Jifunze jiografia kabla ya kuilaumu Nchi yako. Kenya itaendelea kutusumbua as long as watalii watakuwa wakitokea Kaskazini mwa Dunia. Ni mtalii gani atoke Ulaya, asishukie Nairobi kama lengo la Tour yake ni kuangalia tu migration? Siyo Watalii wote wanaokuja Afrika Mashariki wanataka kupanda Kilimanjaro ama kwenda Hifadhi za Momela, Arusha, Manyara, Tarangire, Ngorongoro na Serengeti, so lazima atachukua short-cut ya Nairobi - Masai Mara.
Hata hivyo, pamoja na wao kupata Watalii wengi kutuzidi, bado Tanzania imekuwa ikipata mapato mengi yatokanayo na utalii kuzidi Kenya tangu kitambo (possibly hata kabla ya 1990s).