Hotuba ya JK ya Mwaka Mpya 2010

Is he not the same guy who told us in 2006 that matatizo ya mgao wa umeme yatakuwa kwishney?

2006 alidai Watanzania tusisikitike sana kuhusiana na matatizo ya umeme maana yanasababishwa na Muumba! Katika nchi zote za Afrika huyo Muumba kila mwaka aisakame Tanzania tu! ili iwe na matatizo ya umeme na hii sasa ni miaka 18 ya matatizo haya ya umeme ambayo yalianza 1992 wakati Mzee Rukhsa yuko madarakani, nakumbuka ilikuwa ni July au August ya mwaka huo.
 
Is he not the same guy who told us in 2006 that matatizo ya mgao wa umeme yatakuwa kwishney?

Amesahau mambo yote mazuri aliyoahidi kuwafanyia watanzania. Mi nilitegemea kwavile huu ndo ulikuwa mwaka wake wa mwisho kuelekea uchaguzi angejikita zaidi ktk mambo muhimu ambayo ameyafanya na anategemea kufanya nini kwa mwaka huu.
Hapa katusomea yale watu waliyoandaa kwa maslahi yako na siyo ambayo yeye kama yeye ndo ameona ya muhimu kuyasema.
 
Kwenye suala la Kilimo, aidha mimi ndio nina matatizo ya kuelewa au hii issue ni complex mno mpaka imenizidi kimo::

Upungufu wa chakula vijijini umeongezeka kwa 50% according to JK, na chakula cha misaada kinachotolewa na serikali kimeongezeka almost *10!!

at the same time, JK anasema mafanikio makubwa yamepatikana kwenye kilimo kwanza na budget imeongezwa kwa kiasi kikubwa na mafanikio lukuki.

Sasa upungufu wa chakula unakuja vipi kwa kiasi kikubwa hivi?? Ukisema ukame, kilimo cha umwagiliaji kama investment ya kutosha ikiwepo si kingepunguza tatizo hili??

Mimi nadhani badala ya maneno mengi budget ijayo ifanye hivi kwenye kiini cha budget::

1) Double kilimo budget, na ongezeko lote liende kwenye kununua matrekta na vifaa vyake, mbegu bora na mbolea ambazo zitakopeshwa wakulima vijijini kwa ufanisi na uangalifu wa hali ya juu ilim benefit ziwe wazi.

2) Double Afya budget, na ongezeko lote liende kwenye ujenzi na ukarabati wa hospitali za wilaya, hospitali za mikoa na vituo vya afya especially vijijini, na upatikanaji wa dawa na ajira kwa wana afya especially vijijini.

3) Double elimu budget, na ongezeko lote liende kwenye ukarabati wa shule za msingi, sekondari na baadhi ya vyuo vya juu pamoja na kuajiriwa wa walimu na wahudumu wengine.


Baada ya hii blueprint, ni suala la wazi kuwa lazima budget za wizara nyingine zipunguzwe kwa kiasi kikubwa na matumizi ya serikali nayo yapungue. Yafuatayo yatasaidia

1) Kwa mwaka 2010/2011 FREEZE safari zote za nje kwa civil servants na politicians wote ( Hata kama kuna umuhimu gani tutamiss kwa mwaka mmoja kisa tunafanya ya maana zaidi)

2) Freeze, mikutano yote na semina mikoani au mahotelini na information zote zitumwe kwa wahusika kwa email attachments kwa mwaka mzima.

3) frreze manunuzi ya magari, vifaa vya ofisi, majumbani nk kwa mwaka mmoja.


Tunachofanya sasa hivi ni kuspend hela kwenye hizo freeze suggestion hapo juu na kusema hatuna hela kwenye mambo muhimu ya Afya, kilimo na Elimu.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Kuhusiana na hotuba ya Mh. Rais Kikwete kumaliza 2009 na kuukaribisha 2010:

Kwanza kabisa, naungana naye katika kuomboleza msiba mkubwa uliolikumba Taifa letu kwa kuondokewa na mmoja wa waasisi wa Taifa letu, Mzee Kawawa. Mwenyezi Mungu Ailaze Pahali Pema Peponi Roho Yake. Amina.

Narudi kwenye salamu hizi na maudhui yake;

==> Mh. Rais ametumia zaidi ya maneno 5000 katika kuwakilisha salamu zake kwa umma wa Tanzania, wakati mwenzake Mh. Kibaki ametumia maneno takribani 1000 (shukrani kwa aliyeweka nukuhu). Hii inaonesha nini?!

-- Watanzania ni wapenda majungu badala ya kujikimu kwenye vitendo.

-- Aliyetayarisha hotuba alikuwa na lengo la kuwa-confuse Watanzania kwa maneno meeeengi wakimsikiliza Mh. Rais mpaka wajisahau ni kipi aliongelea au kipi hakuongelea. Huku yeye akijitua mzigo kwa kujisifu kuwa ametimiza wajibu kwa 'kuwahutubia' wananchi na kuwaeleza mambo mbalimbali. Wakati mambo yenyewe yako very general.

Ni mambo ambayo yapo kwenye magazeti na vyombo vya habari kila kukicha. Kuna haja gani basi kuwaketisha wananchi kitako kwa muda mrefu namna hiyo kuongelea kitu kilekile, maana maelezo mengi kwenye hotuba wala hayaelezei specific solution bali yana highlight tu mambo yaliyopo. Asilimia kubwa ya salamu hizi ukiachilia mambo ya msiba na mwaka mpya yangeliweza kabisa kuwa covered katika hotuba za Mh. Rais za kila mwezi.

-- Aidha basi, hotuba ndeeefu namna hiyo inaonesha ni jinsi gani Mh. Rais alivyokuwa na vipolo vya kuongelea au kuwataarif wananchi. Na hii kwa undani inaonesha ni kwa kiwango kipi mambo ambayo yanatakiwa yatekelezwe na kutangazwa kwa umma mara kwa mara huwa hayafanyiki.

Umma hauelimishwi na kuelezewa mambo yanayolikabiri Taifa hili (hata kama yote yaliyoongelewa yangelikuwa mapya), kutokana na uzembe au kwa makusudi ili kutokuwa na umma ulio kuwa 'informed' kwa lengo la kuondoa bugudha au kuficha uzembe na maovu yaliyopo. Kwani by the time wananchi wanaelezwa, jambo limeshatendeka na inakuwa too late to talk about or rectify. Naweza nikasema , ni tactic katika ujenzi wa "Taifa Bubu." Ni salamu za mwaka mpya, kwanini aifanye hotuba ya mwaka?!

==>Baadhi ya mambo aliyo yaongelea.
Mh. Rais, kwa heshima na taadhima napenda kukueleza kuwa, watu wanaochochea kugawa Taifa hili ni baadhi ya wale viongozi wastaafu na waliomo madarakani waliokumbwa katika kashfa mbalimbali za kuhujumu Taifa letu. Na cha ajabu zaidi kuhusu watu hawa ni kwamba, wengi wao bado wanapeta mitaani wakiwa huru na wakiendeleza biashara zao. Na wengine wakizidi kuteuliwa kushika madaraka mengine au kubakia kwenye uongozi. Hili ni kero kwa wengi wetu na ni jambo linalovuta hisia za uovu dhidi yao na kwa wanao walinda. Utawala wa sheria wa Taifa dhidi ya wahalifu hawa haufanyi kazi, na huku ndiyo kuligawa Taifa!

Mh. Rais, tunathamin na kuutukuza uhuru uliotupatia wa kujieleza. Ahsante. Katika hili napenda kusema kwamba, kuna wakati utafika ambapo amani na utulivu wa Watanzania utafika kikomo, iwapo hali inayoendelea (kama nilivyo elezea hapo juu kuhusiana na wahujumu uchumi) haitazuilika. Kila kitu kiko perishable pale ukikitumia isivyo. Na hili ni swala kubwa linaloonekana katika hali yetu ya kisiasa Kitaifa. Kila jambo tunasingizia wachafua amani na utulivu. Tuulinde amani na utulivu wetu kwa kuwajibika kama viongozi wa Taifa letu tukufu na siyo kutafuta scape goats.

Kwa mfano, kisa cha hivi sasa cha BoT na ujenzi wa nyumba za magavana. Nikiamini jambo hili limekera Watanzania wengi nami nikiwemo, cha kujiuliza ni kwamba, inakuwakuwaje Waziri wa fedha alikuwa hajui hata wewe kutokuwa na taarifa hizo ilihali ni mwaka jana tu taasisi hiyo ilikuwa iko kwenye kashfa kubwa Kitafa hata kimataifa?! Why do you allow such things to happen, why?! Kwanini magavana hawa waendelee kuwepo kwenye nyadhifa hizi? It beggars belief!

Mh. Rais, unakubali kuwa kuna uhalifu pia kuna wahalifu waliokamatwa na Jeshi letu Tukufu la Polisi. Cha kujiuliza hapa ni, ni akina nani hawa na sasa hivi wako wapi?!

Ngoja niishie hapa. Ahsanteni.


Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Afrika,
Kheri ya Mwaka Mpya 2010!

SteveD.
 
wadanganyika ni majitu ya ajabu, kabisa kazi yao kulaumu tu hamuoni hapo kwenye hotuba ya (ni rahisi au rais mimi sajui kiswahili bana) kila jambo litafanyika mwaka 2010? ("Matengenezo ya mtambo wa Songas ulikamilika na Kihansi bado mpaka Januari 2010". "Wakati wowote mwezi Januari mwaka 2010 umeme utawaka Kilindi', "Kwa upande wa usafiri wa anga mwaka huu Serikali imeendelea na jitihada za kuimarisha utendaji na uendeshaji wa Shirika la Ndege la Tanzania. Pamoja na hayo, pia Serikali imeendelea na mchakato wa kupata mbia wa kushirikiana nae kuendesha shirika hilo. Ni matumanini yangu kuwa mchakato huo utakamilika mapema mwaka 2010 ili shirika letu tulipe matumaini mapya ya uhai na maendeleo".
Katika mwaka ujao tunategemea mambo kuwa mazuri zaidi. Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa zile barabara za Tanga – Horohoro, Tunduma – Sumbawanga na Namtumbo – Songea – Mbinga zitaanza kujengwa. Mchakato wa ujenzi wa barabara hizo zinafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia mfuko wa Millennium Challenge Account, hivi sasa imefikia hatua ya uteuzi wa makandarasi wa barabara hizo. Kazi hiyo ya uteuzi inatarajiwa kukamilika robo ya kwanza ya 2010 na ujenzi kuanza katikati ya mwaka. Ratiba ni hiyo hiyo kwa miradi mingine inayofadhiliwa na MCC.
) yaani miaka yote alikuwa najipanga na kuandaa mambo hivyo utekeleza wa mambo yote ni kuanzia mwanzoni mwa 2010 mpaka kufikia october 2010 yote yatakuwa yamefanyika na kukamilka, yaani ni kama kulipua boma ya pwaaaa kila kitu kimefanyika na kukamilia. jinsi raisi alivyoutaja mwaka 2010. kwanza kaanza kwa kuukaribisha mwaka 2010. pili UHALIFU KUZIBITIWA nanukuu "nawapongeza sana wenzetu wa jeshi la polisi kwani kwa mwaka 2009 walitajwa kwa kuongoza kwa ruswa nchini nawaomba mwaka 2010 waongeze juhudi mara dufu mimi naendela kuwahaidi msaada na ushirikiano wangu".

"Napenda kumalizia salamu zangu za mwaka mpya kwa kumshukuru tena Mwenyezi Mungu kwa rehema zake alizotujalia mwaka 2009. Tumuombe atuzidishie maradufu yale yaliyo mema na kutunyooshea yasiyokuwa na maslahi mema kwetu katika mwaka ujao 2010". (yahaani unamshukuru mungu kuwa ufisadi mliofanya mwaka 2009 kuwa ni rehema na kuwa azidi kuwanyooshea yale yasio na mslahi kwa taifa mzidi kuyafanya kwa mwaka 2010 au unamaanini nini hapo ?)


WALAU HII ITAPUNGUZA SAFARI MOJA YA NJE

Pengine katika heshima kubwa na muhimu tuliyoipata mwaka huu ni ile ya kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa masuala ya kiuchumi Barani Afrika uitwao World Economic Forum on Afrika. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mikutano hyo kufanyika nje ya Cape Town, Afrika Kusini. Ni heshima kubwa kwa Tanzania, hivyo nawaomba Watanzania wenzangu na hasa wananchi wa Dar es Salaam kuwapokea vizuri wageni wetu wazito kwa utajiri na maarifa. Tuoneshe ukarimu wetu wa kawaida kwa wageni wetu ili wapende kurudi tena Dar es Salaam na Tanzania kwa mikutano mingine au matembezi na shughuli nyingine.



huwenda niko kwenye wale asilimia 70 aliowataja maana hapa sijaona alichoongea.
 

Usafiri wa Anga[/U]

[/SIZE][/FONT]

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa usafiri wa anga mwaka huu Serikali imeendelea na jitihada za kuimarisha utendaji na uendeshaji wa Shirika la Ndege la Tanzania. Pamoja na hayo, pia Serikali imeendelea na mchakato wa kupata mbia wa kushirikiana nae kuendesha shirika hilo. Ni matumanini yangu kuwa mchakato huo utakamilika mapema mwaka 2010 ili shirika letu tulipe matumaini mapya ya uhai na maendeleo.

Serikali imeendeleza juhudi za ujenzi na uimarishaji wa viwanja vya ndege nchini. Shughuli za ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere zimeendelea kufanyika. Mwaka huu tunatarajia kazi hiyo kuendelezwa kwa upana na kina zaidi. Aidha, kazi ya kuimarisha viwanja vya ndege vya Arusha, Mwanza, Mpanda, Bukoba na Mafia imeendelea kama ilivyopangwa. Katika mwaka huu, kwa msaada wa wabia wetu wa maendeleo matengenezo makubwa yatafanywa kwa viwanja vya Tabora, Kigoma, Bukoba na Mafia. Naomba Wizara ya Miundombinu na hasa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wamsimamie kwa karibu mkandarasi anayejenga Uwanja mpya wa ndege wa Kimataifa wa Songwe ili uanze kutumika mwaka 2010. [/B]


.................hii ni aibu kubwa zaidi kwa serikali ya Tanzania.........miaka karibui 50 ya uhuru,hakuna shirika linaloelweka??? kazi ni kuongea tuuuu na kuomba misaada?? Mjifunze kusimama wenyewe,kawaulizeni Ethiopia wanafanyaje....just imagine, tiketi ya ATC toka Mwanza- Dar, ambayo sio go and return inauzwa Tshs 170,000, lakini kutokana na uvivu wa nchi hii, juzi na jana tiketi hizi zimeuzwa hadi Tshs 348,000!!???? Na kuficha hujuma hii, tiketi hauiandikwi details zozote.......Aibu gani hii!!!!!!!!!
 


Mawazo safi kabisa. Ninaamini yatafanyiwa kazi.

Hivi bajeti yetu ya kilimo cha Umwagiliaji ni shilingi ngapi kwa mwaka huu wa fedha wa 2009/2010?
 

Asante sana Mr Pesident kwa hutuba yako nzuri. Lakini nafikiri kwamba lazima unawaogopa MAFISADI. Unawaogopa MAFISADI inawezekana aidha kwa usalama wa maisha yako au unawaogopa wasije wakakuumbuwa. Niiini hasa hebu tueleze!!! Lipi haaaassa katika hali ya shauku hiii tuliyonayo waTZ kuona wanachukuliwa adahabu kali zikiwemo za kifo wewe ukae kimya kuhusu hili??? Kwanini hujagusia hata kidogo ??? Tafadhali Mheshimiwa, ashakum si matusi, usitubabaishe!!! usitudanganye, tumeshachoka na bla, bla bla, bla. Hoja ya kwamba masuala yao yanashughulikiwa na vyombo vya sheria ni uwongo mtupu. Ni uongo mtupu kwasababu bado wanaendelea kuwa untouchables wakiwa mafichoni ndani ya chama chako CCM. Prosecutors wanawaogopa wakiwa huko, na kila mtu analijuwa hilo. Na hali ikiendelea kuwa hivi, katu hawatachukuliwa hatua yeyote, maishaaa, nawewe naamini unalijua hilo. Unajua waTZ tuna usongo nao hawa??? Unajua kwamba kichwa na roho za rushwa, umasikini, kurudi nyuma kimaendeleo ni UFISADI NA UFISADI PEKEE, au hujui kwamba UFISADI AUKIONDOKA TU, basi bila shaka rushwa, ubaguzi, umasikini, nk, nk VYOTE VITAKA ROHO, vitake visitake???? Na as long as MAFISADI NA UFISADI wao wanaendelea kunawiri basi matokeo yake ambayo ni rushwa, umasikini, ubaguzi nk nk vitaendelea kutumong'onya mpaka kiama??? Hili lazima ulijue.

Kama kuna ukweli, basi tulitaka na kutegemea kusikia sio chini (not short of): Watuhumiwa MAFISADI wote ndani ya maficho ya chama chako, UNAWAPA MWEZI MMOJA WAJIUZULU WENYEWE, AMA UNAANZISHA MKAKATI WA WAO KUVULIWA UANACHAMA, KUFUKUZWA/KUSIMAMISHWA KUTOKA CHAMANI. UNAJUA KABISA KWAMBA HILI LIKITOKEA MADARAKA YOOOOTE WALIYONAYO YA KUCHAGULIWA NA WANAYORINGIA YATAWAVUKA, mfano, ubunge, nk. HAPO TENA WANATUKUWA WATUPU KWA SHERIA KUCHUKUWA MKONDO WAKE. Kinyume na hivyo basi ujue umetuangusha kwa mara nyengine tena, maana unajua kwamba, so far umeshatuangushaaaa, nasi kwanini tusikuangushe katika uchaguzi??? na tutakaemleta Mungu akipenda pengine atatusukiliza na kutuinua

TULITAKA KUSIKIA VILEVILE UNAKUSUDIA KUZUNGUMZIA NA CABINET YAKO NA KUMUAMRISHA WAZIRI WAKO HUSIKA (aidha Mambo ya ndani, Mwanasheria Mkuu, au yeyote atakaehusika) KUHAKIKISHA NDANI YA MIEZI MITATU YA KWANZA YA DECADE ANALETA BUNGENI MSWADA WA MABADILIKO AU KUUNDWA SHERIA AMBAO UTAHAKIKISHA MAFISADI wanakumbana na ADHABU YA KIFO, WANATAIFISHWA MALI ZAO ZOTE, (kwa tafsiri ya haraka haraka Mafisadi ni wale inapotajwa fasada majina yao huambatana na mamia ya mamilioni, bilioni, and above. Majina yao huambatana na vyeo kama vile former au current president, minister, deputy minister, katibu mkuu wa wizara, mkurugenzi wa wizara au yeyote miongoni mwa karibu nafasi 7000 za ngazi za juu serikalini).

Vipi tunaaga mwaka, hawa cancer, najisi hawa wasitajwe hata kidogo???
 
wakati huo huo, si vibaya tukisoma na ya Mhe. Emilio;

Waridi ahsante kwa hotuba ya Emilio. Unahitaji 5 minutes kuzipitia hizi hotuba kujuwa yupi ni rais na yupi ni msanii wa kutupwa.Hapa ndipo kwenye tofauti yetu kimaendeleo. Jamani mimi sielewi hivi kama Kenya ndio ingekuwa tz na tz ikawa ndio kenya kijiografia hali ingekuwaje? Siku zote nikikutana na kenyans huwa wanamadmire sana presidaa wetu me nadhani wanaangalia sura zaidi kuliko kazi. Utasikia oh wao wanaibiwa sana, sijuwi nani kawaambia kwamba sisi pamoja na tabasamu kuwa hatuibiwi? Serikali yao inapiga kazi lets be serious kwa kweli. Yaani hata ukisoma mipango utaona kbisa kwamba wapi wanaelekea hapa kwetu duh Mungu wangu hata sijuwi tulikosea wapi jamani.
 
Hivi mlitegemea msikie nini jamani...........from the same "Kikwete"?........

Ogah you have said it all! Mungu wangu hivi huwezi kutusamehe kweli na kutuepushia mbali haya mabalaa ukifika wakati wa uchaguzi mwaka huu? Its too too too much. Taasisi ya urais imefanywa kuwa rahisi kiasi hiki?
 
Nilitegemea mafanikio aliyoyapata miaka minne iliyopita but sijaona kitu. Au tutegemee mafanikio tukishamchagua tena? Sasa nakumbuka ule wimbo wa kijana mmoja anaitwa prof j ndio Mzee!!!
 
Hii hotuba ni bure kabisa; hakuna lolote la maana katika hotuba hii ila nitatoa sababu zangu baadaye kwa nini nasema hivyo.
 

Great thinking which ended up with great suggestions, congraturations. My worry is if such great suggestions can be adopted for implementation by our government. Because the systems (decision makers) are motivated with personal gains and not national gains. Let's pray for them so as they can behave like wise men/women and decide strongly for the public interest!
 

...mmnnnnnh, mdau unahabari Tanzania tunanunua/(kununuliwa!) ndege zetu, wakati wenzetu hao uliowataja Ethiopia, na hata Kenya hawana ndege zao? ...usiyaone ma Boeing series- 737, 767 na 777 yanaruka tu, yote yamekodiwa tu yale.

Anyway, kinachonishangaza ni kwanini serikali isibadili mfumo wa uendeshaji shirika, kwani tayari ishaonekana uendeshaji kwa mfumo uliopo ni hasara tu!
 

Mara nyingi sasa nimekuwa nikiongelea habari ya sisi watanzania kupenda bla bla, mara hivi halafu vile pasipo umuhimu wowote. Wewe sikiliza hotuba za Rais wetu anazohutubia nje ya nje, hadi zinaboa. Meneno mengi kiasi cha pengine hata jambo la kunukuu ndani yake hakuna. Yale yale masuala ya kila siku kwenye magazeti na vyombo vya habari vingine ndiyo ya kuongelewa pia.

Nasita kusema kwamba sijui nikubaliane na wanaosema kwamba Rais wetu hashauriki, ama washauri wana matatizo!! Kwa kweli hotuba hasa iliyoandaliwa kisayansi haihitaji maneno mengi pasipo lazima. Hotuba ya Rais wetu ya juzi, ukiondoa salamu za kuwatakia watanzania heri ya mwaka mpya na masuala ya kifo cha mzee wetu; ilitakiwa iwe imejaa takwimu tu zinazolinganisha hatua iliyofikiwa hasa kiuchumi, kijamii, siasa kwa miaka ya 2008 na 2009. Hapo tungeelewa na kupata picha halisi kwamba wapi kama nchi tulilegea na sababu zake ni zipi. Wapi tumepiga hatua zaidi, sababu zake ni zipi ili kwa kufanya hivyo wananchi wataacha mabaya yaliyosababisha kuwaangusha na kuendeleza yaliyofanya kupiga hatua zaidi.

Sasa mara wanaovuruga amani wakati hao wanafahamika kwamba ni "mafisadi" ambao wananchi wamechoka na Serikali kuwanyamazia tu wakifanya wapendavyo! Anatumia maneno mengi kuelezea watu kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Nani hao? au maigizo ya akina Yona na Mramba? Wako wapi wamiliki wa Kagoda Agriculture? Wako wapi waliofuja mali ya Umma kupitia MEREMETA Na TANGOLD? Hatua gani zimechukuliwa katika utekelezaji wa maagizo ya chombo cha juu kabisa katika nchi yetu (Bunge) kuhusiana na Richmond?

Miradi hiyo ya kinyonyaji imepoteza fedha kiasi gani hadi kulazimisha bajeti ya kilimo isiwe asilimia 10 kama inavyotakiwa kuwa? Hayo mengine yamejitokeza ya ufujaji wa mali za umma pale TANESCO na BOT, mbona kama ni kufanya hotuba iwe ndefu hatuyaoni kusemwa?

Nchi yetu kupitia wananchi wake hadi Rais naomba tuache ubabaishaji! Mimi binafsi nawataka radhi watanzania wenzangu kama kuna mahali sikuwajibika ipasavyo mwaka 2009. Niko tayari kuwa mwananchi mwema aliyetayari kutumikia watanzania hasa masikini.

Mungu ibariki Tanzania!!
 

...kweli eeeh? charity starts at home, hebu jifikirie kwenye bajeti ya mwaka mzima nyumbani kwako, ilhali wewe ndiye unashikilia funguo za Fedha na Uchumi. Ukabana kila kitu ili ufanikishe kilimo kwenye ekari zako kadhaa. Fikiria, ukajiwekea fungu la kutosha tu kwenye bima ya afya au sijui AAR, na fungu jingine ukawekeza kwenye Elimu!...

Vipi gharama masuala ya Miundombinu ya kukupeleka huko kwenye hizo Investments na kwenye mihangaiko yako ya kila siku?, hii yawezekana ikawa ni daladala, teksi, lori au hata motokaa.

Vipi gharama za Ulinzi kulinda nyumba ukiwa huko maungani? na je, ushirikiano na majirani zako achilia mbali ndugu jamaa na marafiki wa Kimataifa maana vikadi vya mchango haviishi...wakati huo huo, gharama za Luku, Mkaa, Kuni au gesi za kupikia na Mishumaa inakusubiri kwenye Nishati!

Naendelea kutoa mifano ya kufinya bajeti; Mawasiliano na technolojia, hata kama kuna longa longa na cheka time, bado vocha inakula pochi, achilia mbali airtime angalau kudodosa mawili matatu JF?.

Tukija kwenye Mambo ya ndani ndio usiseme, familia ina mahitaji yao muhimu tena ya kila siku, na inakubidi uyadhibiti ili kuweza kudhibiti sheria na katiba ili maliasili watu na wasilia visihujumiwe... pamoja na yote bado kuna mahitaji ya Chakula, Mifugo, na hata watoto kwenye Ustawi wa Jamii...

...hapo bado hujajikatia allowance kidogo, au kaji day-out katika kuburudisha mawazo kwenye 'michezo,' mila na utamaduni! All in all, juhudi yako yote kwenye ile Doubling up bajeti ya Afya, Elimu na hasa Kilimo, haitakuwa na maana iwapo hujawekeza kwenye kutangaza soko la bidhaa zako, hapa namaanisha Biashara!
...kwenye hii dunia ya tatu, mtumishi wa serikali au mashirika ya umma itabidi tu upokee 'mlungula'.

Serikali wao hawana 'mlungula', ila huomba misaada nje kufidia pale penye mapungufu kwenye pato la taifa.
Great Job Muungwana na team yako, lakini juhudi zaidi zinahitajika ili kuikwamua nchi na wananchi wake.

Kumradhi kwa mfano niliotoa, lakini nimejaribu kuangalia picha kwa ukubwa wake.
 
As usual, you can "RECYCLE" in Tanzania too.

We have seen the same thing over and over again. There's no new ideas in the speech or any new challenges facing the nation. All he did is to get new words like Kilimo Kwanza to polish it and look like we have something new.

One question to Mr. President, the Tourist of the Year 2009, (2009 is over so this is official), what are the three (3) things are you planning to give first priority this year, try to solve it so that next January we won't see again in the speech?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…