Zanzibar wanae Waziri wao wa fedha, kama walivyo na Waziri wa Afya, Mawasiliano na kadhalika. Mawaziri hao, si wa muungano. Mawaziri wa Muungano ni pamoja na, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Ulinzi. Lakini hilo si hoja.
Mimi nawaelewa waZanzibar wanapotaka rasilimali zao zibaki kwa maendeleo ya Zanzibar kwasababu zifuatazo:
1. Maliasili/utajiri wa bara kwa kiasi kikubwa hubaki Bara
2. Zanzibar haina rasilimali nyingi, na ili iweze kuendelea kwa kasi, ni lazima iweze kujikimu
3. Fedha za mikopo na misaada ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hupata, kiasi kikubwa haipelekwi Zanzibar
Nadhani kama kuna nia ya dhati ya kudumisha Muungano, ni vyema wakarudi kwenye makubaliano ya Muungano na kuuacha kama ulivyokuwa awali au kuufanya uwe bora kwa pande zote mbili.
Makubaliano yale kwa uchache yalikuwa kwamba, Rais akiwa wa Bara, Makamu wa Rais atakuwa kutoka Zanzibar. Nia ilikuwa ni kulinda maslahi ya pande zote. Ilivyo sasa, ni rahisi kusema Muungano umevunjwa kama ilivyo kwa siasa ya Ujamaa na Kujitegemea (bila kelele).