Mazingira na nyakati yamesababisha Lissu kugombea uenyekiti, na hakuna kanuni wala sheria aliyovunja kwa kugombea uenyekiti. Mojawapo ya sababu zilizomsukuma kugombea ni kukiokoa chama, hila na uhuni wa Mbowe kwenye uchaguzi kanda ya Nyasa ku.pitisha Sugu mpambe wake na ule ws Victoria kumbeba Wenje ni tosha kwa mwenye mapenzimema na CHADEMA kuja kukiokoa.Huyu ameamua kugombea Uenyekiti kwa sababu tu Wenje aliamua kugombea nafasi ambayo aliamini ilikuwa yake. Na alipotangaza tu kugombea uenyekiti zikaanza kampeni za kumtaka Mbowe asigombee. Hakuwahi kuzikana hizo kampeni.
Kukiri kuwa alistushwa na Lissu kugombea sio kumzuia kugombea. Mbowe hajawahi kumzuia mtu kugombea na hamna kampeni zilizofanyika za kumtaka Lissu asigombee. Watu wa Lissu walitegemea kuwa wakipiga kelele na kumchafua kutamfanya Mbowe aone kuwa bora asigombee. Hiyo mbinu ime backfire.
Katika huu uchaguzi ni Mbowe na Odera peke yao waliosema kuwa watakubali matokeo ya uchaguzi bila masharti yeyote. Lissu atakubali matokeo kama utakuwa huru na wa haki. Maana yake ni kuwa akishindwa hautakuwa huru na wa haki.
Amandla...
Kuhusu kuchafuana naona umekaririshwa au akili yako imekataa kukubali kweli, baada ya Lissu kutangaza nia yake ya kugombea wapambe wa Mbowe akina Paul Ntobi na Yericho Nyerere na akina Wenje na wengineo ndio walioanza kumponda Lissu mitandaoni kumwita mropokaji hana hekima nk. Na Mbowe hakuwahi kuwakemra hata mara moja, hadi kamati ya nidhamu ya mkoa wa Shinyanga ilipomvua madaraka.
Watu na wanachama wa CHADEMA kwa mara ya kwanza wameonyesha dhamira ya kutaka mabadiliko, na kwa kazi aliyoifanya Mbowe wameona bora apishe ilu Lissu aendeleze kazi aliyoifanya asiaibike kwenye sanduku la kura.
Dalili za rushwa kwa wapambe wa kambi ya Mbowe zimeonekana dhahiri mfano kwenye uchaguzi wa BAVICHA, na Mbowe hakemei. Uchaguzi wa kanda ya Nyasa na Victoria uliharibiwa na Mbowe akiwapitisha wapambe wake Sugu na Wenje, kwa hiyo akisababisha hila alizofanya kuwapitisha au kupita akirudia upuuzi huo ajue kambi ya Lissu hawatikubali.