Hotuba ya Freeman Mbowe (CHADEMA) kwa Taifa - Aprili 11, 2021

Hotuba safi sana toka kwa kiongozi makini
 
Hawa wasengenyaji wanaoongea baada ya mwanaume kukata kauli wanaonesha madhaifu yao tu.
 
Haya matusi aliyooga MBOWE leo mitandaoni atakuwa amejifunza kitu.
 
"Itoshe kusema bila unafiki; Utawala wa Awamu ya Tano umeiumiza na kuipasua nchi yetu kwa kiwango cha kutisha. Kikubwa na kibaya zaidi, umepandikiza chuki na mpasuko wa kutisha miongoni mwa Watanzania. Yes, Never and Never Again!!."
Nchi imeparaganyika sana hii.
Samia lete umoja wa kitaifa.
 
Mbowe asitupotee muda watanzania tuna mambo mengi ya msingi ya kufanya. Arudi Hai akalime nyanya
Kweli! Kwa sasa tuko bize kuutazama ukwapuaji mkubwa kuliko wote uliofanywa na hayati!! Angalau yeye ana mashamba ya kulima nyanya huko Hai,sisi huku ccm hatujui tutatokaje hapa,hatina chochote,mifuko empty,akili zenyewe za kuokoteza,atuache kwanza,magu alituvuruga kwa kweli.
 
"Hata hivyo, sisi wa CHADEMA, kwa kiwango kikubwa, bado mioyo yetu inabubujikwa na damu. Macho yetu bado yanatiririka machozi mara kwa mara kwa tuliyopitia na tunayoendelea kupitia."
CCM ya Magufuli na Serikali yake, imetuumiza sana CHADEMA. 😭😭
 
Hotuba nzuri sana na yenye hoja muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu. Ila naomba neno "kuthibiti" litamkwe na liandikwe "kudhibiti" (to control), sambamba na "alithibiti" iwe "alidhibiti".

Thibiti inahusiana na kuhakiki, kuhakikisha au kukubaliana (to confirm or to certify). Kongole ndugu yangu Freeman Aikaeli Mbowe!
 
Yaani wewe wa kunipa taarifa za DRC? Umesemema vema Jambo moja ambalo nakubaliana nalo.ndoa ya Rc na ccm haivunjiki leo. Naona Kila dalili hiyo
 
Keshasema hataki kodi za dhuruma obvious hatopenda kura za dhuruma.....so komaeni njia nyeupe....
nadhani atakubali kuachia madaraka CCM wakishindwa uchaguzi
Saidien kukomaa, mafanikio sio ya mbwe au wapinzani, badilini huu mtazamo mazee
 
Hotuba nzuri.....Mwendazake kama Kaiona anatamani Mbowe apigwe risasi 2000,sema huwezo hana tena wa kuagiza hivyo.
 
Yeye aliumiza na kudhalilisha familia ngap? Mie najua mtoto aliyeambiwa na watoto wenzake ndo maana rais alisema baba yako no mpumbavu.
 
#UpdatesKishikaji

Kutoka kwenye Hotuba ya Freeman Mbowe

1. KUHUSU MIMI
👉Kuanzia tarehe 4/12/2020 nilikuwa nje ya nchi Kwa miezi minne.

👉Hii ilileta taharuki,na wengine walinizushia Kifo lakini sikuwa naumwa. Nilikuwa nje kibiashara na mambo ya Chama.

👉Nilienda nchi za nje kutafuta uwezo wa kufanya biashara nje maana Tanzania na JPM waliaapa sitaweza kufanya Biashara.

2. KUHUSU MAGUFULI

👉Miaka 5 ya JPM imetupa somo Kubwa. Lakini inatakiwa tufikirie Kwa utulivu ni yapi ya kuenzi na kukosoa,na tufanye hivyo Bila upofu wa itikadi zetu.

👉Kesho yetu iliyosalama na Bora hatuna Budi kufikiria tulipotoka,tulipo na tunapokwenda.

👉Hotuba yangu itafikirisha Taifa Kwa Yale yote ya miaka 5 tuliyokubali kuchezewa na Kikundi cha Watu wachache,wakainajisi nchi, Serikali, taasisi yake na katiba yetu.

👉Hatupaswi kuruhusu U-Magufuli kurudi tena Tanzania.

👉Hayati Magufuli atakumbukwa Kwa mazuri na mabaya mazuri Ni haya mawili;maamuzi magumu na kucctiza Kaz

👉Magufuli na Chama cha mapinduzi walitumia nguvu kubwa kuficha ukweli

👉Taifa limeachwa kwenye maumivu makali Kwa kuharibu mifumo ya kiutawala,hakuheshimu haki za binadamu, hakuheshimu mawazo ya watu, hakuheshimu upatikanaji wa Utendaji.

👉Aligeuza Serikali kuwa tawi la CCM. Aliamini watumishi wa Umma lazima wawe CCM. Akajaza watendaji wa serikali kutokea CCM.

👉Aliwaajiri watendaji na kuwataka wahakikishe CCM inashinda kila Uchaguzi. Aliaagiza RCs na DCs kuweka watu ndani.

👉Aliamini Sana matumizi ya ziada ya Majeshi yetu. Alijijengea Sana ulinzi ambao ulizidi miapaka ya kawaida unayowezae kuifikiria.

👉Silaha za Kivita,Doria za nchi kavu an anga,makomandoo, Askari kanzu na Majeshi mengine ambayo hatukuyajua. Uzio wa Chuma uliosafirishwa kila alipokuwa.

👉Mkuu wetu wa Majeshi,Polisi,Zimamoto,uhamiaji na usalama wa Taifa wote waliandamana na Rais popote alipokuwa. Hakuheshimu kabisa bajeti ya Serikali.

👉Deni la Taifa lilikuwa kuwa Kasi ya kawaida. Mpaka sasa Deni la Taifa linazidi Kwa trillion 60.

👉 Hakuheshimu wajibu na nafasi ya asasi za kiraia. Watanzania wenzangu Hatupaswi kuruhusu haya tena. Na haya yanamhusu Hadi yeyote atakayeongoza nchi yetu.

3. KUHUSU BUNGE

👉 JPM alidhibiti Bunge Bila kujali ni mhimili unaojitegemea. Bila hofu aligawa Rushwa Kwa wabunge wa CCM,ili kupitisha Bajeti au Sheria mbovu. Najua Hadi kiasi alichokuwa anawapa. Na kama watahitaji ushahidi tutauweka hadharani.

👉Wakatunga Sheria z kuwalinda;Rais,Makamu wa Rais,Waziri Mkuu,Spika na Naibu Spika. Kupitia Spika alitengeneza Bunge kuwa Chombo cha kumtukuza.

👉 CAG aliondolewa Bila utaratibu na Ndugai alisikika akisema atamuongezea JPM muda,alizuia hotuba za wapinzani.

👉Aliruhusu kukiuka katiba waziwazi na kuwaruhsu watu wasio na vyama vya siasa kuwa wabunge. Muda utazungumza

4. KUHUSU MAHAKAMA

👉Wakati wa JPM hakuheshimu mhimili huu

👉Majaji walitumika kuhujuma haki ya raia Kwa maelekezo ya Serikali.

Kuhusu Siasa
👉JPM hakuwa muumini wa Demokrasia,alitesa na kuumiza wenye Mawazo mbadala na Chadema tumekuwa wahanga.

👉Alidhibiti hadi Demokrasia ndani ya Chama Chake na alitamka hadharani kuwapoteza wale wanaoenda kinyume na yeye.

👉Alipinga rushwa mdomoni lakini alikuwa muumini wa Kutoa rushwa;alinunua Wanasiasa wa upinzani, wakosoaji na alitumia vyombo vya serikali.

👉Tume ya Uchaguzi na CCM waliichezea tume hiyo. Wakashirikiana kuvuruga daftari la wapiga Kura na kuiba Kura kwenye uchaguzi.

👉Uchumi wa Nchi yetu uneyumba. Umeathiriwa na mifumo mibovu ya Kodi. Wawekezaji walinyang'anywa mitaji.

👉23/11/2018 Mimi na Esther Matiko tuliondolewa dhamana kwenye kesi ya Uchaguzi tukapelekwa gerezani Segerea. TRA wakaniandikia barua ya kuidai Kampuni yangu billion 02, Kiuhalisia haikuwa kweli. Wakanipa siku 30 za kupeleka pingamizi mahakamani.

👉Wakafunga Kampuni,Wakafunga akaunti za Biashara na Hadi akaunti zangu binafsi. Baada ya Samia kuingia madarakani wananitumia SMS eti akaunti zangu zimefunguliwa lakini hawajasema fedha kiasi gani wamechukua.

5. KUHUS COVID

👉Tanza ilionekana kituko kwa kupuuza sayansi na kuamua kutumia tiba za asili zisizothibitishwa. Mawaziri wakabaki kuhubiri nyungu.

👉Kuna watu wamekufa vifo ambavyo vingeepukika. Tumepoteza viongozi ambao pia waliipuuzia Corona.

👉Naomba Samia alikimbize Jambo hili Kwa haraka. Mimi binafsi nimechanjwa Chanjo ya Astrazeneca maana nilikuwa kwenye nchi zinazolitambua hili.

👉Samia aunde ile Kamati alosema Kwa haraka. Hata kama hatuna wataalamu wa kutosha basi ajaribu kuchanganya na wa nje.

6. KUHUSU DIPLOMASIA

👉 Serikali ya Awamu wa 5 iliharibu diplomasia iliyojengwa na watangulizi wa JPM Kwa miaka ya nyuma.

👉 Rafiki zetu WA muda mrefu hawakuheshimiwa. Tukaanza kuita watu mabeberu. Lakini hao mabeberu ndo wanatupatia Dawa ZA polio,Ukimwi,nk.

👉Unafiki,Ujinga,Umasikini na Uoga umetufikisha hapa tulipo. Utawala wa Awamu ya 5 umeiumiza na kuipasua nchi yetu Kwa kiwango cha kutisha.

👉Chama cha CCM hakiwezi kukwepa lawama hizi. Kimebariki kila aina ya ukatili baada ya kujihakikishia watabaki Madarakani hata Kwa kutumia vyombo vya Dola. Taifa linawadai CCM.

👉Makundi mbalimbali yalijenga Unafiki wa Kumtukuza JPM;Makanisa, Vyombo vya habari,nk.

👉Bila hofu Serikali ilipora uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu. Tunaongozwa na watu tusio wachagua.

7. KUHSU SAMIA

👉Baada ya kuapishwa alisema katika kipindi cha muda wote wa maombolezo tunatakiwa kuzika tofauti zetu,na Si wakati wa kutazama yaliyopita Bali tutazame yajayo.

👉 Sisi CHADEMA tumeuandikia barua ya kuonana naye,bado mioyo Yetu inavuja damu,na tumemuomba kuonana naye ili kumueleze jinsi tunavuja damu. Hatupo kwenye biashara ya siasa bali kujenga Tanzania iliyo Bora.

👉Rais wetu alikuwa mshiriki namba mbili wa serikali ya Awamu ya 5,Kwa vyovyote vile hawezi kukwepa lawama ZA uozo wa serikali iliyopita. Lazima Pawe na collective responsibility.

👉 Nyerere alizungumza dhana ya kujisahihisha. Rais Samia ana nafasi ya kujisahihisha. Ana doa,ana uchafu na ana damu za Watu. Huenda mengine hakuyajua lakini Sisi tunamuomba asimame aliombe Taifa ladhi.

Mungu amuongezee kipigo huko alipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…