Hivyo lini umewasikia wale kule (Zenj) kupigia kelele -hata huo mchele wenu wa Kyela. Si wanakuja na kuununua (kwa mujibu wa taratibu za biashara)
Dondoo Muhimu:
- Kwa ujasiri mkubwa na lugha ya kistaarabu sana, ameyaomba gesi na mafuta yao, yawe yao, kama ilivyo bara na dhahabu yetu.
Katika hili la makubaliano kati ya Rais Karume na Seif Hamad, nahisi kuna siri kubwa sana. Naona makubaliano yao yamewaunganisha sana kiasi ambacho hakikutegemewa. Natumaini wataendeleza ushirikiano wao. Uchaguzi Mkuu wa ZNZ, mwaka huu nadhani hautakuwa na fujo hata kidogo.
Tangu lini SMT ikawasaidia wananchi wa Zanzibar katika mambo yao ya ustawi wa jamii- Elimu kwa watoto wao, afya kwao na watoto wao kilimo chao japo ni cha mpunga na viazi tona, Umeme ( si ndio mna ona hilo sakata sasa nani anahangaika SMT au Mansour). Fundi kuwa Fundi bwana . Mimi nategemea kuwa wewe unayaangalia haya mambo kwa utuo. Futa kama lipo ni lao la Zenj,. Na dhahabu hawafaidiki. Ikienda hazina wanapata majeshi na Mapolisi upo hapo?
Zanzibar wanae Waziri wao wa fedha, kama walivyo na Waziri wa Afya, Mawasiliano na kadhalika. Mawaziri hao, si wa muungano. Mawaziri wa Muungano ni pamoja na, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Ulinzi. Lakini hilo si hoja.
Mimi nawaelewa waZanzibar wanapotaka rasilimali zao zibaki kwa maendeleo ya Zanzibar kwasababu zifuatazo:
1. Maliasili/utajiri wa bara kwa kiasi kikubwa hubaki Bara
2. Zanzibar haina rasilimali nyingi, na ili iweze kuendelea kwa kasi, ni lazima iweze kujikimu
3. Fedha za mikopo na misaada ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hupata, kiasi kikubwa haipelekwi Zanzibar
Nadhani kama kuna nia ya dhati ya kudumisha Muungano, ni vyema wakarudi kwenye makubaliano ya Muungano na kuuacha kama ulivyokuwa awali au kuufanya uwe bora kwa pande zote mbili.
Makubaliano yale kwa uchache yalikuwa kwamba, Rais akiwa wa Bara, Makamu wa Rais atakuwa kutoka Zanzibar. Nia ilikuwa ni kulinda maslahi ya pande zote. Ilivyo sasa, ni rahisi kusema Muungano umevunjwa kama ilivyo kwa siasa ya Ujamaa na Kujitegemea (bila kelele).
Katika hili la makubaliano kati ya Rais Karume na Seif Hamad, nahisi kuna siri kubwa sana. Naona makubaliano yao yamewaunganisha sana kiasi ambacho hakikutegemewa. Natumaini wataendeleza ushirikiano wao. Uchaguzi Mkuu wa ZNZ, mwaka huu nadhani hautakuwa na fujo hata kidogo.
Tuliyaona haya Kenya pia na ikawa vizuri kabisa. Sasa Mzee Moi anaishi kwa raha mustarehe.
Wazanzibari wengi tu wameelimishwa bara wakati amabapo elimu ilikuwa bure.
Tunarudia makosa yale yale tuliofanya kwenye Muungano wetu. Huu muafaka ulitakiwa upate baraka za wanachama wa vyama vyote viwili kabla hauja-sainiwa. Ulitakiwa uwe wazi na kila mwanachama ajue nini hasa kilichokubaliwa. Muafaka wa kudumu hauwezi kuingiwa kwa siri kati ya Karume na Maalim Seif peke yao. Utakosa legitimacy. Tumeona tunavyosumbuka na huu Muungano walioingia viongozi wetu bila kutushirikisha wananchi. Bila kuweka wazi makubaliano haya basi yaliyopita yatarudiwa tena. Kwa kufanya hivi, kesho na kesho kutwa hakuna atakayekuwa na uwezo wa kuupindisha kwa manufaa yake bila wananchi kumstukia.
Amandla.........
Bara hata wapate mafuta kedekede lakini yataishia kwenye mikono ya wahindi na papa wa mafisadiHilo ndiyo tatiza la wanzanzibari hata sijui hizo pesa za muungano wanafikiri zinatoka wapi sijui.
Waache wanunue mbeleko kabla ya uzazi kwa maana ninaamini TZ-Bara yatapatikana mafuta mengi na vilevile madini kedede hasa nyanda ya juu kusini. Sijui ikiwa hivyo watataka kugawana.
UKIWA MROHO USIWE MCHOYO
Bara hata wapate mafuta kedekede lakini yataishia kwenye mikono ya wahindi na papa wa mafisadi
Mtanganyika kuingia Zenj lazima afanye hivyo akiwa na passport.....
Jaribu kwenda kama utaulizwa hiyo pasipoti...Mkuu JokaKuu, hii ni sawa? sijawahi kufika Zenji ati....
Katika kipindi cha tuongee cha Star TV asubuhi leo, Mhe Augustine Lyatonga Mrema amesema Rais Amani Karume anafaa kuendelea kuwa Rais wa zanzibar katika kipindi cha awamu ya tatu, licha ya ukomo wa kikatiba wa awamu mbili, akidai kwa kufanya hivyo atalinda maridhiano - yake na Seif Sharif Hamad Katibu mkuu wa CUF ambayo anaamini ni msingi mkubwa wa kurejea kwa amani na maelewano Zanzibar.
Anadai muda uliobaki kati ya sasa na oktoba kwenye uchaguzi mkuu hautoshi kutekeleza maridhiano kikamilifu na kama atakuja mwingine maridhiano yanaweza yasiendelee na zanzibar watareja kwenye mpasuko.
Pia anataka vyama vya siasa CCM na CUF vifutwe huko Zanzibar kwa kuwa hivyo ndivyo msingi wa machafuko zanzibar. Pia anataka Serikali ya Mseto iwepo Zanzibar kwa kuwa siasa ya wengi wape haiwezekaniki zanzibar.
Na anasema kugombea Urais ni Biashara kichaa kwake, na anasema Mwl Nyerere alimshauri kugombea ubunge, akapuuza na kugombea Urais, ikala kwake, na asiyesikia la mkuu, huvunjika mguu, na kwamba sasa anaamua kwenda kugombea Ubunge Vunjo, kwa kuwa Hayati Baba wa Taifa ni Muasisi wa CCM basi wana CCm wanapaswa kumuunga mkono.
Kwa wazanzibari na sio kwa wazanzibaraNa Zanzibar yataishia kwa wakina nani?
Amandla.......
Na Zanzibar yataishia kwa wakina nani?
Amandla.......
..lakini Wazenj si wanakuja huku Tanganyika na wanaweza hata kumiliki mashimo ya dhahabu,tanzanite,etc.
..Mtanganyika kuingia Zenj lazima afanye hivyo akiwa na passport. Wazenj wao wanaingia Tanganyika bila kuulizwa maswali yoyote yale.