Hotuba ya mwisho aliyoindika Muammar Gaddafi

gaddafi had to help amin, kwa sababu tanzania ambayo ni nchi yako wewe ilivamia uganda mara 2, na mara zote hizo watu walikufa,maelfu, uganda haikuwahi kuivamia tanzania,
na kosa hilo la kuivamia uganda lilisababisha wazee enzi hizo pamoja na watoto wadogo wasio na hatia wateseke na njaa huku tanganyika
 
Hii hotuba inagusa/inatoa funzo kwa wenye akili
 
Kosa lake kubwa ni kujiona yeye ndiye anayestahili kuwa kiongozi wa libya pekee

Hili lilikuwa kosa kubwa sana ambalo hakulijua au alilijua akalipuuzia

Ni bora angeachia madaraka akamwachia mwingine, ungekuta mpaka Leo anadunda tu.
Yani mnalishwa upumbavu na mataifa ya magharibi na nyie mnashiba? Kweli tuna safari ndefu.........

Hivi baba yako(kiongozi) akiwa anakupa elimu bure, miundombinu bora/ afya bure, chakula maji na misaada mbalimbali.....

Then unakaa baada ya muda unasema baba huyu simtaki nataka baba mwingine....Hii ndiyo sababu walibia wanajuta hadi dunia iishe kwa kudhani kwamba maana ya demokrasia eti ni kibadilisha kiongoz kila miaka mitano

Hivi unajua malkia ana nguvu na maamuzi Uingereza?

Mbona hao tunaowaita wastaarabu wa demokrasia hawamtoi malkia ukafanyika uchaguz wa malkia mwingine?

Kwani urusi haijaendelea?

Mbona rais Putin wa Russia yupo kwa miongo kadhaa na bado nchi ina uchumi wa kutosha?

Kwa nyie mnaoamini (kama mlovyomezeshwa) kwamba demokrasia ni kukaa miaka mitano na kuachia mwingine...kama ingekua hivyo nchi yetu ingekua kama marekani mana huo ndio utaratibu wetu kwa miaka mingi sasa
 
Cha kusikitisha hapa ni kwamba stori za gadafi watu huzipata kutoka kwenye vyombo vya kipropaganda vya kimagharibi kama CNN BBC amnestry internaional e.t.c

Hivi ndio huuaminisha ulimwengu kua gadafi alikua dictator na muuaji na watu wakaamini hizi information zilizopakwa cosmetics
 
ndio tatizo la mtu mweusi huwa hana taratibu ya kuchunguza
mobutu aliipa amani na maendeleo nchi yake kadiri alivyoweza huku akijichukulia vi pesa kidogo mara moja moja huku zingine akipata kwenye investments zake,ila vyombo vya habari vya ulaya vikawaaminisha watu kuwa ana utajiri wa zaidi ya 15 billion usd, ila alivokufa wamefatilia hawajakuta zaidi ya 40 million usd
 
Mwanadamu anataka uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa,na kukaa miaka mingi kwenye uongozi haimaanishi kuwa yeye ana akili nyingi kuliko wengine....angeachia mapema wakati vuguvugu ndio imeanza si ajabu mpaka leo hii angekuwa anaishi.
 
Damu nyeusi hua hairidhiki hata uinyweshe balimi itataka Heineken Na ukiipa Heineken itataka bingwa Na matap tap
Kumbuka sisi binadam asili yetu hatupendi kutawaliwa ndio maana hata Mungu ametuacha huru tuamue sisi wenyewe kati ya njia ya uzima na njia ya uharibifu.

Tatizo Gaddafi hakusoma nyakati, utafikiri hakuna viongozi bora kama yeye ndani ya Libya hilo ndiyo kosa kubwa alilolifumbia macho na masikio.
 
Hebu tumia akili kidogo. Hivi hata ingekuwa ni wewe unapata vitu vyoye hivyp kutoka kwa kiongozi aliyepo madarakani ungetamani aondoke?
Mimi binafsi sipendi kutawaliwa, ni heri Nile ugali kwa maharagwe yaliyooza kwa uhuru na amani kuliko kula wali nyama kwa masimango.

Nikweli walibya walipewa huduma bora lakini ilikua ni "shut your mouth" kitu ambacho si asili ya mwanadam kuto kuwa huru.
 
Labda wewe. Walibya sas wanamtamani gadafi. Wanashindwa hata kutoka nje kufanya shughuli za maendeleo
 
Kosa lake kubwa ni kujiona yeye ndiye anayestahili kuwa kiongozi wa libya pekee

Hili lilikuwa kosa kubwa sana ambalo hakulijua au alilijua akalipuuzia

Ni bora angeachia madaraka akamwachia mwingine, ungekuta mpaka Leo anadunda tu.
Mi naona hata bora angemtengeneza mtu wake akampachika pale. Shida ya viongozi wa Africa kukatalia madarakani.
 
Kosa kubwa la Gaddafi alitaka kuipindua dollar . Alitaka itafutwe currency mbadala au waitumie dhahabu kwenye biashara za kimataifa
 
Hivi mnavyosema aliandika mwishoni alijua atauawa au kufa kwa namna aliyokufa au!?
 
Hebu tumia akili kidogo. Hivi hata ingekuwa ni wewe unapata vitu vyoye hivyp kutoka kwa kiongozi aliyepo madarakani ungetamani aondoke?
Uhuru wa watu ndio maendeleo ya kwanza mtu kukupa kila kitu kakunyima uhuru ni sawa na kukufuga ni sawa na kuku unampa pumba lkn hawezi toka bandani lazima binadamu wanao tawala wajue kwamba uhuru wa mtu ni jambo la kwanza ktk sector ya maendeleo .uhuru wa kulima na kuuza bidhaaa .sio nilime mm wewe unipangie tarehe ya kuuza na kupata pesa kama tulilima wote wakati wewe unategemea mshahara
 
Nakumbuka akiwa mbele ya Jengo la Ikulu iliyopigwa kombora Usiku...mchana wake aliisoma hotuba hii... Aliondoka kwa msafara wa magari kutokomea na kuanza kusakwa pande zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…