Ninalazimika kuuleta uzi huu baada ya hatimaye kupata nafasi kuisikiliza sehemu ya hotuba ya mheshimiwa Mbowe:
Katika hotuba hii, sioni popote penye tatizo lolote na mtanzania yeyote:
1. Kwamba kuna wagonjwa wa Corona na watu wanakufa nchini kote?
2. Kwamba wahanga hawa wanalazimika kujigharimia kwa ajili ya matibabu dhidi ya ugonjwa huu?
3. Kwamba bei elekezi za matibabu ni kama anavyosema mwenyewe akiwa shahidi?
4. Kwamba msimamo wa serikali ya awamu ile ulikuwa ule tulioujua?
5. Kwamba msimamo wa serikali hii ni huu tunaouona sasa?
6. Kwamba kuna kubeza, kelele au manung'uniko kuhusiana na hotuba hii?
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Labda kama waasisi wa manung'uniko hayo watakuwa:
(a) hata chanjo wao walishapokea.
(b) hata wako nje ya nchi.
(c) ni kwa kuwa na uelewa wao mdogo.
Inafahamika kuwa kwa hawa waliokwisha pokea chanjo, wao wako salama na suala la ugonjwa huu ni historia na kimsingi kwao ugonjwa huu haupo tena.
Kwa hakika kwetu sisi tulio wahanga watarajiwa, kuibeza hotuba hii, ni kujaribu kutucheza shere wazi wazi na kwa makusudi mazima:
- Kutoka kwa wahanga watarajiwa wa Covid-19
--------
My take:
Ni dhahiri kuwa kuna upotoshaji mkubwa kuhusiana na alichokisema mheshimiwa Mbowe.
Bila shaka lengo likiwa kuwatoa watu kwenye reli au hoja halisi zilizozungumzwa.