Kuhusiana na hotuba ya Mh. Rais Kikwete kumaliza 2009 na kuukaribisha 2010:
Kwanza kabisa, naungana naye katika kuomboleza msiba mkubwa uliolikumba Taifa letu kwa kuondokewa na mmoja wa waasisi wa Taifa letu, Mzee Kawawa. Mwenyezi Mungu Ailaze Pahali Pema Peponi Roho Yake. Amina.
Narudi kwenye salamu hizi na maudhui yake;
==> Mh. Rais ametumia zaidi ya maneno 5000 katika kuwakilisha salamu zake kwa umma wa Tanzania, wakati mwenzake Mh. Kibaki ametumia maneno takribani 1000 (shukrani kwa aliyeweka nukuhu). Hii inaonesha nini?!
-- Watanzania ni wapenda majungu badala ya kujikimu kwenye vitendo.
-- Aliyetayarisha hotuba alikuwa na lengo la kuwa-confuse Watanzania kwa maneno meeeengi wakimsikiliza Mh. Rais mpaka wajisahau ni kipi aliongelea au kipi hakuongelea. Huku yeye akijitua mzigo kwa kujisifu kuwa ametimiza wajibu kwa 'kuwahutubia' wananchi na kuwaeleza mambo mbalimbali. Wakati mambo yenyewe yako very general.
Ni mambo ambayo yapo kwenye magazeti na vyombo vya habari kila kukicha. Kuna haja gani basi kuwaketisha wananchi kitako kwa muda mrefu namna hiyo kuongelea kitu kilekile, maana maelezo mengi kwenye hotuba wala hayaelezei specific solution bali yana highlight tu mambo yaliyopo. Asilimia kubwa ya salamu hizi ukiachilia mambo ya msiba na mwaka mpya yangeliweza kabisa kuwa covered katika hotuba za Mh. Rais za kila mwezi.
-- Aidha basi, hotuba ndeeefu namna hiyo inaonesha ni jinsi gani Mh. Rais alivyokuwa na vipolo vya kuongelea au kuwataarif wananchi. Na hii kwa undani inaonesha ni kwa kiwango kipi mambo ambayo yanatakiwa yatekelezwe na kutangazwa kwa umma mara kwa mara huwa hayafanyiki.
Umma hauelimishwi na kuelezewa mambo yanayolikabiri Taifa hili (hata kama yote yaliyoongelewa yangelikuwa mapya), kutokana na uzembe au kwa makusudi ili kutokuwa na umma ulio kuwa 'informed' kwa lengo la kuondoa bugudha au kuficha uzembe na maovu yaliyopo. Kwani by the time wananchi wanaelezwa, jambo limeshatendeka na inakuwa too late to talk about or rectify. Naweza nikasema , ni tactic katika ujenzi wa "Taifa Bubu." Ni salamu za mwaka mpya, kwanini aifanye hotuba ya mwaka?!
==>Baadhi ya mambo aliyo yaongelea.
Mh. Rais said:
Aidha, taifa letu limeendelea kuwa moja na watu wake wameendelea kuwa wamoja, licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale zilizotokana na harakati za vyama vya siasa na kauli za baadhi ya wanasiasa na viongozi wa kijamii wakiwemo wale wa dini. Wakati mwingine, matendo na kauli zao zimekuwa na mwelekeo wa kuwagawa Watanzania katika makundi yenye mifarakano na uhasama.
Mh. Rais, kwa heshima na taadhima napenda kukueleza kuwa, watu wanaochochea kugawa Taifa hili ni baadhi ya wale viongozi wastaafu na waliomo madarakani waliokumbwa katika kashfa mbalimbali za kuhujumu Taifa letu. Na cha ajabu zaidi kuhusu watu hawa ni kwamba, wengi wao bado wanapeta mitaani wakiwa huru na wakiendeleza biashara zao. Na wengine wakizidi kuteuliwa kushika madaraka mengine au kubakia kwenye uongozi. Hili ni kero kwa wengi wetu na ni jambo linalovuta hisia za uovu dhidi yao na kwa wanao walinda. Utawala wa sheria wa Taifa dhidi ya wahalifu hawa haufanyi kazi, na huku ndiyo kuligawa Taifa!
Mh. Rais said:
Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru kwa dhati Watanzania wenzangu kwa ukomavu wa kisiasa, moyo wao wa uzalendo na busara waliyotumia ya kukataa kuwa wahanga wa njama hizo ovu. Badala yake mmechagua kufuata na kufanya mambo yenye maslahi kwa umoja, maendeleo na usalama wa taifa letu. Hakika ni moyo huo na ufahamu huo ndiyo umeliweka taifa letu kuwa moja na lenye amani na utulivu tulionao tangu uhuru wa Tanganyika, mapinduzi ya Zanzibar na baadae Muungano mpaka leo. Nawaomba ndugu zangu tushikilie msimamo huo hasa katika mwaka ujao wa uchaguzi ambapo haya yaliyofanywa mwaka huu yanaweza kufanywa maradufu.
Tusiwape nafasi wakafanikiwa wale watu wabaya wanaotaka kutugawa kwa dini, kabila, rangi, Bara na Visiwani au Unguja na Pemba. Pia tusiwape nafasi wale wote wanaotaka kuleta machafuko nchini. Kamwe tusikubali kuwa kama wale wenzetu tuliowapa hifadhi hapa kwetu au tunaowaona kwenye luninga na kuwasikia katika redio na kuwasoma katika magazeti wakiuana, kuumizana na kuharibiana mali huko nchini kwao. Nina imani kubwa kwamba hatutaiacha nchi yetu ifike hapo.
Mh. Rais, tunathamin na kuutukuza uhuru uliotupatia wa kujieleza. Ahsante. Katika hili napenda kusema kwamba, kuna wakati utafika ambapo amani na utulivu wa Watanzania utafika kikomo, iwapo hali inayoendelea (kama nilivyo elezea hapo juu kuhusiana na wahujumu uchumi) haitazuilika. Kila kitu kiko perishable pale ukikitumia isivyo. Na hili ni swala kubwa linaloonekana katika hali yetu ya kisiasa Kitaifa. Kila jambo tunasingizia wachafua amani na utulivu. Tuulinde amani na utulivu wetu kwa kuwajibika kama viongozi wa Taifa letu tukufu na siyo kutafuta scape goats.
Kwa mfano, kisa cha hivi sasa cha BoT na ujenzi wa nyumba za magavana. Nikiamini jambo hili limekera Watanzania wengi nami nikiwemo, cha kujiuliza ni kwamba, inakuwakuwaje Waziri wa fedha alikuwa hajui hata wewe kutokuwa na taarifa hizo ilihali ni mwaka jana tu taasisi hiyo ilikuwa iko kwenye kashfa kubwa Kitafa hata kimataifa?! Why do you allow such things to happen, why?! Kwanini magavana hawa waendelee kuwepo kwenye nyadhifa hizi? It beggars belief!
Mh. Rais said:
Katika mwaka huu tunaoumaliza leo tumeshuhudia kuimarika kwa juhudi za kupambana na uhalifu na maovu katika jamii. Matokeo ya juhudi hizi yameonekana katika kudhibitiwa kwa uhalifu. Wahalifu wengi wamekamatwa na kufikishwa Mahakamani. Njama kadhaa za uhalifu zimezuiliwa. Watuhumiwa wengi wa makosa ya rushwa wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Nawapongeza sana wenzetu wa Jeshi la Polisi na Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini kwa kazi nzuri walioifanya. Nawaomba mwaka 2010 waongeze juhudi maradufu. Mimi naendelea kuwaahidi msaada na ushirikiano wangu na wa Serikali.
Mh. Rais, unakubali kuwa kuna uhalifu pia kuna wahalifu waliokamatwa na Jeshi letu Tukufu la Polisi. Cha kujiuliza hapa ni, ni akina nani hawa na sasa hivi wako wapi?!
Ngoja niishie hapa. Ahsanteni.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Afrika,
Kheri ya Mwaka Mpya 2010!
SteveD.