Hotuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliyoitoa jana Aprili 11, 2021

Mwanangu tulia kunywa maji pressure itashuka.
 
Ujinga mtupu,mtu yeyote tu kwa hiyo anaweza kukurupuka na kusema anahutubia taifa.Chokochoko zimeanza za operation zenu zile mkifikiri nchi ipo usingizini.Bado tupo kwenye hangover ya maombolezo, tukishakaa sawa wembe ni uleule.
 
Yaani unasoma hii hotuba wala huchoki siyo ya yule Mwendazake kwanza nilikuwa nazima TV akiwa anaongea.
Kama alikutumbuabua wewe au wazazi wako ni lazima uzime tv.

Lakini Magu alijua kupiga loba watu kwa hilo mtamkumbuka mpk mnakufa.
 
Akili zako znatosha kuvuka lami tu
 
Hi nchi ilikokua inaslemea mungu mwenyewe ananua ,ndio mAANA amemng'oa yule jamaaa...
 
Zama zenu zimeisha tulia dawa ipenye
 
Kama alikutumbuabua wewe au wazazi wako ni lazima uzime tv.

Lakini Magu alijua kupiga loba watu kwa hilo mtamkumbuka mpk mnakufa.
Zama za ushamba,kuteksna,kununua watu zimeisha poleni mazwazwa
 
Sijui akili za wapi hizi?? Kwahiyo akikosolewa ndio wavunje hiyo miradi??
Tatizo mliaminishwa kua yule ni mungumtu hakosei, akajipa umalaika mkampachika umungu mtu, mzee wako kangi akamuita masihi. Na wewe ni muhanga wa hilo kuamini kua alikua hakosei kisa ulikua hujui makosa yake.

Alijitakia mwenyewe wacha yampate.
 
NEVER AND NEVER AGAIN.

Hotuba nzuri kabisa inayopambanua mambo kwa upana wake. Huyu mzee anajua kupanga hoja mno. Kaongea yanayomhusu na nina hakika ana ushahidi wa aliyosema ana ushahidi sababu kubwa ni kwamba yeye ni muhanga namba 1 wa hayo yote. Sote mashahidi mwendazake alimkandamiza mno huyu mzee ni vile tu mkwanja upo la sivyo huenda hata leo asingehutubia taifa.
 
Mbowe ni wanasiasa aliekomaa kuliko mwanasiasa yeyote Katika Taifa hili.Mtake msitake. Ukisoma btn the lines utaelewa Hii ni Machine!!Kudos Mh Mbowe!!
 
Hotuba nzuri sana ya kiungwana,Mama ataielewa bila shaka.
Kazi ipo kwa mataga,vichwa maji,wanasubiri teuzi na chaguzi hii hotuba hawawezi kuisoma na kuimaliza waelewe.
 
TUYAZINGATIE MANENO MHIMU YA MHE MBOWE YA KUMUENZI HAYATI JPM.

Na Elius Ndabila
0768 239284

Mhe Mbowe amezungumza maneno mazito na ya kuenziwa. Lakini ninasikitika ameongea haya maneno ambayo yataendelea kuishi vizazi na vizazi Mhe Magufuli akiwa ametwaliwa. Haya maneno pengine angeyaongea marehemu akiwa hai yangempa bidii zaidi ya kukamilisha ndoto yake kwa Tanzania.

Maneno ya Mhe Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA yanazidi kumtambulisha Hayati Magufuli kuwa hakuwa mtu wa kawaida na Umati ule uliojitokeza kumuaga ulikuwa unamtambua JPM kama ambayo Mhe Mbowe amejitokeza hadharani leo kukiri uhodari, umahili na Vipawa alivyokuwa amejaliwa Mhe Rais. Mhe Mbowe amesema:-

"Mazuri tunayoweza kumkumbuka nayo, ninamuunganisha nayo kwani aliyaishi haya kwa ukamilifu wake, kwa kuyahubiri na kwa kuyatenda bila kujali au bila kuogopa athari zake. Mambo haya mawili ninayoyazungumza, sifa za kipekee za hayati Magufuli. Moja ni uthubutu wa kufanya maamuzi magumu. Rais wetu huyu alikuwa na uamzi wa kufanya maamuzi magumu ambazo busara za kawaida za binadamu zisingeweza kufanya. Yeye alikuwa na kipaji hicho. Ninakiita kipaji, aliweza kufanya maamzi magumu kweli kweli

Jambo la pili, aliamini na kusistiza ufanyaji wa kazi kwa bidii. Hii ni sifa nzuri. Rais Magufuli hakuwa mtu mvuvi, alifanya kazi, alijituma. Alifanya kazi usiku na mchana. Sasa tija ya kazi ni jambo moja, sasa kwamba alikuwa ni mchapa kazi ambaye vile vile ali insist watu wafanye kazi, aliishi filosofia ambayo CHADEMA tunaiamini kwamba asiyefanya kazi na asile. Jambo lile sisi tulilikubali. Tulilikubali kabisa kwa sababu CHADEMA tumehubiri mara nyingi kuwa asiye fanya kazi na asile. Hapa ndugu zangu Watanzania sijadili maisha yake binafsi, ninamjadili aliyekuwa Rais wa nchi, aliyekuwa na dhamana kubwa ya uhuru, haki na maendeleo ya nchi yetu na siyo chifu wa kabila au mwenyekiti wa ukoo wa familia. Lakini muda kwetu, muda kwetu siku zote ni dakitari na mengi tutajifunza tunapoendelea kumtambua na kumtambua". Freeman Mbowe

Kwa mkutadha huo ni kuwa CHADEMA wanakiri kuwa kazi kuwa aliyofanya JPM haina mfano wake. Na hili liko wazi kwa Watanzania wote. Binafsi ninampongeza Mhe Mbowe kuyasema hayo hadharani.

Lawama zingine za Mhe Mbowe hazina ushahidi wa wazi kama ushahidi huu wa bidii ya hayati JPM ambazo kazi zake zinaonekana kwa macho. Kama kuna mahali JPM alikosea basi tutambue kuwa alikosea kama binadamu Mwingine lakini ilikuwa katika nia ya kuhakikisha anachotaka kukiacha kwa Watanzania kinakamilika kwa wakati.

Kasi yake na maamzi yake ambayo Mhe Mbowe anakiri kuwa si ya binadamu wa kawaida bali binadamu mwenye kipaji cha hali ya juu cha kuamua, kutekeleza, kusimamia na kuchapa kazi pengine ndicho kilipelekea hayo mengine tusiyo na ushahidi nayo kutokea.

Tuendelee kumuenzi JPM kwa hayo makubwa mawili ambayo ndiyo msingi wa uongozi bora kwa Taifa linalokua kiuchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…