha miaka ile. Miradi yote alihakikisha anaipeleka kwao na mikoa ya ijirani zake tu barabara ya lami, umeme, shule.Hivi vyote walihakisha wanajenga kwao tu!
 
Wangetafuta wafanya biashara wawape punguzo la kodi maalumu wajenge , hizi ni Biashara ndogo sana kwa taasisi Kubwa na hawana uzoefu wa kufanya Biashara
 
Bujibuji waache Mkuu miaka yao ishaisha hiyo...sisi tuendelee kupiga makofi tuu Mkuu
 
Mwenye mali kaona kuna soko la hotel, shida iko wapi
 
hoteli ya serikali niijuayo sikumbuki zaidi ya twiga pale udizungwa nyingi niza wafanya biashara...leo chato wameipata haha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…