Freddie Matuja
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,479
- 2,877
Hotuba ya Rais Museveni kwenye Kuapishwa kwa Rais Magufuli, imenitafarisha mambo 4; karibu tujadili tukiwa na open mind.
Naomba ku-declare interest ninamuunga mkono JPM kwa nafasi ya Urasi 2020-25. Kama unaidhika usiendelee kusoma huko chini.
Ila kama una imani ya kusifu tu, pia usisome ili usikwazike. Kwa mwenye jicho la tatu, karibu tujifahamishe mambo machache toka kwa Museveni kwa jicho/mtazamo wangu muandishi.
Tuendelee
Hotuba fupi ya Mzee Yoweri Museveni imenifikirisha sana kwa mambo manne ambayo ameyazungumza kama vipaumbele vya wafuasi wa falsafa ya baba wa Taifa la Tanzania mwl. JKN.
Either Jenerali Museveni katabainisha kuwa nchini kwake Uganda ni 32% ya wananchi ndio wanajishughulisha "commercial activities" tofauti na wengi ambao wanahangaikia mkate/ugali wa kula siku.
Kwa kutambua uzalishaji wa Uganda, Museveni akapigia chapua kuomba soko la sukari toka Uganda, mahindi toka Uganda, Maziwa na ndizi (industrial products)
Mwisho Museveni alijikita kwa kutaja vipaumbele vinne vya falsafa ya Mwl. Nyerere ambavyo ni
1. Ukombozi
2. Prosperity
3. Strategic Security na
4. Udugu
Mtazamo wangu juu kile Museveni kazungumza,
Bila shaka ukombozi dhidi ya ukoloni ulifanyika miaka ya '60 kwa nchi zetu hizi, ila bado kunahitajika jitihada ya kutosha ili kufikia ukombozi wa kiuchumi. Moja ya eneo ambalo mzee Kaguta kasisitiza, ni msingi wa kukuza uzalishaji wa bidhaa na huduma ili kukuza uchumi na sio kutembeza "bakuli" kwa wakoloni wetu wa zamani.
Hata kwetu, Rais Magufuli hana budi kuja na mkakati jumuishi wa kibiashara hasa kwa kutumia Benki ya Kilimo na Banki ya Uwekezaji ambao wanatakiwa kuwa "investment financiers" kwenye strategic investment.
Museveni katuomba tununue Sukari Uganda, ni jambo jema sana kwake. Ila najiuliza, kwanini nchi ambayo tumeisaidia kumtoa nduli Idd Amin na kumsaidia Museven kuingia madarakani, leo wana surplus ya sukari sisi (Tanzania) nchi yenye ukubwa wa ardhi na rasimali maji kwa wingi kuliko Uganda, tunashindwaje kuwekeza kwenye kuzalisha sukari?
Takwimu zaonesha, Tanzania ina-import sukari zaidi ya tani laki 2 (domestic sugar); ukijumuisha na industrial sugar kwa ajili ya viwanda vya artificial juice na soda ambavyo ni vingi; hapa hatuwezi kutegemea "bla bla" kutoboa. Lazima tuje na strategic investment projects ambapo tunaweza kabisa kuzalisha na kuzalisha ajira ili nguvu kazi ya Watanzania ipate ajira pia.
Tufanye tuwezavyo kuongeza strategic pertnetship kati ya serikali na local visionaries kwenye investment kwenye kuchakata
pamba,
kahawa
korosho
katani
chai
pareto
mchele na unga wa mahindi tunaweza kuongeza uzalishaji kabisa na ku-commercialize export ya unga na mchele wenye aroma ndani ya SADC na Middle East (GCC Market)
Kuna haja kubwa kuendelea kuchakata nyama na kuuza diverse products za mifugo ikiwemo ngozi. Ni faraja kwa kiwanda chini ya magereza kilicho mkoani Kilimanjaro.
Prosperity (mafanikio) hayatakuja by default; lazima ku-bridge gap namna gani itokee. Kwa akili ile ile ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wasome vyuo vikuu (japo hatujajiandaa kuzalisha ajira ili walipe mikopo wakipata kazi); basi tuje na strategic investment projects ambazo zitawapa Watanzania fursa ya kutumia nguvu na akili zao kuzalisha ili uchumi wetu uwe jumuishi zaidi.
Strategic Security ni neno lenye upana mkubwa. Kuna jitihada za kulinda mipaka tusivamiwe na maadui, ila nadhani moja ya eneo kubwa ambalo athari yako ya ulinzi yahitajika ni kuwafanya Watanzania wa-experience kuwa sehemu ya keki ya Taifa.
Sio wote watakuwa wanasiasa kwa kuchaguliwa au kuteuliwa serikalini au taasisi za serikali; iko haja serikali ikaja na mfumo kutoa Bank-guarantee kwa strategic investment projects kwa serikali kuwa shareholder pia.
Kuna miradi ya uwekezaji watu wa nje hawatakuja kuwekeza kabisa kwa kuwa watakuwa wanaua viwanda vyao vya nje; mathalani, Tanzania ni nchi ya wakulima, wavuvi na wafugaji; kwanini serikali isitoa bank guantee au soft loan za kuzalisha mbolea na viwatilifu vya kilimo/mifugo?
Mpaka lini tuendelee ku-import sulphur, CAN, Urea, DAP, NPK ambazo zikiingia via imports soko lake lipo?
Kama tunaweza kuwa na ubunifu TIC na Wizara ya fedha na wizara ya uwekezaji; moja ya shule mpya ya usalama kwa wenzetu inajumuisha kukuza uzalishaji wa bidhaa na huduma ambazo soko lake liko readily available.
Sifa pekee kwa JPM hazitoshi; iko haja kum-stretch ili aweke mkono wa serikali katika mambo kama hayo hapo juu. Kila mwaka tunaangiza reagents za practicals za mashule; kwanini graduates wa Chemistry wa nchi hii wasiwe na viwanda vya kuzalisha ili mashule na vyuo vinunue huko?
Hongera JPM kwa mitano tena, tuna haja ya kukaa nawe ili kufanya zaidi. Tupo kushirikiana nawe kwenye kuyafanya haya yatokee. Yanaweza yasitokee kwa public sector pekee, ila yanaweza kutokea katika private sector ambayo serikali inakuwa mbia wa uwekezaji wa kimkakati. Sio furaha/raha kuona watu wenye uwezo wa kufanya tofauti wapo na siko lipo na hela zinabaki TIB kila mwaka kwa kuwa mashrati ya kukopesha ni magumu, kumbe mkakati wa uwekezaji unaweza kufanya utofauti mkubwa kwa manufaa bora ya Tanzania tunayoitaka.
Wasalaam
Freddie