By Bright, Political Analyst
Rais Kenyatta alipokuwa anahotubia Bunge alizungumza maneno mengi ila kwa sasa nitafanya uchambuzi kwenye maneno machache tu aliyo yatamka kuhusiana na kile kinachoendelea nchi jirani na Kenya.
1. Rais Kenyatta hajamtaja mtu na haja point specifically nchi husika: Kenya imezungukwa na nchi nyingi kidogo na kila nchi ina mfumo wake wa kuendesha siasa ambapo kila mmoja ana mtazamo wake kuhusu wapinzani wake, namna alivyoingia madarakani na anavyotaka kuwepo madarakani na atakavyoachia madara, hii humpa kila mtu fursa ya kujiamlia kivyake, kwa matakwa yake, matakwa ya katiba ya nchi yake na katiba ya chama chake. Ni pamoja na kupuuza katiba zote.
2. Kenyatta yumo kwenye Jumuiya ya Africa Mashariki kwanini hakumuomba mwenyekiti wa sasa kwenye jumuia ili wakutane walijadili swala hili analolizungumzia yeye, maana Africa Mashariki wana political federation ambayo imepangwa kuwepo ila hadi sasa kuna sehem wamekwama kutokana na kila mwanachama kuwa na mtazamo wake wa kisiasa ambao mpaka sasa hataki ubadilishwe labda akitoka au akiachia madaraka. Ni ukweli usiopingika maana hadi sasa political federation ingekuwa imeshaanza kama zingine (customs union...), walichotaka kukubaliana ni kitu kimoja maana yake democrasia ya kweli ambayo ndani nya nchi hizi wengine wameonyesha kutokuwa tayari kwa democrasia ya kweli.
Rais Kenyatta kutomuomba mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukutana ili wajadili maswala ya kisiasa yanayoendelea kuna tafsiri yake. Je, kwanza mwenyekiti haoni na hajui kinachoendelea? Au mwenyekiti na yeye ni mwenye mrengo huo huo ndio maana hawezi kuitisha kikaco ha dharura kujadili maswala haya?
3. Rais Kenyatta alikuwa miongoni mwa walio mpa pongezi Rais wa Tanzania kuhusu kura za ushindi lakini badae ameibuka na hotuba hii, kwanini hakukaa kimya kutompa pongezi wakati anajua hotuba kama hii inakuja ili iwe ndio neno lake moja tu kwa nchi jirani kama anavyosema. Yote sawa kutoa pongezi na kuja na hotuba hii ni kutoa picha halisi ya kile ambacho alikuwa anamaanisha kwenye ile pongezi.
4. Hata kama Kenyatta hakutaja nchi ila matukio yanayoendelea kwa sasa katika nchi 2 Uganda na Tanzania huenda ndio zimempa ujasiri wa kutoa hotuba hii akilinganisha na yeye alivyokuwa karibu na mpinzani au wapinzani wake ili kuonyesha mshikamano na nchi zinakuwa zimetulia kisiasa na kwa ustawi wa uchumi wa nchi zao.
5. Rais Kenyatta anajiamini sana na hana hofu yoyote kuhusiana na uchumi wa nchi yake na maswala ya kisiasa nchini kwake ni jasiri sana, Kenyata hakutaka kuwa muwazi kwa namna anavyojua yeye ni kama alikuwa na ushauri flani kwa watu flani wa tabaka flani na wenye tabia flani ili wajifunze kwake, ametoa ushauri kwa watakaosikia na kuelewa hotuba yake wajaribu.
6. Rais Kenyata amesisitiza kuwa nchi jirani wanahitaji siasa ambazo ushindani haugeuki kuwa uadui na vita ni kwa sababu anajua alichopitia alipo jaribu kutaka kuishi na wapinzani wake kama ma adui, nchini kwake kuliibuka ghasia, machafuko na mauwaji lakini yote haya yalimfanya ajifunze kitu flani ambacho hakutegemea katika maisha kuwa kingeweza kutokea na amejifunza kuwa hawezi kurudia makosa maana ni hatari sana kwa afya yake, familia na vizazi vyake, mtazamo wake ni mpana na maoni yake ni msaada kwa wengine kuwa wasipo jifunza basi watajua huko mbeleni ila kazi yake ameifanya ya kushauri kwa njia ya bunge. endapo majirani wangeomba mushauri kwake angekuwa tayari kwuashauri ili nchi zao zitulie kama yakwake kwa sasa na zisikutane na matatizo.
7. Rais Kenyatta anonyesha makundi ambayo huwa ni hatari sana kuibuka na kuibua vitu ambavyo havikuwahi kutokea, kuna usemi unaosema ni bora kuganga badala ya kutibu maana yake ugonjwa ukitokea kuutibu huchukua muda sana na si ajabu usitibike haraka na usiwe na uwezo wa kifedha kuweza kupata tiba inayo stahili, maana yake ni kwamba tatizo likitokea na likipatiwa ufumbuzi mapema ugonjwa hautapata nafasi.
Rais Kenyatta ametaja Vijana waliokata tamaa hajasema walevi au wanywa viroba hapana akimaanisha kuwa hawa vijana ni vijana mabao wanaweza wakawa na maamuzi ambayo tunaweza tukasema ni sahihi au sio sahihi ndio maana amewaonyesha viongozi wa nchi jirani kuwa wawaangalie sana hawa vijana sio wa kupuuzwa bali washikwe mikono.
8. Rais Kenyatta ameonyesha ni jinsi gani vijana walio kata tamaa wanaweza wakaanzisha uasi dhidi ya nchi zao na wazee wao, hii akimaanisha yeye ameyapitia mengi na ameyaona mengi ambayo yalimsumbua na si ajabu bado kuna chembe na hivyo hawezi kushauri wengine kutowashika mkono vijana hawa ni ushauri tu ambao ukipuuzwa huenda hotuba yake na ushauri wake utakumbukwa siku za mbeleni, wahenga wanasema jifunze kutoka kwangu, ni kweli mafanikio mengi hutokana na watu kujifunza kutoka kwa wengine na majanga mengi hutokana na matatizo ya watu kupuuza ushauri na kuamua bila kuomba ushari kabla ya utekelezaji
9. Nanukuu "Tumejifunza kama Wakenya kwamba uchaguzi pekee hauwezi kuleta amani na umoja kwa watu waliogawanyika. Kwa hilo, viongozi lazima wafikiane na kuwa madaraja ya kuwavusha watu keuelekea kwenye usalama na ustawi". Rais kenyatta amewapa somo wanao fikiria kwamba amani ya nchi na umoja wa wananchi hutokana na uchaguzi, mara nyingi viongozi wa nchi jirani wamekuwa wakiibuka kuwaomba wananchi wao wawe na amani wakisahau kuwa mahubiri ya haya ili yawe na nguvu lazima Haki iwe kwa vitendo kila mwananchi apewe haki yake anayo stahili maana ndio msingi wa amani, haki inapopatikana ndipo amani huwa imetawala.
Rais Kenyatta amesisitiza kuwa wanasiasa wazee wasiwachokoze wanasiasa vijana amelirudia hili badala yake wawalee kwa upendo hii ina maana kubwa sana maana future wanayo vijana, wazee wanaweza wakawachokoza na ikawa mwisho wao wakuwepo duniani na vizazi vyao.
10. Mwisho kabisa ni kwamba Rais Kenyatta ameonyesha kuwa hata kubali uchumi wa nchi yake utetereke kisa siasa za nchi jirani hatakuwa tayari kwa hilo maana yake kuna namna atafanya ili kurekebisha ili uchumi wa nchi yake uendelee kuwa imara siku zote. Kenyatta amejipanga, Kenyatta ameshauri, Kenyatta ameonyesha njia. Nini tena tunacho kihitaji kama wananchi wa nchi jirani na Kenya.