Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
HOTUBA YA MKURUGENZI MKUU DKT. IRENE ISAKA KWENYE UZINDUZI WA MIFUMO NA MPANGO WA TOTO AFYA KADI
DODOMA, TAREHE 17 DESEMBA, 2024
Waziri wa Afya na Mgeni Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (Mb),
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge – Afya na Ukimwi
Katibu Mkuu-Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu,
Viongozi kutoka Wizara ya Afya
Viongozi wa Taasisi mbalimbali zilizoalikwa,
Washirika na Wadau wa Maendeleo (baadhi tuna ushirikiano wa muda mrefu)
GIZ – 2014 (CHF)- (kwa UHI 2023),
KfW- 2011 (Tumaini la Mama), (kwa UHI Juni, 2024),
PharmAccess – 2014 (kwa UHI April 2024),
NHIS-Korea - Septemba 2024,
Benjamin Mkapa Foundation - Januari 2024,
FSDT/TCDC - Septemba 2024 .
Menejimenti na Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,
Ndugu Waandishi wa Habari,
Wageni Waalikwa
Mabibi na Mabwana.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
DODOMA, TAREHE 17 DESEMBA, 2024
Waziri wa Afya na Mgeni Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (Mb),
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge – Afya na Ukimwi
Katibu Mkuu-Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu,
Viongozi kutoka Wizara ya Afya
Viongozi wa Taasisi mbalimbali zilizoalikwa,
Washirika na Wadau wa Maendeleo (baadhi tuna ushirikiano wa muda mrefu)
GIZ – 2014 (CHF)- (kwa UHI 2023),
KfW- 2011 (Tumaini la Mama), (kwa UHI Juni, 2024),
PharmAccess – 2014 (kwa UHI April 2024),
NHIS-Korea - Septemba 2024,
Benjamin Mkapa Foundation - Januari 2024,
FSDT/TCDC - Septemba 2024 .
Menejimenti na Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,
Ndugu Waandishi wa Habari,
Wageni Waalikwa
Mabibi na Mabwana.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Mhe. Waziri na Wageni waalikwa,
- Awali ya yote, naomba nimshukuru Mungu Mwenyezi, mwingi wa rehema kwa kutupa afya njema na kutuwezesha sote kukutana kwa pamoja siku ya leo ambayo ni muhimu sana kwetu kama NHIF katika utendaji au utoaji wa huduma zetu kwa wadau.
- Naomba nitoe shukrani za pekee kabisa kwako Mhe. Waziri wa Afya kwa kutenga muda ndani ya ratiba yako ngumu kuja kuzindua Mifumo ya Mfuko wa Bima ya Afya pamoja na Mpango wa Toto Afya Kadi ambao umekuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi kutokana na umuhimu wake kwa kundi la Watoto wenye umri chini ya miaka 18.
- Lengo la hafla hii,
- Mhe. Waziri na Waalikwa wote,
- Lengo la halfa hii ni kuzindua Mifumo miwili ambayo ni Mfumo wa Usajili wa wanachama na Mfumo wa uchakaji wa Madai. Mbali na Mifumo, Mhe. Waziri pia utatuzindua vifurushi vya ziada pamoja na Mpango wa Toto Afya Kadi ambao unakwenda kurejesha utaratibu wa kumsajili mtoto mmoja mmoja.
- Utekelezaji wa Shughuli za Mfuko,
- Kabla sijaongelea shughuli ya leo naomba kuongelea utendaji wa Mfuko
- Mheshimiwa Mgeni rasmi
- Mfuko umeendelea kuongeza Wigo wa Wanachama ili kuhakikisha wananchi wengi wanapata huduma kupitia Mfumo wa bima ya afya na Wanufaika. kipindi cha Julai 2023 hadi Oktoba 2024, Mfuko ulifanikiwa kusajili wanachama wapya 839,331 sawa na asilimia 94 ya lengo. Idadi hiyo ya wanachama waliosajiliwa, imewezesha Mfuko kuwa na wanachama wachangiaji 1,359,772 na wanufaika 5,106,957 sawa na asilimia 8.4 ya Watanzania wote.
- Mapato ya Mfuko
Katika kipindi cha mwaka 2023/24 Mfuko ulikusanya mapato jumla ya shilingi bilioni 756.48 ukilinganisha na shilingi bilioni 696.72 zilizokusanywa mwaka 2022/23. Hii ni sawa na asilimia 108.6 ya lengo.
Kwa upande wa michango ya wanachama, lengo ilikuwa kukusanya shilingi bilioni 668.03 ambapo uliweza kukusanya michango jumla ya shilingi bilioni 699.26 sawa na asilimia 105 ya lengo. Kutokana na jihada mbalimbali zikiwemo za kubana matumizi, Mfuko kwa sasa umeongeza uhimilivu wake kutoka miezi 6 hadi mwaka mmoja.
Urari wa Mapato na Matumizi
Hadi kufikia tarehe 31 Oktoba, 2024 ya Mwaka wa Fedha 2024/25, Mfuko ulikuwa umekusanya jumla ya shilingi bilioni 294.55 na jumla ya matumizi yalikuwa shilingi billioni 217.43 sawa na ziada ya shilingi billioni 77.12
Usajili wa Vituo vya kutolea huduma
Hadi kufikia mwezi Juni 2024, Mfuko ulikuwa umesajili jumla ya vituo vya matibabu 10,004 nchini kote. Kati ya vituo hivi, vituo vya Serikali ni 7,181 (72%), vituo vya Mashirika ya Dini ni 848 (8%), na vituo vya watu binafsi ni 1,975(20%).
Udhibiti wa vitendo vya udanganyifu
Hadi Oktoba, 2024 Mfuko ulitekeleza kazi zilizolenga kudhibiti na kuibua vitendo vya udanganyifu Mfuko ulibaini jumla ya shilingi bilioni 7.94 kinachotakiwa kurejeshwa kilichotokana na madai yenye udanganyifu kutoka kwa watoa huduma. Mfuko umeokoa Zaidi ya shilingi billion 18 kupitia uhakiki kwenye vituo vya kutolea Huduma. Jumla ya Kadi za wanachama 12,685 zilifungiwa na shilingi bilioni 2.59 zilirejeshwa. Mfuko utaendelea kutekeleza shughuli za kukabiliana na udanganyifu kwa kuimarishaji ugunduzi na udhibiti kwa kutumia mifumo ya TEHAMA, kuendelea kushirikiana na wadau wakuu katika kupambana na vitendo vya udanganyifu na kuongeza elimu ya uelewa kwa wadau wote wa Mfuko.
- Mikopo Nafuu kwa Watoa Huduma
- Kwa ujumla tangu kuanzishwa kwa mpango huo hadi Juni, 2024, Mfuko umetoa mikopo ya vifaa tiba yenye thamani ya shilling billioni 32.131 kwa vituo vya afya vilivyoidhinishwa 287; mikopo ya dawa yenye jumla ya shillingi bilioni 3.907 kwa vituo 45 na mikopo ya uboreshaji wa miundombinu ya shilling billioni 11.918 kwa vituo 96.
- UZINDUZI WA MIFUMO
- Mheshimiwa Mgeni rasmi,
- Nikianza na Mfumo wa Usajili, Mfumo huu umetengenezwa na Wataalam wetu wa ndani kwa sh. Millioni 445 ikilinganishwa na sh. Bln 3.5 iwapo tungetumia akandarasi za nje. Mifumo yetu inasomana na (NIDA, RITA, NECTA, NACTVET, NSSF, WCF, MCT, GEPG, UTUMISHI, MOF, BRELA). Mifumo hii miwili imerahisisha sana utendaji, Mfumo wa usajili wanachama unawawezesha wanachama kujihudumia wenyewe bila kulazimika kufika katika Ofisi za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Kwa kurahisisha kujiunga na kutuma michango Mfumo utaondoa malalamiko ambayo awali yalisababishwa na mapungufu ya kibinadamu lakini kubwa zaidi na kuondoa gharama za fedha au muda ambao awali ulitumika kwenda kwenye Ofisi zetu. Mfumo umehakikiwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao eGa na hivyo kuahikikisha kuwa ni salama.
- Kwa upande wa Mfumo wa Uchakataji Madai, Mfumo huu pia nao umetengenezwa na Wataalam wa ndani ambao umeleta mapinduzi makubwa katika eneo la uwasilishaji na uchakataji wa madai. Tulikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wanachama na Watoa huduma ya ucheleweshaji wa huduma au ulipaji wa madai Madai yalichukua hadi siku 90 wakati kwa mujibu wa Sheria tunapaswa kuchukua siku 60. Hivi sasa tuna wastan wa siku 45 kwa yale madai ambayo yamewasilishwa kwa wakati na hayana viashiria vya udanganyifu. Kwa mwezi tunapokea madai toka vituo zaidi ya 5010 yakiwa na wastan wa folio 1, 190,000.
- Mheshimiwa tulikuwa na malalamiko mengi ya kukata madai yaani rejection rates hadi asilimia 20 ila sasa kwa kutumia mifumo rejection zimepungua hadi kufikia wastan wa 9% lengo letu ni kufika asilimia 5.
- Toto Afya Kadi
- Mhe. Waziri na Wageni Waalikwa, Mpango wa Toto Afya Kadi ni mpango ambao ulianzishwa mwaka 2016 lakini kutokana na mwitikio mdogo, wtt waliojiunga walikuwa ni wagonjwa tu kwa hiyo iliondoa dhana ya bima ya afya kwa kuwa mtoto mmoja alitumia wastan wa mara 6 zaidi yakiwango kilichochangwa.
- Mfuko umepokea maelekezo yako ya kufanya mapitio ya fao la Toto Afya lililositishwa, kwa lengo la kulifanya liwe endelevu na stahimilivu. Watoto wataendelea kuandikishwa kupitia makundi yao ya shule kwa michango ya awali ya shilingi 50,400.00 kwa mwaka, Aidha watoto watakaojiunga kwa utaratibu wa hiyari wajiunga kwa viwango vilivyorejewa kama inavyoonyeshwa katika jedwali lifuatalo:-
Jedwali: Marejeo ya fao la Toto Afya na viwango vya Ukomo
Maelezo Chaguo 1 Chaguo 2 Chaguo 3 Malipo 658,000 237,000 150,000 Kiwango cha Ukomo Wanaolazwa 22,000,000 8,000,000 2,000,000 Wagonjwa wa Nje 3,000,000 2,000,000 1,000,000
Maeneo makubwa ambayo Mfuko umejiandaa na umeanza utekelezaji wake ni pamoja na usajili wa kundi la Wanafunzi kuanzia ngazi ya Awali hadi ngazi ya Chuo Kikuu. Aidha, Mifumo hii ambayo utaizindua muda mfupi ujao itawezesha Watanzania kupata taarifa muhimu kwa wakati na kuweza kujihudumia kwa kujiunga kiurahisi kama nilivyoeleza huko awali.
- Kutokana na haya, niwaombe sana wananchi watumie fursa hii kujiunga na NHIF ili waweze kunufaika na huduma zilizoboreshwa kwa kuzingatia mahitaji hali na gharama kulingana na vipato vya wananchi wetu.
- Mhe. Waziri na Wageni Waalikwa,
- Baada ya kusema haya, naomba sasa nimkaribishe ili aweze kukukaribisha kwa hatua inayofuata.
- Asanteni kwa kunisikiliza.