Pre GE2025 Hotuba ya Lissu Uchaguzi Mkuu CHADEMA: Asema amekuwa na Mbowe kwa zaidi ya miaka 20 bila kugombana, amshukuru

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Moderators pandisheni hii link HAPO JUU
 
Lissu anauzika kuliko Mbowe, sasa Mbowe akishinda nani atakua mgombea Urais hiyo Oktoba? Huyu mzee tamaa tu ila akishinda anajua kabisa momentum ya chadema inaenda kufa mazima.
Kwani ni mashindano ya urembo? Anatafutwa mtu wa kukiongoza chama, sio mgombea urais. Mtu atakayehakikisha kuwa chama kinapata wagombea bora, kuwa kina uwezo wa kugharamia shughuli zake siku zote na sio panapokuwa na uchaguzi Mkuu tu. Mnachotaka ni kukigeuza kuwa chama cha uchaguzi kama vyama kama DP.

Akishinda Mbowe CDM haitakufa maana ameonyesha ana uwezo wa kukiongoza na kukikuza katika mazingira magumu. Huyo mtu wenu akishinda ndio atagundua kuwa kuongoza chama ni zaidi ya kusimama jukwaani au kuwa Clubhouse.

Amandla...
 
Lissu anataka kuwa Mwenyekiti. Akishinda atagombea pia urais.

Amandla...
Vyeo vya kugawana havina nafasi hivi si vikao vya familia au vya kugawana madaraka. Mwenye uwezo anayekubalika na wengi ikiwezakana agombee vyote.

MBOWE MUST GO
Amandla
 
Vyeo vya kugawana havina nafasi hivi si vikao vya familia au vya kugawana madaraka. Mwenye uwezo anayekubalika na wengi ikiwezakana agombee vyote.

MBOWE MUST GO
Amandla
Mliotaka mtu wenu apite bila ushindani si nyie? Aliyeamua kugombea baada ya kupata mshindani si mtu wenu?

Amandla...
 
Mliotaka mtu wenu apite bila ushindani si nyie? Aliyeamua kugombea baada ya kupata mshindani si mtu wenu?

Amandla...
Rudisha kumbukumbu vizuri, baada ya kumleta Wenje agombee nafasi ya makamu mwenyekiti nikaamua kugombea uenyekiti na huyo aliyemtuma. Hii inaonyesha mtu anayetaka kupita bila ushindani?

Aliyalalamika kuwa hakuniambia kuwa atagombea uenyekiti ni nani, na inaashiria nini kama siyo kupita bila ushindani?

MBOWE MUST GO
Amandla
 
Huyu ameamua kugombea Uenyekiti kwa sababu tu Wenje aliamua kugombea nafasi ambayo aliamini ilikuwa yake. Na alipotangaza tu kugombea uenyekiti zikaanza kampeni za kumtaka Mbowe asigombee. Hakuwahi kuzikana hizo kampeni.

Kukiri kuwa alistushwa na Lissu kugombea sio kumzuia kugombea. Mbowe hajawahi kumzuia mtu kugombea na hamna kampeni zilizofanyika za kumtaka Lissu asigombee. Watu wa Lissu walitegemea kuwa wakipiga kelele na kumchafua kutamfanya Mbowe aone kuwa bora asigombee. Hiyo mbinu ime backfire.

Katika huu uchaguzi ni Mbowe na Odera peke yao waliosema kuwa watakubali matokeo ya uchaguzi bila masharti yeyote. Lissu atakubali matokeo kama utakuwa huru na wa haki. Maana yake ni kuwa akishindwa hautakuwa huru na wa haki.

Amandla...
 
Too late. Ameruhusu wapambe wake wamchafue Mbowe.

Amandla...
Unaweza kutusaidia hili, "unawezaje kudhibiti vinywa vya wafuasi wako kumzungumzia vibaya mshindani wako" Remember midomo ni yao, wanaweza kutumia watakavyo, now how do you control them? Advice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…